WAMISRI WAPIGA KURA RASIMU YA KATIBA

Watu nchini Misri wameanza kupigia kura ya maamuzi rasimu ya katiba mpya huku hali ya usalama ikiwa imedhibitiwa vikali.

Katiba mpya ndio itatoa njia kwa uchaguzi mkuu mpya kufanyika.

Madhumuni ya katiba hiyo mpya ni kutupilia mbali katiba ya zamani iliyopitishwa na iliyokuwaserikali ya Mohammed Morsi miezi kadhaa kabla ya jeshi kumuondoa mamlakani.

Jeshi linataka watu waipigie kura ya Ndio katiba hiyo ambayo ndiyo ishara ya kuondoka kabisa kwa Morsi ambaye wafuasi wake wamekuwa wakisema ni rais halali wa Misri.

Vuguvugu la Muslim Brotherhood ambalo sasa limetajwa kuwa kundi la kigaidi linasusia uchaguzihuo.