MAMLAKA YA HALI YA HEWA YATOA TAHADHARI

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kuwepo kwa upepo mkali, mawimbi makubwa baharini pamoja na mvua kubwa kuanzia kesho hadi Januari 16, 2014.

Maeneo yatakayo kumbwa na upepo mkali ni: Pwani ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Maeneo yatakayokuwa na Mvua Kubwa ni: Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Mtwara pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro.