MESSI KUPEWA TUZO YA HESHIMA

Chama cha soka cha Hispania (LFP) kimetangaza kitampa Lionel Messi tuzo ya heshima kwa kuvunja rekodi ya ufungaji bora wa la liga kwa muda wote.

Messi amevunja Rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Telmo Zarra ya kufunga Bao 251 alipofunga mabao matatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Sevilla.

Rais wa chama cha soka cha Hispania Javier Tebas, amethibitisha kuwa watatoa tuzo hiyo kwa mshambuliaji huyo wa timu ya Barcelona.

Messi atapewa Tuzo hiyo Januari 11 katika Uwanjani Nou Camp wakati Barca itakapocheza Mechi ya Atletico Madrid.

Mpaka sasa Messi, amekwisha funga jumla ya mabao 258 katika ligi ya Hispania, huku hasimu wake wa karibu Cristiano Ronaldo akiwa nafasi ya tisa katika historia ya ufungaji bora wa muda wote.

BARCELONA WAFUNGIWA KUSAJILI MPAKA 2016

Shirikisho la soka dunia FIFA limeitupilia mbali rufaa iliyokatwa na klabu ya Barcelona kuhusu kuizuia kusajili kwa kukiuka kanuni ya usajili.

Barca walifungiwa kwa miezi 14 kusajili baada ya kufanya makosa kwa kusajili kinda wa chini ya miaka 18, Ikiwa ni kinyume na kanuni za usajili za Fifa.

Kwa maamuzi haya timu hii haitakua na uwezo wa kusajili mchezaji mpya mpaka Januari 2016.

Barcelona wanatarajia kukata rufaa tena maamuzi haya ya Fifa kwenye mahakama ya usuhuhishimichezoni(Cas).

Miamba hiyo ya soka ilifanikiwa kuwasajili mshambuliaji Luis Suarez , mabeki Thomas Vermaelen Jeremy Mathieu golikipa Claudio Bravo na kiungo Ivan Rakitic mwanzoni mwa msimu baada ya baada ya kupewa ruhusa maalumu na Fifa.

AJIZALISHA NA KUTUMBUKIZA MTOTO CHOONI

MSICHANA mmoja mkazi wa Mtaa wa Zaire eneo la Kijenge Kaskazini mkoani Arusha, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru chini ya ulinzi mkali wa Polisi baada ya kujizalisha mwenyewe na kisha kumtumbukiza mtoto wake kwenye ndoo ya maji.Baba mwenye nyumba ambayo binti huyo alikuwa amepanga chumba cha kuishi, Reuben Mollel alisema msichana huyo alikuwa anajulikana kama 'Dada Pendo,' na kwamba maisha yake hayakuwa wazi.

"Alipokuja kupanga hapa alidai kuwayeye ni mwanafunzi, ila hivi karibuni pia alionekana kuwa na mimba, hakuna kilichojulikana tena hadi jana, ambapo nyumba hii ilizingirwa na wanakijiji ambao hatimaye waligundua kitoto kinachodhaniwa kuwa ni chake, kikiwa kimezamishwa kichwa chini, kwenye ndoo ya maji," alisema baba huyo mwenye nyumba.

Taarifa za uwezekano wa kuwepo mtoto katika chumba cha dada Pendo ziliibuliwa na mpangaji mwenzake, Mama Martha Lucas, ambaye alidai kuwa alisikia sauti ya mtoto mchanga akilia usiku kucha na baadae kutoweka majira ya asubuhi.

Hata hivyo, jirani huyo aliamua kutoa taarifa kwa wapangaji wenzake pamoja na wakazi wenginewa Kimandolu, ambao walimuita Mjumbe wa Mtaa wa Kijenge Kaskazini, Gabriel Joseph na pamoja walianza msako wa kukitafuta kichanga hicho, hii ikiwa ni pamoja na kujaribu kuvunja choo cha shimocha nyumba hiyo, wakidhani kuwa mtoto alitupiwa humo.

Baada ya juhudi zao kuambulia patupu, mkazi mmoja wa eneo hilo,Nelson Kweka, alihisi kuwa pengine chumba cha huyo dada hakikukaguliwa vizuri na ndipo alipofunua mfuniko wa ndoo ya maji ya plastiki na kumkuta mtoto mdogo wa kiume akiwa ametumbukizwa humo, na tayari alikuwa ameshakufa.

Hatimaye polisi walipewa taarifa, lakini mara walipofika kwenye eneola tukio, walimkuta dada mtuhumiwa naye akiwa katika hali mbaya kiafya, pengine kutokana na juhudi za kujizalisha mwenyewe usiku.

Dada Pendo alikimbizwa hospitalini Mount Meru, huku mtoto wake ukipelekwa kuhifadhiwa katika nyumba ya maiti hospitalini hapo.

Ofisa Habari wa Polisi mkoani hapa, Rashid Nchimbi alisema polisi wanasubiri afya ya dada huyo itengemae ili aweze kulisaidia jeshi hilo katika uchunguzi zaidi.

-:Habari Leo

ALBINO ATEKWA NA WATU WASIOJULIKANA

Nchini Tanzania katika Kijiji cha Ndami, tarafa ya Mwamashimba wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza watu wasiofahamika wamevunja nyumba na kumteka mtoto mwenye ulemavu wa ngozi maarufu kama albino na kutoweka naye.

Watu hao walivamia nyumba ya wazazi wa mtoto Pendo Emmanuel, mwenye ulemavu wangozi wakiwa na mapanga na kisha kutoweka naye gizani baada ya kuwazidi nguvu wazazi wake.

Emmanuel Shilinde mzazi wa mtoto huyo ameieleza polisi kuwa majira ya saa nne usiku watu wawili waliuvunja mlango wa nyumba yake kwa jiwe wakamchukua mtoto kwa nguvu kisha wakakimbilia gizani kwa pikipiki.

Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi mkoani mwanza Valentino Mlowola , ameitaarifu BBC kuwa leo ni siku ya tatu na polisi bado ina matumaini ya kumpata akiwa hai motto huyo, kwa kuwa bado hawajaupata mwili wake akiwa amepoteza uhai. Msako unaendelea na tayarikuna watu watano wanazuiliwa napolisi ili kusaidia kufahamu mtoto huyo yuko wapi.

Takwimu za kuanzia mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74 wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wamepata ulemavu mwingine wa kudumu.

MIILI 40 YA ABIRIA YAOPOLEWA BAHARINI

Kufuatia kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At, miili arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji unaendelea.

Miili hiyo ilionekana ikielelea karibu na taka za bahari pwani ya Indonesia, eneo la Borneo moja ya eneo la utafutaji mabaki ya ndege hiyo.

Na taarifa kutoka serikali ya Indonesia zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika ndege iliyopotea.

Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa imebeba abiria mia moja na sitini na wawili ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore, ilipotea siku ya Jumapili.

Utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo umeingia katika siku ya tatu, na eneo la utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na tatu hii inashirikisha nchikavu na baharini.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria ikielea majini.

Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.

Baadaye askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini iliopolewa na meli ya kivita.

Mkurugenzi mtendaji wa Air Asia Fernandes aliingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za rambi rambi.

Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini, ndege kumi na tano na chopa saba.

NYALANDU NAE AJITOSA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS

MBIO za urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimechukua sura mpya baada ya jana Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kutangaza rasmi nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka kesho.

Nyalandu anaungana na makada wengine wa CCM wakiwemo mawaziri waandamizi katika serikali ya Rais Kikwete, mawaziri wakuu wastaafu na hata wabunge waliotangaza nia au kutajwatajwa kwa nafasi hiyo, hivyo kuongeza joto la urais ndani ya CCM.

Akizungumza katika mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wake kwenye uwanja wa michezo wa Shule ya Msingi Ilongero Wilaya ya Singida Vijijini jana, Nyalandu mmoja wa waziri vijana, alisema muda wa Tanzania kupata maono mapya umefika.

"Muda wa Tanzania kupata maono mapya umefika, nitachukua hatua ya kuelekea Dodoma kuchukua fomu muda ukifika, maelfu ya watu watanisindikiza,wanawake, vijana, wanawake kutoka mikoa mbalimbali. "Naitazama mpya siku ambayo ndoto yangu itakamilika, Mungu atanyanua vyombo na kushangaza wakubwa. Najua tulikuwa wadogo kama Nazareti, lakini Ilongero imekuwa na mchango mkubwa ambao utakuwa si faida kwa wana Singida bali taifa zima la Tanzania," alisema Waziri Nyalandu.

Alisema kila mtu ambaye ametangaza nia ya kuwania urais ndani ya CCM, lazima kazi zake zipimwe kwa moto.

"Wale wote waliotangaza nia ndani ya chama chetu, kazi zao lazima zipimwe kwa moto na zianikwe hadharani ili mwisho wa siku CCM yenyewe itazipima,"alisema Nyalandu.

Aliongeza kuwa, pindi Rais Jakaya Kikwete atapohitimisha utawala wake, lazima atakabidhi kijiti kwa kizazi kipya, hivyo ndani ya CCM anaamini utakuwa mwaka wa mabadiliko na fikra mpya.

"Tuna wajibu wa kubadili fikra zetu,watu wasimamie Tanzania kuchukua hatua, licha ya ukweli kwamba CCM tuna utaratibu na itikadi zetu,tumeondoa zuio kwa vijana wasiwe waoga…tumejipanga kuwashangaza wengi,"alisema Nyalandu. Wapinzani Alisema muda wa kuwashangaza wengi unaanzia kwa vyama vya upinzani, zikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)."

Katika safari yangu ya miaka ya ubunge, Mungu ametusaidia kusonga mbele, safari moja huanzisha nyingine, nawaomba tusonge tena kwa hatua nyingine, mlianzisha safari yangu ya kisiasa nilikuwa kama mzabibu uliotoa matunda, mkaniita 'Mwanyengu' maana yake mtoto wa tai la kuishangaza dunia.

Safari hii imekuwa ya milima na mabonde kwa pamoja tumeweza, Mungu ameona,Kikwete ameona sawasawa.

"Nikitazama naona nchi hii inahitaji kubadilika kama nyingine zilizopiga hatua, Rais Kikwete amesimama kama jemedari, shujaa, mpambanaji hapa alipofika lazima tuwapongezee," alisema Nyalandu.

Alisema anatambua atapitia kwenye ushindani mkubwa ndani ya chama, ambao utatoa mtu mmoja wa kupeperusha bendera ya chama hicho kugombea urais waTanzania.

"Nawambia wale wote wanaoogopa kushindanishwa ni waoga, siku, saa,mwezi na hata mwaka utakapofika chini ya Kikwete,wachukue fomu na kupeleka kazi zao ili zipimwe," alisema Nyalandu.

Katika mchuano ndani ya CCM, Nyalandu anatarajiwa kuchuana na wanaotajwatajwa, wakiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mawaziri waandamizi, Stephen Wasira (Ofisi ya Rais, Uratibu na Mahusiano), Bernard Membe (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.

Wengine ni wabunge, Dk Hamisi Kigwangalla, William Ngeleja na wengine ambao wanahusishwa, lakini hawajajianika hadharani.

NDEGE YA AIR ASIA YAPOTEA NA WATU 160

Shirika la ndege la Air Asia linasema kuwa limeanzisha shughuli ya kuitafuta ndege yake iliyopoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege dakika 45 baada ya kuondoka kwenye mji wa Surabaya nchini Indonesia.

Zaidi ya watu 160 walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Airbus 320 iliyokuwa safarini kwenda nchini Singapore.

Wengi wa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanatoka nchini Indonesia.

Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.

Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta

KIONGOZI WA AL SHABAAB AKAMATWA

Maafisa nchini Somali wanasema kuwa kiongozi mkuu wa kundi la wapiganaji wa Al shabaab amekamatwa karibu na mji mmoja karibu na mpaka wa Kenya na Somali.

Kamishna wa Wilaya ya El Wak mjini Gedo ameiambia BBC Somalia kwamba vikosi vya usalama vilimkamata Zakariya Ismail Ahmed Hersi katika maficho yake ndani ya nyumba moja baada ya kupashwa habari.

Mwaka 2012 Marekani ilitoa zawadi ya dola millioni 3 kwa yeyote yule ambaye angeweza kutoa habari za Hersi.

Kundi la Al Shabaab limejiondoa kutoka miji kadhaa nchini Somalia tangu uzinduzi wa mashambulizi makali dhidi ya kundi hilo yanayotekelezwa na vikosi vya AMISOM vikishirikiana na wanajeshi wa serikali ya Somalia.

Bwana Hersi alikuwa kiongozi wa kundi la Al shabaab upande wa Amniyat.

Mapema mwaka huu alikosana nakiongozi wa kundi hilo Ahmed Abdi Godane ambaye aliuawa katika mashambulizi ya Marekani mnamo mwezi Septemba.

ATUPWA JELA MAISHA KWA ULAWITI

MFANYAKAZI wa nyumbani, Hatibu Adamu (20) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikanana hatia ya kumlawiti mtoto wa kikewa miaka sita.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Said Mkasiwa alisema kuwa upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi watano na kwamba mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa.

Awali, Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto alidai mahakamani hapo kwamba kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ubakaji nchini, mshitakiwa huyo apewe adhabu kaliiwe fundisho kwa wengine.

Kabla ya hukumu hiyo, Adamu alidai kwamba anasumbuliwa na vidonda vya tumbo hivyo aliomba apunguziwe adhabu. Hata hivyo mahakama hiyo haikusikiliza maombi hayo.

Mshitakiwa huyo ambaye ni mkazi wa Majohe, Dar es Salaam, alidaiwa kwamba tarehe isiyofahamika Septemba, mwaka jana, maeneo ya Majohe Wilaya ya Ilala, Adamu alimlawiti mtoto huyo mwenye miaka sita huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

WAWILI MBARONI KWA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO

WATU wawili wametiwa mbaroni na Polisi mjini Mpanda kwa kukutwa nameno ya tembo waliokamatwa yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 157 ndani ya basi la Adventure.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema vipande vilivyokamatwa ni 22 vyenye uzito wa kilo 46.3 sawa na tembo saba waliouawa.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Justine Baruti (39) mkazi wa kijiji cha Ivungwe – Katumba katika Kambi ya Wakimbizi kutoka nchi jirani ya Burundi iliyoko wilayani Mlele mkoani Katavi.

Mtuhumiwa mwingine ni Boniface Hoza (40) mkazi wa kijiji cha Kalela wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Akisimulia mkasa huo Kidavashari alisema Desemba 24 mwaka huu saa 12:00 alfajiri, askari polisi wakiwa doria katika Kituo Kikuu cha mabasi kilichopo eneo la Mji wa Zamani mjini Mpanda walimtilia shaka mmoja wa watuhumiwa Jusitine Baruti ambaye akiwa na kifurushi tayari kupanda basi la abiria la Kampuni la Adventure.

