TAARIFA ZA SHAMBULIO HUKO NIGERIA

Taarifa mpya zimeibuka kuhusu shambulizi lililofanywa dhidi ya kanisa moja katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria siku ya Jumapili.

Askofu wa kanisa hilo Yola, Mamza Dami Stephen, ameiambia BBC kuwa wapiganaji walilifunga kanisa hilo, katika kijiji cha Waga Chakawa, baada yamisa na kuwapiga risasi wale wote waliojaribu kutoroka kwa kupita kwenye madirisha. Inaarifiwa takriban watu 30 waliuawa kwa njia hiyo.

Siku hiyo hiyo washambuliaji walivamia kijiji cha Kawuri na kuwaua watu 52. Kundi la Boko Haram limelaumiwa kwa kufanyamashambulizi hayo. Amesema kuwa baadhi yao walikatwa koo zao.

Takriban watu thelathini walifariki kufuatia shambulizi hilo ambalo inasemekana limesababishwa na kundi la wapiganaji wa kiislamu laBoko Haram.

Shambulizi lingine liliwaacha watu hamsini wakiwa wamefariki katika jimbo la Borno.

Wapiganaji wa Boko Haram wanataka kutawala kutumia sheria za kiisilamu katika nchi ambayo imegagawanyika kati ya wasilamu na wakristo.

Kundi hilo limewaua maelfu ya watu katika kipindi cha miaka minne iliyopita, huku kundi hilo likisemekana kuwa tisho kubwa sana kwa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Majimbo ya Borno na Adamawa pamoja na jimbo la Yobe yako chini ya sheria ya hali ya hatari tangu mwezi Mei mwaka jana huku jeshi likijaribu kupambana na wapiganaji hao wa kiisilamu.