Arfi Atupa Kadi Ya Chadema

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezidi kuandamwa na
migogorobaada ya jana kuibuka mwingine mkubwa katika kikao chake cha
ndani mkoani Katavi kiasi cha kumfanya Makamu Mwenyekiti wachama hicho
Taifa, Said Arfi, kutupa kadi yake' Huu ni mgogoro wa pili mkubwa
kuripotiwakatika kipindi cha juma moja lililopita baadaya ule wa
wilayani Karatu ambako pamoja namambo mengine uliishia kwa Kamati
Kuusimamisha uongozi wote wa chama hicho wilaya. Taarifa zilizolifikia
gazeti hili jana zimeelezakuwa Arfi ambaye ni Mbunge wa Mpanda Mjini,
alitishia kujitoa Chadema jana, katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya
chama hicho Mikoa ya Katavi na Rukwa kilichoketi Namanyere, Nkasi na
kufikia uamuzi wakumsimamisha Mwenyekiti wa Baraza laVijana Mkoa wa
Rukwa, Laurent Mangweshi.Katika kikao hicho, Arfi anadaiwa kuichukua
kadi yake ya Chadema na kumtupia Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa
Rukwa,John Mallack akitangaza kuachia nyadhifa zote alizonazo, kisha
kuondoka ukumbini kabla ya kufuatwa na wazee wa chama hicho na kumsihi
aichukue kadi yake hiyo. Alifikia hatua hiyo baada ya kutokea
sintofahamu kati ya wajumbe wa kikao hicho katika uamuzi huo
uliofikiwa kwa kupiga kura za ndiyo na hapana. Vyanzo vya habari
kutoka ndani ya kikaohicho vilifafanua kuwa Arfi alikerwa na kauli
iliyotolewa na Mangweshi kuwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alipokea
rushwa kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Vyanzo hivyo vya habari
vimeeleza kuwa kutokana na hali hiyo, Arfi alipandwa nahasira na
kuamua kumrushia kadi Mallack kisha kutoka nje ya ukumbi. "Hatua hiyo
ilifanya wajumbe wa kikao hicho nao kutoka nje ya ukumbi na kuanza
kumbembeleza ili asichukue uamuzi huo nakisha wakamwekea kadi yake ya
uanachamakatika mfuko wake wa shati," alisema mmojawa makada hao. Arfi
mwenyewe hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo baada ya simu ya
mkononi kuita muda wote bila kupokewa nahata alipotumiwa ujumbe,
hakujibu. Mallack akizungumza na gazeti hili kwa simu alikiri Arfi
kurusha kadi mezani kisha kutoka nje ya ukumbi, lakini akasema suala
hilo lilishughulikiwa na wazee na kumalizwa."Ni kweli unajua huyu ni
Makamu Mwenyekitiwetu wa Taifa, sasa inapotokea vijana wadogo
wakamtuhumu kwa tuhuma za uongo na ambazo hazipo inatia hasira, ndiyo
maana huyo kijana tumemvua uongozi," alisemaMallack. Mangweshi
alisimamishwa uongozi baada yakutuhumiwa kwa mambo mbalimbali
yakiutendaji ndani ya chama hicho ikiwamo kumkashifu Arfi.Katika
mkutano wake na waandishi wa habari Mallack alisema kuwa Magweshi
amevuliwa uongozi baada ya chama hicho kujiridhisha kuwa alitenda
makosa hayo.Alisema kamati ya ushauri ilimwita ili kujibu tuhuma
mbalimbali zilizokuwa zikimkabili ikiwamo kutoa taarifa zisizo rasmi
bila kufuata taratibu za chama."Pia amepatikana na hatia ya kuandika
barua za kashfa na kuzipeleka makao makuu ya chama kumkashifu Arfi
pamoja na viongozi wengine wa chama akiwamo Katibu Mkuu Dk Willibrod
Slaa.Katibu Mwenezi wa Chadema Mikoa ya Rukwa na Katavi, John Matongo
alisema kabla yakupewa adhabu ya kusimamishwa amewahi kuonywa mara
kadhaa lakini ameshindwa kujirekebisha.



Chanzo: www.mwananchi.co.ctz

Ndege Ya Tanapa Yapata Ajali

Ndege inayomilikiwana shirika la hifadhi za taifa ya wanyama pori
TANAPA yenye usajiri wa namba 5H-FZS yapata ajari muda wa saa kumi na
dakika 50 wakati ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa Mkoani Katavi
Wilaya ya Mpenda. katika Runway namba 027 mita 300 kutoka kwenye
Fence(Uzio) wa uwanja huo.
Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria wanne, ni Rubani aliyejeruhiwa katika ajari hiyo na kuweza kupelekwa hospitali.
Picha: Nkwabi T. Kisanga