Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) itaanza kupeleka fedha za wanafunzi katika vyuo kuanzia wiki hii.
Ahadi hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, George Nyatega, alipozungumza na NIPASHE.
Nyatega alisema jumla ya wanafunzi 29,113 wa elimu ya juu nchini kutoka
vyou mbalimbali waliochaguliwa kupata mkopo, fedha zao zitaanza
kupelekwa kuanzia wiki hii.
Nyatega alisema baada ya kutoa majina hayo,bodi ya wakurugenzi
ilitarajiwa kukutana Jumamosi kufanya tathmini kisha fedha zao zianze
kupelekwa vyuoni.
Hata hivyo alisema kwa mwaka huu idadi ya walioomba mikopo imeongezeka
tofauti na mwaka jana na kuongeza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni
ufinyu wa bajeti.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandara,
jana aliiambia NIPASHE kuwa chuo hichi kimekubaliana na HESLB kwamba
kuanzia Alhamisi wiki hii fedha zitapelekwa.
Chanzo:NIPASHE
chuotanzania.blogspot.com