DK. MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA MABASI YAENDAYO KASI

Kampuni ya Strabag International GmbH inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni hapa jijiniDar es Salaam imetakiwa kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo kama mkataba wao unavyoelekeza.

Waziri wa Ujenzi Mhe. Magufuli alitoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Dar es Salaam Bus Rapid Transit - BRT) ambao umeelezewa kuwa na changamoto nyingi kiasi cha kusababisha usumbufu kwa watumia barabara hiyo kwa kipindi kirefu.

Akimpatia taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale alimjulisha Waziri Magufuli kuwa kwa hivi sasa changamoto nyingi zimefanyiwakazi na mradi unaendelea kusimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha kuwa hukuna ucheleweshaji zaidi katika hatua hii iliyobaki.

Mkataba wa ujenzi wa barabara hizi pamoja na vituo vya mabasi ulisainiwa mwezi Desemba mwaka 2012 ukiwa umepangwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu kwa gharama ya Shilingi bilioni 280.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Saddik ambaye aliambatana na Waziri Magufuli katika ziara hiyo, amewataka wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao ndani ya sehemu ambayo mkandarasi anaendelea na kazi waondoke kwani hiyo mbali ya kuwa kinyime na taratibu za uendeshaji biashara zilizowekwa lakini pia imekuwa ni moja ya kisingizio kinachotolewa kwamba uendeshaji wa shughuli hizo unachangia kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo.

Waziri Magufuli akizungumza wakati wa kuhutimisha ziara hiyo, amemtaka mkandarasi kuhakikisha anaukamilisha mradi huo kwa muda na viwango vilivyokusudiwa.

"Na kwa wale walio ndani ya eneo la ujenzi ni lazima sheria ichukue mkondo wake" alisisitiza Waziri Magufuli huku akimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni Mhandisi Mussa Natty kuhakikisha anasimamia zoezi hilo la kuondoa haraka wale wote wote walioingia katika eneo hilo la barabara kinyume na sheria.

Aidha, Waziri Magufuli alielezea kushangazwa kwake kwa kuchelewa kuondolewa kwa nyaya za Tanesco katika maeneo ya City Squire na Morocco kwani fedha za kutekeleza kazi hiyo tayari zimelipwa muda kirefu.

"Ucheleweshaji wa ainaa hii ndiyo unaotoa mwanya kwa mkandarasi kuanza kutoa visingizio vya kutokamilika kazihii kwa wakati" ametahadharisha Mhe. Magufuli.

Hata hivyo katika hatua nyingine Mhe. Magufuli amemtaka mkandarasi kuharakisha taratibu za kuifungua barabara hiyo upande wa kuingia Dar es Salaam ambako kwa sasa hivi hakuna shughuli kubwa zinazofanyika ili kupungiuza adha ya msongamano wa magari yanayopishana katika njia moja ya upande wa kutokea mjini katika barabara hiyo ya Morogoro hasa kwa eneo kati ya Ubungo na Kiamara.

Naye Msimamizi wa mradi huo kutoka TANROADS Mhandisi Barakaeli Mmari ameelezea kuwa, utekelezaji wa mradi huu wa usafiri wa haraka utajengwa katika awamu sita.

Awamu ya kwanza ambayo ujenzi wake ndio huu unaoendelea inahusisha barabara zenye jumla ya kilometa 20.9 ambazo ni Kimara – Kivukoni, Magomeni –Morocco na Faya – Karikaoo. Hadi sasa mkandarasi amekwisha kamilisha asilimia 55 ya mradi wote.

MTU MMOJA AFARIKI, 38 WAJERUHIWA

Mtu moja amefariki duni na wengine 38 wamejeruhiwa baada ya basi la Bunda kugonga kichwa cha treni katika makutano ya reli na barabara wilayani Manyoni.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha basi la Bunda lenye usajili wa namba T 782 BKZ lililokuwa likitokea mkoani Dodoma na kuelekea mkoani Mwanza, mkuu wa wilaya ya Manyoni bi Fatuma Toufiq amesama ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi saa mbili tarehe 28 katika makutano ya barabara na reli mjini Manyoni.

Akiongea na ITV na Radio one muuguzi mkuu wa haspitali ya wilaya ya Manyoni Bi. Heliechi Malisa amesema wamepokea maiti moja ambayo imetambulika kwa jina la Perina Bikombo mkazi wa Manyoni na majeruhi thelasini na nane wamelazwa na wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Manyoni.


Chanzo:ITV

SERIKALI YANUNUA AK-47 500

Siku moja baada ya Tanzania kutajwa na Shirika la Polisila Kimataifa (Interpol) kuwa kinara wa biashara ya meno ya tembo Afrika Mashariki, Serikali imelipia kodi na kukabidhiwa bunduki 500 aina ya AK47 ili kukabiliana na ujangili katika hifadhi na mapori ya akiba nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema jana kuwa silaha hizo zilizokuwa chini ya Mamlaka yaMapato Tanzania (TRA), tangu Novemba 2012 kutokana na kutokulipiwa kodi, zitasambazwa Ngorongoro, Selous, pamoja na Hifadhi za Taifa za Tanapa.

Kati ya silaha hizo, 250 zitapelekwa Idara ya Wanyamapori, 200 Tanapa na 50 Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro.

"Silaha hizi jumla ya Sh427 milioni kuzinunua lakini zilikwama TRA kwasababu ya kutolipiwa kodi na ushuru mbalimbali, hivyo wizara yangu leo inatoa Sh212 milioni kwaajili ya malipo hayo," alisema Waziri Nyalandu.

Alisema silaha hizo zimekombolewa ikiwa sehemu ya kutekeleza maazimio ya Bunge na ahadi ya Serikali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira.

Akizungumzia sababu za kuchelewa TRA, Nyalandu alisema kulikuwa na ubishi wa ama zilipaswa kulipiwa kodi au la, lakini mamlaka hiyo ilifafanua kuwa hayo ndiyo matakwa ya sheria, hivyo akaamua kutoa fedha hizo.

Alipoulizwa ni jinsi gani Serikali itadhibiti silaha hizo, Nyalandu alisema wizara yake inaandaa miikoya matumizi yake ikiwamo kufuatilia makabidhiano yake na askari wanaokabidhiwa.

"Kumbuka hizi si silaha za kwanza kuwa nazo, tunazo nyingine za AK47 na hizo zimetuwezesha kukamata silaha haramu zaidi ya 2,000 zinazotumiwa na majangili," alisema.

Silaha hizo zimepatikana ikiwa ni takriban wiki mbili tangu Rais Jakaya Kikwete abanwe na vyombo vya habari vya kimataifa akitakiwa kueleza mikakati iliyopo kupambana na ujangili ambao umeharibu sura ya Tanzania nje ya nchi.

Itakumbukwa kuwa miezi miwili iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alilazimika kupangua Baraza la Mawaziri na kuwatimua mawaziri wanne kutokana na vitendo vya kinyama vilivyobainishwa na Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira wakati wa Operesheni Tokomeza Ujangili.


*MAJANGILI PAPA 40

Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Waziri Nyalandu alisema majina ya majangili papa 40 ambayo Rais Kikwete alisema anayo, 'yatabandikwa' hivi karibuni.

"Serikali ina mkono mrefu sana, hatupendi mtu aache mke na watoto wake afungwe miaka 50. Kama ni majina tutayabandika, nimeshakubali, tutayabandika, ni kwamba tu sina hiyo orodha hapa," alisema.

Alisema, Serikali inawafahamu majangili hao kwa undani, wanapokunywa chai, wanapotembelea na shughuli zao za kila siku.

Alisema majina yao si siri kwani tayari wameshafunguliwa mashtakana wapo chini ya mfumo wa Mahakama na wamekamatwa na vidhibiti.

Hivi karibuni, Rais Kikwete alihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), alisema Serikali ina majina 40 ya majangili papa na mkuu wao yuko Arusha.


*SELOUS YAIMARISHWA

Katika hatua nyingine, Nyalandu alitangaza kuzipandisha hadhi kanda nane zilizopo katika Pori la Akiba la Selous ili ziweze kujitegemea kiutendaji kwa kuwekamkuu wa kila kanda.

Alisema pori hilo lina ukubwa unaokaribia hifadhi zote za Taifa chini ya Tanapa, jambo linalolifanyakuwa kubwa kimenejimenti na kiuendeshaji.

Pori la Selous lina kilomita za mraba 55,000 wakati mapori yote nchini kwa ukubwa wake ni kilomitaza mraba 57,000.

Katika kuweka mazingira ya uangalizi wa kina ya kupambana na ujangili aliiagiza Idara ya Wanyamapori kukamilisha mchakato wa kufungua akaunti maalumu za benki kwa kila kanda ili kuwawezesha wakuu wa kanda kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Chanzo:Mwananchi

WAJUMBE ODM WAZUA VURUGU

Vurugu zimezuka katika uchaguzi wa kuwachagua maafisa wapya wachama kikuu cha upinzani cha ODM nchini Kenya, chake aliyekuwa waziri mkuu wa taifa hilo Raila Odinga.

Polisi waliwasili katika ukumbi wauwanja wa michezo wa kimataifa wa Kasarani viungani mwa jiji la Nairobi kurejesha utulivu baada ya baadhi ya wafuasi wa chama hicho waliodaiwa kuwa walinda usalama kurusha viti pamoja na masanduku ya kupigia kura wakijaribu kuvuruga uchaguzi huo.

Ugomvi ulizuka baada ya kuzuka madai kuwa kulikuwa na orodha ya wajumbe bandia iliyokuwa ikisambazwa pamoja na makaratasi bandia ya kupigia kura. Mbunge maalum Isaac Mwaura ambaye anaishi na ulemavu wa ngozi-Albino-alionekana akisukwasukwa na wajumbe baada ya kuzua zahama kuhusu madai hayo ya udanganyifu katika zoezi hilo la upigaji kura.

Chama cha ODM ndicho chama kikubwa zaidi cha kisiasa nchini Kenya kikiwa na idadi kubwa ya wabunge katika bunge la kitaifa pamoja na Senate. Chama hicho kimemudu mgao mkubwa zaidi wa pesa za kufadhili shughuli za vyama vya kisiasa kutoka kwa serikali ya Kenya.

Kutokana na raslimali za chama hicho uchaguzi wa leo umeonekana kuzua msisimko mkali pamoja na patashika baina ya wanasiasa mashuhuru ambao wanagombania vyeo mbali mbali.

Bwana Odinga ambaye alishindwana rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliokumbwa na madai ya udanganyifu mwezi Machi mwaka uliopita anatetea kiti chake kama kiongozi wa chama, dalili kwamba huenda akagombea tena kiti cha urais mwaka 2017.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji kura Bwana Odinga alizungumzia maswala mbali mbali yanayohusiana na usalama nchini Kenya pamoja na kuiponda serikali ya mpinzani wake Rais Uhuru Kenyatta kwa kushindwa kuleta suluhu ya matatizo ya kiuchumi yanayowakabili wakenya.

BENKI YA DUNIA YABANA MSAADA KWA UGANDA

Benki ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda , siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kuizinisha sheria mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.

Benki hiyo imesema kuwa inataka kufanya tathmini yake kuhakikisha kuwa malengo yake ya maendeleo nchini Uganda katika sekta ya afya, ambayo msaada huo ulikuwa unanuiwa, hayata athirika.

Sheria iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Wafadhili wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda.

Wahisani kama Denmarkna Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja badala ya serikali.

Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.

Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.

Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.

Hadi kufikia sasa Waziri wa FedhaWa Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yoyote inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.

Jana serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya Uganda.

Norway na Denmark pia zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.

TFF YAVUNJA MKATABA NA KIM POULSEN

Hatimaye Shirikisho la Kabumbu nchini Tanzania TFF limetangaza kuvunja mkataba wake na Kocha mkuu wa Timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars Kim Poulsen kwa kile kilichoelezwa maafikiano ya pamoja baina ya kocha huyo, TFF, na Serikali.

Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa Shirikisho la soka Tanzania amesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida hasa baada ya wadau mbali mbali kuona kuwa huu ni wakati wa kufanya mabadiliko ya lazima katika benchi la ufundi la Taifa Stars ambayo inajiandaa kwa mechi za kufuzu kwa Fainali za kombe la mataifa Afrika hapo mwakani zitakazofanyika nchini Morocco.

Kuhusu gharama za kuvunja mkataba na Kocha huyo Bwana Malinzi amesema serikali haitagharamia uvunjaji huo wa mkataba na kocha huyo na badala yake wapo wadau waliojitokeza kugharamia kutokana na kuona umuhimu wa kufanya mabadiliko katika kipindi hiki kwa faida ya soka la Tanzania.

Kwa Upande wake Kocha Kim Poulsen amesema na rekodi yake inaonyesha kuimarika kwa soka la Tanzania katika kipindi cha takriban miaka miwili aliyokuwa akikinoa kikosi cha Taifa Stars lakini kusitishwa mkataba ni jambo la kawaida kwa kocha yeyote baada ya kipindi fulani kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine na ndiyo sehemu ya maisha.

"Kama kocha unapoona ndiyo umefanya kazi yako, unapaswa kuangalia mbele zaidi baada ya kufanya kazi yako si lazima uendelee kuwa hapo, mnakaa na kujadiliana na kuachana kwa amani kisha unapaswa kusonga mbele, ninaondoka nikiwa najivunia kipindi nilichofundisha soka hapa, na ninawatakia kila la kheri Tanzania na Taifa Stars kwa ujumla."alisema Poulsen.

Kuhusu Kocha mpya wa Taifa Stars Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa TFF amesema hadi sasa wapo makocha watatu raia wa Uholanzi ni wawili na Mjerumani mmoja wanaosailiwa kwa ajili ya kumrithi Kim Poulsen,lakini mojaya vigezo Malinzi amesema kuwa ni lazima kocha huyo awe amewahi kuipeleka kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika moja ya nchi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara.

Katika hatua nyingine kocha Salum Madadi ameteuliwa kukaimu nafasi iliyoachwa wazi na Kim Poulsen ambapo kocha huyo akisaidiwa na Hafidh Badru kutoka Zanzibar watasimamia Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyoko kwenye kalenda ya FIFA baadaye mwezi ujao.

MADRID YAIFUMUA SCHALKE 04, CHELSEA YABANWA MBAVU

Mchezaji bora duniani mwaka huu Cristiano Ronaldo Gareth Bale na Karim Benzima walifungamabao mawili kila mmoja na kuisaidia Real Madrid ya uhispania kufuzu kwenye robo fainali ya kombe la mabingwa barani ulaya baada ya kuinyeshea Schalke 04 ya Ujerumani mabao 6-1 katika mkondo wa kwanza uliosakatwa huko Ujerumani.

Benzima ndiye aliyefungua kivuno hicho cha mabao baada yanipe nikupe kunako dakika ya 13.

Mchezaji aliyeigharimu Madrid kitita kikubwa zaidi msimu huu Gareth Bale akafanya mambo kuwa mawili kwa nunge dakika saba baadaye.

Kuanzia hapo kampeini ya vigogo hao wa ligi ya uhispania kunyanyua taji lao la kumi barani Uropa ilikuwa mbioni kufuzu kwa hatua ya robo fainali.

Ronaldo alimpangua Joel Matip kwa miondoko ya aina yake na kufunga la tatu akimwacha kipa wa Schalke Fahrmann asijue azibe wapi azue wapi.

Masaibu ya wenyeji hao yaliongezeka Karim Benzema alipofuma bao la nne.

Bale akaongezea bao la tano kisha nyota wa Ureno Ronaldo akafunga kiziba mkonga na kudidimiza kabisa mtumaini ya timu ya tatu ya Ujerumani baada ya mabingwa Bayern Munich na washindi wa pili Borussia Dortmund kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya mchuano huo msimu huu.