Inadaiwa kuwa basi hilo la Adventure lenye nambari za usajili T992 DDT lilikuwa limepaki katika Kituo Kikuu cha mabasi mjini Mpanda tayari kwa safari ya kuelekea mjini Kigoma.

"Mtuhumiwa huyu alijaribu kuwatoroka askari hao wa doria lakini walifanikiwa kumkamata na kumweka chini ya ulinzi. Walipopekua mabegi mawili aliyokuwa nayo walikuta vipande 15vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 33.
Vipande hivi kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh 90,000,000 ni sawa na tembo wanne waliouawa," alieleza. Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, basi hilo la abiria liliamriwa kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kilichopo mjini Mpanda ambapo baada ya upekuzi wa kina, mtuhumiwa mwingine Boniface Hoza alikamatwa akiwa ameficha begi kwenye uvungu wa kiti alichokalia chenye namba K3.

Chanzo: Habari Leo

KAMBI YA AU SOMALIA YAVAMIWA NA AL-SHABAAB

Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika nchini Somalia limesema askari wake watatu na kandarasi raia wameuawa katika shambulio lililofanyika katika makao yake makuu mjini Mogadishu.

Taarifa ya Umoja wa Afrika imesema wapiganaji wa al-Shabab waliingia katika kambi wakivalia sare kama askari wa jeshi la serikali ya Somalia.

Taarifa hiyo imesema washambuliaji watano waliuawa na wengine kadha kukamatwa.

Pamoja na kutoa eneo hilo kuwa makao makuu ya majeshi ya kulinda amani ya AU nchini Somalia, eneo hilo lililoimarishwa pia makao ya balozi za Uingereza na Italia.

WAPIGANAJI WA IS WAIDUNGUA NDEGE YA JESHI LA MUUNGANO

Wapiganaji wa Islamic State nchini Syria wamedai kuidungua ndege ya kivita ya muungano wa jeshi unaoongozwa na Marekani.

Shirika linalochunguza maswala ya haki za kibinadamu lenye makao yake mjini London ambalo linaunga mkono upinzani nchini Syria limesema kuwa ndege hiyo ilianguka karibu na mji wa kazkazini wa Raqqa unaodhibitiwa na IS.

Shirika hilo linasema kuwa rubani, raia mwarabu aliyekuwa akiendesha ndege hiyo ametekwa.

Baadhi ya ripoti zinadai kuwa rubani huyo ni raia wa Jordan.

Jordan ni miongoni mwa mataifa ya kiarabu ambayo yanashiriki katika mashambulzi dhidi ya Islamic State.

KATIBU MKUU MASWI ASIMAMISHWA KAZI

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda ,Eliakim Maswi, Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia , Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayokama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatuahiyo "Kwa mujibu wa Kifungu 4(3)(d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)"ambapo "Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.

Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi utakapo kamilika.

Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia imekariri kauli ya Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa jana, Jumatatu, Desemba 22, 2014 ambako Rais alisema:

"Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwana Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa."

Ndugu Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Ndugu Frederick Werema pamoja na Mawaziri wawili walituhumiwa wakati wa Kikao cha Bunge kilichopita kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.

Wakati huo huo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine zinazochukuliwa, Shirika la Umeme (TANESCO) waendelee na majadiliano na IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha tozo la uwekezaji (capacity charge) zaidi ya punguzola awali lililopatikana kupitia Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro ya Kimataifa.

MOHAMMED ALI ALAZWA HOSPITALI

Aliyekuwa bingwa wa ndondi ulimwenguni Mohammed Ali amelazwa hospitalini baada ya kuugua maambukizi ya mapafu.

Ali ambaye ana umri wa miaka 72 na ambaye ana ugua ugonjwa wa Parkinson anadaiwa kuwa katika hali imara.

Msemaji wake amesema kuwa ugonjwa huo uligunduliwa mapema.

Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi na kutaka haki ya faragha ya familia ya bondia huyo mkwongwe kuheshimiwa.

Ali alipataikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka 1984,miaka mitatu baada ya kuustafu katika masumbwi.

Alionekana hadharani katika sherehe moja mnamo mwezi Septemba nyumbani kwake Louisville Marekani wakati wa kutoa tuzo za kibinaadamu za bondia huyo.

MWANAMKE ACHINJWA NA KUTENGANISHWA KICHWA

MKAZI wa kijiji cha Ilalangulu, kata ya Kibaoni wilayani Mlele, ElizabethRichard (16) ameuawa kwa kuchinjwa shingo, kichwa kikitenganishwa na kiwiliwili chake na watu wasiofahamika kisha wakanyofoa sehemu zake za siri na kuondoka nazo.

Aidha watu hao wamemkata mikono yake na titi lake la kushoto kwa kitu chenye ncha kali.

Kamandawa Polisi mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alibainisha kuwa mikono ya Elizabeth na titi lake la kushoto vilifukiwa ardhini karibu na ulikofukiwa mwili wake.

Kidavashari aliongeza kuwa chanzo cha mauaji hayo yaliyotokea juzi, saa 4:00 asubuhi kijijini Ilalangulu inaonekana ni imani za kishirikina.

Kwa upande wake mume wa marehemu, Hevinie Kagembe (45) alidai kuwa asubuhi ya siku hiyo ya tukio aliongozana na mkewe kwenda shambani eneo la Kazarohokulima.

"Mimi na mke wangu kila mmoja wetu ana shamba lake na yako maeneo tofauti," alidai Kagembe. Inadaiwa ilipotimu saa kumi mchana mume wa marehemu alirejea nyumbani kijijini humo lakini hakumkuta mkewe.

"Kawaida ya wanandoa hao , mke alikuwa akirudi nyumbani mapema na kuandaa chakula lakini siku hiyo haikuwa hivyo ... ilipotimu saa mbiliusiku marehemu alikuwa bado hajarejea nyumbani ... mume wa marehemu aliingiwa na mashaka hata alipompigia simu mama mzazi wa marehemu alijibiwa kuwa siku hiyo marehemu hakuwahi kufika nyumbani kwake, " alieleza Kamanda Kidavashari.

Inadaiwa siku iliyofuata saa mbili asubuhi mkazi wa kijijini humo ambaye alikuwa akipita shambani kwa marehemu akielekea shambanikwake kulima aligutuka kuona kifusicha udongo kikiashiria kufukiwa kwakitu ardhini.

Akizungumzia mkasa huyo , shuhuda huyo alieleza kuwa baada ya kuona kifusi hicho cha udongo alichukua kijiti na kuanza kufukua ghafla akaona nywele na hereni ambapo alikimbia kurudi kijijini na kutaarifu uongozi ambao ulilitaarifuJeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari askari Polisi walipofika eneo la tukio waliufukua mwili wa marehemu kichwa kikiwa kimetenganishwa na kiwili chake lakini haukuwa na mikono wala titi la kushoto pia nyeti zake zilikuwa zimenyofolewa.

"Ndipo walipoona dalili ya kufukiwa kitu karibu na ulipofukiwa mwili wa marehemu walipofukua walikuta mikono ya marehemu na titi lake lakushoto vikiwa vimefukiwa," alibainisha Kidavashari.

Kamanda Kidavashari alidai kuwa Jeshi la Polisi linaendesha msako katika maeneo mbalimbali wilayani ili kuwakamata wote waliohusika na mauaji hayo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Chanzo: Habari Leo

MWANAMKE MMOJA AMTUPA MJUKUU WAKE DIRISHANI WAKATI BASI LIKIWA KWENYE MWENDO

Katika hali isiyo kuwa ya kawaida mama moja aliye kuwa akisafiri na mtoto wake mmoja na wajukuu zake wawili, aliamua kumtupa mjukuu wake wa miaka sita dirishani huku basi likiwa katika mwendo kasi na kusababisha kifo chake baada ya kufikishwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Thobias Sedoyeka, amesema mama huyo aliye tambulika kwa jina la Lawaridi Saidi mweye umri wa miaka 46 aliyekuwa akisafiri na basi namba T 981 ALS kampuni ya Salumu Clasc lilokuwa likitokea Dar-es-salaam na kuelekea Kigoma.

Amesema alipofika katika kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama siku ya tarehe 18/12/2014 saa 2 usiku alimtupa mjukuu wake Mayasa meshaki dirisani huku basi likiwa katika mwendo kasi.

Kwa upande wake mganga wa zamu katika hospitali ya mkoa wa Singida Dkt Adamu Hussein amesema walimpokea mtoto huyo akiwa katika hali mbaya akiwa hapumui vizuri na damu kutoka katika masikio, baada ya kumpatia matibabu alilazwa na siku ya pili alifariki kutokana na kupasuka kwa fuvu la kichwa.

Akieleza jinsi alivyo mtupa mjukuu wake huku basi likiwa katika mwendo kasi Lawaridi Saidi ambaye ni mkazi wa Kongowe jijini Dar-es-salaam amesema baada ya kuamka akiwa katika hali ya usingizi alijikuta akimchukuwa mjukuu wakeMayasa na kumtupa dirishani na hatimaye abiria wakaanza kumpiga na kuamuru basi lisimame na kumtafuta mtoto huyo.

MBUNGE ADAI KUVULIWA NGUO WABUNGE WENZAKE BUNGENI

Kufuatia vurugu na purukushani zilizoonekana katika bunge la Kenya wakati wa kupitishwa kwa mswada wa usalama ,mbunge mmoja mwanamke sasa amejitokeza na kudai kwamba wabunge wenzake watatu wanaume walijaribu kumvua nguo.

Mbunge huyo Millie Odhiambo aliandika katika mtandao wake wa facebook kwamba wabunge wengi walipigwa huku yeye akidai kupigwa ngumi machoni na mbunge mmoja kabla ya wabunge wawili kujaribu kumvua nguo.

Hivi ndivyo ujumbe huo ulivyosoma katika mtandao wake wa facebook:''Tulijaribu kulemaza kikao hicho asubuhi yote, Lakini ilipofika mwendo wa saa nane waliwasili wakiwa wamejitayarisha ya kutosha, Wabunge wengi walipigwa. Mimi mwenyewe nilipigwa ngumi machoni na mbunge mmoja huku wengine wawili wakijaribu kunivua nguo. Lakini mimi si wa kulia lia kwamba nimepigwa kofi! Mbunge aliyenipiga amejua kwamba mimi ni mbunge wa Mbita aliyechaguliwa na wala si kuteuliwa, Walipojaribu kunivua nguo mimi mwenyewe niliwamalizia kuwavulia nguo. Mimi siogopi na nashkuru nilivyoumbwa. Sitakubali kutishwa kwa kutumia jinsia yangu'',aliandika bi Millie..

Maandishi haya baadaye yalifuatiwa na mengine yaliosema kuwa ameenda kupigwa picha na kuangaliwa jicho lake hospitali.

RAIS UHURU ASAINI MSWADA WENYE UTATA

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameidhinisha sheria mpya ya usalama ambayo inawezesha majasusi kunasa mawasiliano kisiri au kufanya udukuzi pamoja na kuwazuia washukiwa wa ugaidikwa mwaka mmoja kabla ya kuwafungulia mashitaka.

Kenyatta anasema kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab.

Amesisitiza kuwa sheria hio haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza.

Mnamo siku ya Alhamisi, wabunge wa serikali na wa upinzani walipigana makonde bungeni wakijadili marekebisho kwa mswada kabla ya Rais kuupitisha kuwa sheria.

Katika vurugu hizo mmoja wa wabunge wa upinzani alimmwagia maji naibu spika.

Sheria hizo mpya zilipitishwa na bunge licha ya pingamizi kubwa na vurugu kutoka kwa wabunge hao.

Vyombo vya habari vimesema baadhi ya vipengere vya sheria hio vinabana uhuru wa vyombo vya habari na hata kutishia kwenda mahakamani.

Mswada huo kabla ya kutiwa saini na kufanywa sheria,ulifanyiwa mabadiliko kadhaa katika vipengee ambavyo vilionekana na baadhi ya wabunge kama vilivyokua vikali na kwenda kinyume na katiba.

Polisi sasa watakuwa na jukumu la kuidhinisha taarifa au picha za uchunguzi wa maswala ya usalama na hasa kuhusiana na ugaidi.

Polisi pia ndio watapaswa kuidhinisha picha za waathiriwa wa ugaidi kabla ya kuchapishwa au kuonyeshwa katika vyombo vya habari.

Vyombo vya habari vinasema haya yanakwenda kinyume na uhuru wa vyombo vya habari.

Adhabu itakayotolewa kwa watakaokiuka sheria hii ni hadi faini ya shilingi milioni tano au dola elfu sitini ama kufungwa jela kwa zaidi ya miaka mitatu.

WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA KUMUUA POLISI

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa washitakiwa sita kati ya 14 waliohusika katika mauaji ya askariwa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wa mkoani Morogoro na mfanyakazi wa Benki ya NMB, wakati wa uporaji wa fedha katika eneo la Ubungo Mataa.

Hata hivyo, mahakama hiyo imewaachia huru washitakiwa nane, ambao walionekana hawana hatia kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kutoridhisha.

Washitakiwa waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Mashaka Paulo, John Mdasha, Martine Mdashaa, Haji Kiwelu, Wickliff Limbora na Rashid Abdukadir.

Walioachiwa huru ni Rashid Lembres, Philipo Mushi, Yassin Kanyari, Hamis Daudi, Zinareth Akurike, Emmanuel Lameck, James Chamangwana na Hussein Idd ambao ushahidi uliotolewa dhidi yao haukutosha kuwatia hatiani.

Akisoma hukumu hiyo jana, kuanzia 10: 00 asubuhi hadi saa 12:20 mchana, Jaji Projest Rugazia alisema aliwatia hatiani washitakiwa hao baada ya kusikiliza ushahidi ulitolewa na mashahidi 29wa upande wa mashtaka pamoja navielelezo 78 vilivyowasilishwa mahakamani hapo.

"Maungamo ya washitakiwa, ushahidi wa kitaalamu na utambuziwa washitakiwa katika eneo la tukio, vinaonesha wazi walikuwa nania ya kujaribu kupora Sh milioni 150 mali ya benki ya NMB, zilizokuwa zikisafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro tawi la Wami," alisema Jaji Rugazia.

