ASKARI 96 WAMALIZA MAFUNZO

Jumla ya Askari 96 wa Shirikala Hifadhi la Taifa la Wanyama Pori (TANAPA) wamehitimu mafunzo ya miezi mitatu katika chuo kipya cha wanyama pori cha Mlele kilichopo Mkoa wa Katavi na kutoa kiapo cha utii mbele ya Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan Kijazi.

Askari hao wa TANAPA walimaliza mafunzo hayo hapo juzi kwenye chuo hicho cha wanyama Pori cha Mlele akiwa ni mafunzo ya kwanza hapa nchini kwa TANAPA kutoa mafunzo kama hayo kwa Askari wa wanyama pori kupatiwa mafunzo hayo kabla ya kuanza kazi Katika Risala yao ya wahitimu wa mafunzo hayo ya kulinda maliasili iliyosomwa na Bruno Mbunda walieleza kuwa wamejifundisha mbinu mbalimbali za kulinda rasilimali za Taifa kwa Vitendo na nadharia.

Waliyataja baadhi ya mafunzo waliyoyapata kuwa ni namna ya kufanya doria , kukamata waharifu kumpekua mharifu na kutotumia nguvu sana katika kukamata mharifu pamoja na pia wamejifundisha namna ya kutumia silaha.

Walieleza katika kipindi hicho cha mafunzo wahitimi hao walifanikiwa kukamata waharifu hamsini wakati wakifanya doria katika maeneo mbambali ya Mbuga ya Katavi na kwenye mapori ya akiba ya Rukwa Lwafi.

Wahitimu hao walieleza kuwa mafunzo hayo yaliwashirikisha Askari 99 lakini watatu kati yao wameshindwa kuhitimu zikiwemo sababu mbambali kama utoro na utovu wa nidhamu hari ambayo ilfanya wahitimu waliomaliza kubaki 96 ambapo kati yao mwanamke ni mmoja na wanaume ni 95.

Kwa upande wake mkuu wa mapori ya akiba ya Rukwa Lwafi Joseph Mbung'ombe alimweleza mkurugenzi mkuu wa TANAPA kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali Alizitaja changamoto hizo kuwani ukosefu wa mawasiliano na ubovu wa miundo mbinu ya barabaa na upungufu wa magari pamoja idadi ndogo yawashiriki wa mafunzo kwa wanawake na ufinyu wa bajeti.

Nae Mkurugenzi wa Hifadhi na Ikolojia Martini Loibook alieleza kuwa mafunzo hayo walioyapata yana umuhimu sana hasa kutokana na changamoto zinazoikabili nchi yetu inayokabiliwa na wimbi la ujangili Pia Mkurugenzi wa utumishi na utawalla wa TANAPA Witnes Shoo aliwataka wahitimu hao kufanya kazi kwa uaminifu kwa kujituma na wawe na didamu na wasiwe na tabia ya kutowa siri za ofisi.

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliwaasa wahitimu hao wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu mkubwa hasa katika shughuli zao katika kupambana kukomesha ujangili Aliwataka kutojihusisha na masuala ya ujangiri na badal awahakikishe wanafanya kazi za kupambana na mitandao yaujangiri iliyopo ndani ya nchi na nje ya nchi Alisema wapo baadhi ya watumishi wa TANAPA ambao wamekuwa sio waaminifu hivyo wahitimu hao wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu pasipo kurubuniwa na mtu yoyote yule au watu.


Chanzo:Katavi Yetu