Uchungu uliwazidi mashabiki wa nyumbani na wachache waliosalia uwanjani walishuhudia bao la kukata na shoka la nyota wao Klaas-Jan Huntelaar.

Huntelaar aliyeichezea Madrid (2009) kwa mkopo alifuma mkwaju wa kipekee uliomwacha Iker Casillas ameduwaa.

Hata hivyo bao hilo la kufutia machozi la dakika ya mwisho ya mechi haitakuwa na faida mbali na kunusuru hadhi ya kocha Jens Keller Schalke itakapozuru bernabou baada ya majuma mawili kwa mkondo wa pili.

Katika mechi nyengine iliyosakatwa usiku wa jana huko Instabul, Uturuki ,matumaini ya pekee ya timu ya Uingereza kusonga mbele katika hatua ya robo fainali yalitegemea matokeo baina ya wenyeji Galatasaray na Chelsea

Matokeo ya mkondo wa Kwanza

*.Barcelona 2-0 Man City

*.Paris St-Germain 4-0 Bayer Leverkusen

*.Atletico Madrid 1-0 AC Milan

*.Bayern Munich 2-0 Arsenal

*.Manchester United 0-2 Olympiakos

*.Borussia Dortmund 4-2 Zenit St Petersburg

*.Chelsea 1-1 Galatasaray

*.Real Madrid 6-1 Schalke


Kwa kila hali na mizani mechi hii ilitarajiwa kuwa ngumu kwa Galatasaray chini ya kocha wa zamani wa Manchester city Roberto Mancini ikiongozwa na aliyekuwa mshambulizi wa Chelsea Didier Drogba na Emmanuel Ebuoe zamani akiichezea Arsenal ilikuwa inakabiliana na The Blues chini ya Kocha Jose Mourinho.

Uwanjani mashabiki wa nyumbani walinyamazishwa na bao la dakika ya 9 ya kipindi cha kwanza iliyofungwa na Fernando Torres.

Roberto Mancini alilazimika kufanya badiliko la mapema ilikuzia kuabishwa na wimbi la mashabulizi ya vijana wa Mourinho.

Katika kipindi cha pili juhudi za Galatasaray kujinasua zilizaa matunda Aurelien Chedjou alifunga bao la kusawazisha baadaya kutumia vyema mpira wa kona uliomchanganya Peter Cech.

Bao hilo ndilo litakaloamua mshindi baina ya timu hizo mbili zitakapokutana katika mechi ya mkondo wa pili tarehe 18 mwezi Machi huko Stamford Bridge.

MAREKANI YAIPIGA MKWARA URUSI

Marekani imeionya serikali ya Moscow isithubutu kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Ukraine.

Hatua hii inawadia siku moja tu baada ya Urusi kuamuru kufanyika kwa mazoezi ya kijeshi yanayoshirikisha askari wapiganaji laki moja na nusu kwenye mpaka wake na Ukraine.

Kujitokeza kwa wanajeshi wa Urusi kwenye mpaka na Ukraine kumeimarisha uhasama ulioko kati ya Urusi na mataifa ya Magharibi.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry amesema kuwa Urusi inapaswa kukubali ushauri ya kwamba mataifa ya kigeni yasiingile mambo ya ndaniya Ukraine.

Alisema kuwa kujiingiza kijeshi katika hali ilivyo nchini Ukraine kwa hivi sasa ni kosa kubwa.

Mawaziri wa ulinzi kutoka mataifaya muungano wa NATO wametoa taarifa ambapo wamesema kuwa wanachama wake wataendelea kuunga mkono uhuru na hadhi yataifa la Ukraine.

Serikali ya Marekani imesema kuwa imetenga mbinu mbalimbali inazotazamia kutumia kuimarisha Ukraine kiuchumi, huku kukiendelea kuwa na hofu kuwa huenda taifa hilo likashindwa kuendelea kulipamadeni yake.Kwa wakati huu msaada wa kijeshi pekee kwa Ukraine hautoshi kwani taifa linalotaka kusaidia lazima kwanza liimarishehali ya kukubaliwa kwake katika taifa hili ambalo limegawanyika kwa imani yake kati ya Urusi na mataifa ya Magharibi.

Wabunge kadhaa wa Marekani wameonya kuwa Jumuiya ya Ulaya na Marekani wasipotoa msaada wa pesa taslimu Urusi huenda ikafanya hivyo.

KENYA KUPELEKA MAJESHI SUDAN KUSINI

Kamati Kuu ya Usalama Nchini Kenya imependekeza kwa bunge liidhinishe nyongeza ya idadi ya wanajeshi wake wa kudumisha amani walioko nchini Sudan Kusini, chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa, kwa majeshi 310.

Kamati hiyo chini ya uenyekiti waRais Uhuru Kenyatta imesema imechukua hatua hiyo kufuatia ombi la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lililofanywa Desemba 24, mwaka jana.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa ikulu ya Nairobi usiku wa kuamkia leo, kamati hiyo ambayo imekutana kwa mara ya kwanza tangu Rais UhuruKenyatta kuanza utawala wake mwaka mmoja uliopita ilisema kuwa Kenya itawatoa wanajeshi wengine ili kufanya idadi ya wanajeshi wake walioko Sudan Kusini kufikia 1,000.

Taarifa hiyo ilieleza wazi kuwa wanajeshi wa Kenya wanaingia huko chini ya Umoja wa Kimataifa na wala sio kama taifa huru.

Itakumbukwa kuwa mara tu baada ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kuanza kati ya jeshila Sudan Kusini linalomuunga mkono Rais Salva Kiir na wanajeshi waasi wanaomuunga mkono makamu wa rais wa zamani Daktari Riek Machar, Uganda iliwatuma wanajeshi nchini humo kuunga mkono Rais Salva Kiir.

Katika taarifa hiyo kamati ya usalama nchini Kenya ilisema kuwa hali ya usalama nchini Sudan Kusini imeathiri Kenya.

Wakimbizi wengi wametorokea Kenya, taifa ambalo kwa hivi sasalinakabiliwa na matatizo yake mengi ya kiuslama kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wa Somalia.

Miongoni mwa matatizo ya kiusalama yaliyotajwa katika taarifa hiyo ni mapigano kati ya makabila mbalimbali nchini Kenya na pia hatari ya mashambulizi ya kigaidi katika uwanja wake wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Mkutano huo wa usalama ulioongozwa na Rais Uhuru Kenyatta ulisema usalama katika uwanja huo utaimarishwa kwa kuimarisha mitambo ya kuwapekua wasafiri wa kimataifa.

Nairobi ni kitovu kikubwa cha usafiri kwa watalii na wafanyabiashara katika eneo zima la ukanda wa mashariki na upembe wa Afrika.

Rais Uhuru Kenyatta hii leo atasafiri hadi mji Mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kama hatua mojawapo ya viongozi wa eneo la Afrika Mashariki la kutafuta suluhu la mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini humo.


*OBAMA KUONDOA MAJESHI AFGHANISTAN

Rais Obama ameagiza makao makuu ya ulinzi nchini Marekani Pentagon kuandaa mipango ya kuwaondoa wanajeshi wake wote kutoka Afghanistan ifikapo mwisho wa mwaka huu iwapo hakutakuwepo maafikiano rasmi na Serikali ya Afghanistan.

Rais Obama alimpigia simu Rais Karzai wa Afghansitan juu ya mipango hiyo yake.

Rais Karzai amewaudhi Marekani kwa kukataa kata kata kutia sahihi muafaka ambao ungeruhusu baadhi ya wanajeshi kuendelea kukaa Afghanistan baada ya mud auliokubaliwa awali wa mwisho wamwaka huu wa 2014.

Mpango huo ambao tayari ulikuwa umekubaliwa na baadhi ya viongozi wa kikabila wa Afghanistan - unaandaa wajibu wawanajeshi wa NATO unaoshirikisha kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Afghanistan na kusaidia Serikali ya taifa hilo kukabiliana na wapiganaji wa Kitaliban.

Mkataba huo pia unawapa kinga ya kisheria wanajeshi wa Marekani walioko nchini Afghanistan.

Ikulu ya White House inasema kuwa hakuna uwezekano wa Karzai kutia sahihi mapatano hayo kabla ya kuondoka mamlakani Aprili mwaka huu.

DAKTARI FEKI AKAMATWA MUHIMBILI

Hospitali ya taifa Muhimbili imemkamata daktari feki hospitalini hapo asubuhi ya tarehe ishirini na tano akiwa na baadhi ya kadi za wagonjwa na vipimo huku historia yake ikionesha aliwahi kuajiriwa na serikali kama utabibu katika hispitali ya amana na Mwananyamala kabla ya kuacha kazi mwaka 1997.

Akitoa taarifa za kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo afisa uhusiano mwandamizi wa hospitali hiyo Bw. Aminieli Aligaesha amemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la Kitano Kitani mwenye umri wa miaka 52 ambaye alijifanya daktari upande wa wazazi alikamatwa bada ya kujaribu kuwatapeli watu mbalimbali hospitalini hapo na amekuwa akionekana mara kwa mara na wagonjwa wengi walidhani kuwa yeye ni daktari halali.

Mtuhumiwa huyo licha ya kukiri kufanya kazi ya utabibu kwa miaka mingi amekana kuhusika na tukio lolote la utapeli hospitalini hapo na kubaini amekuwa akifika hospitalini hapo kwa mambo yake binafsi na kukiri kuendelea kutoa huduma mtaani mara baada ya kuacha kazi ya utabibu.

Raisi wa chama cha madaktari Tanzania daktari Primas Saidia amekiri ongezeko la madaktari feki kwenye hospitali mbalimbali nchini na kushindwa kuthibitisha moja kwa moja kama wanashirikiana na madaktari halali kwenye hospitali husika na kuwa tayri wamejipanga kupambana na matukio hayo kwa kuwapa madaktari mihuri na makoti maalimu yenye nembo ili kuwafanya wagonjwa kutambua nani daktari halali ama la.

BOKO HARAM WAUWA WANAFUNZI

Wanamgambo wa Kiislam wa kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria wametuhumiwa kushambulia shule moja na kuwaua wanafunzi kadhaa.

Polisi nchini Nigeria wameliambia Shirika la Habari la Uingereza, Reuters kwamba wotewaliouawa ni wavulana na kwamba baadhi ya miili ya wanafunzi hao imeungua na kubaki majivu.

Taarifa ya jeshi la Nigeria imesema shambulio hilo limefanyika katika jimbo la Yobe.

Wakaazi wa mji wa Buni Yadi katika jimbo hilo, wamesema washambuliaji hao walivamia usiku na kuwachinja baadhi ya wanafunzi.Wamesema baadhi waliuawa kwa kupigwa risasi.

Walimu katika chuo cha serikali ya shirikisho katika mji wa Buni Yadi wameliambia shirika la habari la AP kwamba wanafunzi wapatao 40 waliuawa katika shambulio hilo ambalo lilianza mapema Jumanne asubuhi.

Jeshi limethibitisha kwamba shambulio hilo limetokea katika hosteli za wanafunzi lakini limesema haliwezi kutoa taarifa zaidi kwa sasa.

Kundi la Boko Haram limekuwa likishutumiwa kuendesha vitendovya mauaji kaskazini mwa Nigeria, yakiwemo mauaji ya mapema mwezi huu katika jimbola Yobe.

Boko Haram, lina maana ya"Elimu ya Magharibi ni dhambi" katika lugha ya Kihausa, mara kwa mara limekuwa likishambulia shule katika siku za nyuma.

Watu kadhaa wameuawa katika mashambulio mawili yaliyotokea wiki iliyopita.

Katika tukio moja, wanamgambo hao wa Boko Haram, waliteketeza kijiji kizima na kuwapiga risasi wakaazi wa eneo hilo waliokuwa wakijaribu kutoroka.

MOURINHO ALALAMA KUREKODIWA KWA SIRI

Kocha wa timu ya Chelsea ya England, Jose Mourinho ameshutumu tabia ya kurekodi kwa siri mazungumzo yake kuhusu wachezaji wa timu hiyo.

Mourinho amesema lilikuwa jambo la aibu kuona kwamba mazungumzo binafsi kuhusu wachezaji wa timu yake, yanawekwa hadharani na kampuni moja ya televisheni nchini Ufaransa.

Mourinho amesema alikuwa anatania alipokuwa akilalamika kuwa Chelsea inakosa wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji na alimtania Eto'o kuhusu umri wake.

"The problem with Chelsea is we lack a scorer," the Portuguese said in footage captured by Canal Plus."I have one (Eto'o) but he's 32. Maybe 35, who knows?."

"Yalikuwa mazungumzo ya utani na mtu ambaye hahusiki na masuala ya ulimwengu wa soka," amesema Mourinho.

"Ni fedheha kwa mtu kurekodi mazungumzo binafsi."

MAREKANI KUANGALIA UHUSIANO WAKE NA UGANDA

Marekani haikufurahishwa na hatua ya Uganda kuidhinisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.

Waziri wa mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry amesema tangu Uganda iidhinishe mswada huo miaka minne iliyopita, Marekani ilieleza wazi kwamba sheria hiyo inakiuka jukumu la kuhakikisha kuwepo haki za binaadamu ambalo tume ya haki za binaadamu Uganda inatambua linaambatana na sheria ya Uganda.

Kerry amesema,' Baada ya kuidhinishwa sheria hii, tunaanza ukaguzi wa ndani wa uhusiano wetu na serikali ya Uganda, kuhakikisha kwamba pande zote za uhusiano wetu, ukiwemo miradi ya msaada, zinapinga sera na sheria zinazowaonea watu na tuwe na uhusiano unaodhihirisha maadili yetu'.

Sheria mpya imezusha hisia kaliTamko hilo limetolewa siku moja baada ya rais Yoweri Museveni kukaidi shinikizo la kimataifa na kutia saini sheria hiyo iliyo zusha mzozo, inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja Uganda, hatua iliyozushahisia kali.

Baadhi ya mataifa ya magharibi tayari yanatishia kukatiza msaada wa moja kwa moja kwa serikali ya Uganda.

Marekani inasema kuidhinishwa kwa sheria hiyo kunatishia hatari ya kurudi nyuma katika uwajibikaji wa Uganda kulinda haki za raia wake nakutishia jamii ya wapenzi wa jinsia moja Uganda.

Hivi kwani ni lazima mtu kufanya kile ambacho wew hufanya, nazani ni muda muafaka kwa viongozi wa afrika kuangalia mara mbili mahusiano yao na nchi za magharibi, pongezi kwa Museveni unastaili kuigwa

MKURUGENZI WANYAMAPORI ATIMULIWA

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amemuondoa katika nafasi yake Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa na kumteua Paul Sarakikya kukaimu nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, Nyalandu alisema amechukua hatua hiyo kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili, yanayoendelea nchini.

"Aidha hatua hii ni utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotolewa Desemba 22, mwaka jana lililotaka Mkurugenzi wa Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza," alisema.

Alisema pia amemuondoa Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Jafari Kidegesho na kumteua Dk Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo.

Katika mabadiliko hayo, Nyalandu pia alimteua Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji- Ujangili huku Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji-Ujangili na Takwimu, Nebbo Mwina akiendelea kushika nafasi hiyo.

Alisema Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori, Herman Keiraryo naye anaendelea kushikilia wadhifa huo.

KWA HILI TUMUUNGE MUSEVENI MKONO

TAHARIRI YA MHARIRI WA GAZETI HABARI LEO.

HATIMAYE Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesaini Muswada wa Sheria inayopiga marufuku vitendo vya ushoga na kuanzia sasakwa mtu atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo, atakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka 14 hadi kifungo cha maisha jela.

Hatua hiyo ya Rais Museveni ni ushindi mkubwa dhidi ya wanaohalalisha vitendo hivyo ambavyo vinaruhusu watu wa jinsia moja kuoana kinyume kabisa na mila na utamaduni wa Mwafrika.