Alisema katika siku hiyo ya huzuni ya Aprili 20, 2006, washitakiwa hao walilivamia gari kwa lengo la kupora lakini bila ya kuwa na huruma yoyote, walimimina risasi na kuwaua D 6866 Konstebo Abdallah Marwa na mfanyakazi wa NMB tawi la Wami Morogoro, Ernest Manyonyi Alizidi kufafanua kwamba tukio hilo la kusikitisha lilifanyika nyakati za saa 6:30 mchana, eneo la Ubungo Mataa jijini Dar es Salaam kwenye makutano ya Barabara ya Morogoro na Sam Nujoma.

Awali, wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, mahakama hiyo ilitupiliambali vielelezo muhimu vya ushahidi katika kesi hiyo ya mauaji,ikiwemo ripoti saba, kati ya nane za uchunguzi wa silaha zilizotumika katika mauaji hayo.

Ripoti hizo zilitupwa baada ya Mratibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Godfrey Luhamba, ambaye ni mtaalamu wa milipuko, kuiomba mahakama hiyo ipokee ripoti hizo kama vielelezo vya ushahidi wa upande wa mashitaka katika kesi hiyo.

Mawakili wa upande wa utetezi wakiongozwa na Richard Rweyongeza, walipinga ripoti hizo kupokewa, wakidai kuwa ziliwasilishwa kinyume cha sheria kwa kuwa hazikusomwa kwa washitakiwa, wakati wa kuhamisha kesi hiyo kutoka Mahakama ya Kisutu kwenda Mahakama Kuu.

Katika uamuzi wake, Jaji Rugazia alikubaliana na utetezi kuwa ripoti hizo hazikuwahi kusomwa kwa washitakiwa, basi mahakama hiyo haiwezi kuzipokea kwa kuwa uwasilishwaji wake ulikuwa ni kinyume sheria.


Chanzo: Habari leo

MTANZANIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA MAUWAJI YA WANAE

MTANZANIA Charles Mihayo (36), ambaye amechukua uraia wa Australia, amehukumiwa kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuua watotowake wawili wa kike Aprili mwaka huu.

Watoto waliouawa ni Savannah (4) na Indianna (3), ambao Mihayo aliwaua kwa kuwaziba pumzi kwa mto wa kulalia. Vifo vya watoto hao vimeacha simanzi kwani kwa mujibu wa Mihayo, alifanya ukatili huo kutokana na chuki aliyonayo dhidi ya mama wa watoto hao, ambaye ameshatengana naye kwa muda sasa.

Katika uchunguzi wa mauaji hayo yaliyotokea Aprili 20, mwaka huu huko Melbourne, Australia, Mihayoaliwaambia Polisi ilikuwa ni lazima afanye hivyo.

Siku ya mauaji Uchunguzi umeonesha kuwa siku moja kabla ya mauaji, Mihayo alimtumia ujumbe mfupi wa simu mzazi mwenzie akimuomba aone watoto wake kwa mara ya mwisho, na kumwambia kuwa ameshinda.

Katika maandalizi ya kuona watoto hao, ambao walikuwa wapelekwe nyumbani kwa baba yao, Mihayo aliwanunualia nguo mpya na viatu na kisha walipofika kumuona baba yao, aliwavalisha na kucheza nao. Wakati akicheza na malaika hao, Mihayo aliyekuwa akicheza na watoto wake, aliamua kuwaua kwa kuwanyima pumzi kwa kutumia mto wa kulalia.

Baada ya mauaji Baada ya kufanikisha unyama huo, Mihayo aliogesha miili ya watoto wake kisha akaivalisha nguo zao, ndipo akapiga simu Polisi kutoa taarifa.

Hata hivyo, baada ya muda mama wa watoto hao aliyekuwa nje ya nyumba hiyo akisubiri watoto wamalize kucheza na baba yao, aliona kimya na ndipo akaenda kwenye mlango wa mzazi mwenzake na kugonga na kujibiwa asubiri kidogo ataona.

Wakati huo Polisi walifika na kugonga mlango na kisha Mihayo akafungua mlango huku akisema 'nimeshamaliza, nimewaua, nimeua watoto wangu'. Sababu, adhabu Polisi waliofika waliuliza kwa nini ameua watoto wake na Mihayo alimuangalia mzazi mwenzie na kusema "muulizeni huyu".

Ila mwishowe aliwaambia askari Polisi: "Hamtaelewa nini kinanisibu kufanya haya, na hata nikitoa sababu haitasaidia," alisema Mihayo. Baada ya mauaji hayo, familia ya mwanamama huyo ilitoatamko ikisema "hakuna adhabu ya kutosha au kifungo kinachoweza kuondoa huzuni zetu kuhusu tukio hili, tutawakumbuka, na tuliwapenda sana hatutasahau".

"Tunawashukuru wote wanaoendelea kutufariji kwa sala na maombi katika kipindi chote kigumu, tunatoa shukrani zetu kwaPolisi na maafisa washauri waliotusaidia," lilisomeka tamko hilo.

Akisoma hukumu hiyo juzi, Jaji wa Mahakama Kuu ya Victoria mjini Melbourne, Lex Lasry, alisema ukatili uliofanywa na Mihayo ni tukio moja baya ambalo anapaswa kupewa adhabu ya kutumikia miaka 40 jela, na kisha kutumikia kifungo cha maisha.

Alisema ni lazima vyombo vya haki vijifunze kupitia tukio hilo na kubainisha wazazi wenye roho za kikatili kama hiyo ya Mihayo, ili kutoa ulinzi kwa watoto na kuepuka madhara kama hayo yasitokee tena.

AUWAWA KWA WIZI WA KUKU WATATU

MTU mmoja ambaye hajatambuliwa jina lake na pia anakoishi, amekutwa amekufa baada ya kushambuliwa na watu wenye hasira baada ya kushutumiwa kuiba kuku watatu, ambao tayari alikuwa amewachinja huko Dunga vilima viwili wilaya ya Kati Unguja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Juma Sadi Khamis alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Alisema juzi Polisi walipigiwa simu na kupewa taarifa kwamba yupo kijana amejeruhumiwa vibaya na watu wenye hasira kwa tuhuma ya wizi wa kuku watatu.

Alisema Polisi walipofika katika eneo la tukio, walimkuta kijana huyo akiwa amejeruhiwa vibaya, akiwa na kuku watatu waliochinjwa, ambao kwa mujibu wa maelezo ya watu wanaoishi eneo hilo, wameibwa.

"Ni kweli tumepata taarifa ya kijana mmoja anayekisiwa kati ya umri wa miaka 25 ameiba kuku na tulipofika alikuwa katika hali mbaya huku akiwa amekatwa viganja vyake viwilivya miguu yote na tulipomfikisha katika hospitali ya Mnazi Mmoja alifariki muda mfupi," alisema Sadi.

Sadi alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi, kujua chanzo cha tukio hilo na mazingira ya kifo chake na wapi aliiba kuku hao.

"Jeshi la Polisi mkoa wa Kusini linafuatilia zaidi tukio hilo kujua chanzo na mazingira ya kifo cha kijana huyo pamoja na kuwatafuta ndugu wa marehemu," alisema.

WAKURUGENZI 6 WATIMULIWA KWA KUVURUNDA UCHAGUZI

SERIKALI imechukua hatua kali kwa wakurugenzi 17 wa halmashauri mbalimbali nchini, ambapo sita uteuzi wao umetenguliwa, watano wamesimamishwa kazi, watatu wamepewa onyo kali na watatu wamepewa onyo.

Wote hao wamepewa adhabu hiyo kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wao katika kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika Jumapili.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri MkuuTawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Hawa Ghasia alisema hayo Dar es Salaam jana.

Alikuwa akitangaza uamuzi wa serikali dhidi ya wakurugenzi hao, waliosababisha kutokea kwa kasoro na kuvurugika kwa uchaguzi huo na kusababishwa kuahirishwa katika baadhi ya maeneo.

Alisema ofisi yake ilitimiza wajibu wake wa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ukamilifu kwa kutoa miongozo na mafunzo kwa watendaji wa halmashauri na kuwezesha kwa fedha mikoa na halmashauri ili kugharamia maandalizi muhimu, ikiwa ni pamoja na kuandaa vifaa na karatasi za kupiga kura.

"Kimsingi kama maelekezo, miongozo na mafunzo yaliyotolewa yangezingatiwa na kila mmoja, uchaguzi wa Serikali za Mitaa ungefanyika vizuri nchini kote. Wakurugenzi walikuwa wanawajibika kutambua nafasi zao kama wasimamizi wakuu katika kufanikisha uchaguzi huo," alisema.

Alisema kutokana na ripoti walizopokea kuhusu masuala yaliyojitokeza katika uchaguzi huo nidhahiri kwamba wakurugenzi wa Halmashauri zenye dosari, wameonesha udhaifu mkubwa katika kutekeleza jukumu la usimamizi wa uchaguzi, ambalo ni moja ya majukumu ya ukurugenzi

Alisema wakurugenzi hao wametenda makosa ambayo yanawaondolea sifa za kuwa wakurugenzi, ikiwemo kuchelewa kuandaa vifaa vya kupigia kura na kukosa umakini katika kuandaa vifaahasa karatasi za kupigia kura na hivyo kuwa na makosa.

Alitaja makosa mengine kuwa ni kuchelewa kupeleka vifaa kwenye vituo vya kupigia kura, uzembe katika kutekeleza majukumu yao nakutoa taarifa za kupotosha kuhusu maandalizi ya uchaguzi kuwa yamekamilika huku wakijua siyo kweli.

Aidha, alisema wapo waliodiriki kumsingizia Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kuwa alipelekewa nyaraka kwa ajili ya kuzichapa, lakini akazikosea, wakati siyo kweli kwa sababu zilipelekwa kwa watoa huduma binafsi.

"Tumeridhishwa na hatua ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumchukulia hatua mtumishi wake aliyemsingizia Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, ni jambo baya kutenda kosa na kusingizia watu au ofisi zisizohusika. Naelekeza uongozi wa Ilala umwombe radhi Mpiga Chapa Mkuu kwa upotoshaji uliotolewa dhidi yake," alisema.

Alisema, "kutokana na udhaifu waliouonesha wakurugenzi hao, kwamamlaka aliyo nayo chini ya Ibara ya 36(1)(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Rais ameridhia wachukuliwe hatua hizo," alisema.

Aliwataja wakurugenzi sita ambao uteuzi wao umetenguliwa na watapangiwa kazi za taaluma zao wakati uchunguzi zaidi ukiendelea ili kubaini dhamira ya vitendo vyao kuwa ni Benjamin Majoya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuranga, Mkurugenzi Mtendaji wa Kaliua, Abdalla Ngodu na Mkurugenzi Mtendaji wa Kasulu, Masalu Mayaya.

Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti, Goody Pamba, Mkurugenzi Mtendaji wa Sengerema, Julius Madigana na Mkurugenzi Mtendaji wa Bunda, Simon Mayeye.

Aidha, aliwataja wakurugenzi watano wanaosimamishwa kazi ya Ukurugenzi ili kupisha uchunguzi zaidi wa kiwango cha ushiriki wao katika kasoro zilizojitokeza kwenye halmashauri zao kuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hanang', Felix Mabula, Mkurugenzi Mtendaji wa Mbulu, Fortunatus Fwema, Mkurugenzi Mtendaji wa Ulanga, Isabella Chilumba, Mkurugenzi Mtendaji wa Kwimba, Pendo Malabeja na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Sumbawanga, William Shimwela.

Ghasia aliwataja wakurugenzi watatu wanaopewa onyo kali na ambao watakuwa chini ya uangalizi ili kubaini kama wana udhaifu mwingine ili wachukuliwe hatua zaidi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Rombo, Mohamed Maje, Mkurugenzi Mtendaji wa Busega, Hamis Yuna na Mkurugenzi Mtendaji wa Muheza, Jovin Jungu.

Alitaja wakurugenzi wanaopewa onyo na kutakiwa kuongeza umakini wanapotekeleza majukumu yao kuwa ni Mkurugenzi wa Manispaa yaIlala, Isaya Mngulumi, Mkurugenzi wa Hai, Melchizedeck Humbe na Mkurugenzi wa Mvomero, Wallace Karia.

"Nasisitiza kwamba kila kiongozi na mtumishi wa TAMISEMI anao wajibuwa kutekeleza majukumu yake yotekwa weledi na uadilifu ili kuepuka kasoro zinazoweza kuepukwa," alisema.

Aidha, alisema TAMISEMI haina nia ya kuadhibu watendaji wake, lakini haitasita kuchukua hatua stahiki kwa wote watakao kiuka maadili ya kazi au watakao pungukiwa uwezo wa kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa.

Wakati huo huo, matokeo ya jumla ya awali ambayo yametangazwa jana na Tamisemi, yanaonesha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda kwa asilimia 80.58 katika matokeo ya awali ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepata asilimia 13.79 na kinachofuatia ni Chama cha Wananchi (CUF) asilimia 3.6.

Chama cha NCCR-Mageuzi kimepata asilimia 0.19, TLP asilimia 0.03, NLD asilimia 0.00 na ACT asilimia 0.04.

Matokeo hayo yalitangazwa jana na Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa kutoka Tamisemi, Calist Luanda katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Alikuwa akitoa tathimini ya baadhi ya mikoa iliyofanya uchaguzi, halmashauri za miji na majiji. Kwa upande wa Vitongoji, CCM imeshinda kwa asilimia 83.05 ikifuatiwa na Chadema asilimia 13.9, CUF asilimia 36, NCCR asilimia0.09, TLP asilimia 0.03, NLD asilimia 0.00, ACT asilimia 0.02 Alisema katika vijiji 9,047, CCM imepata vijiji 7,290 , Chadema vijiji 1,248, TLP vijiji viwili, NLD vijiji viwili na UDP vijiji vinne.

Kwa upande wa mitaa 3,078 iliyofanya uchaguzi, CCM imeshinda katika mitaa 2,116, Chadema mitaa 735, CUF mitaa 235, NCCR mitaa nane ,TLP mtaa moja, ACT mitaa tisa, UDP mtaa moja na NRA mtaa moja.

Kwa upande wa vitongoji 42,824, CCM imepata vitongoji 35,564, Chadema 5,670, CUF 1,555, NCCR 80, TLP 11, NLD kitongoji kimoja, ACT vitongoji 10.

Alisema uchaguzi katika maeneo mengine, unaendelea na matokeo yatatangazwa baada ya zoezi hilo kukamilika.

Chanzo: Habari leo

WANAJESHI 54 WAHUKUMIWA KIFO

Mahakama ya Nigeria imewahukumu kifo wanajeshi 54 kwa kukataa kupambana na wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram.

Wanajeshi hao, walikutwa na hatia ya uasi, walishtakiwa kwa kukataa kuchukua miji mitatu ambayo ilikuwa imeshikiliwa na Boko Haram mwezi Agosti.

