ARSENAL BADO NGANGARI

Arsenal jana usiku wamefanikiwa kurejea katika nafasi yao ya kwanza kwenye ligi ya Premier baada ya kuicharaza Aston Villa mabao mawili kwa moja.

Gunners waliwapiku Manchester City na Chelsea na kurejea juu ya orodha.

Ulikuwa ushindi rahisi kwa Arsenal kutokana na mabao ya Jack Wilshere na Olivier Giroud ndani ya dakika moja wakati wa kipindi cha kwanza . Bila shaka Arsene Wenger alikuwa mwingi wa furaha.

Villa muda wote walionekana tu kukimbiza vivuli vya wachezaji wa Arsenal ingawa hatimaye walifanikiwa kuingiza bao la kichwa kupitia kwa Christian Benteke na kuzua wasiwasi kwa watani wao Gunners walipata ushindi waliostahiki huku wakizidisha idadi ya mechi walizoshinda hadi mechi 15 tangu mwaka 1998.

Na kulikuwa na habari zaidi njema, ingawa mwanzo Theo Walcott hatacheza tena msimu huu naye mchezaji mwengine Alex Oxlade-Chamberlain amerejea uwanjani kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu.


Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo jana usiku alinyakua tuzoya mchezajii bora wa soka wa fifawa mwaka 2013 na kuwashinda Lionel Messi wa Barcelona na Frank Ribery wa Bayern Munich.

Ronaldo ambaye alinyakuwa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara kwanza mwaka 2008 alitangazwa kunyakua tuzo mwaka 2013 baada ya kupigiwa kura na makocha, manahodha na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa matokeo Ronaldo alipata kura 1365 akimshinda Messi aliyepata kura 1,205 na Ribery akiambulia kura 1,127.

Kwa upande wa wanawake golikipa wa Ujerumani Nadine Angerer alinyakuwa tuzo ya fifa ya mchezaji bora wa soka kwa upande wanawake huku aliyekuwa kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes akinyakua tuzo ya kuwa kocha bora wa dunia.