Uganda kwa hilo imethibitisha uhuru wake mbele ya macho ya mataifa ya Magharibi ambayo yamekuwa yakitishia kuibana nchi hiyo kama Rais wake atasaini Muswada huo, yakiongozwa na Marekani.

Hatua ya Serikali ya Uganda imekuja siku chache baada ya Rais wa nchi hiyo pia kusaini Muswada mwingine kuwa sheria ya kupiga marufuku mavazi yanayotia ashiki, ambayo ni vimini na vitopu kwa wasichana.

Hiyo ni dhamira ya dhati kuondoa uhuni na vitendo vinavyokiuka utamaduni wa Mwafrika na hivyo kuifanya nchi kutawaliwa na staha na si ukahaba na umalaya ambao unaichafua jamii ya Kiafrika.

Kuachwa kwa hali kama hiyo iendelee katika jamii, ndiyo sababu sasa tunasikia baadhi ya wasichana wa Afrika Mashariki na hasa Tanzania wanakwenda Mashariki ya Mbali na kujiuza na wengine kuingia katika dawa za kulevya.

Tunampongeza Rais Museveni kwa hatua aliyochukua ya kulinda nchi yake isitumbukie kwenye tabia chafu zinapoigwa kutoka mataifa vya Magharibi ambayo yanadhani haki za binadamu ni pamoja na kukiuka uumbaji alioufanya na kuubariki Mungu.

Wanafanya huku wakijua kabisa kilichotokea Sodoma na Gomora, ambako waliofanya vitendo kama hivyo walilaaniwa; hivyo kuendeleakuunga mkono vitendo hivyo vya kifirauni ni kumuasi Mungu.

Ni vema sasa hata kama Marekani na mataifa washirika wake watapiga kelele, mataifa ya Afrika yakatae vitendo hivyo, ingawa takriban mataifa 14 yanahalalisha kisheria vitendo hivyo kutokana naulevi tu wa kuiga vitendo vya Magharibi.

Hakika kama alivyosema Museveni kama Serikali ya Marekani inapingana na hatua hiyo ya Uganda, basi Taifa hilo kubwa lishirikiane na wataalamu wa Uganda kufanya utafiti na kubaini kama kuna watu walizaliwa wakiwa mashoga.

Akasema kama hilo litathibitika, basi sheria hiyo itapitiwa upya na kubatilishwa, lakini kama hilo halipo basi ni vema kukosa msaadawa Marekani wa dola milioni 400 za Marekani inayopokea kila mwaka badala ya nchi na watu wake kuchafuka.

Tumwunge mkono Museveni kwa ujasiri wake.

ATUHUMIWA KUUZA NYAMA YA MTU

Mkazi wa Kijiji cha Kihinga, Kata ya Bugarama wilayani Ngara mkoani Kagera(jina tunalo), anashikiliwa katika kituo kidogo chapolisi cha kata hiyo baada ya kutuhumiwa kuuza kilo moja ya nyama ya binadamu kwa Sh100,000.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kihinga, Hassan Mohamed alisema kuwa jana saa mbili usiku, wananchi walipeleka fedha nyumbani kwake kununua nyama hiyo na alipowaona alikimbia na wananchi hao kwa hasira walimkimbiza ili kumuua na hapo hapo kuunguza nyumba yake.

"Mgambo ndio walimnusuru asiuawe na wananchi wenye hasira kali na alikimbizwa kituo kidogo cha polisi Kata ya Bugarama ili kuokoa maisha yake ".

Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa mgambo wa kijiji hicho, Emanuel Kaloli alisema wananchi waliandamana baada ya kusikia taarifa za kuwapo mtu anayeuza nyama ya binadamu na kutaka kuhakikisha ukweli huo.

Alisema baada ya wananchi kufika, walianza kumshambulia na kutaka kumuua, lakini wanamgambo wa kitongoji walifika kisha kumuokoa mtuhumiwa na hatimaye kumfikisha kituo cha polisi kwa ajiliya usalama wake.

"Kijana aliyefahamika kwa jina la Man Balyamwabo mkazi wa Shina laKalenge katika kitongoji hicho, ndiye aliyeambiwa kuwa angeuziwa nyama hiyo ya binadamu na kuleta taarifa katika uongozi wa kijiji ili uweze kuchukua hatua zaidia" Alisema Kaloli.

Alisema nyumba aliyounguziwa pamoja na mali iliyokuwamo ndani hasa maharage, mavazi na vitu vinginevyo inakadiriwa kuwa na thamani ya Sh2.6milioni. Pamoja na kuwepo kwa tukio hilo, baadhi ya wananchi walisema mtuhumiwa inasemekana ni raia wa nchi jirani ya Burundi na alianza kuishi katika kitongoji hicho tangu mwaka 1981 kama kibarua wa kilimo kwenye mashamba.

Taarifa zinasema kuwa katika kuishi kwake na ndugu yake aliyefahamika kwa jina la Kahungu walikuwa wakituhumiana kwa uchawi na ilifikia mahala wakatofautiana na kaka yake ambaye alirejea kwao.

Polisi wilayani Ngara imethibitisha kumpokea mtuhumiwa huyo na kwamba linafanya mahojiano ya kina kwa kushirikiana na viongozi wa kijiji ili kubaini ukweli wa tukio hilo.


Chanzo: Mwananchi

SABATO MATENGENEZO LAPIGWA MARUFUKU

Serikali wilayani Kakonko mkoani Kigoma, imelipiga marufuku kanisa moja la dini ya Kikristo linaloitwa Sabato Matengenezo, ambalo limeanzishwa na watu sita ambao kwa sasa wanashikiliwa polisi.

Waumini hao wanadaiwa kuwanyima haki za msingi watoto wao, ikiwamo kuwakataza kwenda shule, kupata matibabu katika hospitali na zahanati kwa kile wanachodai kuwa imani ya dini yao hairuhusu.

Habari kutoka kijijini hapo, zinasema kutokana na tukio hilo, watoto wawili wamefariki dunia baada ya wazazi wao kuacha kuwapeleka hospitali kwa kile walichodai kuwa ni kimyume na imani ya dini yao.Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Kigoma, Dismas Kisufi alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo pamoja na vifo hivyo alisema hajapata taarifa ya tukio hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Peter Toyima naye alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alikiri kuwa na taarifa kuhusu kanisa hilo na kusema kanisa hilo jipya limekuja na sera ya kuwazuia watoto wao kwenda shule, hospitali kupata matibabu nakulipa nauli wanapokuwa katika vyombo vya usafiri, hatua inayopingana na azma ya Serikali kutaka watoto wapate haki zao za msingi.

"Serikali haitakuwa tayari kuona baadhi ya watu wanazuia haki za msingi za watoto wao kwa kuwakataza kwenda shule, kupata matibabu katika hospitali au zahanati kwa kisingizio cha imani zakidini, jambo hili haliwezi kukubalika," alisema Toyima.

Waumini hao wanaoshikiliwa na polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi Kakonko wametajwa kuwa ni; Ndayizeye Gervas, Majaliwa Gervas, Paschal Silvanus, Inocent Ernest, Medadi Laurent na Julietha Medadi ambao ni wakazi wa Kijiji cha Nyabibuye, Kata ya Rumashi wilayani Kakonko na wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Mkuu huyo wa wilaya, aliwataka wananchi kuachana na dini zisizoeleweka na zinazoleta mifarakano katika jamii, na wakati wengine wakisisitiza kuwapatia elimu watoto wao, kanisa hilo linakataza kusomesha watoto kwa madai kwamba kuwapeleka shule na hospitali ni dhambi kwa Mungu.

Alisema jitihada za Serikali wilayani Kakonko zimesaidia kuwachukua watoto wawili waliofaulu kwenda Sekondari za Kanyonza na Nyamtukuza na kuwawezesha kuanza masomo ya kidato cha kwanza.

Kanisa hilo jipya linadaiwa kujimega kutoka katika Kanisa la Sabato ambalo ni moja wapo ya makanisa yenye idadi ndogo ya waumini mkoani Kigoma ikilinganishwa na Kanisa Katoliki, Anglikana na Assemblies of God.

MILIPUKO YARINDIMA ZANZIBAR

Watu wanne wamejeruhiwa baada ya milipuko minne inayoaminika kuwa ni mabomu kutokea katika maeneo matatu tofauti Zanzibar.

Katika moja ya matukio hayo, watu wanne walijeruhiwa, mmoja akikatika mguu, katika eneo la Unguja Ukuu, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Majeruhi wawili wamelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja.

Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Mkoa wa Kusini Unguja, Hamad Said Masoud alisema mlipuko wa kwanza ulitokea juzi katika eneo la Fuaoni Maili Nne wakati watu wasiojulikana waliporusha kitu kinachoaminika kuwa ni bomu wakati waumini wa Kanisa la Evangelist wakiendelea na ibada ya Jumapili.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame alisema tukio la juzi, kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kilirushwa wakati waumini wa kanisa hilo wakiendelea na ibada na kutoa mlipuko na kishindo kikubwa. Alisema wakati wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo, milipuko mingine mitatu ilitokea jana.

Katika mlipuko wa kwanza kwa jana uliotokea saa 6.30 mchana katika kituo kimoja cha fundi vyuma aliyetambulika kwa jina la Juma Abdallah huko Unguja Ukuu ndiko kulikokuwa na watu waliojeruhiwa.

Waliojeruhiwa katika tukio hilo ni Pandu Haji Pandu aliyekatika mguu na Shaaban Khamis Ibrahim ambaye aliumia sehemu za kiuno.

Hamad alisema mtu mmoja aliokota chuma kizito na kukipeleka kwa fundi akitaka atengenezewe nanga kwa ajili ya uvuvi.

Alisema mhunzi huyo alipokea kazi hiyo na alipokuwa akijiandaa kwa matengenezo ndipo mlipuko huo ulipotokea.

Mlipuko huo ulitokea sambamba na mwingine katika Mgahawa wa Mercury’s uliopo Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi na kusababisha huduma za chakula kusitishwa kwa muda.

Tukio la mwisho lilikuwa saa 7:15 mchana katika Kanisa la Anglikana, Mkunazini. Katibu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Zanzibar, Nuhu Saranyaalisema: “Nilisikia kishindo cha mlipuko, wakati nikitafakari ni kitu gani hicho, nikasikia mlipuko wa pili nje ya kanisa letu,” alisema.

Mmoja wa majeruhi, Mohamed Ibrahim alisema hakujua kilichotokea huku akilalamika kuwa masikio yake hayasikii vizuri kutokana na kishindo hicho.

UKRAIN YATOA HATI YA KUKAMATWA RAIS YANUKOVYCH

Ukraine imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais aliyeondolewa madarakani, Victor Yanukovych, Waziri wa mambo ya ndani wa mpito ametangaza hatua hiyo.

Arsen Avakov amesema katika ukurasa wa Facebook amesema kesi dhidi yake imefunguliwa dhidi ya Yanukovych na maafisa wengine kuhusu mauaji ya makubwa ya watu.

Wabunge walipiga kura kumuondoa Yanukovych siku ya jumamosi baada ya maandamano ya miezi kadhaa yaliyojitokeza baada ya kupinga kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Machafuko yaliyotokana na maandamano hayo yalisababisha watu kadhaa kupoteza maisha juma lililopita.

Avakov amesema Yanukovych alionekana mjini Balaklava siku ya jumapili, lakini mpaka sasa hajulikani mahali alipo.

BARAZA LA MAWAZIRI LAJIUZULU MISRI

Waziri mkuu wa Misri, Hazem el-Beblawi na baraza lake la mawaziri wamejiuzulu.

Katika taarifa ya moja kwa moja kupitia televisheni, Bwana El-Beblawi alisema kuwa Misri imeshuhudia ongezeko la migomo katika sekta ya umma katika wiki chache zilizopita.

Alisema kuwa hakuna hata serikali moja duniani ambayo inaweza kutimiza mahitaji ya watu wake katika kipindi kifupi sana.

Serikali hiyo ya mpito ilianza kazi mwezi Julai mwaka jana baada ya jeshi kumpindua aliyekuwa Rais Mohammed Mosri.

Taarifa zinasema kuwa uamuzi wabaraza la mawaziri kujiuulu ulitokea baada ya mkutano kati ya mkuu wa majeshi na waziri waulinzi Field Marshal Abdul Fattah al-Sisi.

Inaarifiwa kuwa al-Sisi anatarajiwa kujiuzulu kutoka katika wadhifa wake ili kugombea Urais.

MUSEVENI ASAINI MUSWADA WA KUPINGA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini mswada wenye utata unaotoa adhabu kali kwa watakaopatikana wakishiriki mapenzi ya jinsia moja.

Rais Museveni alitia saini mswada huo nyumbani kwake katika hafla iliyoshuhudiwa na maafisa wakuuwa serikali pamoja na wandishi wa habari.

Mswada huo ambao sasa utakuwasheria, unatoa adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wale watakaopatikana na hatia kwa mara ya kwanza, Adhabu ya maisha jela itatolea kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja zaidi ya mara moja kati ya watu wawili waliokubaliana kufanya hivyo.

Adhabu hiyo pia itatolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha watoto katika vitendo hivyo, walemavu au kumuambikiza mtu virusi vya Ukimwi.

Mswada huo umepigiwa debe sana nchini Uganda, lakini mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameulaani.

MUGABE AJISIKIA KAMA MTOTO WA MIAKA 9

Maelfu ya watu wa Zimbabwe wamehudhuria sherehe rasmi za siku ya kuzaliwa Rais Robert Mugabe.

Bwana Mugabe ambaye ameongoza nchi tangu mwaka wa 1980, alipeperusha mabofu 90 katika uwanja wa michezo wa Marondera, mashariki ya Harare.

Rais Mugabe, ambaye amerudi punde kutoka Singapore kwa matibabu, alisema ajisikia mzimana kijana kama mtoto wa miaka 9 Aliuambia umati kuwa ushindi aliopata kwenye uchaguzi wa mwaka jana ulishangaza nchi za magharibi zinazomlaumu.

Sherehe hiyo inakisiwa kugharimu dola milioni-moja na hivyo kuzusha malalamiko katika nchi ambayo ina matatizo ya kiuchumi.

TUTU AMSIHI MUSEVENI

Askofu mstaafu wa Cape Town, Desmond Tutu, amemsihi Rais Museveni wa Uganda asitie saini mswada ulioleta utatanishi kuhusu wapenzi wa jinsia moja.

Askofu Tutu, aliyewahi kupata tuzoya amani ya Nobel, alisema amevunjika moyo kuwa Rais Yoweri Museveni anaonesha kubadilisha msimamo wake, kwa vile awali alisema kuwa hata ruhusu mswada huo kuwa sheria.

Desmond Tutu alisema haistahikikuwa na ubaguzi kama huo, na alitoa mifano ya mfumo wa zamani wa ubaguzi wa rangi uliokuwako Afrika Kusini na ubaguzi wa Wa-Nazi wa Ujerumani.

Alisema hiyo ni mifano mibaya kabisa.

Awali mswada wa Uganda ulipendekeza kifo kwa vitendo vya kulawiti na baadae kubadilishwa kuwa adhabu ya kifungo.

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KUMUINGIZIA MTOTO UUME MDOMONI

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu Athuman Mussa mwenyeumri wa miaka 54 Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa Mjini hapa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na kosa la kumwingizia uume mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne.

Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntegwa baada ya mahakama kulidhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapona upande wa mashitaka na upande wa mashitaka.

Mshitakiwa alidaiwa kutenda kosa hilo la kumwingizia uume mdomoni mtoto huyo wa kike hapo juni 26 mwaka jana majira ya saa kumi na mbili jioni nyumbani kwake.

Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka mkaguzi wa polisi Ally Mbwijo alidai mahakamani hapo kuwa siku hiyo ya tukio mshitakiwa alimkuta mtoto huyo akiwa anacheza na watoto wenzake karibu na nyumba yake na ndipo alipomwita mtoto huyo na kuingia nae ndani kwa lengo la kumpa jojo.

Alidai kuwa baada ya mtoto huyo kuingia ndani ya nyumba Athumani alimvutia kwenye kochi sebuleni na kisha alimwingizia uume wake kwenye mdomo wa mtoto huyo hadi hapo alipomaliza haja yake.

Mwendesha mashitaka Ally Mbwijo aliieleza mahakama kuwa baada ya mshitakiwa kumaliza haja yake alimwachia mtoto huyo na ndipo alipotoka mbio na kwenda nyumbani kwao huku akiwa analia.

Aliiambia mahakama baada ya mtoto huyo kufika nyumbani kwao mama wa mtoto huyo alimuuliza analia nini badala ya mtoto kumjibu mama yake mtoto huyo alitema mbegu za kiume ambazo zilikuwa mdomoni mwake na kisha alimwelezea mama yake unyama aliofanyiwa na mshitakiwa.

Alieleza baada ya mama kuelezwa unyama huo aliofanyiwa mtoto wake alianza nae kulia kwa nguvu hari ambayo ilisababisha majirani kufika kwenye eneo hilo na baada ya kuelezwa unyama aliofanyiwa mtoto huyo majirani walikwenda nyumbani kwa mshitakiwa na waliweza kumkamata na kumfikisha kwenye kituo cha polisi.

Hahimu mkazi mfawidhi Chiganga Ntengwa alieleza mahakamani hapo kuwa mahakama baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi wa pande zote mbili za mashitakana utetezi mahakama imemwona mshitakiwa amepatikana na hatia hivyo kabla ya mahakama haijatowa adhabu kwa mshitakiwa inatowa nafasi ya mshitakiwa aiombe mahakama kama anasababu za msingi za kuomba apunguziwe adhabu.

Mshitakiwa aliiomba mahakama imwachie huru kwani hakufanya kitendo hicho na zile mbegu za kiume alizotema mtoto huyo zilikuwa ni karanga sio mbegu za kuume.

Mwendesha mashitaka Ally Mbwijo alipinga vikari utetezi huo na kuiomba mahakama itowe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwefundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Hakimu mkazi mfawidhi Chiganga Ntengwa baada ya kuzisililiza pande hizo mbili aliieleza mahakama kuwa mshitakiwa amepatikana na hatia ya kifungu cha sheria namba 154 kifungu kidogo cha kwanza a na cha pili suraya 16 cha marekebisho ya mwaka 2009.

Hakimu Chiganga Ntengwa aliiambia mahakama kuwa kutokana na mshitakiwa Athumani Mussa kupatikana na hatia mahakama imemuhukumu kwenda jela kifungo cha maisha.

PICHA YA SIKU

AUWA MTOTO KWA KUMCHINJA NAE AUWAWA KWA MAWE

Watu wawili wamefariki dunia katika tukio lililokuwa na mwendelezo, mmoja akimchinja mtoto na yeye kuuawa kwa kupigwa mawe na wananchi wenye hasira.

Polisi walithibitisha mauaji hayo ya kutisha na kueleza kuwa yalitokea juzi saa 12 jioni maeneo ya Mbagala Charambe Foma, jijini Dares Salaam, ambapo katika tukio la kwanza Mohamed Said (36), alimkamata Jamal Salum (12) aliyedaiwa kuwa mwanafunzi wake na kumchinja kama kuku.

Habari zinaeleza kuwa Said akiwa nyumbani kwake alimkamata Jamal ambaye alikuwa mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Nzasa na kumlaza chini, kisha akamchinja.

Hali hiyo inaelezwa kuibua hasira za wananchi wenye hasira na kuvamia nyumbani kwa Said na kumpiga mawe hadi naye kupoteza uhai wake.

Mkuu wa Upelelezi, Wilaya ya Kipolisi Mbagala, ASP Walelo, alieleza kuwa siku ya tukio (Juzi), Jamal alikuwa na mwenzake Ramadhani Salum (11) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne, Shule ya Msingi Kichechem aliyemsindikiza Jamal katika nyumba ya Said ambapo mjomba wake amepanga na walipokuwa wakitoka wakakutana na Said, ambaye alimshika Jamal, akamlaza chini na kumchinja kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

"Wakati akimchinja, Ramadhani akakimbia kutoa taarifa kwa watu waliokuwa karibu, walipofika walikuta tayari Salum ameshachinjwa," alisema Walelo nakuongeza:

"Baada ya hapo, wananchi wenye hasira walivunja mlango wa nyumba ya Said na kumkuta akiwa ameshika kisu alichofanyia mauaji na kumpiga hadi kupoteza maisha."

Alifafanua kuwa Said, anafanya kazi katika Shule ya Al-nur-al iliyopo Charambe Foma na kwamba alikuwa ni mwalimu wa madrasa.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Charambe, John Bazil, alisema kuwa anadhani Said alikuwa na matatizo ya akili.

"Nimehamia hapa juzi juzi, sifahamu sana, lakini taarifa nilizokuwa nazo ni kwamba, Said ana matatizo ya akili ambayo humjia na kuondoka, kitu ambacho watu waliokuwa wakiishi naye walikuwa wanakiona cha kawaida kwa kuwa walimkuta akiwa hivyo," alisema Bazil.


Chanzo: Mwananchi

RAIS WA UKRAIN AKIMBIA MJI MKUU

Rais wa Ukrain Victor Yanukovych ameondoka mjini kiev na anadaiwa kuwa mashariki mwa taifa hilo.

Bwana Yanukovych amekataa kusalimu amri licha ya bunge hapo awali kupiga kura ya kumuondoa ofisini.

Akizungumza katika runinga moja katika mji wa Kharkiv ,bwana Yanukovych ameelezea vitendo vinavyofanyika dhidi ya serikali yake kama vya mapinduzi.

Magavana wa majimbo ya mashariki mwa Ukrain wamefanya mkutano katika mji wa Kharkiv, uliohudhuriwa na maafisa wa Urusi ili kuzungumzia kuhusu udhibiti haramu wa mji mkuu wa kiev.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa hiyo ni ishara tosha ya kutokea kwa mgawanyiko nchini humo mbali na kuongezeka.

Wakati huohuo aliyekuwa waziri mkuu wa Ukrain Yulia Tymoshenko ambaye amewachiliwa huru na bunge baada ya kuhudmia kifungo cha miaka miwili jela amepokelewa na hisia tofauti alipokuwa akiwahutubia maelfu ya waandamanaji katika medani ya Uhuru katikati ya mji mkuu wa Kiev.

Akiwa ameketi katika kiti cha magurudumo, amewaambia waandamanaji kwamba wanasiasa nchini humo hawana thamani ya 'tone la damu yao' iliomwagika wakati wa maandamano hayo.

Lakini mwandishi wa habari wa BBC amesema kuwa watu wengi katika kongamano hilo waliondoka wakati bi Tymoshenko alipoanza kuhutubia umati huo, wakisema kuwa hawakilishi upinzani.

Wengi waliohojiwa wameiambia BBC kwamba hawamtaka kuwa rais mpya.

PADRI MMOJA AFIA GUEST HOUSE, HUKU MWINGINE AKIFIA KWA HAWARA

Kiongozi wa Kanisa amekutwa akiwa amefariki dunia kwenye nyumba ya kulala wageni jijini Nairobi na kufanya vifo vya kutatanisha vya viongozi wa kidini kufikia wawili wiki hii.

Katika tukio la juzi, Padri wa Kanisa Katoliki, Otto Myer (70) ambaye ni raia wa Italia, alikutwa akiwa amefariki saa tano usiku chumbani mwake kwenye nyumba ya kulala wageni ya the Consolata huko Westlands, Nairobi.

Mwili wa padri huyo ulipatikana kwenye chumba hicho kando yake kukiwa na dawa, na baadhi ya jirani zake walisema alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mfupi.

Juzi, Mkuu wa Polisi Jimbo la Nairobi, Benson Kibue alisema maofisa wake wanachukulia kifo chake kuwa cha ghafla, hasa kutokana na kwamba amekuwa akiugua kwa siku kadhaa.

"Hatutaharakisha kusema kilichomuua. Kwa sasa tunajua hiki ni kifo cha ghafla, ikizingatiwa kuwaamekuwa akiugua. Upasuaji wa maiti ndio utakaoeleza zaidi kilichomfanya afariki," akasema Kibue.

Lakini maofisa wa polisi waliofika mahali hapo pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa gesti hiyo ambao hawakutaka kutajwa, walisema kwamba chumbani alimokufa padri huyo mlikuwa na dawa pamoja na pombe.

Wakizungumza na waandishi wetu, walisema kwamba padri huyo alikuwa ameenda katika hospitali ya karibu kutafuta tiba siku ya Jumanne.

*MWINGINE AFIA KWA HAWARA

Kifo cha Padri Myer kilitokea saa chache baada ya kifo cha mchungaji Geoffrey Maingi wa Kanisa la Redeemed Gospel nyumbani kwa mmoja wa washirika wake katika Mtaa wa Buruburu, Nairobi.

Sawa na Padri Myer, Kasisi Maingi pia alikuwa na umri wa miaka 70 napia alifariki dunia kwenye vyumba katika hali ya kutatanisha.

Kwenye kisa cha Buruburu, Kasisi Maingi alisemekana kuegesha gari lake nje ya duka la jumla la Tuskys na kwenda nyumbani kwa mwanamke mshirika wa Kanisa lake, ambaye alikiri kuwa mbali na kuwa kiongozi wake wa kiroho, yeye pia alikuwa rafiki yake.

Mwanamke huyo alisema kuwa mchungaji huyo alikuwa nyumbani kwake kwa maombi. Tukio hilo lilishuhudiwa katika mtaa wa Buruburu mjini Nairobi Kenya Mwili wa Maingi, ulikutwa ndani ya chumba cha mwanamke huyo, baada ya kufariki kutokana na sababu ambazo hazijulikani

MKUU WA CHUO CHA CBE ATOA UFAFANUZI JUU YA TAARIFA ZILIZOANDIKWA KATIKA VYOMBO VYA HABARI

Mkuu wa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dar es salaam Prof. Emanuel Mjema amesema kuwa habari zilizoandikwa na kuchapishwa na gazeti moja la kila siku na baadhi ya mitandao ya kijamii hapa nchini zililenga kukidhalilisha chuo na kuipotosha jamii kufuatia chuo hicho kuendelea kufanya vizuri katika kulinda maadili na viwango vya taaluma hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mkuu wa chuo hicho amesema kuwa habari zilizochapishwa kuhusu kuwekwa kwa mfumo wa kamera za kisasa madarasani na taarifa ya kufukuzwa kwa mwalimu mmoja wa chuo hicho akihusishwa na vitendo vya ngono na wanafunzi zimepotoshwa na vyombo hivyokwa kukosa weledi wa kushindwa kupata uhalisia na usahihi wa habari husika kutokamamlaka za chuo hicho.

Prof. Mjema amesema kuwa Chuo cha Elimu ya Biashara ni Chuo cha Serikali ambacho kimekua kikitoa Elimu ya Biashara kwa miaka 49 na kuongeza kuwa chuo hicho kinaajiri wakufunzi wake kupitiautaratibu wa serikali wa kutangaza nafasi za kazi kupitia Tume ya Ajira iliyopo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma.

Ameongeza kuwa chuo hicho kina wakufunzi na wataalam wanaoheshimu maadili ya utumishi wa umma na taaluma zao na kuongeza kuwa chuo hicho kina wakufunzi wenye sifa ambao hawahitaji kufuatiliwa na mtu katika kazi zao.


"Nachopenda kusema ni kwamba chuo chetu sasa kinao wataalam na wakufunzi wenye sifa na walioajiriwa kwa kuzingatia kanuni na vigezo vilivyowekwa,taarifa zilizotolewa hazina ukweli wowote na zimelenga kukidhalilisha chuo na kuipotosha jamii"

Amesema kuwa kamera za kisasa ziilizofungwa katika vyumba vya madarasa vya chuo hicho zimewekwa kwa lengo la kudhibiti udanganyifu katika mitihani na kuimarisha ulinzi nausalama wa mali za chuo na kuongeza kuwa juhudi zinafanyika katika mwaka ujao wa fedha kuongeza vifaa hivyo hasa katika maeneo ya kuingilia na yale yanayotumiwa na watu wengi chuoni hapo.

"Napenda kuwafahamisha kuwa kamera za CCTV tulizonazo zimefungwa katika vyumba vya madarasa kulingana na teknolojia iliyopo sasa na ni jambo la kawaida na zimefungwa kwa lengo la kuimarisha ulinzi kwa lengo la kutoa wataalam waliobobea na si kama ilivyoandikwa kwa kupotoshwa na gazeti hilo na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa zinalenga kudhibiti vitendo vya ngono darasani" amesema Prof. Mjema.

Aidha kuhusu hali ya ulinzi na usalama chuoni hapo amesema kuwa chuo hicho kimekuwa na utaratibu wa kuweka walinzi getini kwa miaka 49 na kuongeza kuwa hakuna walinzi wapya walioajiriwa kwa ajili ya kukagua mavazi ya wanafunzi hao huku akibainisha kuwa utaratibu uliopo sasa wa kukagua vitambulisho kwa wanafunzi wanaoingia chuoni hapo na wageni wengine wanaoingiia ni wa kawaida kwa ajili ya usalama wa chuo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa chuo hicho amesema kuwa chuo hicho kitaanza kutoa masomo ya juu kwa ngazi ya shahada za uzamili kuanzia mwaka ujao wa kitaaluma na kutoa wito kwa wananchi kuichangamkia fursa hiyo.


Pia amesema kuwa chuo hicho kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha "Eastern Finland" kitaanza kutoa shahada za umahiri na kufafanua kuwa wataalam wa kuifanya kazi hiyo hapa nchini wapo.

"Tutaanza kutoa mafunzo kwa ngazi ya shahada za uzamili katika mwaka ujao wa kitaaluma, wahadhiri wanaofundisha sasa hapa chuoni wana elimu za juu hivyo kuwezesha mchakato huo kuanza."

Katika kuboresha kiwango cha elimu chuoni hapo Prof. Mjema ameeleza kuwa Chuo chake tayari kimeingia mkataba na chuo Kikuu cha masuala ya Teknolojia cha Shenyang , kilichopo nchini china ambapo wanafunzi wa vyuo vya CBE nchini wataweza kwenda China kumalizia masomo yao kwa mfumo wa kubadilishana."

Ni hatua nzuri katika maboresho ya elimu katika chuo chetu kwa kushirikiana na vyuo vya nje hasa Finland na China na sasa baadhi ya wanafunzi wameshaanza kunufaika" ameeleza Prof. Mjema.

MATOKEO KIDATO CHA NNE YAMETOKA

Matokeo ya kidato cha 4 mwaka 2013 yametangazwa, ufaulu umeongezeka kwa asilimia kati ya 0.61 na 16.72 ukilinganisha na mwaka 2012.

Jumla ya wanafunzi laki 151,187 wamepata '0' (division ziro) . Wasichana ni 72,237 na wavulana ni 78,950.

Jumla ya watahiniwa 427,679 waliandikishwa kufanya mtihani ila waliofanikiwa kufanya mtihani ni watahiniwa 404,083.

Jumla ya watahiniwa laki 235,227 sawa na asilimia 58.25 ya waliofanya mtihani wamefaulu.

Wasichana waliofaulu ni laki 106,792 na wavulana waliofaulu ni laki 128,435.

Wanafunzi 74,324 sawa na asilimia 21.09 wamefaulu katika madaraja ya I -III.

Wavulana waliopata daraja la kwanza (division one) ni 5,030 na wasichana ni 2,549.