Mwanasheria wa wanajeshi hao alisema maafisa hao 54 watapigwa risasi.


Watano waliachiwa.

Vikosi vya kijeshi vililaumu kwamba havikuwa vimepewa silaha za kutosha na zana za kivita kupambana na Boko Haram.

Kundi hilo limekuwa likifanya mauaji tangu 2009 na linataka kuunda serikali ya Kiislamu kaskazini-mashariki mwa Nigeria.

Zaidi ya watu 2,000 wameshapoteza maisha katika mashambulizi hayo yanayodaiwa kufanywa na Boko Haram mpaka sasa na maelfu zaidi wamekosa makazi kutokana na mapigano hayo.

BODABODA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU

Mwendesha pikipiki(BODABODA) aliyejulikana kwa jina la Zakaria Lungwa(24) mkazi wa Mtaa wa Kawajense Madukani Wilayani Mpanda Mkoani hapa ameuwawa kikatili kwa kuchomwa na vifu tumboni na watu wawili ambao alikuwa akiwafafamu kwa sura na kupolwa pikipiki yake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema mauwaji ya kikatili ya Bodaboda huyo yalitokea hapo majira ya saa saba na robo usiku katika mtaa wa Nsemulwa Kichangani mjini Mpanda Alisema siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa na pikipiki yake aina ya Sanya yenye rangi nyekundu yenye namba za usajiri T.752 CQS akiwa huko kwenye maeneo ya Night Club iliyoko mtaa wa Madini akiwa kwenye shughuli zake za kila siku Akiwa kwenye eneo hilo la Night Club marehemu alipata mteja mmoja wa kiume ambae alimbeba kwenye pikipiki yake na kuelekea Mtaa wa Nsemulwa Kichangani

Kamanda Kidavashari alieleza walipofika katika eneo la Mtaa wa Nsemulwa Kichangani mteja yule aliyempakia alimuamuru marehemu asimame katika eneo ambalo hata alikuwa na nyumba yoyote hapo.

Ghafla katika eneo hilo alitokea mtu mwingine mwanaume na alianza kumwambia marehemu ashuke kwenye pikipiki yake na kisha alimvuta chini pembeni ya barabara.

Alisema baada ya kuona hari hiyo marehemu alipiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani wa eneo hilo hata hivyo hakuweza kupata msaada wowote kutoka kwa majirani wanaoishi kwenye eneo hilo

Mmoja kati ya watu wale wawili alitoa kisu na kisha alimchoma marehemu tumboni na kisha marehemu alianguka chini na watu hao walichukua pikipiki na kisha walitokomea kusiko julikana huku wakiwa wamemuacha marehemu akiwa anagalagala chini akiwa anatokwa na damu.

Kamanda Kidavashari alisema marehemu alipata msaada wa kupelekwa hospitali ya Wilaya ya Mpanda baada ya mtu mmoja aliyekuwa akipita kwenye eneo hilo akiwa na gari lake alipomwona marehemu akiwa anagalagala pembeni ya barabara.

Alisema marehemu baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda alianza kupatiwa matibabu na wakati akiwa anaendelea kupatiwa matibabu ambapo ilipofikia majira ya saa kumi na mbili jioni alifariki Dunia

Kidavashari alieleza Jeshi la Polisi linamshikilia mtu mmoja anaejulikana kwa jina la Khalid Seif (24) Mkazi wa Mtaa wa Nsemulwa kuhusiana na tukio hilo ambae anadaiwa kuwa alionekana katika eneo hilo la Night Club akiwa na mteja aliyeondoka na marehemu

Alisema hata hivyo jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ilikubaini watuhumiwa waliohusika na mauwaji hayo ya kikatili

Kamanda Kidavashari ametowa wito kwa madreva wote wa Bodaboda wa Mkoa wa Katavi wanapo ona kumekuwa usiku kama wamepata mteja basi wawe wanakuwa madreva wawili wanaongozana ilikuweza kusaidiana kama kutatokea tatizo lolote.

Chanzo:Katavi yetu

RAIS KIKWETE AMTEUA MWANASHERIA MKUU MPYA

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Justice Ibrahim Juma kuwa mwanasheria mkuu wa serikali (AG).

Uteuzi huo umefuatia baada yaaliyekuwa mwanasheria mkuu Frederick Werema kutangaza kujiuzulu kutokana na skandali ya mabilioni ya akaunti ya Escrow.

Mapema mwezi huu Rais Jakaya Kikwete pia alimteua Profesa Juma Assad (CAG) kuwamkaguzi na mdhibiti wa hesabuza serikali baada ya Ludovick Utouh kumaliza muda wake.

WABUNGE WACHAPANA MAKONDE BUNGENI KENYA

Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bungeni na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswada tatanishiwa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.

Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badalaya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.

Wabunge wa upinzani walipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.'

Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja aliamuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kwa upande wa upinzani.

Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwa waugaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.

Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.

Pia ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.

Mswada huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab wakilalamika na kutaka wanajeshiwa Kenya kuondolewa Somalia

Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangui mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.

MWANASHERIA MKUU ANG'OKA

WAKATI Watanzania wakisubiri kusikia uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete juu ya maazimio manane yaliyotolewa na Bunge kuhusu sakata la uchotaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu wadhifa huo.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, iliyotolewa jana na Mkurugenzi wake, Salva Rweyemamu kwa vyombo vya habari imethibitisha kujiuzulu kwa Werema kuanzia jana.

Amekuwa kwenye wadhifa huo tangu mwaka 2009, alipochukua nafasi ya Johnson Mwanyika aliyestaafu. Taarifa hiyo iliongeza kuwa Rais Jakaya Kikwete amekubali ombi la kujiuzulu kwa mwanasheria huyo.

Kabla ya kugeukia taaluma ya sheria, Werema alikuwa mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert jijini Dar es Salaam kati ya mwaka 1979 na 1980.

Kabla ya kuwa Mwanasheria Mkuu, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tangu 2007 mpaka 2009. Mwaka 2004 hadi 2006 alikuwa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Werema alihitimu Shahada ya kwanza ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1984 na shahada ya pili ya sheria mwaka 1993 katika Chuo Kikuu cha American, Washington DC nchini Marekani.

Kisa ni Escrow "Katika barua yake kwa Mheshimiwa Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusu suala la Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa iliongeza kuwa Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu. Katika Mkutano wa 16 na 17 wa Bunge uliohitimishwa Novemba 28, mwaka huu, moja ya mambo makubwa yaliyoibuka na kuzua mjadala mzito ni sakata la uchotwajiwa fedha katika akaunti ya Escrow, kiasi cha kutaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali, baadhi ya mawaziri na watendaji Serikali wajiuzulu.

Bunge liliazimia Jaji Werema kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria kutokana na kuipotosha Serikali kuhusu malipo ya Sh bilioni 306 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow, akishauri fedha hizo zilipwekwa Kampuni ya IPTL iliyo na mkataba wa ufuaji umeme na Tanesco bila ya kukata kodi.

Hata hivyo, Jaji Werema hakusalimu amri wakati Bunge likijadili tuhuma dhidi yake, akisema anaamini alichofanya na kutaka abebeshwe msalaba na wakati fulani alishiriki kupendekeza jinsi ya kufikia maazimio ya Bunge dhidi ya watuhumiwa.

Aidha, alilalamikia uamuzi wa Bunge uliokuwa umependekeza yeye na baadhi ya vigogo wachukuliwe hatua, akidai kuwa haukuwa wa haki kwa wote waliotuhumiwa na ulifanywa kwa hasira na kufuata mkumbo.

Akizungumzia maazimio ya Bunge katika sakata la uchotaji wa fedha hizo, Jaji Werema alisema: "Kilichofanywa na Bunge ni mob justice (uamuzi wa kufuata mkumbo) kwa sababu hata waliowatuhumu, hawakupewa nafasiya kujieleza.

(Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna) Tibaijuka na (mmiliki wa hisa za IPTL, James) Rugemalira hawakusikilizwa lakini wamehukumiwa… ilionekana dhahiri jinsi Bunge linavyoingilia uhuru wa Mahakama kwa kutoizingatia hukumu ya Jaji (John) Utamwa.

"There was no justice at all (hakukuwa na haki kabisa).

Bado haijathibitika ukweli kuhusu fedha zile kama ni za umma au la. Ninyi waandishi bado mna nafasi ya kufanya uchunguzi ili muwaeleze wananchi ukweli kuhusu wasichokijua," Akijizungumzia yeye mwenyewe, alisema: "Nitasimama mwenyewe kujitetea, lakini nawaomba, tafadhalini msichafuane.
Acheni kutoa makaratasi na vitabu. Kesi hii inaendeshwa kiuchunguzi. Tuache kuchafuana."

Aidha, katika hilo, alisisitiza kuifuata Katiba ya nchi akisema ndio mwongozo unaokubalika. Werema alitaka pia Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iueleze umma ili kuondoa sintofahamu iliyopo juu yammiliki halali wa fedha zilizokuwamo katika akaunti hiyo.

Bunge lilihitimisha mjadala wa kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow, kwa kupitisha maazimio manane, ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Bunge hilo pia lilipendekeza kuwajibishwa kwa wajumbe wa Bodiya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme (Tanesco) na lilipendekeza kuwavua nyadhifa zao wenyeviti watatu wa kamati za kudumu za Bunge ambao ni mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja na Kamati ya Bajeti, Andrew Chenge.

Akisoma maazimio hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe alisema kuwa baadhi ya watu waliochukua fedha hizo ni viongozi wa umma na maofisa wa Serikali kama mawaziri, majaji, wabunge, wenyeviti wa kamati za Bunge, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi.

Maazimio yaliyopendekezwa ni pamoja na kulitaka Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuchukua hatua stahiki kwamujibu wa sheria za nchi ili kukabiliana na kile kinachoonekana kuwa ni rushwa katika utoaji wa mabilioni yaliyokuwemo katika akaunti hiyo.

Azimio la tatu lilikuwa ni kuzitaka Kamati za kudumu za kuwavua nyazifa zao za wenyeviti wa kamati husika za Bunge kabla ya mkutano wa 18 wa Bunge hilo na la nne likiwa ni kumwomba Rais aunde tume ya kijaji kuchunguza tuhuma za ukiukwaji wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

MBWEMBWE WAKATI WA KUMPOSA MPENZI WAKE ZAMTOKEA PUANI

Mwanamume mmoja raia wa udachi amejikuta akikimbilia usalama wake baada ya jaribio la kutaka kumposa mpenzi wake kwa mbwembwe kwenda mrama.

Mtu huyo ambaye hakutajwa kwa jina anayeishi mjini Ijsselstein alikodisha 'kreni' au Crane na kuipanda akipanga kwamba kreni hilo imtoe chini na kumpandisha hadi dirishani mwa mpenzi wake ambapo angemchezea wimbo na kisha kumposa.

Badala yake yaliyomkuta hakuyatarajia kabisa.

Kreni hiyo ilianguka chini na kupita dirishani kwa mpenzi wake huku ikiangukia nyumba za majirani.

Mwanamume huyo alilazimika kukimbilia usalama wake na hakuna aliyejeruhiwa katika tukiohilo lililowaacha wengi wakiangua kicheko.

Kwa mujibu wa jarida la Algemeen Dagblad, mpenzi wake mwanamume huyo alimkubali nakusema yuko radhi kuolewa naye licha ya tukio hilo.

Baada ya kuongea na polisi, wawili hao walisafiri kwenda mjini Paris Ufaransa kusherehekea.

Kreni hio ilianguka tena kwa mara ya pili ilipokuwa inainuliwa na hata kuharibu zaidi nyumba zamajirani. Meya wa mji huo, amezomewa na wengi baada ya eneo hilo kusemekana kutokuwa salama.

TALIBAN YAUA 100 SHULENI, WAKIWAMO WANAFUNZI 80

Takriban watu 100 wakiwemo wanafunzi 80 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya wapiganaji wa Taliban kuvamia shule moja inayosimamiwa na jeshi huko Peshawar kaskazini - magharibi mwa Pakistan.

Wakuu wa Hospitali wanasema kuwa zaidi ya watu 40 wanasemekana kujeruhiwa japo idadi hiyo inatarajiwa kupanda zaidi.

Maafisa mjini Peshawar wanasema kuwa wanaume watano ama sita waliokuwa na silaha waliingia shuleni hapo wakiwa wamevalia magwanda ya kijeshi.

Wanafunzi mia tano na waalimu walikuwa katika shule hiyo ya umma ya kijeshi wakati sham,bulizi hilo lilipotokea.

Wakazi wa eneo hilop wanasema kuwa walisikia milio ya bunduki iliyodumu kwa dakika kadhaa.

Wanasema pia kuwa walisikia sauti za kelele za wanafunzi na waalimu.

Haijabainika wazi ni kwa namna gani wanamgambo wa Talebain waliweza kupenya hadi kuingia ndani ya majengo hayo yanayomilikiwa na jeshi.

Jeshi la Pakistan limesema operesheni ya uokozi ilikuwa ikiendelea na kwamba wengi wa wanafunzi na waalim wameokolewa toka eneo la hatari.

Shambulio hilo limetokea wakati operesheni kubwa ya kijeshi ikiendelea dhidi ya wapiganaji waTaleban wa Pakistan na wanamgambo wengine wanaoendesha harakati zao kaskazini mwa jimbo la Waziristan.

MGANGA WA KIENYEJI AWACHOMA MOTO WATEJA WAKE

Mganga wa tiba za asili, Omari Kikukwa (32) mkazi wa Kijiji cha Bondo , Kata ya Mswaki wilayani hapa anashikiliwa na polisi kwa kuwachoma moto wateja wake na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Aziza Hassani (35) mmoja wa mwanafamilia aliyenusurika kwenye mkasa huo akisimulia kuwa ilikuwa tarehe 27 mwezi uliopita yeye, mama yake pamoja na watoto wake wawili walipelekwa kwa mganga wa kienyeji na baba yao wa kufikia kwa ajili ya kufanyiwa tambiko.

Alisema kuwa walifika kwa mganga huyo na kuanza kufanyiwa dawa ambapo ilifanyika ndani ya shimo ambalo liliezekwa nyasi kavu juu yake na kuachwa nafasi ndogo kwa ajili ya kuingilia ndani ya shimo hilo waliloambiwa ndiko dawa inatakiwa kufanyika huku baba yao akibaki nje na mganga.

