MADIWANI WATUPIANA MAKONDE MWANZA

Vurugu kali zimezuka katika kikao cha cha mapitio ya bajeti ya manispaa ya Ilemela kwa mwaka wa fedha 2014/15.

Vurugu hizi zimeambatana na hatua ya madiwani wa Chadema kumfungia ndani ya ofisi yake Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Zuberi Mbyana wakishinikiza kurejeshwa kwa madiwani waliofungiwa kushiriki vikao katika manispaa hiyo.

Wakati huo huo Kufuatia kuikataa bajeti ya mwaka wa fedha 2014/15 baraza la Madiwani wa halmashauri ya jiji la Mwanza limewasimamisha watendaji wanne wa idara ya mapato ya jiji kwa upotevu wa shilingi milioni 28.

Mbali na watumishi hao mweka hazina wa jiji la Mwanza amepewa onyo la miezi mitatu huku akichunguzwa muenendo wake katika utumishi.

Hali si shwari katika manispaa ya ilemela mkurugenzi yuko chini ya ulinzi baada ya ofisi yake kupigwa kufuli na madiwani wa Chadema hali inayopekea tafrani mahali hapa.


Hatimaye hali inatengemaa, kati ya madiwani 13 walio katika kata hii ni madiwani watano pekee wanafanikiwa kupitisha bajeti hii kabla ya kikao kufikia tamati.

Kando baada ya kikao cha baraza, Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kinakiri kufanya kitendo hicho ili kufanikiwa azma yao ya kurudishwa kwa madiwani wa kata za Ilemela, Kirumbana Nyamanoro.

Kamati ya Fedha ya baraza la madiwani jiji la Mwanza inalazimika kukutana tena kujadilihoja ya ukusanyaji mapato kabla ya kukutana na kisanga cha kuwepo kwa ubadhilifu.

Baada ya masaa takribani 6 huku vikao vya kamati za fedha na nidhamu vikishika hatamu baraza linakutana na kutoa maazimio haya.