Waliopata daraja la pili (Division 2) Wavulana ni 14,167 na wasichana ni 7,561.

Wavulana waliopata daraja la tatu (Division 3) ni 27,904 na wasichana ni 17,113.

Jumla ya wanafunzi waliopata daraja la 4 (division 4) ni laki 126,828, wasichana wakiwa 62,841 na wavulana 63,987.

Shule 10 zilizoongoza ni St.Francis Girls, Marian Boys, Feza Girls, Precious Blood, Canossa, Marian Girls, Abbey, Anwarite Girls, Rosmini, na DonBosco Seminary.

Zilizofanya vibaya ni: Kisima, Kitongoni, Tongani, Njechele, Lumemo, Mvuti, Tambani, Nasibugani, Ungulu na Kitonga, Singisa, Hurui, Barabarani, Nandanga, Vihokoli, Chongoleani, Likawage, Gwandi, Rungwa, Uchindile.

Watahiniwa kumi bora ni: 1. Robina S. Nicholaus (Marian Girls), 2. Magreth Kakoko (St.Francis Girls) 3. Joyceline Leornard Marealle (Canossa), 4. Sarafina W. Mariki (Marian Girls) 5. Abby T. Seembuche (Marian Girls), 6. Sunday Mrutu (Anne Marie), 7. Nelson Anthony (Kaizerege) 8.Emmanuel Gregory (Kaizerege), 9. Janeth Urassa (Marian Girls), 10. Angel Ngulumbi (St Francis)

Watahiniwa 31,518 wa shule ambao hawajalipa ada ya mtihani, matokeo yao yatatolewa watakapolipa ada wanayodaiwa.

Wanafunzi 10 waliobainika kuandika matusi katika mitihani yao, wamefutiwa matokeo.

Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 272 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani yao.

Bofya hapa kuangalia 41.188.155.122/CSEE2013/olevel.htm

GAVANA WA BENKI KUU ATIMULIWA KAZI NA RAIS

Gavana wa benki kuu ya Nigeria, Lamido Sanusi amesimamishwa kazi kwa muda akisubiri matokeo ya uchunguzi wa kile kinachosemekana kuwa makosa makubwa katika rekodi za benki.

Bwana Sanusi alizua hisia nchini Nigeria aliposema kuwa Dola Bilioni 20 za mapato yaliyotokanana mafuta hazijulikani ziliko.

Shirika la mafuta la serikali, limekanusha madai kuwa halijawasilisha rekodi zake kuhusu lilivyotumia pesa hizo likisema kuwa madai hayo hayana msingi.

Bwana Sanusi anaheshimika sana nchini Nigeria hasa baada ya kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya benki tangu kuteuliwa kama gavana mwaka 2009 Alitajwa kuwa gavana bora zaidi wa beni kuu mwaka 2010 na jarida la Banker magazine.

Nigeria ni moja ya nchi zenye kuzalisha mafuta kwa wingi duniani lakini sekta hiyo imekuwa ikikumbwa na madai ya wizi na ufisadi.

Mnamo mwezi Februari, bwana Sanusi aliambia kamati ya Baraza la Senate kuwa kati ya Dola Bilioni 67 za kimarekani thamani ya kiwango cha mafuta kilichouzwa kati ya mwezi Januarimwaka 2012 na Julai 2013, dola bilioni 20 bado hazijajulikana ziliko.

Shirika la mafuta la serikali lilisema kuwa madai hayo sio ya kweli na kwamba hayana msingi.

Bwana Sanusi anahudhuria mkutano wa kikanda wa wakuu wa benki kuu nchini Niger.

Nafasi yake itachukuliwa na naibu wake Sarah Alade, aliyeandamana naye kwenye mkutano huo.

Rais Jonathan alimuomba Sanusi kujiuzulu mwezi Disemba lakini akakataa.

Rais hana mamlaka ya kumfuta kazi gavana wa benki kuu. Ni bunge pekee linaloweza kufanya hivyo.

Muda wake unapaswa kukamilika mwezi Juni lakini duru zinasema kuwa uamuzi wa kumwachisha kazi kwa muda ni muhimu sana.

Taarifa ya Rais ilisema kuwa Sanusi anaachishwa kazi kwa sababu ya kuvunja sheria za benki kuu.

20 WAJERUHIWA KATIKA GHASIA BUKAVU

Watu ishirini wamejeruhiwa baada ya polisi kufyatua risasi katika mji wa Bukavu, mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Ghasia zilitokea pale polisi ilipojaribu kumzuia kiongozi wa upinzani asihutubie wafuasi wake.

Vital Kamerhe ambaye alikuwa hapo zamani spika wa Bunge na pia msaidizi wa karibu wa Rais Joseph kabila, aliyejiunga na upinzani miezi michache kabla yauchaguzi wa mwaka 2011, anafanya ziara ya amani mashariki mwa Congo, eneo lililoathirika na vita vya karibu miaka 20.

Kamerhe alisema kuwa polisi waliwapiga risasi wafuasi wake wakati wa mkutano wao mjini Bukavu.

Gavana wa jimbo alikanusha madai kuwa watu walipigwa risasihuku akisema kuwa wafuasi ndio walikuwa wakali kwa polisi.

Ifikapo mwaka 2016, wakati uchaguzi mkuu utakapofanyika, Kabila atakuwa amekamilisha mihula miwili mamlakani na anazuiwa na katiba kugombea tena urais Makundi kadhaa ya upinzani yanamtuhumu Kabila kwa kutaka kubadilisha katiba na kutaka kugombea muhula wa tatu.

Kamerhe aliyekuwa mmoja wa watu wakuu katika kampeini ya uchaguzi wa Urais wa Kabila mwaka 2006 alisema kuwa Kabila anaogopa upinzani kujitokeza dhidi yake kwa sababu hana ushawishi mkubwa sana.

Alivunja uhusiano wake na Rais Kabila mwaka 2010 baada ya Kabila kuruhusu majeshi ya Rwanda kuingia nchini humo kuwasaka wapiganaji wa kihutu Mashariki mwa Congo.

Alibuni chama chake cha kisiasa na kushindana na Kabila mwaka 2011 huku akishikilia nafasi ya tatu.

Kamerhe alisema kuwa maafisa wakuu walimruhusu kufanya mkutano wake katika uwanja wa michezo wa Bukavu lakini kumbe uwanja huo ulikuwa umepangiwa kutumiwa kwa mechi.

HAPPY BIRTHDAY MUGABE

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amefikisha miaka 90 leo na kuwa rais mkongwe zaidi barani Afrika.

Amekuwa Rais wa Zimbabwe tangu nchi hiyo ijipatie uhuru mwaka 1980.

Hata hivyo sherehe za siku ya kuzaliwa kwake zitafanyika Jumapili huku kukiwa na tetesi kuhusu hali yake mbaya ya kiafya pamoja na mvutano kuhusu uongozi wa chama tawala.

Sherehe hizo zinakisiwa kugharimu dola milioni moja.

Mugabe alichukua mamlaka mwaka 1980 wakati Zimbabwe ilipojinyakulia uhuru kutoka kwa Uingereza na amekuwa akisemekana kuwa mgonjwa sana.

Amekuwa akienda nchini Singapore, kwa ukaguzi wa kimatatibabu mara kadhaa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Taarifa zilifichuliwa mwaka 2008 kuwa Mugabe anaugua Saratani ya tezi kibofu, madai ambayo serikali ilikanusha vikali.

Taarifa hizi ziwe za kweli au za uongo, cha mno ni kwamba kwa sasa Zanu-PF kinajiandaa kwa maisha bila ya Rais Mugabe.

Hata hivyo mnamo siku ya Alhamisi Mugabe alisema hakunaumuhimu wowote wa kuanza kuzungumzia swala la Urithi wakati yeye yungalipo.

"kwa nini swala hili lijadiliwe wakati muda bado? Je muda umewadia wa kulizungumzia?'' alinukuliwa akihoji na gazeti la The Herald nchini Zimbabwe

"uongozi bado upo . Yaani bado nipo,'' alisema Mugabe

GHANA YATOA WASIFU KWA KOMLA DUMOR

Hafla mabli mbali za siku tatu kumuenzi aliyekuwa mtangazaji wa BBC Komla Dumor-aliyefariki ghafla mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 41,zitaanza leo nchini Ghana kabla ya maizko yake.

Baada ya kifo chake,rambirambi zilitolewa kutoka kote dunia na rais wa Ghana, John Mahama,alisema kuwa Ghana imempoteza balozi.

Kama ilivyo desturi nchini Ghana,hafla ya mazishi yake itachukua muda wa siku tatu ikianza na misa ya kuomboleza katika kanisa la Accra Roman Catholic cathedral ambapo wananchi wataruhusiwa kutazama mwili wake. Umati mkubwa unatarajiwa kuhudhuria.

Jumamosi, wasifu wake utasomwa ukisifia yale aliyofanya nchini mwake.

Ibada hiyo itafanyika katika uwanja wa Ikulu ya Ghana Ikifuatwa na ibada ya mazishi itakayohusisha familia yake pekee.

Komla Dumor alikuwa mtangazaji maarufu katika stesheni moja ya redio nchi Ghana kabla ya kujiunga na BBC miaka saba iliyopita na aliweza kufahamika kama mtangazaji wa redio na televisheni mwenye haiba kubwa duniani kote.

Katika kazi yake alipenda kuonyesha watazamaji wake kuhusu bara la Afrika na kuwawezesha kuelewa Afrika kwakina. Kufuatia kifo chake,aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Kofi Annan alisema kuwa Afrika imempotezammoja wa talanta zake chipukizi.

Aliongeza kwamba, Komla Dumor alikuwa mtangazaji mwenye kupeana motisha aliyedhamiria kuchimbua ukweli na kutangaza ukweli kila wakati.

Maneno haya yalilingana na yale yaliyotolewa na wabunge wa Ghana siku ya Alhamisi.

Katika ibada hiyo,mbunge mmoja alitajakuwa serikali ilikuwa imekubali kuipa jina barabara moja jijini kama ishara ya kumkumbuka.

IKULU YA RAIS YASHAMBULIWA

Wapiganaji wa kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia meshambulia Ikulu ya Rais katika mji mkuu Mogadishu.

Umoja wa mataifa unasema umefahamishwa kuwa rais wa nchi hiyo hakujeruhiwa na yu salama na kwamba shambulizi la wanamgambo hao lilitibuka.

Waziri wa mambo ya usalama wa nchi hiyo Abdi Karim Hussein, amesema baadhi ya washambuliaji wamefariki na wengine kukamatwa.

Kundi la Al- Shaabab linalopigana na utawala nchini humo limedai kuhusika na shambulio hilo na kusema makabiliano yangali yanaendelea.

Walianza mashambulizi yao, kwa kutumia gari lililokuwa na bomu ndani yake kwa kuliegesha kando ya ukuta na kisha kuanza kupigana ili kuweza kuingia ndani.

Milipuko mikubwa ilisikika pamoja na milio ya risasi.

Majeshi ya muungano wa Afrika yamekuwa yakipambana na wapiganaji hao na hata kuwafurusha kutoka mji mkuu Mogadishu. Hata hivyo bado wanadhibiti sehemu nyingi nje ya Mogadishu.

KAGAME KUKUTANA NA JK

MARAIS Jakaya Kikwete na Paul Kagame wa Rwanda, wamepanga kukutana mara kwa mara kujadili matatizo yanayoibuka na kuhatarisha amani baina ya nchi hizo.Pia Tanzania imechaguliwa kwa mara ya pili kuwa mjumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) katika mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Hayo yalibainishwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya utekelezaji ya mwaka ya Wizara yake.

"Kama itakavyokumbukwa, vyombovingi vya habari viliripoti kudorora kwa uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda. Baada ya mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame jijini Kampala Septemba mwaka jana, hali ya uhusiano wetu iliboreka," alisema Membe. Hata hivyo, alisema hivi karibuni vyombo ya habari vya Rwanda ukiwamo mtandao wa "News of Rwanda" vilitoa taarifa za kuishutumu Tanzania na viongozi wake.

Pia alisema kumekuwa na taarifa za kuishutumu Tanzania kufanya mazungumzo na viongozi wa upinzani nchini Rwanda akiwamo Waziri Mkuu wa zamani wa Rwanda, Faustine Twagiramungu.

Membe alisema Serikali ya Tanzania ilishajibu shutuma hizo kwa kueleza kuwa Tanzania haisaidii vikundi vya waasi na haijawahi kufanya mazungumzo wala kukaribisha viongozi wa Upinzani wa Rwanda.

"Historia ya nchi yetu tangu uhuru inajulikana kuwa tumekuwa tukisisitiza amani Afrika na hivyo hatuna sababu ya kusaidia waasi kuchochea migogoro.

"Hivyo, tunaomba kuchukua nafasi hii kuonya wanaotaka kuchafua sifanzuri ya Tanzania kuacha mara moja. Aidha, tunaomba wanahabari kutoshabikia taarifa hizi za uzushi," alisisitiza.

Alisema tangu mwaka 1963 Tanzania imekuwa ikitumika kama makao makuu ya vyama vya kupigania uhuru na imekuwa ikipokea watu walioomba hifadhi na ushauri ambao huhifadhiwa na kusuluhishwa kisha hurejea nchini mwao.

"Kama tungekuwa na tunaingilia migogoro ya watu na kusaidia makundi fulani kwa historia ya nchihii, tungekuwa tunapigana vita na bara zima la Afrika," alisema.

Alisema Tanzania siku zote inataka uhusiano mzuri na jirani zake, lakini isiwe kupenda amani kwake kuwe sababu ya watu kutaka kuichafua.

Aidha, alisisitiza kuwa Tanzania haina mpango wala haifikirii kuanzisha mgogoro wa kivita na nchi yoyote ya jirani ikiwamo Rwanda, kwa kuwa nchi hizo ni kama ndugu kwa Watanzania na inapaswa kusaidiana.

Akizungumzia kuchaguliwa kwa Tanzania kuwa mjumbe wa Baraza la Usalama la UN, Membe alisema nchi hiyo imechukua nafasi hiyo kwa mara ya pili baada ya kushindakwa kura za nchi 40 kati ya 53.

Alisema sababu ya kuwania tena nafasi hiyo ni kutokana na heshimailiyojijengea kimataifa, hususan katika utatuzi wa migogoro ya kikanda kama ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Madagascar, lakini pia kuwa mstari wa mbele kuchangia vikosi vya kulinda amani kwenye maeneo yenye migogoro kama vile Darfur, DRC na Lebanon.

Sudan Kusini Kuhusu mgogoro unaoendelea Sudan Kusini, alisemaTanzania imeridhia ombi la Baraza la Usalama la UN kuitaka ipeleke vikosi vyake kujiunga na Jeshi la UN nchini humo na imeshaanza kujiandaa kupeleka bataliani moja.

Alisema Baraza liliiomba Tanzania kupeleka vikosi vyake nchini humo kutokana na sifa kubwa ambayo majeshi ya Tanzania yamejijengea nje ya nchi na kuheshimika.

"Lakini pia sisi tunataka kuanzisha mpango wa nchi za Afrika kushughulikia matatizo yao zenyewe na si kutegemea majeshi ya nchi za Magharibi," alisema.

Ujangili Kuhusu mkutano ulioandaliwa na Mtoto wa Malkia wa Uingereza, Prince Charles na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, David Cameron wa kuzuia biashara ya pembe za ndovu, Membe, alisema Rais Kikwete atayapitia maagizo yaliyotolewa katika mkutano huo ikiwemo kutouza pembe za ndovu zilizokamatwa na kuhifadhiwa hapanchini na badala yake kuziteketeza.