Anaeleza kuwa baada ya muda walidhani mganga ameshamaliza na kumuuliza wanaweza kutoka ila aliwajibu dawa bado inaendelea ambapo ghafla mganga huyo aliwasha moto juu ya zile nyasi na moto mkubwa ukaanza kuwaka ndipo akawaamrisha watoke shimoni huku moto ukiendelea kuenea hadi mlangoni.

Alisema ilibidi aanze kumrusha nje mwanaye mdogo Hassani Rajabu (4) halafu kuanza harakati kwa ajili ya kumsaidia mama yake na mwanaye Zuhura Rajabu ambapo hakufanikiwa kutokana na motokuwa mkubwa hivyo yeye aliungua kichwani huku mama yake na mwanaye miili yao ikiwa imeungua vibaya.Alisema baada ya moto kupungua walitoka huku wenzie wakiwa hawajiwezi kabisa ambapo baba yake na mganga walimkataza wasipeleke majeruhi hospitali ila kuna daktari wao anakwenda kuwatibu katika kijiji cha jirani na hapo.

Aziza alisema huko kwa huyo daktari hakuna kilichofanyika kwa siku tatu hadi kufikia Desemba mosi mama yake Hadija Abdallah(65) alifariki dunia hapo hapo kijijini huku hali ya mwanaye nayo ikizidi kuwa mbaya kutokana na kukosa tiba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fraisser Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa amekamatwa na tayari ameshafikishwa mahakamani Desemba 8 mwezihuu kwa kosa la mauaji na kujeruhi kwa moto watu watatu.


Chanzo:Mwananchi

AMKATA MKE WAKE MASIKIO YOTE KUTOKANA NA WIVU WA MAPENZI

POLISI mkoani Katavi inamsaka mkazi wa kijiji cha Majimoto wilayani Mlele, Ndomo Mwandu (32) akituhumiwa kumsababishia ulemavu wa kudumu mkewe wa ndoa Agnes Sikazwe (28) kwa kumkata masikio yote mawili kwa kisu akiwa amelala.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari akithibitisha mkasa huo ambao umetokea hivi karibuni kijijini humo usiku wa manane kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.

"Tunaendelea kumsaka kwa udi na uvumba mshtakiwa huyu ambaye baada ya kumkata mkewe huyo masikio yake akitumia kisu na kumsababishia ulemavu wa kudumu maishani.....baada ya kumkata alikimbia na masikio hayona kutokomea kusikojulikana," alieleza Kamanda Kidavashari.

Akisimulia unyama huo, Kidavashari alieleza kuwa mara kwa mara mtuhumiwa alikuwa akisikika akimtuhumu mkewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine, lakini mkewe huyo siku zote alikuwa akikanusha kwa nguvu zake zote.

PACQUIAO NA MAYWEATHER KUCHAPANA MAY 2

Bondia Floyd Mayweather ametaja tarehe 2 mwezi May mwaka 2015 kama siku ya piganokati yake na Manny Pacquiao.

Kulingana na gazeti la Daily mail nchini Uingereza ,uvumi kwamba pigano hilo ambalo litakuwa la kiwango kikubwa cha malipo kuwahi kutokea katika historia ya ndondi ulianza pale Pacquiao alipoonyesha mchezo mzuri kati yake na Chris Algieri mjini Macauwiki mbili zilizopita.

Na sasa Maywheather kupitia kampuni yake moja ya mauzo amesema kuwa yuko tayari kupambana na Pacman katika pigano lake linalokuja.

Bondia huyo ambaye ndiye mwanamichezo tajiri duniani amesema kuwa mashabiki wa ndondi wamesubiri sana pigano hilo na sasa yuko tayari.

''Kizuizi kikubwa cha pigano hilo ni promota wa Pacquiao Bob Arum ,lakini najua kwamba sisi sote tunalihitaji pigano hili'',alisema Mayweather.. Kwa hivyo ni wakati lifanyike.

Mayweather alikiri kwa mara ya kwanza majadiliano yanaendelea kwa siri na kuongeza kwamba hamuogopi mtu yeyote.

''Miaka iliopita tulikuwa na tatizo la kupimwa mikojo na damu, swala ambalo Pacman amekuwa akilipinga'' aliongezea Mayweather.

Hata hivyo upande wa Mayweather ni vile kitita cha pigano hilo kitakavyo gawanywa.

Inakadiriwa kuwa pigano hilo litagharimu dola millioni 300.

Upande wa Pacman tayari umekubali fedha hizo kugawanywa kwa 60-40 huku Mayweather akichukua kitita kikubwa, ijapokuwa kuna madai kwamba Mayweather huenda akadai asilimia kubwa zaidi iwapo makubaliano yataafikiwa.

MPANDA DC WAMALIZA UJENZI WA MAABARA

HALMASHAURI ya Mpanda katika Mkoa wa Katavi imetekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete kwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vyote 17 vya maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi katika shule sita za sekondari wilayani humo, ujenzi uliogharimu zaidi ya Sh milioni 568.6.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda, Estomihn Chang'ah alimweleza Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima kuwa utekelezaji wake umefikia asilimia 90 ambapo kazi iliyobaki ni kuweka vifaa vya maabara tu katika majengo hayo.

Alieleza kuwa ujenzi wa maabara hizo ulianza Januari 14 mwaka huu na kwamba zaidi ya Sh milioni 688.3 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi huo wa maabara. Hata hivyo zaidi ya Sh milioni 568.6 zimetumika.

Alizitaja shule hizo ambazo zimekamilisha ujenzi wa majengo ya maabara hizo kuwa ni pamoja na Mwese, Karema, Ikola, Mpandandogo, Ilandamilumba na Kabungu.


Chanzo: Habari leo

MUUZA CHIPS ATUNUKIWA NISHANI NA RAIS KIKWETE

MUUZA chipsi wa Dar es Salaam, Kassim Said (28), alivuta hisia za waalikwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Jakaya Kikwete, juzi jioni kwenye sherehe za kutunuku nishani, baada ya kupewa Nishani yaUshupavu, aliouonesha baada ya kumpiga jambazi kwa chepe na kufanikisha kukamatwa kwake.Sherehe za kutunuku nishani hizo zilifanywa juzi katika viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam ambapo Rais Kikwete aliwatunuku nishani viongozi na raia 28, walio hai na wafu, ambao katika uhai wao walikuwa na sifa zinazokidhi matakwa ya nishani husika.Nishani ya Ushupavu aliyopewa Kassim, hutolewa kwa maofisa wa majeshi ya ulinzi na usalama na watu wengineo kwa vitendo vya ushupavu walivyoonesha, ambapo Kassim yeye alionesha ujasiri wa kumpiga jambazi kwa chepe, kisha kuzirai na kurahisisha kukamatwa kwake.

Akisimulia tukio hilo, mara baada ya kuvalishwa nishani hiyo na Rais, Kassim alisema anakumbuka ilikuwaJulai 7, mwaka jana saa 3 usiku eneo la Buguruni Malapa, ambapo akiwa kwenye eneo lake la kazi ya kuuza chipsi kama mwajiriwa, alikuja jambazi huyo na kujidai ni mteja.

Baada ya muda jambazi huyo alitoa silaha na kuanza kutishia wateja na baadhi ya wateja walikimbia huku na huko, huku bosi wake akitishiwa kwa silaha kichwani, ndipo akapata wazo la kuchukua chepe na kumpiga nalo mara mbili kichwani na ndipo jambazi huyo akaanguka na kupoteza fahamu.

Tukio hilo lilisababisha iwe rahisi kuchukua silaha aliyokuwa nayo na kisha polisi walifika na kuondoka na mtuhumiwa na kijana huyo kwenda kutoa maelezo Polisi ya jinsi alivyofanikisha tukio hilo, lisilete madhara makubwa.

"Niliwaza sasa kama huyo jambazi atachukua na hizo hela, ina maana mimi leo sitapata kitu, ujira wenyewe ni mdogo halafu niukose, nikaona njia pekee ni kumdhibiti huyo jambazi ili asilete madhara zaidi, na kweli nilifanikiwa", alisema Kassim.

Katika hatua nyingine, watunukiwa 27 walipokea nishani zao, ambapo baadhi yao ni marehemu ambao waliwakilishwa na ndugu na jamaa zao.

Katika nishani hizo, Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alikuwa miongoni mwa watunukiwa wa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50, ya Muungano Daraja la Pili.

CIA YATUHUMIWA KWA MBINU ZAKE ZA MATESO

Ripoti ya Seneti Marekani imekosoa vikali mbinu zinazotumiwa na CIA, kuwahoji washukiwa wa uhalifu, kwamba ni za kikatili na zisizofaa.

Ripoti ya kamati ya bunge la Seneti nchini Marekani imekosoa vikali mbinu zinazotumiwa na Shirika la Ujasusi la nchi hiyo za kuwahoji washukiwa wa uhalifu na kuelezea kwamba ni za kikatili na zisizofaa.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama ya bunge la seneti Dianne Feinstein amesema katika baadhi ya matukio wanavyotendewa washukiwa hao ni sawa na mateso.

''Watu waliowekwa kizuizini walipaswa kutii mbinu zilizokuwa zikitumiwa, kuvuliwa nguo na kuachwa watupu, walikuwa wakiwekwa katika hali ya mateso ya muda mrefu.

Walikuwa wakizuiwa kulala kwa siku kadhaa, hadi saa 180- ikiwa ni sawa na siku saba na nusu, zaidi ya wiki bila ya kulala, kawaida wakiwa wamesimama au katika hali ya kuwachosha na wakati huohuo mikono yao ikiwa imefungwa pamoja juu ya vichwa.

Mbonu hizo za utesaji zilianzishwa baada ya shambulio la kigaidi la Septemba 11, mwaka 2001 nchini Marekani...''

Mbinu hizo zinazotumiwa na shirika hilo la ujasusi zimeelezwa na wabunge hao wa seneti kuwa zinamapungufu na kwamba CIA imekuwa ikitoa taarifa zisizo sahihi kwa umma.

KABILA AINGIZA WAPINZANI SERIKALINI

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila amebuni serikali ya Muungano ambayo inajumuisha viongozi kadhaa wa upinzani.

Afisaa mkuu wa chama cha upinzani cha '' Movement for the Liberation of Congo'' ametajwa kama naibu waziri mkuu.

Viongozi wengine wa zamani wa upinzani pia wamepewa nyadhifa katika serikali hio.

Serikali hio ya Muungano, imebuniwa huku kukiwa na wasiwasi kuwa Bwana Kabila, ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka 2001, anaweza kujaribu kubadilisha katiba ili awanie muhula wa tatu.

Wadadisi wanasema kuwa kujumuishwa kwa wapinzani katika serikali ya muungano inawezekana ni njama ya kuongeza ufuasi wake na kudidimiza upinzani.

Wanaongeza kuwa hatua ya Kabilani ya kujiandaa kwa mageuzi ya kikatiba au hata kuchelewesha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2016.

Evariste Boshab, kiongozi wa chama cha (People's Party for Reconstruction and Democracy), pia ametajwa kama naibu waziri mkuu.

ALIYOTOROSHA TWIGA JELA MIAKA 60

HATIMAYE Mahakamaya hakimu mkazi Moshi, mkoani Kilimanjaro, imemhukumu miaka 60 jela, Kamran Ahmed, raia wa Pakistani kwa kosa la kutorosha wanyama hai 153, wakiwemo Twiga wanne Hata hivyo mtuhumiwa huyo mpaka sasa haijulikani alipokimbilia baada ya kutoweka hapa nchini tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi mfawidhi ,Simoni Kobelo, alisema Mahakama hiyo imewaachia huru Watanzania watatu baada ya kutokuwapo kwa ushahidi wa kuwatia hatiani.

Kobelo, alisema Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na dhidi ya mtuhumiwa huyo na kumtia hatiani kwa makosa yote manne yaliyowasilishwa na Jamhuri Kobelo alisema Mahakama imewaachia huru Watanzania watatu ambao ni Hawa Mang'unyuka, Mathew Kimathi na Michael Odisha Mrutu kwa sababu ya Jamhuri kushindwa kuthibitisha ushahidi stahiki.

Alisema ushahidi uliowasilishwa haukuonesha kuwaunganisha washitakiwa hao moja kwa moja na kosa la kusafirisha wanyama hai nje ya nchi.

Katika hukumu hiyo, Kamran, alikutwa na makosa manne, kushiriki na kula njama ya kutenda uhalifu kinyume cha kifungu 57 (1), sehemu ya 4(1), sura ya kwanza ya kosa la uhujumu uchumi na kushiriki utoroshaji wa wanyama hai wenye thamani ya shilingi milioni 170.5

Kosa la pili ni kufanyabiashara ya kukamatana kusafirisha wanyama hai wakiwemo Twiga, Chui, Pofu, Punda Milia, Swala ndege wa aina mbalimbali, Duma, Nyati bila leseni.

Kosa la tatu ni kukutwa na Nyara za Serikali katika uwanjawa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Novemba 26, mwaka 2010 na kosa la nne ni la kuisababishia serikali hasara ya Dola 113.7 kwa kufanya biashara kinyume cha sheria.

Kuhusu mshitkakiwa wa pili Hawa Mang'unyuka anayetajwa kuwa mmiliki wa kampuni ya Harm Marketing na Luwego Bird Trappers, inayodaiwa leseni yake kutumika kuhalalisha ukamatajina utoroshaji huo, Hakimu Kobelo alisema kwa mujibu wa vielelezo vilivyowasilishwa kampuni ya Hawa, ilipewa kibali halali cha kukamata wanyama hai na mamlaka husika Washitakiwa Mathew Kimathi na Michael Mrutu, Kobelo alisema kwa sababu hakuna sehemu yoyote inayoonesha ushiriki wao katika utoroshaji zaidi kutekeleza wajibu wao kama walivyoekezwa na wakuu wao wa kazi kipindi hicho.

Machi mwaka huu Mahakama ya HakimuMkazi, ilitoa amri ya kukamatwa ndani ya saa 24, mshitakiwa namba moja(Kamran)baada yakushindwa kuhudhuria mahakamani hapo kwa zaidi ya vikao viwili mfululizo.

Amri ya kukamatwa kwa raia huyo wa Pakstani ilitolewa Machi 23 mwaka huu Hakimu Kobelo baadaya kutoa hati ya kukamatwa kwa raia huyo kufuatia ombi lamawakili wa upande wa Jamhuri kuomba hati hiyo kutolewa kutokana mshitakiwa kutofika mahakamani.

Kutoroka kwa mtuhumiwa huyo kuliilazimu Mahakama kutoa hati ya hati ya kukamatwa (Arrest warrant) kwa wadhamini wawili wa mshitakiwa huyo ambaye ilidaiwa tayari ametorokea nje ya nchi.

