ZAIDI YA WATU 200 WAZAMA NA BOTI MTO NILE

Zaidi ya watu 200 raia wa Sudan Kusini wamezama katika ajali ya boti kwenye mto Nile wakikimbiavita vinavyoendelea katika mji wa Malakal.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Sudan Kusini.

Boti hiyo iliyozama, ilikuwa imewabeba watu wengi kupindukia. Watu hao walikuwa wanatoroka vita vinavyotokota katika mji wa Malakal.

Mapigano yalizuka Sudan Kusini mwezi Disemba mwaka jana baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake wa Rais Riek Machar, kwa kuwa na njama ya kumpindua.

Umoja wa Mataifa unasema kuwazaidi ya watu 1,000 wameuawa tangu ghasia kuanza nchini humo.