"Kama mnakumbuka, tuliomba ruhusa ya kuuza pembe hizi za ndovu tulizokamata kutoka kwa majangili ili kupata fedha za kuwapeleka kwenye mafunzo askari wa Wanyamapori, kununulia vifaa na magari ya ulinzi katika hifadhi zetu, lakini katika mkutano huo, Uingereza ilikataa kuziuza bali tuziteketeze," alisema.

Alisema iwapo Rais ataridhia kuziteketeza, inabidi suala la malipo ya fidia lizungumzwe ili kupatikana kwa fedha kwa ajili ya maandalizi mazuri ya kukabiliana na majangili hao.

Uraia Kuhusu suala la uraia wa nchimbili, alisema Wizara yake imeandaa taarifa ya kuwasilisha kwenye Bunge Maalumu la Katiba inayotaka suala hilo liingizwe na kuruhusiwa nchini ili kusaidia Watanzania walioko nje nao waweze kushiriki shughuli za kiuchumi nchini.

"Tumeona hatuwapatii haki Watanzania walio nje wenye uraia wa nchi nyingine kwa kuwanyang'anya uraia wa Tanzania, wakati nchini kuna sheria inayoruhusu raia wa nje aliyeishi nchini kwa miaka 10 kupewa uraia akiomba," alisema.

MWANAMKE MWENYE NDEVU KAMA MWANAUME APOKEA VITISHO

Harnaam Kaur, mwanamke mwenye umri wa miaka 23 anayeishi katika mji wa Slough, Kusini Mashariki mwa Uingereza amepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa watu asiowafahamu kwenye mitandao kwa sababu ya ndevu zake nyingi zinazomfanya asitofautishwe kirahisi na mwanaume.

Mwanamke huyo ambaye anakabiriwa na tatizo la kuwa na vinyweleo vingi kupita kiasi, tatizo linalojulikana kitaalamu kama 'polycystic ovary syndrome', ameeleza kuwa alianza kupata tatizo hilo akiwa na umri wa miaka 11 na kwamba alikuwa akizinyoa mara mbili kwa wiki.

Ameeleza kuwa alipokuwa shuleni alikuwa akionewa sana kwa kuitwa majina mengi ya kejeli kama 'jike dume', na kwamba alikuwa anashindwa hata kuwaangalia watu usoni na alipotoka shule alijifungia ndani siku zote asionekane mara kwa mara.

Ameongeza kuwa kutokana na kuishi katika hali hiyo alifikia hatua akafikiria kujiua.

Hata hivyo, Harnaam amesema kuwa amejiunga na dini ya Sikh na kubatizwa, na kwamba imani ya dinihiyo hairuhusu watu kunyoa vinyweleo vyao kwa kuwa Mungu ndiye aliyewaumba hivyo. Kwa hiyo ameziachia nywele zake na sasa anaonekana kama mwanaume akiwa na nywele nyingi kidevuni, mikononi na kifuani.

Imani hiyo imempa ujasiri zaidi juuya muonekano wake, na anajiona mwanamke mwenye mvuto zaidi.

"Nahisi nimekuwa mwanamke zaidi,nina mvuto zaidi na nadhani naonekana hivyo pia.

Nimejifunza kupenda jinsi nilivyo na hakuna kitakachonitikisa sasa hivi." Amesema Harnaam.

"Naweza kwenda kwenye maduka ya wanawake bila kuhisi kuwa sitakiwi kuwa kule.

Navaa skirts, gauni na vidani na napenda kutengeneza kucha zangu kama msichana mwingine yeyote."

SAKATA LA POSHO LAUNDIWA KAMATI

Sakata la posho kwa wajumbe wa bunge la katiba laundiwa kamati.

Sakata la posho na fedha za kujikimu kwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba limechukua sura mpya baada ya mwenyekiti wa muda wa bunge maalum la katiba Mh. Pandu Amir Kificho kuteua majina ya wajumbe sita watakaounda kamati ya kujadili malalamiko ya wajumbe hao huku sheria na rasimu ya katiba zikiwasilishwa bungeni ambapo wajumbe wameonywa juu ya kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Hatua hiyo ya mwenyekiti wa bunge maalum la katiba imefikiwa baada ya uwepo wa mvutano kuhusu posho na fedha za kujikimu kwa wajumbe hao ulioibukia ndani ya ukumbi wa bunge wakati ambao waandishi wa habari walitolewa nje ya ukumbi huo katika kipindi ambacho wajumbe walikuwa wakikabidhiwa nakala za rasimu ya kanuni za bunge maalum kutokana na wajumbe wa Tanzania bara kupata taarifa kuwa wenzao wa baraza la wawakilishi, wanalipwa kiasi cha shilingi laki nne na ishirini elfu tofauti na wale wa bara wanaoolipwa kiasi cha shilingi laki tatu kwa siku.

Katika hatua nyingine mwanasheria mkuu wa serikali jaji Fredriki Werema amewasilisha sheria ya mabadiliko ya katiba na kuwatahadharisha wabunge kuhakikisha kuwa masuala ya uwepo wa jamhuri ya muungano, serikali, bunge na mahakama hayaguswi kwa namna yeyote ile na kuwataka wajumbe hao kujiepusha na rushwa wakati wa uchaguzi wa viongozi wa bunge hilo maalum.

Mara baada ya werema kuwasilisha sheria hiyo ya mabadiliko ya katiba wajumbe wakapata fursa ya kusimama kuomba ufafanuzi, kuuliza maswali ama kutoa michango yao kutokana na uelewa wao.

WABUNGE WAKATAA POSHO YA 300,000 KWA SIKU

WAKATI mjadala wa kihistoria wa kuunda Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukiwa katika hatua ya kupata kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, baadhi ya wajumbe wameamua kuelekeza nguvu kudai posho nono.

Wajumbe hao wanapinga posho ya sasa ya Sh 300,000 kwa siku, ambayo kwa wananchi wa kawaida inaonekana ni kubwa, lakini vielelezo vyao ni taarifa, kwamba wajumbe ambao wanatoka Baraza la Wawakilishi, wanalipwa zaidi ya hapo.

Mbali na hoja hiyo ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, ambayo sasa wajumbe ambao ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wanafikiria kumbana Spika Anne Makinda, ili nao waongezwe posho kama wenzao wa Zanzibar, hoja nyingine imetajwa kuwa ni hadhi yawabunge kwamba haifanani na Sh 300,000.

Aliyeanzisha hoja hiyo jana ni Richard Ndassa, Mbunge wa Sumve,ambaye mbali na kutaka nyongeza ya posho, alipinga utaratibu wa kusaini asubuhi na jioni kwa ajili ya posho zinazotolewa 'rejareja', akipendekeza waaminiwe na walipwe fedha nyingi kwa mkupuo.

Mjumbe mwingine, Suleiman Nchambi, alimwunga mkono Ndassa, lakini akahoji iweje wajumbe wa Tume ya Kurekebisha Katiba walipwe posho kubwa nao walipwe kidogo.

Mezani kwa Serikali Kutokana na hoja hizo, Mwenyekiti wa muda wa Bunge, Pandu Ameir Kificho, alisema suala hilo linachukuliwa kwa umuhimu na watazungumza na Serikali liamuliwe baadaye.

"Kuhusu masuala ya posho, kama nilivyosema tunalichukua ili tuangalie uwezekano wa kuzungumza na Serikali, hili tutaamua hapo baadaye," alisema Kificho.

Tume Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge, Ndassa alisema wajumbe wa Tume walikuwa wakilipwa Sh 500,000 kwasiku huku madereva wakilipwa Sh 220,000.

"Mimi ninayehangaika kuanzia asubuhi na mimi nalipwa Sh 220,000? Mimi mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na dereva wa Tume ni sawa?" Alihoji Ndassa.

Katika Sh 300,000 kwa siku, Sh 80,000 ndiyo posho ya kujikimu ambayo wajumbe wa Bunge la Katiba watapewa kila siku, iwe amefanya kazi au la, na Sh 220,000 ni posho ya kazi, ambayo itatolewa kwa waliofanya kazi tu.

Hadhi ya Mbunge "Mimi kwenye hizi laki tatu (Sh 300,000) zangu zote, ni pamoja na dereva wangu, simu, chakula, mafuta, lakini pia unamtaka mbunge eti lazima asaini kwanza!" Alionesha mshangao.

Bila kupendekeza kiwango cha kulipwa, Ndassa alitoa mchanganuo wa matumizi ya mbunge, akisema hoteli ya hadhi yake ni Sh 70,000 kwa usiku mmoja.

Mbali na gharama hiyo ya malazi, alisema gharama za chakula, mafuta ya gari, dereva na msaada atakaotakiwa kutoa kwa watu mbalimbali Sh 80,000 haitoshi.

"Hoja yangu ya msingi, ni kwamba Serikali ijaribu kuangalia suala hili kwa upana, tukiliacha hivi hivi linaweza kuleta tatizo," alisema Ndassa.

Kususa Ndassa alisema wabunge wengine ni wafanyabiashara ambao hawawezi kukubali kukaa bungeni kwa muda wote wakilipwa posho ya Sh 300,000.

Alipohojiwa anatarajia mtazamo gani kutoka kwa wananchi wanaoishikwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku (Sh 1,600), huku yeye akikataa Sh 300,000 kwa siku, Ndassa alisema:

"Ukiweka matarajioya jamii itasemaje, huwezi kufanya kazi. Maswali kama hayo huwezi kuyakwepa, binadamu hamwezi kulingana nyote duniani, hata vidole viko tofauti."

Nchambi alisema kwa upande wao, wabunge hawana tatizo isipokuwa anatetea wajumbe wengine ambao hawalipwi kiinua mgongo wala mshahara.

"Mbunge anatakiwa alale kwenye hoteli ya angalau Sh 70,000. Hata wananchi wanatakiwa waelewe kwamba wabunge wamekuja kufanyia kazi Katiba ambayo ndiyo msingi wao," alisema Nchambi.

Ubaguzi Suala lingine lililoibuliwa na Ndassa nje ya ukumbi, ni kuhusu tofauti ya kiasi cha posho kwa alichosema wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wameongezwa Zanzibar wakati wengine wakipokea Sh 300,000.

Bila kutaja kiasi kilichoongezwa, Ndassa alisema:

"Lakini wenzetu Wazanzibari wameongezwa na Baraza la Wawakilishi, wote ni wajumbe wa Bunge hilohilo… lazima kutakuwa na mgawanyiko. Na sisi tukisema hawa wabunge wamekwenda kwao wameongezwa na sisi tumwambie Makinda atuongeze, hawa makundi maalumu watakwenda kuongezwa wapi? "Kwa kufanya hivyo umeshaweka mgawanyiko inatakiwa tuwe kitu kimoja, kama ni Sh 20 wote tupeweSh 20, kama ni Sh 800 wote tuwe sawa," alisema Ndassa.

Mwandishi wa habari hizi hakufanikiwa kumpata Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Yahya Khamis Hamad kufafanua hilo kutokana na kuwa kwenye kikao.

Lakini taarifa kutoka kwa baadhi ya watendaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), zilithibitisha kwamba wawakilishi waliomba waongezwe Sh 500,000 lakini hawakupewa zote; wamepewa chini ya hapo.

"Si kweli (hawapokei Sh 420,000) lakini waliomba Sh 500,000 ila hawakupewa hizo, wamepewa chini ya hapo," alisema mtoa habari ambaye hakusema ni kiasi walichoongezwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Utaratibu Kwa mujibu wa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, wabunge hao wameshapewa posho ya kujikimu ya Sh 80,000 kwa siku kuanzia Februari 16 hadi 28.

Aliongeza kuwa posho maalumu ya kazi ya Sh 220,000 kwa siku, ambayo hupigiwa hesabu kutokana na ushiriki wa mjumbe kusaini mahudhurio kila siku asubuhi na jioni, itakuwa ikiingizwa kwenye akaunti za wajumbe kila baada ya wiki moja ya kazi.


Chanzo: Habari leo

PACHA WALIOTENGANISHWA WAREJEA NCHINI

Watoto pacha, Elikana na Eliud waliokuwa wameungana wamerejea nchini jana wakitokea India walipokuwa kwa ajili ya kutenganishwa, tayari kwa kusherehekea kumbukumbu yao ya kutimiza mwaka mmoja leo.

Waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa 10:30 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Oman,wakiwa na mama yao, Grace Joel (20) ambaye muda wote alionekana mwenye furaha.

Elikana na Eliud walizaliwa Februari20, mwaka jana wilayani Kyela, Mbeya wakiwa wameungana na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambako walipata rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Juni mwaka jana, Serikali iliwapeleka Hospitali ya Chennai, India ambako Desemba 16, mwaka jana walifanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha.

Akizungumza baada ya kutua jana, Grace alisema: "Nina furaha ya ajabu, sijui nimshukuru vipi huyu Mungu wangu, ni mkuu mno.

Ninawashukuru sana madaktari wa India, nina washukuru madaktari wa Muhimbili na sana naishukuru Serikali yangu kwa kunipa msaada huu mkubwa. Siamini kama leo ningekuwa narudi salama na watotowangu kila mmoja akijitegemea," alisema Grace."

Kesho (leo) ni birthday yao, wanatimiza mwaka mmoja, ni furaha ya ajabu niliyo nayo, siwezi kuelezea.

Siku nilipoambiwa watoto wangu watafanyiwa upasuaji mkubwa na watapumulia mashine kwa wiki moja, nilichanganyikiwa kwa kweli, sikutamani tena hata hiyo operesheni ifanyike ila sikuwa na jinsi zaidi ya kumwomba Mungu."

Akizungumza uwanjani hapo, Dk Glory Joseph kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando ambaye aliongozana na watoto hao kurudi nchini alisema:

"Watoto wamerejea salama na wanaendelea vizuri ila watakuwa Moi (Hospitali ya Mifupa Muhimbili), kwa uangalizi maalumu mpaka hapo madaktari watakapoona inafaa ndipo watapewa ruhusu ya kurudi nyumbani kwao Mbeya.

"Agosti watarudishwa tena India kwa ajili ya upasuaji katika njia ya mkojo na kufunga sehemu ya utumbo," alisema.

Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja alisema upasuaji wa watoto hao ulichukua saa 18.

Katika muda huo, saa 13 zilitumika kutenganisha viungo vilivyoungana sehemu ya chini ya uti wa mgongo, sehemu ya utumbo mpana, njia ya mkojo, kibofu na sehemu ya uume,wakati saa tano zilitumika kuunganisha sehemu zilizotenganishwa.

Pacha hao walifanyiwa upasuaji na madaktari 20 na wataalamu wengine wa afya ambao walitumia saa 18 kuwatenganisha. Kiasi cha Sh100 milioni kilitumika.

Meneja wa Huduma za Wagonjwa wa Kimataifa wa hospitali hiyo, Senu Sam alizungumza na gazeti dada la Mwananchi, The Citizen juzina kusema wamefanya sherehe kwa ajili ya mafanikio ya upasuaji huo.

Sam alisema pacha hao wameonana ana kwa ana kwa mara ya kwanza, wiki tatu baada ya upasuaji... "Imekuwa faraja kuwaona wakitazamana.

Eliudi alivishika vidole vya mkono wa Elikana na kuvichezea. Wanaonekana kufurahia mazingira mapya," alisema Sam.


Chanzo: Mwananchi

MKE NA MUME WAZUA BALAA BUNGE LA KATIBA

Chama cha National League for Democracy (NLD) Zanzibar kimemtaka, Rais Jakaya Kikwete kufuta uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupitia chama hicho kwa madai kuwa walioteuliwa katika chama hicho ni mtu na mkewe na kufanya uteuzi huo kukosa sura ya Muungano.

Tamko hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa NLD - Zanzibar, Khamis Haji Mussa katika taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari mjini hapa juzi, kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Dk Emmanuel Makaida amewasilisha majina mawili, la kwake na la mkewe, Modesta Ponera kwa ajili ya uteuzi.