Wadhamini waliotajwa mahakamani hapo , Jackson Kimambo na Peter Temba,ambao awali walipewa wito wa kufika mahakamani hapo kutoa uthibitisho wa uwepo wao ikiwa ni pamoja na kusaidia mahakama kumpata mshitakiwa huyo kama walivyosaini katika hati yao ya udhamini.

Hata hivyo Mdhamini mmoja Peter Temba ndiye alikamatwa na kuhukumiwa kifungo jela na Jackson Kimambo hakukamatwa.

Kesi hiyo iliyokuwa na mvuto wa kitaifa na kimataifa, Novemba 25 mwaka 2010 watuhumiwa hao wanadaiwa kula njama ya kusafirisha nje ya nchi zaidi ya wanyama hai na ndege 100 wakiwemo Twiga wanne ambao thamani yake inakadiliwa kufikia dola za marekani 113,715.

Kamran amebainika kutenda kosa la kusafirisha wanyama hai kwenda Doha, nchini Oman kwa kutumia ndege aina ya C.17 yenye nambari AMA/MAB mali ya shirika la Qatar Airways.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka ni kwamba wanyama hao, walisafirisha kwenda Falme za Kiarabu baada ya kupita vizuizi yakiwamo mageti ya namba 5A na 5B katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Chanzo: Tanzania Daima

WAANDISHI WA HABARI WAZUIWA KUINGIA MAHAKAMANI KESI YA IPTL

KATIKA hali ya kushangaza, Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara imewazuia waandishi wa habari kuingia mahakamani kusikiliza maombi ya kampuni ya Pan Africa Power Solutions (PAP) na Kampuni ya Independent Power Tanzania (IPTL) kwa Bodi ya Rufaa yaKodi nchini, kutaka Kamishna Mkuu wa TRA akamatwe na kupelekwa gerezani.

Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, waliofika mahakamani hapo jana kusikiliza maombi hayo, walishindwa kusikiliza kinachoendelea baada ya kuambiwa kuwa waandishi wamezuiwa kusikiliza.

Mmoja wa makarani wa mahakama hiyo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa hawaruhusiwi kusikiliza maombi hayo, lakini hakuwaeleza sababu.

Maombi yenyewe Juzi PAP na IPTL ziliwasilisha maombi kwa Bodi ya Rufaa ya Kodi (TRAB) zikitaka iamuru Kamishna Mkuu wa TRA, akamatwe kwa kukiuka amri wa Bodi hiyo iliyozuia kufuta hati za kuthibitisha ulipaji wa kodi wa kampuni hiyo, katika mauzo ya hisa za IPTL.

Hatua ya TRA kufuta hati hizo ilitokana na madai kwamba PAP ilifanya udanganyifu kwa kuwasilisha nyaraka za kughushi za ununuzi wa hisa, zinazodaiwa kuiwezesha kukwepa kodi ya Sh bilioni 8.68.

Maombi ya kampuni hiyo inayomilikiwa na Harbinder Singh Seith, yaliwasilishwa chini ya hati yadharura, yakiambatana na kiapo cha Mkurugenzi Mwendeshaji wa IPTL, Parthiban Chandrasakaran.

Kamishna Mkuu wa TRA anadaiwa kukaidi amri halali iliyotolewa na bodi hiyo Novemba 26 mwaka huu, iliyozuia kwa muda kuziondoa hati hizo.

"Tunaomba bodi imwamuru Kamishna Mkuu wa TRA kutekeleza amri iliyotolewa, pia bodi itoe amri ya kuondoa barua ya Kamishna ya Novemba 27 mwaka huu ambayo ilifuta hati za kodi, mpaka maombi ya msingi yatakaposikilizwa," ilidai hati hiyo ya maombi.

Hati za PAP zilizofutwa zilitolewa kwa ajili ya uuzaji wa hisa saba za IPTL kutoka Kampuni ya Mechmar kwenda Piper Links Investment, na ununuzi mwingine wa hisa hizo hizokutoka kampuni ya Piper Links kwenda PAP.

Historia ya hati Katika hati hiyo ya kiapo, Chandrasakaran alidai Desemba 23 mwaka jana walipata hati hizo za kuthibitisha walilipa kodi kwa ajili ya uuzwaji wa hisa hizo.

Anadai kwamba Novemba 19, walalamikiwa (TRA) walitoa taarifa ya siku sita kwa BRELA wakionesha nia ya kuziondoa hati hizo, kwa mazingira kwamba walalamikaji walipata mkataba feki wa mauzo ya hisa hizo.

"Kamishna si tu anabanwa na mamlaka, pia anatakiwa kufuata sheria za nchi zikiwamo za bodi, kwa kukiuka amri anapoteza sifa za kuendelea kushikilia nyadhifa hiyo aliyonayo," alidai Chandrasakaran katika hati ya kiapo.

Hata hivyo, kutokana na maombi hayo kuwasilishwa chini ya hati ya dharura, bodi hiyo mbele ya Katibu wake, Respicius Mwijage iliamuru yasikilizwe jana, lakini waandishi wakatimuliwa.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), ameelezea kushangazwa na madai ya Seith, aliyokaririwa hivi karibuni katika vyombo vya habari, kuwa suala la Akaunti ya Tegeta Escrow na umilikiwa Kampuni ya IPTL lilivyoendeshwa na Bunge, limesababisha atafakari kama ataendelea kuwekeza Tanzania au la.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya NCCR Mageuzi jana, Kafulila alidai kuwa Seith hapaswi kutafakari kwa kuwa yeye sio mwekezaji na anapaswa kukamatwa na vyombo vya dola, kujieleza namna alivyonunua IPTL.

" Ripoti ya CAG imebainisha wazi kuwa Seith alinunua IPTL kwa nyaraka za kughushi ambalo ni kosa la jinai," alisema. Hata hivyo, Seith amekuwa akisisitiza kuwa ununuzi ulifanywa kwa kihalali bila kukiuka sheria.

Aidha, Kafulila pia alisema NCCR-Mageuzi, imeanza tena ziara mkoani Kigoma kuendeleza kampeni zake za kuhamasisha wananchi kupigia kura viongozi wa chama hicho, katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Jumapili ya wiki ijao.

Kafulila anasema kampeni hizo zinaanza kesho hadi wakati wa uchaguzi na NCCR itatumia fursa hiyo kuwahabarisha wananchi kuhusu sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow na umiliki wa Kampuni ya IPTL.

Chanzo: Habari Leo

AJIFUNGUA MTOTO AKIWA NA SURA YA CHURA

MKAZI wa kijiji cha Chibwechangula –Behelo katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Ruth Matonya (26)amejifungua mtoto wa ajabu ambaye nusu ya sura yake inafanana na binadamu na nusu ikifanana na chura.

Mtoto huyo alizaliwa Desemba 2, mwaka huu katika Kituo cha Afya cha Mtakatifu Luka kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mpwapwa. Alifariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk Edwin Kihura mara baada ya mama huyo kufika katika kituo hicho cha afya alikuwa na uchungu ambao haukuwa na kikomo, lakini alishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida licha ya njia ya uzazi kufunguka.

Alisema kutokana na hali hiyo iliwalazimu kumfanyia upasuaji mama huyo kwa lengo la kuokoa maisha yake na mtoto. Alisema wakati mama huyo akihudhuria kliniki walipojaribu kupima miezi yamwisho mama huyo, mkao wa mtoto ulikuwa haupatikani pamoja na mapigo ya moyo lakini mtoto alikuwa anacheza tumboni jambo ambalo lilikuwa likiwashangaza waganga na wauguzi kituoni hapo.

Dk Kihura alisema mara baada ya mama huyo kufanyiwa upasuaji waliweza kutoa mtoto wa jinsi ya kike ambaye alikuwa na sura isiyoeleweka na kichwa kilikuwa na sura ya binadamu na nusu ikiwa ni sura inayofanana na chura huku viungo vingine vyote vya mwili vikiwa kamili.

Alisema zipo sababu kadha zinazoweza kusababisha tatizo kamahili ambapo alisema kuwa ni baadhiya akina mama kukosa baadhi ya madini mwilini na uumbaji kutokamilika kutokana na sababu za kibaiolojia.

Alieleza kuwa hali ya mama huyo inaendelea vizuri na kwamba mtotohuyo alikuwa ni mtoto wake wa tano.

NDEGE YA JESHI LA KENYA YAANGUKA KISMAYU

Ndege ya jeshi la KDF nchini Kenya imeanguka katika eneo la Kismayu nchini Somali.

Ndege hiyo ilianguka siku ya Alhamisi mwendo wa saa tisa na robo ilipokuwa ikirudi Kenya baada ya kutekeleza mashambulizi katika eneo la Jamaame kusini mwa Somalia.Kulingana na msemaji wa Jeshi kanali david Obonyo: ''Ndege ya KDF iliokuwa ikirudi nchini Kenyabaada ya kufanya mashambulizi katika eneo la Jamaame kusini mwa Somali, ilikumbwa na matatizo ya kiufundi na kuangukakatika eneo la Kismayu.

Kanali Obonyo hata hivyo hakusema iwapo kulikuwa na majeruhi yoyote.

Jeshi la Kenya limesema kuwa ndege hiyo ilianguka kutokana nahitilafu za kimitambo baada ya kufanya oparesheni katika eneo la Jamaane Kusini mwa Somalia.

Hata hivyo baadhi ya mitandaoa iliyohusishwa na kundi la AL shabaab imechapisha habari kuwa AL shabaab wamedai kuwa ndio waliodungua ndege hiyo mwendo wa saa tisa Alasiri, Afrika Mashariki.

Msemaji wa kiksoi cha kivita cha Al shabaab Sheikh Abdi Azizi Abu Musab amenukuliwa akisema kuwa walishambulia ndege hiyo kwa kombora baada ya kulipua kijiji cha Bulaguduud.

Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC wa idhaa ya kisomali, ni vigumu kwa Al Shabaab kufanya shambulio kama hilo katika mji wa Kismayu kwa kuwa eneo hilo zima limefurika vikosi vya usalama vya AMISOM.

Mnamo mwaka wa 2012, majeshiya Kenya yaliuteka mji wa bandari wa Kismayu, unaotazamiwa kuwa mji muhimu sana wa kiuchumi katika eneo zima la Somalia kutoka kwa wanamgambo hao wa Al shabaab.

AISHI NA MAITI NDANI KWA MIEZI 6 AKIZANI ITAFUFUKA

Familia moja nchini Canada iliishi na maiti katika chumba cha juu cha nyumba yao kwa miezi sita kwa kuwa waliamini marehemu atafufuka iwapo wataendelea kumuomba mungu,lakini mwili huo ukapatikana baada ya familiahiyo kushindwa kulipa mkopo waliochukua kununua nyumba hiyo.

Kaling Wald mwenye umri wa miaka 50 alipatikana na makosa ya kushindwa kuwaarifu maafisa wa polisi kwamba mumewe alifariki ,kosa ambalo na akahukumiwa kuwekwa katika muda wa majaribio na ushauri,wakili wake alikiambia chombo cha habari cha Reuter siku ya Jumanne.

Peter Wald mwenye umri wa miaka 52 alifariki mnamo mwezi machi mwaka 2013 kwa kile mamlaka inasema ni sababu za kawaida kufuatia maambukizi ya mguu wake yanayodaiwa kusababishwa na ugonjwa wa sukari.

Mkewe Kaling Wald alimwacha kitandani na kufunga chumba hicho katika nyumba yao ya Hamilton ,Ontario ili kuzuia harufu kali iliokuwa ikitoka chumbani humo kuwafikia watu waliokuwa wakiishi nyumbani humo.

Kama vile Yesu alivyomfufua Lazaro baada ya siku ya nne ,pia yeye aliamini kwamba Mungu atamfufua mumewe wakili wa mwanamke huyo alisema.

WACHINA 77 WADAKWA NA KUWEKWA NDANI KWA UDUKUZI KENYA

Polisi nchini Kenya wamewafikisha mahakamani raiya 77 wa Uchina kwa kushukiwa kushiriki udukuzi wa mawasiliano na ulanguzi wa fedha.

Washukiwa hao wamewekwa rumande kwa siku tano zaidi ili kutoa nafasi kwa polisi kufanya uchunguzi wa kina.

Wakili wa washukiwa hao anataka waachiliwe kwa dhamana na ombi lake litasikizwa kesho katika mahakama kuu mjii Nairobi.

Washukiwa hao 77 walikamatwa katika nyumba moja kwenye mtaa wa kifahari wa Runda jijini Nairobi siku ya Jumatatu na hapo jana na wanadaiwa kushiriki katika vitendo vya udukuzi na ulanguzi wa fedha.

Upande wa mashtaka uliomba mahakama muda zaidi kuwachunguza washukiwa hao.

Hata hivyo wakili wa washukiwa hao Tom Wachakana aliishawishi mahakama kusikiza ombi lake kutaka washukiwa waachiliwe kwadhamana.

Wakati maafisa wa polisi walipovamiwa makazi ya washukiwa hao walipata mitamboya teknolojia ya hali ya juu inayodhaniwa inatumika kufanya ujanja katika mitandao.

Mbali na maafisa wa polisi, wakuu katika wizara za mambo yanje na habari na mawasiliano walihusishwa katika msakao huo. Afisa katika ubalozi wa Uchina mjini Nairobi ambaye hakutaka kutajwa aliiambia BBC kuwa watashirikiana na serikali ya Kenya inayochunguza asili ya raia hao katika kuangalia stakabadhi zao za usafiri.

Washukiwa hao wamekamwatwa wakati kampuni nyingi za Kichina zimewekeza katika biashara hasa katika sekta ya ujenzi.

Kadhalika serikali ya Kenya imetia saini mikataba mingi na wachina huku baadhi yao wakihusisha katika miradi ya serikali hususan katika taasisi za elimu ya juu.

KESI ZENYE MVUTO KURUSHWA LAIVU KUTOKA MAHAKAMANI

MAHAKAMA inaangalia uwezekano wa kuruhusu vyombo vya habari kurekodi picha na sauti kuwezesha vituo vya radio na televisheni kuripoti habari za mahakama wakati kesi zinaendelea.

Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman alisema jana mahakama inajifunza kutoka kwa nchi zinazoruhusu vituo vya redio na televisheni kurekodi na kuripoti habari wakati kesi zinaendelea.

Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jana wakati wa mkutano baina ya Baraza la Vyombo vya Habari na Mahakama uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema utaratibu huo utaanza kwa kuripoti kesi za madai zenye mvuto kwa jamii na kwamba utaratibu mzima unapaswa kufanyika kwa umakini mkubwa baada ya mahakama na vyombo vya habari kukaa pamoja na kujadiliana juu ya maadili, uhuru na mipaka ya mhimili wa mahakama na vyombo vya habari ili kuondoa migongano katika kuandika na kuripoti habari za mahakama kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Hivi sasa waandishi wa habari hawaruhusiwi kupiga picha za video wala kurekodi sauti wakati kesi zikiendelea.

