Kuna minong'ono kwamba huenda Generali Al Sisi akawania Urais wa Misri katika miezi michache ijayo.
Anaaminika kuchangia pakubwa katika kumuondoa madarakani Rais aliyeegemea misingi ya kiisilamu Mohammed Morsi mwaka jana kufuatia maandamano makubwa dhidi yake.
Abdel Fattah al-Sisi, anaonekana kupendwa sana kiasi kinachofananishwa tu na alivyopendwa Gamal Abdel Nasser lakini baadhi wanahisi kuwa kutawala kwake kunaweza kurejesha hali ya ukandamizaji ulioshudiwa chini ya utawala wa Hosni Mubarak.