MAKUBALIANO YA IRAN YAAFIKIWA

Marekani, Umoja wa Ulaya na Iran zimesema kuwa maelezo yote kuhusu makubaliano muhimu ya mradi wa nuklia wa Iran yamemalizwa, na mkataba huo utaanza kutekelezwa tarehe 20 Januari.

Rais Obama amekaribisha makubaliano hayo ambayo yalimalizwa kwa ukamilifu juma lilopita kwenye mazungumzo mjini Geneva.

Kufuatana na makubaliano, Iran inatarajiwa kuacha sehemu za mradi huo na badala yake vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi hiyo vitalegezwa.

Iran imekanusha kuwa mradi wake umekusudiwa kutengeneza silaha za nuklia. Inasema lengo ni kutoa nishati