Badala yake, wanaruhusiwa kuandika habari hizo kisha kuripoti kile walichoandika bila kuonesha mwenendo mzima wa kesi kwa kutumia sauti na picha za video.

Jaji Othman alifafanua kuwa ni lazima mahakama na vyombo vya habari kuweka utaratibu wa kuripotikesi kwa kurusha sauti na picha bila kuvuruga mwenendo wa kesi kwa kukiuka haki hasa za washitakiwa, waathirika na mashahidi kwa kuwa wote wanahitaji haki sawa katika kupata ulinzi na hifadhi kulinda utu wao.

"Mfano sio haki kuwaonesha hadharani waathirika wa kesi ya ubakaji, pia mshitakiwa yeyote hawezi kuitwa mwizi au muuaji hadi mwisho wa kesi ambapo mahakama inazingatia ushahidi na kutoa hukumu," alisema.

Aliendelea kusema, "Ukitangaza kuwa mtu ni mwizi kabla ya hukumu, ni kumkosea haki kisheria hivyo ni lazima tuangalie yote hayo kabla ya kuruhusu utaratibu wa kunakili sauti na picha wakati kesi zinaendelea."

Jaji alitoa maelezo hayo wakati wa kuzungumzia mapendekezo yaliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga ambaye alisema ili kuboresha uhusiano wa vyombo vya habari na mahakama, mahakama inapaswa kuwa na msemaji.

Mukajanga alipendekeza pia mahakama kuandaa taarifa kwa kutumia sauti na picha za video kuhusu mwenendo wa kesi, kutoa mwongozo wa kutumia simu za viganjani na vifaa vingine vya mawasiliano kwa njia ya digitali.

Baraza hilo la kihistoria kati ya mhimili wa Mahakama na vyombo vya habari, limeazimia kuimarisha ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja kwa kuheshimu uhuru na mipaka ya kila mmoja na kuzingatia kuwa wote wanafanya kazi ya kutetea haki za wananchi na wote wamekuwa kimbilio la wanyonge.

Chanzo: Habari leo

BABA WA KAMBO AMNYONGA MTOTO WA MWAKA MMOJA

Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja mkazi wa kijiji cha kindo wilaya ya mvomero mkoani morogoro amekufa baada ya kunyongwa na baba yake wa kambo kufuatia migogoro ya kifamilia kati yake na mkewe.

Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Leonard Paul amesema mtoto Abdalla Hamis amenyongwa na baba yake wa kambo Zamili Shabani (27) muda mfupi baada ya mamawa mtoto kwenda dukani kununua mahitaji na aliporejea aliingia chumbani kumwamsha mtoto ndipo akagundua kuwa mtoto amekufa ambapo muhumiwa kwa wasiwasi alianza kukimbia na mama huyo alipiga kelele ya kuomba msaada kwa majirani hadi alipokamatwa.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoa wa morogoro linamshikilia mtuhumiwa mmoja Abadalla Kifungo (40) mkazi wa malola wilaya ya ulanga mkoani morogoro kwa tuhuma kukutwa na silaha aina ya shortgun na risasi mbili ambapo inasadikiwa na tuhumiwa alikuwa akijihusisha na matukio ya ujangili ambapo watuhumiwa hao wa matukio mawili tofauti watafikishwa mahakamani kujibu Mashtaka.

BURUNDI, UGANDA NA KENYA ZAONGOZA KWA UFISADI

Ufisadi nchini Kenya bado uko katika kiwango cha juu licha ya juhudi kukabiliana na swala hilo nyeti.

Kulingana na ripoti ya shirika la Tranparency International ya mwaka 2013,kenya imerodheshwa ya 136 kati ya mataifa 177 ikiwa na alama 27 katika kipimo cha 0-100.

Sufuri ina maanisha kwamba ufisadi umekithiri huku na 100 ikionyesha kwamba taifa hilo halina ufisadi.

Hata hivyo ni taifa la Burundi lenye ufisadi mkubwa miongoni mwa mataifa ya Afrika mashariki likifuatiwa na Uganda na baadaye Kenya kulingana na utafiti huo.

Kulingana na mkurugenzi wa shirika hilo nchini Kenya Samuel Kimeu,Kenya haijabadilika katika nafasi yake tangu mwaka 2012.

Amesema kuwa taasisi za umma zinahitajika kuwa wazi kuhusu maamuzi yao.

Katika afrika mashariki ,ni taifa la Rwanda Pekee ambalo limeonyesha juhudi za kukabiliana na ufisadi.

Rwanda imeorodheshwa ya 49 ikiwa na alama 54, Ushelisheli iko katika nafasi ya 47 ikiwa na alama 54 na Mauritius ikiwa katika nafasi ya 52 ikiwa na alama 52 ikitamatisha mataifa matano bora barani Afrika.

Botswana imesalia kuwa taifa ambalo halina ufisadi barani Afrika likiwa katika nafasi ya 30 na alama 64 likifuatiwa na Cape Verde ilio katika nafasi ya 41 na alama 58.

Baadhi ya mataifa yalio na ufisadi duniani ni Somali,Sudan,Sudan Kusini Libya na Guinea Bissau.

DAKTARI AFANYA UPASUAJI KWA KUTUMIA PAMPU YA BAISKELI

Jimbo moja nchini India limesitisha shughuli ya kufungwa kizazi wanawake baada ya daktari mmoja kupatikana akitumia pampu ya kuweka pumzi kwenye baiskeli kuweka hewa kwenye matumbo ya wanawake waliokuwa wanafanyiwa operesheni hizo.

Daktari Chandra Rout, aliyetumiapampu hiyo kwa wanawake 56, Ijumaa wiki jana, aliambia BBC kuwa pampu hizo hutumiwa sana katika jimbo hilo la Orissa.

Maafisa wa serikali walisema gesiya kaboni, ndio inapaswa kutumiwa kwa operseheni hizo wala sio pampu za kuweka hewa baiskeli.

Maafisa hao wamesema kuwa watu wanaweza kutumia hewa ya kaboni lakini utumizi wa pampu hiyo ni hatari kwa maisha ya binaadamu.

Mwezi Uliopita ,kashfa nyingine ilizuka kuhusu ukataji wa kizazi baada ya wanawake 15 kufariki walipofanyiwa upasuaji katika jimbo jengine.

Madawa ya kulevya yalitumika wakati wa upasuaji huo katika jimbo la Chhattisgarh.

Kambi za ukataji kizazi hufanyika mara kwa mara ili kuwakata kizazi kwa pamoja wanawake nchini India kama moja wapo ya mipango ya kudhibiti ongezeko laidadi ya watu nchini humo.

Ripoti kwamba daktari Rout alitumia pampu ya baiskeli ili kuyafurisha matumbo ya wanawake kwa lengo la kupata nafasi ya vifaa vya upasuaji kuingia ndani, imezua pingamizi nchini India tangu habari hizo zitangazwe.

Maafisa wa serikali wamesema kuwa utumizi wa hewa ya kawaida badala ya ile ya kaboni unaweza kusababisha magonjwa kadhaa.

Mkuu wa afya katika jimbo la Orrisa Arati Ahuja amesema kuwa ukataji wa kizazi katika jimbo hilo sasa utafanyika katika hospitali zenye vifaa vyote.

''Madaktari watalazimika kuambatana na maagizo ya kimataifa ili kukinga maambukizi yoyote '',bi Ahuja alsema.

Ukataji wa kizazi hufanyika kupitia kuzifunga tubu zinazobeba mayai ya mwanamke.

Hii hufanyika kupitia kufunga na kamba na baadaye kukata tubu hizo,swala linalozuia mayai na mbegu za kiume kukutana ili kutengeza mimba.

Lakini daktari Rout amesema kuwa amekuwa akitumia pampu kwa zaidi ya mara 100 lakini hakujawahi kutokea tatizo lolote.

Anasema kuwa waliamua kutumia pampu hiyo wakati kifaa kinachojulikana kama Insafleta kilipokosekana kwa upasuaji.

MIKOA YATAKIWA KUWASILISHA MAJINA COPA-COCACOLA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitaka mikoa mitano kuwasilisha usajili wa wachezaji wake kwa ajili ya mashindano ya Taifa ya Copa Coca-Cola 2014 kabla ya Desemba 5 mwaka huu.

Mikoa hiyo ambayo haijawasilisha usajili wake hadi sasa kwa ajili ya michuano hiyoinayoanza Desemba 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni Arusha, Dodoma, Katavi, KusiniPemba, Kusini Unguja, Mjini Magharibi na Simiyu.

Kwa mujibu wa Kamati ya Mashindano ya michuano hiyo, mkoa ambao hautawasilisha usajili wake kwa ajili ya uhakiki wa umri wa wachezaji utakaonza Desemba 10 mwaka huu utaondolewa katika fainali hizo zitakazomalizika Desemba20 mwaka huu.

Wachezaji watakaobainika kuzidi umri hawataruhusiwa kushiriki katika michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 15. Kwa mujibu wa Kanuni ya 29 yamichuano kuhusu idadi ya wachezaji, kila timu inatakiwa kuwa na wachezaji wasiozidi 20na wasiopungua 16.

Hivyo, kila timu inatakiwa kuhakikisha inakuwa na idadi hiyo ya wachezaji, kwani kikanuni wakipungua 16 itaondolewa kwenye mashindano.

Timu 16 kwa upande wa wavulana zitashiriki katika fainali hizo wakati kwa upande wa wasichana ni timu nane.
Mikoa iliyoingiza timu za wasichana kwenye fainali hizo ni Arusha, Dodoma, Ilala, Kinondoni, Mbeya, Mwanza, Temeke na Zanzibar.

ATUPWA JELA MIAKA 50 KWA KUWAHARIBU WATOTO

Mahakama nchini Kenya imemhukumu kifungo cha miaka 50 jela raia mmarekani kwa kutengeza na kusambaza picha chafu za video za watoto wakifanya vitendo vya ngono.

Terry Ray Krieger alikiri makosa yake mbele ya mahakama mwezi jana. Pia alipatikana na kosa la kuwadhalilisha watoto wadogo huku akinasa vitendo hivyo kwa kanda ya video.

Alikamatwa na maafisa wa usalama Kenya baada ya kupata taarifa kutoka kwa shirika la kimataifa la polisi kwamba alikuwa anasambaza video hizo zilizokuwa zinaonyesha watoto wakifanyiwa vitendo vichafu kwenye mtandao.

Krieger amewahi kushtakiwa kwa makosa sawa na hayo na kufungwa jela nchini Marekani miaka 20 iliyopita.

Polisi wa Kenya walipokea taarifda kutoka kwa polisi nchini Marekanmi wakiwaamiwa kuwa kuna raia mmarekani nchini Kenya anayetengeza na kusambaza video chafu za watoto wadogo wakihishwa na vitendo vya ngono.

Aliomba mahakama kumuonea huruma kutokana na maradhi anayougua ya mifupa lakini mahakama ilisema kuwa maradhi yake sio haiwezi kuwa sababu ya kutowajibishwa kwa makosa yake.

UWANJA WA NDEGE MPANDA WAASWA KUTUNZA MIUNDOMBINU

Kufuatia kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani Katavi, Serikali imewaasa watumiaji wa uwanja huo kutunza miundombinu ya uwanja huo ili kuweza kuhudumia wakazi na wageni wapitao uwanjani hapo kwa muda mrefu.

Wito huo umetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi yaRais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani Katavi.

Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imekamilisha kazi ya kuufanya uwanja huo uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za binafsi na biashara, hivyo uongozi wa uwanja huo hawana budi ya kuhakikisha miundombinu ya uwanja huo inatunzwa ipasavyo.

"Kama mnavyo fahamu Serikali imekuwa ikiwekeza sana katika uendelezaji wa miundombinu ya usafiri nchini hasa kuendelea kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga ili kuongeza ufanisi na kuendelea na kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika maeneo ya kimkakati, hivyo kuna haja ya kuunga mkono jitihada hizi za Serikali," aliasa Bibi Mwanri.

Akitoa taarifa ya uendelezaji uwanja huo kwa msafara wa timu ya ukaguzi, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Bw Seneti Lyatuualisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo, unaweza kutumika kutua na kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile ndege kubwa zinaweza kutua kwa dharura.

"Uwanja huu umekarabatiwa na barabara ya kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa kiwango cha lami kutoka urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30 hadi kufikia urefu wa mita 1,820 na upana wa mita 30," alisema Bw. Lyatuu.

Kwa mujibu wa Meneja huyo, kukamilika kwa uwanja huo kumevutia idadi ya abiria wanaoutumia uwanja huo kutoka abiria 285 mwaka 2009 hadi 2,390 mwaka 2013/14.

Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa waMiaka Mitano (2011/12 - 2015/16), Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati, usafirishaji (bandari, reli, barabara na usafiri wa anga), maji (safi, taka na ya uzalishaji) na TEHAMA.

Serikali imeandaa Mpangowa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi. Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa.

Lengo la Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Chanzo: Katavi Yetu

JOTO KALI KUATHIRI DAR, ZANZIBAR NA KILIMANJARO

HALI ya joto katika jiji la Dar es Salaam imeelezwa kupanda kwa nyuzi joto 4.5 kutoka 31.5 hadi 35.5 ambapo hali hiyo inatarajiwa kudumu hadi Februari mwakani.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Hali ya Hewa nchiniwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Hamza Kabelwa ambapo alisema maeneo mengineambayo joto limepanda ni pamoja na Zanzibar na Kilimanjaro.

"Zanzibar joto limefikia nyuzi joto 34.4 kutoka 30.7 na Kilimanjaro ni 35.6 kutoka 31.6 na hali hii inaweza kuendelea katika vipindi tofauti hadi Februari mwakani," alisema.

Alisema hali hiyo inasababishwa naupepo unaotoka nchini Somalia kuja katika maeneo ya Nyanda za Juu Kusini, ambapo alifafanua kuwa kunatokana na kuwepo kwa kiwango cha juu cha joto katika baadhi ya maeneo.

Aidha alitumia nafasi hiyo kuwaondoa hofu wananchi kuwa mifumo ya upepo imebadilika kutokana na kuwepo kwa hali ya mvua katika ukanda huo.

"Mara nyingi ikifika Desemba, Januari na Februari huwa kunakuwa na joto kali katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi na ukanda wa ziwa, kutokana na maeneo haya kuwa na misimu miwili ya mvua kwa mwaka,"alisema Kabelwa.