Alisema NLD - Zanzibar kilianza kufuatilia taratibu za uwasilishaji wa barua tangu Desemba 27, mwaka jana kwa kumwandikia barua Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ baada ya kupokea maelekezo ya Ikulu ya Tanzania kwamba majina ya Zanzibar yatafanyiwa kazi visiwani na ya Bara yangepelekwa Ikulu Dar es Salaam.

Alisema kwa mujibu wa utaratibu huo, vyama vyote vyenye usajili wa kudumu vilitakiwa kila kimoja kutoa mtu mmoja kutoka Tanzania Bara na mwingine Zanzibar ili kuwa na sura ya kitaifa, lakini Dk Makaidi alikiuka utaratibu huo.

MAKAIDI AJITETEA

Akizungumzia tuhuma hizo, Dk Makaidi alikiri kuwa Ponela ni mke wake, lakini akasema ni mwanachama wa NLD, hivyo ana haki ya kuteuliwa.

Alisema alipeleka majina manne Ikulu na kwamba upande wa Zanzibar ulitakiwa kufanya hivyo kupitia Ikulu ya Zanzibar... "Walifanya uzembe, hawakupeleka majina ya wanachama wa NLD, matokeo yake nikapeleka majina manne,tukapata uwakilishi."

Alisema mkewe ni mwanachama wa NLD hivyo ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi yoyote kulingana na sifa zake...

"Wanalalamika nini hata chamatawala cha CCM, Rais Jakaya Kikwete ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mkewe Salma pia ni mjumbewa Nec."

Alisema Ponela kuwa mkewe hakumfanyi akose haki zake za msingi na kwamba sifa zake na elimu ndivyo vilivyomfanya Rais amteue.

Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Florens Turuka alipoulizwa alisema Ikulu haina taarifa za suala hilo lakini wanaamini vyama vya siasa vilikaa na kupendekeza majina manne na kuyawasilisha Ikulu, ndipo Rais alipoteua wajumbe mawili kati yake.

IKULU YAWAJIBU MAASKOFU WA PENTEKOSTE

Ikulu imetoa taarifa ndefu kuhusu madai ya maaskofu wa pentekoste (PCT) kuwa wametengwa kwa mjumbe wao kutokuchaguliwa katika bunge la katiba licha ya kupeleka majina kwa rais.

Kwa ufupi ikulu imesema baada ya uchunguzi imegundua kuwa maaskofu wa pentekoste hawa kuwasilisha majina kwa njia ya kawaida, kujiteua ama kwa kuchelewa kwani database ya ikulu haijaonyesha ripoti ya maaskofu hao kutuma majina kwao.

Aidha ikulu imesema mjumbe mmoja alieteuliwa kwenye taasiai za dini Bi Edna Adam ametoka kanisa la EAGT ambao ni miongoni kwa wanachama wa baraza la maaakofu wa Pentekoste licha ya kwamba jina lake liliwasilishwa na taasisi nyingine ya dini na sio Baraza hilo la Maaskofu wa Pentekoste.

Hivyo ikulu imewaomba maaskofu hao kumtumia mjumbe huyo kama mwakilishi wao na kuwa watawakilishwa kikamilifu.

Nitaiweka statement yote later licha ya kwamba ni ndefu sanaaa.

GAVANA AANZISHA USHURU WA KUAGA MAITI

Katiba Mpya ya Kenya imeanzisha mambo mengi mapya. Imeshusha madaraka kwa wananchi na kuwapa madaraka makubwa magavana ya kuamua mambo mbalimbali.

Kenya ilizindua Katiba mpya Agosti 27 mwaka 2010 kwenye sherehe iliyojaa mbwembwe katika bustani ya Uhuru, Nairobi.

Hiyo ilikuwa baada ya Wakenya kupiga kura kwa wingi wakiunga mkono Katiba Mpya. Badala yake katiba imekuwa chungu kwa Wakenya kwa magavana kuaanzisha ushuru wa aina mbalimbali ikiwemo ushuru wa kuaga maiti.

Inatafsiriwa kuwa, magavana wametumia mamlaka yao kunyanyasa wananchi katika kaunti.

Katika Kaunti ya Kiambu, inayoongozwa na Gavana William Kabogo, kuna ushuru mpya unaotozwa kwa familia iliyopoteza mpendwa ama wapendwa wao.

Hakuna anayekubaliwa kumzika mfu wao bila kulipa ushuru huo. Pia, huwezi kuchinja mfugo wako nyumbani bila kulipa ushuru!
Katika Kaunti ya Kakamega, Gavana amebuni ushuru wa kuku ambapo kila mfugaji atalipa Sh20 kwa kila kuku anayemfuga.


Pia, watu wanapoomboleza, lazima walipe ushuru wa kuomboleza haswa wanapotazama mwili wa marehemu.
Ukiutazama zaidi ya mara mbili, utalipa ushuru zaidi ya mara moja!
Watu hawajui la kufanya na wana majuto makuu kwa kukaribisha Katiba mpya 2010. Walipokuwa wanaipitisha walikuwa na matumaini kwamba ingebadilisha maisha yao kwa kuleta utawala na huduma za Serikali Kuu karibu yao.

Wakati huo wa mchakato wa Katiba mpya, Makamu wa Rais William Ruto alikuwa katika upande uliokuwa ukipinga Katiba hiyo.

Hata hivyo, Muungano wa Jubilee ulipochukua hatamu ya uongozi, Ruto na Uhuru Kenyatta waliapa kuilinda na kuitetea Katiba hiyo.

Katiba ikawa mwanzo wa Serikali mpya iliyoshusha zaidi madaraka kwa wananchi hadi ngazi ya Kunti, kwa lugha ya Kenya inaitwa Serikali ya Ugatuzi, ambapo mipaka ya nchi iliyowekwa wakati wa ukoloni, iligawanywa upya ili mipaka mipya ya Kaunti 47 iundwe.

Machi 4 mwaka 2013, uchaguzi mkuu ukafanyika na viongozi mbalimbali wakiwamo magavana wakachaguliwa, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Kenya kuwa na viongozi wa aina hii.

Sasa Kenya ina magavana 47, baadhi ya watu wanaona kuwa viongozi hawa wanakuwa kama miungu watu ambao Wakenya hawana budi kumshukuru Mola kwa sababu yao.


Hali hiyo inatokana na tuhuma za ufisadi zinazowakabili baadhi magavana, hali iliyowakasirisha Wakenya walio wengi.

Mmoja wa anayekabiliwa na tuhuma hizi ni Martin Wambora wa Kaunti ya Embu. Kiongozi huyu alipoteza wadhifa wake wiki iliyopita, baada ya Bunge la Kaunti kupiga kura ya kumwondoa katika wadhifa wa Ugavana.

Wambora alituhumiwa kujihusisha na ufisadi wa hali ya juu, ambapo Kaunti ilipoteza mamilioni ya fedha baada ya zabuni ya kununua mbolea na mbegu za mahindi kwenda mrama.

Mbegu za mahindi hazikumea na mbolea haikuwa nzuri, huo ulikuwa mwanzo wa masahibu ya Wambora yaliyomfikisha mbele ya Kamati ya Seneti iliyosikiliza kesi yake na kuamua kumfuta kazi.


Naibu wake sasa amechukua nafasi yake na kufanya Kenya kupata gavana wa kwanza mwanamke.

Kufutwa kazi kwa Wambora kulifungua mlango wa Bunge la Seneti kuonyesha kati ya seneta na gavana, ni nani mkubwa.

Wakati Seneti ilikuwa ikitoa uamuzi wake kuhusu hatma ya Wambora, maseneta wawili walisema hawatashiriki kwenye zoezi hilo kwa sababu mchakato mzima haukufuata haki.

Seneta mmoja aliyeunga mkono kufutwa kazi kwa Wambora, aliiambia Seneti kuwa, kuanzia sasa magavana watajua'nani kati yao na sisi ndiye ana uwezo wa kumtimua na kumwadhibu'.


Kwa wadadisi wa kisiasa, hatua ya Seneti kumng'oa mamlakani gavana huyo, ni jaribio la maseneta kutoa ujumbe kwa magavana wanaotuhumiwa kuwapuuza viongozi hao haswa katika suala la kupeleka madaraka kwenye kaunti.

Sasa, Wambora ameenda nyumbani kutafuta kingine cha kufanya na Seneti inapanua upeo wake ili inase magavana zaidi wanaoshukiwa kufuja pesa za umma na kubuni sera potofu za kunyonya jasho la wananchi wa kawaida kwa kuwatoza ushuru.

Kusambaza ufisadi
Ufisadi sasa umesambazwa kutoka Serikali Kuu hadi Serikali za Mashinani na kufanya maisha kuingia kwenye mkondo mbaya zaidi.

Fedha zilizopaswa kutumwa kutoka kwenye Serikali Kuu kwenda kwenye kaunti, hazitumiwi ipasavyo.

Badala yake, pesa hizo za maendeleo ya kikaunti zinafujwa na kuelekezwa kwenye miradi bifasi ya magavana na vibaraka wao.

Ajira katika kaunti ni kama sarakasi kwa sababu magavana hawazingatii sheria na kanuni zinazo ongoza uajiri wa wafanyakazi wa umma.

Magavana wanaajiri jamaa zao wasio na ujuzi au elimu na kuwaacha wataalamu waliosomea nafasi husika.


Uchunguzi uliofanywa miezi mitatu iliyopita, unaonyesha kuwa magavana wametenga mamilioni ya fedha kugharimia safari zao za nchi za nje haswa Uingereza, Amerika na Ufaransa.

Seneta inanuia sasa kukata'pembe'za magavana wote na kuna orodha ya majina tisa ya wale wanaotakiwa kufika mbele ya Kamati ya Seneti kujibu maswali kuhusu matumizi ya fedha za umma.

Majibu yatakiwa
Magavana hao tisa wanatakiwa pia kujibu maswali kuhusu ushuru tata walioanzisha katika kaunti zao.

Anayelengwa zaidi ni Gavana wa Kaunti ya Bomet, Isaac Ruto aliyekuwa amezoea kumzomea na kumkosoa Makamu wa Rais kwa hili na lile. Majibizano kati ya hao wawili yalikuwa yakitawala vyombo vya habari.

Gavana Rutto anaonekana kama'mwenye kichwa kikubwa'na anafaa'kurekebishwa'na Seneti ili afuate mkondo unaotakikana.

Lakini Seneti ina haki ya kuwaadhibu magavana wanavyopenda? Nguvu hizi za Seneti kuwaadhibu magavana zimetoka wapi?
Kwa muda mrefu, mashindano katika ya maseneta na magavana kuhusu'ukubwa'yamekuwa yakitawala vyombo vya habari.

Magavana walioandikiwa barua kufika mbele ya Seneti wanasema maseneta wamekosea kisheria kuwataka wafike mbele yao.


Hatua ya kwanza wanayochukua magavana kujaribu kuwazuia maseneta kuwaadhibu ni kutuma maombi ya kesi kwa kwa mahakama ya kisheria ili iamue nani kati yao ni'ndume'ya mwengine.

Mwaka mmoja umeisha tangu Uchaguzi Mkuu umefanyike, lakini kilichodhairi shahiri ni kwamba maendeleo ya kipekee wanayoyazingatia viongozi waliochaguliwa ni kujipiga kifua kuonyesha nani ni mkubwa zaidi ya mwenzake.

Hayo yakiendelea, barabara zimezorota, sekta ya afya imesambaratika na wananchi wamepoteza matumaini, ya kuona siku moja wataishi maisha yanayofaa na kuachana na ufukura wao wa miaka mingi.

Ufisadi umeota mizizi nchini na ni mzigo kwa maisha ya wananchi, hawaoni tofauti kati ya vitendo vya maseneta na magavana.


Hii ni kwa kuwa wengi wao wanashiriki ufisadi. Ni kweli kwamba kama maseneta wangekuwa na nafasi ambayo magavana wanazo, baadhi yao wangefanya kama vile magavana walivyofanya kwa kufuja mali za umma na kuendeleza ukabila.

Katiba Mpya ilikuwa inaonekana kama baraka kwa Wakenya, lakini kwa hakika imeleta shida nyingi na kufanya maisha kuwa magumu zaidi.

Wanaoumia ni wananchi wa kawaida, huku viongozi wakiendelea kujilimbikizia mali bila kutoa jasho.

Wanaendelea kutajirika huku wananchi wakihangaishwa na maisha. Mwokozi wao ni nani?


Chanzo: Mwananchi

WALIOBAKWA LIBYA KULIPWA FIDIA

Waziri wa Sheria nchini Libya, salaha al-Marghani, amesema kuwa Baraza la mawaziri limekubaliana kuwa Wanawake waliobakwa wakati wa maandamano na harakati za kuuangusha utawala wa aliyekuwa Rais wa taifa hilo Moammar Gaddafi mwaka 2011 watambuliwe kuwa waathirika wavita.

Amesema makubaliano hayo yanayohitaji kuidhinishwa na Bunge kabla ya kuwa Sheria yatamfanya mwanamke awe sawa na wale wapiganaji waasi waliojeruhiwa halikadhalika watalipwa fidia.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu imekusanya ushahidi kuwa vikosi vya waliokuwa wakimuunga mkono Gaddafi walitekeleza vitendo vya ubakaji kama silaha.

Inaelezwa kuwa Wanawake wanaobakwa mara nyingi wamekuwa wakitengwa nchini Libya, hivyo haijafahamika wanawake wangapi watajitokeza.

WHATSAPP KUNUNULIWA NA FACEBOOK

Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya Facebook imesema kuwa itanunua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza zaidi ya dola bilioni tatu zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na wafanyikazi wake.

Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa.

WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.

WhatsAp imeweza kuwasajili zaidiya watumiaji milioni mia nne hamsini.

Katika taarifa, mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa.

FAMILIA NA JAMAA KUKUTANISHWA BAADA YA MIAKA 60

Makundi kadhaa ya watu wakongwe kutoka Korea Kusini wanaelekea Kaskazini kukutana na jamaa zao ambao hawajaonana kwa zaidi ya miaka sitini, tangu vita vilivyotenganisha mataifa hayo mawili ya rasi ya Korea.

Wakongwe hao wamebeba mikoba iliyojaa zawadi, ikiwa ni pamoja na dawa za maradhi ya kawaida, picha za familia na vyakula.

Tukio hilo litakaloibua majonzi litafanyika katika eneo la kitalii upande wa Korea Kaskazini.

Hapajakuwa na zoezi kama hilo lakuunganisha familia tangu mwaka2010.

Awali Korea Kaskazini imefutilia mbali mpango huo wa kuziunganisha familia kujibu vitendo vya Korea Kusini ambavyo Kaskazini inapinga.

Shirika la Msalaba Mwekundu linasema kuwa watu alfu sabini wanaoishi Kusini wanasubiri fursaya kukutana na jamaa zao wa Kaskazini-nusu kati ya watu hao ni wazee walio na umri wa zaidi ya miaka 80.

MINI SKIRT MARUFUKU

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu uchi au kuhusika na vitendo vinavyohusisha picha zenye watu uchi.

Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia sketi fupi sana au 'Mini Skirt' kama zinavyojulikana au blausi ambazo zinaonyesha kifua chao hadharani na kusababisha hisia za kingono.

Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya mafunzo au wakati wa michezo na hafla za kitamaduni.

Akihutubia waandishi wa habari, mjini Kapmala, waziri wa maadili na utawala bora, Reverend Simon Lokodo alisema kuwa Rais Museveni alipitisha sheria hiyo tarehe 6 mwezi huu, miezi mwili bada ya bunge kuipitisha.

Kwa mujibu wa sheria hiyo kamati dhidi ya vitendo hivyo itabuniwa ili iweze kutekeleza sheria hiyo kwa kuhakikisha kuwapicha, au video zenye watu uchi zinanaswa na kuharibiwa.

