OBAMA ASEMA BORA BANGI KULIKO POMBE

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa kuvuta Marijuanaau Bhangi, sio hatari ikilinganishwa na Pombe.

Lakini Obama amesema kuwa Bhangi bado ni mbaya kwa afya ya binadamu.

Katika mohojiano na jarida la The New Yorker, alisema kuwa ni vibaya kuwa na dhana kwamba kuhalalisha dawa hiyo ya kulevya ndio jibu kwa maasi mengi yanayotokea katika jamii Bwana Obama alikuwa akigusia hatua ya hivi karibuni ya majimbo ya Colorado na Washington kuhalalisha utumiaji wa Bhangi.

Obama aliwahi kukiri kutumia dawa hiyo ya kulevya alipokuwa kijana.

"kama mnavyojua nyote nilivuta Bhangi nilipokuwa kijana na ninaiona kama tabia mbaya sawa na kuvuta sigara,'' alisema Obama Lakini aliongeza kwamba athari za Bhangi kwa afya ya binadamu sio mbaya ikilinganishwa na Pombe.

Pia alisema kuwa watu masikini wengi wao wamarekani wenye asili ya kiafrika na walatino, waliadhibiwa visivyo kwa kutumia Bhangi wakati watu wenye kipato cha kadri walikwepa adhabu kali."

Ni muhimu kwa jamii kufahamu kuwa sio sawa ikiwa idadi kubwa ya watu wanovunja sheria huwaadhibiwi vilivyo wakati wachache wanapata kuadhibiwa.

''Obama alitaja kuhalalisha Bhangi katika majimbo ya Colorado na Washington kama hali ya kutatanisha.