"Lakini hali hii hutokea kila baada ya miezi hiyo, ila wananchi wanasahau, cha msingi na wasisitiziwe kuwa wasiwena wasiwasi, hali hii itakwisha, na mwezi huu kutakuwa na mvua kwa vipindi tofauti," aliongeza.

Hata hivyo Kabelwa alisema TMA itakuwa ikitoa taarifa ya mabadiliko ya hali ya hewa kila wiki kuanzia sasa.

WAZIRI ATIMULIWA, IGP AACHIA NGAZI

MBUNGE wa Kajiado ya Kati nchini Kenya, Joseph Nkaissery ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo wa Ndani wa nchi hiyo.

Nkaissery anachukua nafasi hiyo kutoka kwa, Joseph ole Lenku ambaye wakati wa uongozi wake Kenya imekumbwa na ukosefu mkubwa wa usalama.

Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo alitangaza uteuzi huo wakati akilituhubia taifa kuhusiana na hali ya usalama ya Kenya.

Nkaissery anatarajiwa kujiuzulu ubunge mara atakapokubali uteuzi huo.

Wakati huo huo Mkuu wa Polisi nchini Kenya Inspekta Jenerali, David Kimaiyo amejiuzulu wadhifa huo.

Kimaiyo ameachia ngazi saa chache baada ya wapiganaji wa kikundi cha al shabaab cha Somalia kuwaua watu 36 katika Kaunti Mandera nchini humo.

WANANCHI WAPINGA MUBARAK KUFUTIWA MASHITAKA

Polisi nchini Misri wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga hatua ya mahakama nchini humo kutupilia mbali kesi ya mauaji dhidi ya Rais aliyeondolewa madarakani Hosni Mubarak.

Zaidi ya watu 2000 walikusanyika katika viunga vya Tahrir mahala ambapo ndipo zilipozaliwa harakati za mapinduzi ya nchi hiyo mwaka 2011.

Awali Mubarak alihukumiwa kifungo cha maisha jela ambapo kwa sasa anatumikia pia kifungo cha miaka mitatu kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

Kwa sasa Hosni Mubarack anashikiliwa katika hospitali ya jeshi ambako pia anapatiwa matibabu.

Waziri wake wa zamani wa mamabo ya ndani Habib al-Adly na wenzake sita walihukumiwa kifungo cha maisha 2012, inakadiriwa takriban watu 800 waliuawa wakati wa harakati za kumuondoa kiongozi huyo Februari 11.2011.

WATUPWA JELA KWA KUCHEZA WATUPU KWENYE VIGODORO

WAKAZI wanne wa eneo la Masasi Mbovu katika Halmashauri ya mji Masasi mkoani Mtwara wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kucheza wakiwa watupu kwa mtindo wa 'vigodoro' kwenye sherehe ya ndoa.

Akitoa hukumu hiyo juzi hakimu wa mahakama ya wilaya ya Masasi, Halfani Ulaya alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Septemba 30 mwaka huu kwa makusudi hukuwakijua ni kosa la jinai na ukiukwajiwa maadili ya kitanzania.

Waliohukumiwa kwenda jela ni Anna Yohana (25), Aziza Chukachuka (20) Jemima Jordan (22), huku mtuhumiwa mmoja ambaye ni mtoto mwenye umri wamiaka 17 (jina limehifadhiwa) akitakiwa kulipa faini ya Sh 50,000 kutokana na umri wake kuwa mdogo.

Kwa mujibu wa hakimu Ulaya, ameridhishwa na upande wa utetezi ulioletwa na mashahidi watatu mahakamani hapo na kwamba uamuzi huo ni wa haki na kisheria kwani walitenda kosa la jinai namba 167 ya mwaka 2014.

Washtakiwa hao walipotakiwa kujitetea hawa kusema chochote na kwamba wote wamekiri kuwa kwa makusudi walitenda kosa hilo huku mahakama ikitoa onyo kali kwa watakaobainika kuendelea na vitendo hivyo vinavyokwenda kinyume na maadili ya Watanzania.

HELKOPTA YA KUPAMBANA NA MAJANGILI YAANGUKA YAUA WANNE

HELIKOPTA ya Wizara ya Maliasili naUtalii, iliyotolewa msaada kwa ajili ya kupambana na majangili Juni mwaka huu, imeanguka na kuua watu wanne, waliokuwa katika helkopta hiyo wakiwemo marubani wawili wa Jeshi la Polisi, askari mmoja na rubani mwingine ambayeni mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Helikopta hiyo aina ya Robertson R44 yenye thamani ya Dola za Marekani 500,000 (Sh milioni 800), ilitolewa msaada na Taasisi ya Howard Buffet kwa ajili ya kusaidia mapambano hayo.

Ajali ya helikopta hiyo iliyokuwa ikimilikiwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), ilitokea jana saa 4:00 asubuhi maeneo ya Kipunguni B, Moshi Bar, wilayani Ilala, wakati ilipokuwa katika ukaguzi wa kawaida.

Akizungumza katika eneo la ajali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana na upelelezi unaendelea kujua chanzo.

Kamanda Kova aliwataka wananchi na wakazi wa eneo hilo, kutosogea karibu na mabaki ya helikopta hiyo, ili kuepusha madhara makubwa zaidi yanayoweza kutokea kutokana na kuwepo kwa viashiria vya moto.

"Tunaomba msisogee karibu na eneo hili la ajali, panaweza kulipuka hapa na kusababisha madhara makubwa zaidi, tuchukue tahadhari na tukae mbali na eneo hili," alisema Kova.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Kamishna Msaidi (ACP), Hamis Suleiman, alitaja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Mrakibu waPolisi Kapteni Kidai Senzala, Mkaguzi wa Polisi Kapteni Simba Musa, Konstebo wa Polisi, Josso Selestine na Kapteni Joseph Khalfan.

Helikopta hiyo ilikuwa na namba 5H- TWA. Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, alipongeza wananchi hao kwa kutoa taarifa mapema zilizosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza madhara.

Hata hivyo Sadiki alitaka wananchi kutokimbilia maeneo ya tukio la ajali kama hizo zinapojitokeza kwani kuna uwezekano mkubwa wa wao kupata madhara yanayoweza kusababishwa kulipuka kwa chombo hicho.

Mashuhuda wa ajali hiyo, walisema waliona helikopta hiyo ikiyumba na kutoa mngurumo usio wa kawaida na baadaye ikazima ambapo rubani alijaribu kuiwashwa bila mafanikio, lakini baadaye ilianguka.

"Tulisikia mlio wa helikopta usio wa kawaida na baadaye ilizima na kusikika tena ikiwashwa ikagoma ndio baada ya muda mfupi, tukasikia kishindo kikubwa cha helikopta hiyo kuanguka," alisema shuhuda huyo.

SHEKHE PONDA AACHIWA HURU

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemwachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shekhe Issa Ponda kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yake.

Shekhe Ponda aliwahi kutiwa hatianina Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 2, mwaka jana, kwa kosa la kula njama kuingia kwa nguvu katika eneo lililopo Chang'ombe wilaya ya Temeke na kupewa adhabu ya kifungo cha miezi 12 jela.

Akitoa hukumu hiyo jana, Jaji Augustine Shangwa alisema ushahidi uliotumika Mahakama ya Kisutu kumtia hatiani Shekhe Ponda ulikuwa na mapungufu hivyo uliachashaka.

Alisema upande wa mashitaka haukuthibitisha kwamba Shekhe Ponda aliwaamuru wafuasi wake kuvamia katika eneo hilo. Licha ya Ponda kuachiwa huru, bado anakabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro alikokuwa na kesi ya uchochezi.

Shekhe Ponda alishitakiwa katika Mahakama hiyo Agosti 19, mwaka jana, akikabiliwa na mashitaka matatu ya kutotii amri halali ya Mahakama.

Mwendesha mashitaka alidai kwamba Shekhe Ponda walifanya makosa hayo Agosti 10, mwaka jana katika Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege katika Manispaa ya Morogoro. Ponda alidaiwa kukiuka amri ya Mahakama kwa kutoa kauli za uchochezi na kuichochea jamii kufanya fujo.

Kulingana na mwendesha mashitaka, Shekhe Ponda alichochea waumini wa Kiislamu na kwamba Baraza Kuu la Waislamu waTanzania (BAKWATA), walikuwa ni vibaraka wa CCM na serikali na hivyo wanapaswa kuwapiga.

Taarifa hiyo alidaiwa kupinga agizo la Mahakama ya Kisutu.

Inadaiwa kwamba kwa misingi hiyo, kauli iliyotolewa na Ponda ni ya uchochezi kwa makusudi, akisema serikali iliingiza jeshi Mtwara ili kuleta machafuko ya wananchi ambao walikuwa wanapinga ujenzi wa bomba la gesi.

YAMETIMIA ESCROW

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imependekeza kutenguliwa kwa nyadhifa na kuwajibika kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na baadhi ya mawaziri kutokana na sakata la fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL.

Mbali ya mapendekezo hayo, Kamati hiyo imependekeza pia wote waliochukua fedha kutokana na kashfa hiyo iliyohusisha Sh bilioni 306, wafilisiwe mali zao na kushitakiwa mahakamani.

Wanaotajwa kutakiwa kutenguliwa kwa nyadhifa zao mbali ya kuwajibika kwa Pinda ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Naibu wake, Stephen Maselle, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliachim Maswi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.

Kamati hiyo ilitoa mapendekezo yake hayo kutokana na matokeo ya ukaguzi maalumu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Akisoma maoni na mapendekezo yaKamati baada ya Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe kusoma sehemu ya uchambuzi wa sakata hilo, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe alisema kwa uzito na unyeti wa suala hilo, Waziri Mkuu Pinda anapaswa kuwajibika kwa kauli zake na kwa kutotekeleza wajibu wake wa kikatiba ipasavyo, ilikurejesha imani ya wananchi kwa Serikali yao na viongozi wao wa kisiasa.

Kwa mujibu wa Filikunjombe, baadaya kupitia vielelezo vilivyomo katikaripoti ya CAG, "Kamati imejiridhishapasipo mashaka kuwa, Waziri Mkuu alikuwa na taarifa zote kuhusu mchakato mzima wa kuchotwa fedha kutoka katika akaunti ya Escrow."

"Ushahidi ulioletwa na Ofisi ya CAG kwenye Kamati unaonesha kuwa Waziri Mkuu alikuwa akipata taarifa za jambo hili. "Na Kamati imesikitishwa kuona kuwa Waziri Mkuu hakuchukua hatua zozote kuzuia muamala huu usifanyike," aliongeza Makamu Mwenyekiti huyo, na kubainisha kuwa Pinda pia aliwahi kunukuliwa akisema fedha za Escrow si za umma.

Kuhusu Profesa Muhongo, Kamati ilieleza kuwa alifanya udalali wa kuwakutanisha Harbinder Sethi na James Rugemalira (waliokuwa wamiliki wa Independent Power Tanzania Limited) na kuwa alilipotosha Bunge kuhusu fedha za akaunti ya Tegeta Escrow kwamba ndani ya fedha hizo, hakukuwa na fedha za umma."

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, aidha kwa makusudi, ama kwa sababu anazozijua vizuri zaidi mwenyewe, Waziri wa Nishati na Madini ananukuliwa kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge, kwa nguvu kubwa na kwa kujiamini, akitetea uchotwaji wa fedha hizo kinyume cha masharti ya mkataba wa Escrow," alisema Filikunjombe.

Alisema iwapo waziri huyo angetimiza wajibu wake kidogo tu na ipasavyo, fedha za Tegeta Escrow zisingelipwa kwa watu wasiohusika na nchi ingeweza kuokoa mabilioni yaliyopotea kama Kodi ya Ongezekola Thamani (VAT), Capital Gain Tax na ushuru wa stempu ambazo ni sawa na takribani Sh bilioni 30.

"Kamati inapendekeza kuwa mamlaka yake ya uteuzi, itengue uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini kutokana na sababu zilizoelezwa," alisema.

Akimzungumzia Maselle, Filikunjombe alisema Kamati imethibitisha kuwa alisema uongo bungeni kwa kutamka kauli ambazo zilikuwa na lengo la kupotosha umma kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow, ikiwemo kutoa kauli ambazo zingeweza kusababisha nchikuingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na nchi ya Uingereza.

"Kamati inapendekeza kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini)achukuliwe hatua kali za kinidhamu,ikiwemo kutenguliwa uteuzi wake.
"Kamati pia inapendekeza kuwa Naibu Waziri huyu afikishwe mbele ya Kamati ya Bunge ya Maadili ili aadhibiwe kama mbunge kwa kusema uongo bungeni ili liwe fundisho kwa wabunge wengine kuhusu kauli wanazotoa ndani ya Bunge lako tukufu," aliongeza Filikunjombe

Kuhusu Mwanasheria Mkuu Jaji Werema, Kamati ilisema imethibitisha kuwa alitoa ushauri ulioipotosha Benki Kuu ya Tanzania kuhusu hukumu ya Jaji John Utamwa kwa kutumia madaraka yake vibaya.

Alisema Jaji Werema aliagiza kodi ya Serikali yenye thamani ya Sh bilioni 21 isilipwe na hivyo kuikosesha Serikali mapato adhimu."

Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwakujua na kwa makusudi alilipotosha Bunge na Taifa kwamba mgogoro uliosababisha kufunguliwa kwa akaunti ya Escrow ulikuwa ni mgogoro wa wanahisa wa IPTL badala ya mgogoro kati ya Tanesco na IPTL.

"Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe na mara moja afikishwe mahakamani kwa matumizi mabaya ya ofisi yaliyosababisha Serikali kupoteza mabilioni ya fedha," alisema Filikunjombe.

Akimzungumzia Katibu Mkuu Maswi, Makamu Mwenyekiti huyo wa PAC alisema Kamati inapendekeza uteuzi wake utenguliwe na Takukuru wamfikishe mahakamani mara moja, kwa kuikosesha Serikali mapato na matumizi mabaya ya ofisi na kusaidia utakatishaji wa fedha haramu.

Kamati ilisema imethibitisha Maswi amefanya uzembe wa hali ya juu wakushindwa kujiridhisha kuhusu masharti ya sheria ya kodi, na pia imebaini kuwa hakujiridhisha uhalali wa Kampuni ya Mechmar kuuzwa kwa Piperlink na baadaye kuuzwa kwa PAP, na hivyo kusababisha fedha za akaunti ya Tegeta Escrow kulipwa kwa asiyestahili kinyume cha mkataba wa akaunti ya Escrow.