Kamati hiyo, itajumuisha watu kutoka katika sekta mbali mbali ikiwemo ya habari na utumbuizaji.


Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote atakayepatikana akijihusisha na vitendo cya watu kuwa uchi, kuvalia nusu uchi , kuona sinema za watu wakiwa uchi au kuchapisha picha za watu walio uchi kwa lengo la kuleta hisia tofauti utachukuliwa hatua kali za kisheria.

Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia zisizofaa miongoni mwa watu.

Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia visivyo watafungwa hadi miak 10 na wale watakaopatioka na na hatia ya kuhusisha watoto katika biashara ya ngono watafungwa hadi miaka 15.

BUNGE LA KATIBA KUDHIBITIWA KIDIGITALI

BUNGE Maalumu la Katiba, limeanza chini ya mfumo wa kidijitali ambao pamoja na masuala mengine, vipaza sauti vyote viko chini ya udhibiti wa Mwenyekiti hali ambayo haitaruhusu mbunge kuvitumia bila ridhaa ya kiti. Hayo yalifahamika jana bungeni mjini hapa, wakati Sekretarieti ikitoa maelekezo kwa wajumbe kuhusu ukaaji na jiografia ya ukumbi.

Aidha wajumbe wamehakikishiwa kuwepo usalama wa kutosha huku wakiambiwa wakubaliane na upekuzi wa hali ya juu unaofanyika kutokana na mazingira ya sasa ambayo suala la usalama ni tata.

Chini ya usimamizi wa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Yahya Khamis Hamad, ilielezwa, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu sasa anao uwezo wa kuzima kipaza sauti za mjumbe akiwa mezani kwake.

"Sauti ya kaa chini ikisikika, ukitaka kuendelea kuzungumza, sauti haitasikika," alisema Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari (IT), Didas Wambura.


Kutokana na mfumo huo, kipaza sauti cha kwanza kikishawashwa, kinaonesha rangi nyekundu. Wengine wakiwasha, wanaoneshwa rangi ya kijani kuashiria kwamba wasubiri. Viashiria hivyo vinakuwa kwenye kiti ambaye anavitumia kuruhusu wazungumzaji.

Mfumo utaweza? Hata hivyo muda mfupi baada ya wataalamu kuwasilisha maelekezo, walipopewa muda wa kuuliza maswali au kupata ufafanuzi, walijitokeza wajumbe wengi waliotaka kuzungumza ambao baadhi, baada ya kudhibitiwa na mfumo, walipaza sauti bila kutumia vipaza sauti wakitaka wapewe nafasi.

Wakati huo huo Wambura alisema kila mjumbe ana kadi inayomwezesha siyo tu kufungulia mlango, bali kutumia katika kuzungumza kupitia vipaza sauti hivyo na pia inamwezesha kupiga kura.

Kaimu Mkuu wa Usalama wa Bunge, Peter Magati alisema wameongeza vituo vya upekuzi na akaomba wajumbe wakubaliane nahali hiyo.

"Mazingira ya sasa hivi ya hali tata ya usalama ndiyo sababu ya upekuzi wa namna hii," alisema.

Aliendelea kusema, "tumejiandaa kuhakikisha mnakaa kwa amani na utulivu ndani na nje ya Bunge." Kuhusu wageni, alisema watakuja kwa taarifa na akataka wajumbe kuhakikisha wageni wao wanakuwa katika mavazi ya staha yasiyo na walakini.

Masuala mengine waliyohakikishiwa wajumbe, ni umeme kutokatika.

Sanjari na hilo, Mkuu wa Wakala waSerikali Mtandao, Dk Jabir Bakar alisema pia ipo Wavuti ya Bunge Maalumu itakayokuwa ikirusha shughuli zote za Bunge moja kwa moja sanjari na Televisheni ya Taifa (TBC).

Huduma za matibabu zinapatikana katika hospitali iliyoko bungeni na ikitokea matibabu yakashindikana, mjumbe anaruhusiwa kwenda hospitali nyingine ya Serikali au binafsi kwa ushauri wa daktari na gharama za matibabu zitarudishwa.

Aidha wajumbe wamepewa orodhaya hoteli huku wakiaswa kutokwenda maeneo yanayohatarisha maisha yao.

Posho Taarifa ya Mhasibu Mkuu waBunge ilieleza kwamba licha ya wajumbe kulipwa posho ya kujikimu kila siku huku posho maalumu ikilipwa kwa wiki, vile vile wenye wasaidizi watalipwa posho ya kujikimu.


Malipo mengine wanayopewa wajumbe ni gharama za usafiri ambazo zitarejeshwa baada ya mhusika kuwasilisha tiketi ya usafiri aliotumia. Pia upo utaratibuwa kurudisha mafuta kwa waliotumia usafiri binafsi. Wajumbe wenye watoto wachanga wameambiwa wawasiliane na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kwa ajili ya kupewautaratibu juu ya eneo la kutolea huduma.

Ukaaji ndani ya ukumbi huo wenyeviti 676, umezingatia majina, wenye mahitaji maalumu hususaniwenye ulemavu na pia wenye mahitaji maalumu ya kiusalama kama vile Waziri Mkuu.

Wajumbe Baada ya maelekezo kutolewa ukumbini, baadhi ya wajumbe walilalamikia masuala mbalimbali, wakiwemo wenye ulemavu waliotaka mazingira rafikikwao ikiwemo kuwepo wakalimani kwenye televisheni.

Vile vile suala la usawa wa jinsia katika uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu wake, lilijitokeza kutoka miongoni mwa wajumbe.


Mjumbe wa kwanza kusimama alikuwa Tundu Lissu, ambaye alitaka ufafanuzi kutokana na kile alichosema baadhi ya nyaraka muhimu hazimo kwenye makabrasha. Mwingine, Mussa Ali Kombo, alilalamikia posho akisemawapo waliofika Februari 16 mwaka huu lakini hawakujisajili jambo ambalo limewanyima posho ya kujikimu. Alitaka wafikiriwe kupatiwa posho hiyo.

Ernest Kimaya alitaka kufahamu iwapo wenye ulemavu watapatiwa maandishi makubwa. Kwa upande wake, Amon Mpanju alihoji kama kutakuwepo wakalimani wa lugha za alama ili watu walio kundi hilo wafuatilie yanayojadiliwa kwenye Bunge.

Naye Julius Mtatiro alihoji kuhusu stahiki za wajumbe akitaka posho maalumu wanayopewa, viwango vitajwe waelewe. Kwa upande wake, Kangi Lugora alitaka wagawiwe mapema rasimu ya Kanuni za Bunge hilo."Iko tabia ya kuuziwa mbuzi kwenye gunia…tugawiwe haraka.

Lazima tuwe na muda wa kutosha. Mpaka kieleweke mimi sitoki bila kuwa na kanuni," alisema.

Hata hivyo Katibu wa Bunge, Dk Kashililah alisema suala la kanuni inabidi kusubiri apatikane Mwenyekiti wa Muda ambaye ndiye mwenye jukumu la kuandaa kanuni.

Akizungumzia usawa wa kijinsia katika kupata Mwenyekiti na Makamu wake, Kashililah alisema uchaguzi huo ni suala la kisheria."Mnatubebesha mzigo tu, naliacha kwa mtaalamu," aliwaambia wajumbe. Kuhusu maandishi makubwa na wakalimani kwa wenye ulemavu, Katibu wa Bunge alisema huduma hizo zitapatikana mkutano utakapoanza.

Aidha kuhusu hoja ya Lissu, Kashililah alikubaliana naye na akasema nyaraka zinaendelea kuchapishwa na kabla ya kuanza kupitia rasimu ya katiba, zitakuwa zimepatikana.

Akijibu aliyelalamikia posho, Kashililah alisema ambao hawakulipwa posho ya kujikimu lakini walifika DodomaFebruari 16 wawasilishe uthibitisho.

MAKADA WALIOHOJIWA WAPIGWA ADHABU

MAKADA sita wa CCM waliohojiwa hivi karibuni na Kamati Ndogo ya Maadili ya Chama hicho wamepewa onyo kali linaloendana na kuwekwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja.

Waliokumbwa na adhabu hiyo ni mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Steven Wasira.

Wengine ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba na Waziri wa zamani wa Nishati, William Ngeleja. Hatua hiyo imechukuliwa dhidi yao baada ya kuthibitika kuwa walianza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea urais wa nchni mwakani kabla ya wakati.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya Kamati Kuu ya Chama hicho, kuhusu wanachama hao waliohojiwa kuanzia Februari 13 hadi 18.Alisema baada ya kuwahoji walithibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea uraiskabla ya wakati, jambo ambalo ni kinyume na Kanuni za Uongozi na Maadili ya Chama hicho.

Pia walithibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya chama na baadhi yao kufanya vitendo hivyo ndani ya jamii."Kamati Kuu baada ya kuthibitisha makosa hayo imewapa wote adhabu kali na kutaka wajiepushe na vitendo vinavyokiuka maadili naiwapo wataendelea navyo, chama kitawachukulia hatua zaidi," alisema Nnauye.

Alitoa tafsiri ya adhabu ya onyo kali kwa mujibu wa kanuni za uongozi na maadili za chama hicho,kuwa:

"Mwanachama aliyepewa adhabu ya onyo kali atakuwa katika uchunguzi kwa muda usiopungua miezi 12, ili kumsaidia jitihada zake za kujirekebisha."

Alisema akiwa katika kifungo hicho mhusika atakuwa amepoteza sifa za kugombea nafasi yoyote sawa na mtu aliye na kifungo cha nje ambacho kinamtaka asifanye kosa lolote. Alisema Kamati Kuu iliitaka pia Kamati Ndogo ya Udhibiti kuchunguza na kuwachukulia hatua wote waliohusika kwa namna moja au nyingine, mawakala na wapambe kufanyika kwa vitendo vilivyovunja kanuni za chama.

"Aidha, Kamati Kuu imewaonya viongozi na watendaji wa chama nakuwataka kujiepusha na matendo ya wanawania urais yanayovunja nakukiuka maadili ya chama na wametakiwa kuzingatia kanuni na taratibu za chama," alisema.

Akizungumzia hatima ya wanachama hao alisema itategemea na tabia zao na ikiwa vikao husika vitaridhika ndipo hatima yao itajulikana.

Kauli ya JK Wakati huo huo, Nnauye alisema Rais Jakaya Kikwete hatafuta kauli ya kutaka wanachama wa chama hicho kuacha unyonge katika vurugu zinazofanywa na vyama vingine katika uchaguzi mbalimbali bali ataongeza nguvu.

Pia alisema Chadema haina adabu kwa kumpa Rais siku tatu aombe radhi kwani alitoa kauli hiyo kutokana na matendo inayofanya.

Alidai katika uchaguzi uliopita wa madiwani, viongozi na wanachama wa Chadema walifanya vitendo vyakinyama dhidi ya wana CCM wakitumia silaha kama mapanga, visu, bisibisi na marungu.

Nape alionya kutohamasisha mapambano katika uchaguzi mdogo, kwani vitendo vilivyofanyika katika uchaguzi wa udiwani pekee vinatisha na kama ndivyo itakuwaje katika uchaguzi mkuu. Alisisitiza kuwa CCM inapeleka vijana wake Kalenga ili kujilinda na matendo kama hayo.

"Hatujawahi kuwa na makundi kwa ajili ya kupiga watu bali kujilinda na watu wetu na wapigakura kwani Chadema hawataki siasa za kistaarabu," alisema.

Walipohojiwa Walipohojiwa wiki iliyopita, makada hao sita kila mmoja alitoka na kauli yake ambapo baadhi walikana kuwekwa 'kitimoto' wakidai walikuwa wakitoaushauri, huku mmoja 'akifunguka' na kueleza dhahiri kilichojiri ndani ya kikao hicho ambacho kilikuwa kikifanyika si chini ya saa moja na nusu.

Lowassa aliyekuwa wa kwanza kuhojiwa, alisema kilichoongewa ni masuala ya kujenga chama.

"Tumeshauriana na kukubaliana vizuri tu ili kukisaidia chama kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015," alisema. Kuhusu madai kwamba anatajwa kushiriki kuvuruga chama kwa kuanzisha makundi, alisema kitu kama hicho hakikuzungumzwa.

"Sijibu lawama, kwa vile hakikuwa kikao cha lawama, kilikuwa cha mazungumzo na ndani ya kikao hakukuzugumzwa makundi," alisema Lowassa Sumaye Sumaye akiwa wa pili kuhojiwa, alisema;

"Itabidi muwasubiri wakubwa," na kufafanua kwamba baada ya Kamati hiyo kutoa majibu ya kilichojadiliwa, atakuwa na la kusema, lakini kwa siku hiyo hakuwa na cha kuongea.

Ngeleja, baada ya kutoka, alisema kikao kilikuwa kikizungumzia mambo ya kichama zaidi na kwamba ndani ya CCM, wanaongozwa na kanuni na wenye nia ya kugombea muda bado haujafika na si jambo la ajabu chama kuita watu wake kuwahoji.

"Binafsi sijatangaza nia ya kugombea urais… kama kuna ugomvi mimi siko kwenye ugomvi huo," alisema Ngeleja. Makamba Januari alifuata baada ya Ngeleja na kusema hakukuwa na mashitakabali ushauri kuhusu namna ya kupata viongozi ili kuimarisha chama badala ya kukigawa hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.

"Hakukuwa na habari ya mashitaka bali kutoa ushauri na kukumbushana misingi ya namna ya kupata uongozi na kuimarisha chama badala ya kukigawa," alisema.

Wasira Wassira aliyefuata baada ya Januari, na kusema hajawahi kutangaza nia ya kugombea urais na wala si dhambi mtu kutamani kuwa Rais wa Nchi.

Alisema hakuitiwa tuhuma ila waandishi wa habari walifanya mkutano uwe wa tuhuma, lakini walizungumzia mustakabali wa kuelekea uchaguzi mkuu mwakani. Alisema magazeti mengi yaliripoti kuwa wanaitwa kwa tuhuma ya kutangaza nia kabla ya wakati.

"Sijawahi kutangaza kugombea urais…kwani ni kosa kutangaza kugombea urais?" Alihoji Wasira nakuongeza: "Kuna barua na magazeti ambayo yanatofautiana juu ya kuitwa Dodoma, andikeni ukweli mimi ni mjumbe wa KamatiKuu siwezi kuvuruga chama.

"Membe Membe akiwa wa mwisho kuhojiwa, alisema pamoja na baadhi ya wenzake kudai hakukuwana mashitaka, waliitwa kuhojiwa.

"Kamati yetu ya Maadili imejipanga vizuri, na msidanganyike, wanauliza maswali mazito, maswali magumu ama unayoyafanya wewe au mashabiki. Lakini yote yanalenga katika kukiimarisha chama, katika kuimarisha ushindi kwa mwaka 2015 na kuimarisha maadili. Yale ni mambo mazito," alisema Membe na kuongeza:

"Makubwa matatu ambayo Kamati ya Maadili iliuliza, kubwa kabisa ni uzukaji ghafla wa makundi ambayo yanazaliwa kila watu wanapodhani fulani anafaa kuwa kiongozi.

Tunafanyaje kukifanya chama chetu kiwe na kundi moja litakalokwenda mwakani kwenye ushindi."

Lakini la pili, pia ni suala zima la fedha kama msingi wa ushindi. Inatokeaje watu wanatumia mamilioni, mabilioni ya fedha kujinufaisha na kujiandaa kwenda kwenye uchaguzi.

"Lakini tatu ni vyombo vya habari; ninyi waandishi wa habari, mnalishwa vitu gani, mmemeza nini vichwani mwenu mpaka mwone kinachosemwa na fulani ni cha maana hadi kitoke katika magazeti na kingine kikisemwa na fulani, hata kikiwa cha maana kisitoke magazetini, mmemeza mdudu gani?" Alihoji Membe.