Maafisa hao walikataa ombi la awali ambapo Umoja wa Mataifa ulikuwa unataka taarifa za kina kuhusu dhuluma za kingono wakisema kuwa visa hivyo vinapaswa kushughulikiwa na idara ya mahakama katika mataifa ambako visa hivyo vilitokea.
Kashfa katika kanisa katoliki
Ujerumani-Kasisi aliyejulikanaakama Andreas L, alikiri mwaka 2012 kuwa aliwalawiti, watoto watatu wa kiume.
Marekani– ufichuzi kuhusu makasisi wawili Paul Shanley na John Geoghan waliowalawiti watoto mapema miaka ya tisini ,iliwaghadhabisha watu wengi sana.
Ubelgiji- Askofu Bruges, RogerVangheluwe, alijiuzulu Aprili mwaka 2010 baada ya kukiri kuwalawiti watoto wavulana kwa miaka mingi
Italy– Kanisa katoliki mnamo mwaka 2010 ilikiri kuwa visa 100 vya makasisi kuwalawiti watoto viliripotiwa kwa zaidi yamiaka kumi
Ireland– Ripoti iliyotolewa mwaka 2009 iligundua kuwa visa vya makasisi kuwalawiti watoto vilitokea sana mapema karne ya ishirini.
Papa Francis amesema kuwa ni jambo muhimu kukabiliana na visa kama hivyo ili kanisa liweze kupata sifa yake nzuri.
Kanisa hilo limekosolewa kwa kukosa kuchukua hatua za kutosha kuhusiana na madai ya dhuluma za kingono kanisani.
Mwezi jana, Papa Francis alitangaza kubuni kamati ya kukabiliana na visa vya dhuluma za kingono dhidi ya watoto kanisani pamoja na kutoa ushaurinasaha kwa waathiriwa.
Pia alitilia mkazo sheria kadhaa za kukabiliana na watuhumiwa wadhuluma za kingono na kupanua zaidi maana ya uhalifu.