Mwakyembe, Kipande wavurugana TPA

MIEZI sita baada ya Waziri wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe, kumteua Mhandisi Madeni Kipande, kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), viongozi hao kwa sasa hawaivi chungu kimoja, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Tofauti za viongozi hao imeelezwa kuwa ni baada ya Kipande kudaiwa kukaidi maagizo ya Waziri Mwakyembe.

Habari ambazo gazeti hili limezipata, zilisema kuwa  Waziri Mwakyembe amemlima barua kali ya onyo Kipande, akimtaka kusitisha uamuzi wa kuibeba kampuni ya kuhifadhi magari ya SILVER.
Kampuni hiyo imekuwa ikilalamikiwa na kampuni nyingine kwamba inapendelewa na Kipande.
Barua hiyo ya Juni 11 ambayo nakala yake tunayo, Waziri Mwakyembe amembana Kipande kuacha kuipendelea kampuni hiyo.

Katika barua hiyo yenye kichwa cha habari: ‘Kukaidi maagizo ya wizara’, Dk. Mwakyembe alimtaka Kipande atakapojibu atumie kumbukumbu namba CCB 364/505/01.
Dk. Mwakyembe ameandika katika barua hiyo kuwa amepata taarifa ya kuwapo kwa upendeleo wa moja ya makampuni ya kuhifadhi magari kinyume cha maelekezo yake aliyoyatoa Machi 3, mwaka huu alipokutana na viongozi wa wizara na wawakilishi wa ICDSVS.
“Nimefedheheshwa sana na taarifa kuwa kampuni ya kuhifadhi magari ya SILVER bado inapata ‘preferential treatment’ au bado inabebwa na TPA tofauti na kampuni nyingine za aina hiyo na kinyume kabisa cha taratibu za ushindani na kibiashara na maelekezo niliyoyatoa mbele yenu viongozi wa wizara na wawakilishi wa ICDSVS tarehe 5, Machi 2013.

“Kwa staili hii ya uongozi hatufiki, sitisheni ‘preferential treatment’ kwa Silver ‘asap’ na nipate taarifa ya utekelezaji tarehe 15 Juni, 2013 bila kukosa,” imeandikwa barua hiyo.
Nakala ya barua hiyo imepelekwa kwa Profesa Joseph Msambichaka, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Bandari.
Wakati Kipande akiandikiwa barua ya kusitisha uamuzi huo, taarifa nyingine zinaeleza kuwa kaimu huyo amekuwa akilalamikiwa na makampuni tofauti hata nyingine kuamua kutoa notisi ya kukwepa kutumia Bandari ya Dar esSalaam na badala yake kuishia Mombasa.
Kikubwa kinachodaiwa na makampuni hayo kuamua kutoa notisi hiyo ni kukithiri kwa rushwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kuwapo misuguano baina ya wafanyakazi wa bandari na wateja wakubwa wa ndani na nje ya nchi, hasa wenye meli.

Wateja wa ndani wanaodaiwa kulalamikia utendaji wa Kipande ni pamoja na Kampuni ya Tanga Cement, huku Kampuni ya Mesina kutoka nchini Italia ikielezwa kuwa tayari imeshatoa notisi ya kuacha kutumia Bandari ya Dar es Salaam na badala yake kuishia Mombasa nchini Kenya kutokana na ushirikiano mdogo inaodaiwa kutoka kwa Kipande.

Januari 21  mwaka huu  Waziri Dk.  Mwakyembe aliwatimua kazi vigogo watano wa bandari ambao ni Ephraim Mgawe, naibu wake, Hamad Konshuma, Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Casian Nghamilo, Kapteni Tumaini Masalo na Julius Semfuko.
Vigogo hao walidaiwa kukutwa na makosa ya uzembe uliokithiri, kushindwa kudhibiti wizi, kukosa uaminifu kupindukia, matumizi mabaya ya madaraka na kukiuka sheria.
Wakati huo Mwakyembe alisema kuwa makosa hayo yamesababisha kushindwa kudhibiti kiwango cha utoaji mafuta machafu bandarini na kusababisha wizi wa mafuta masafi pamoja na kutoa kibali cha utoaji mafuta hayo kinyume cha sheria.

Waziri Mwakyembe aliongeza kuwa vigogo hao kwa kushirikiana walitumia vibaya madaraka yao kwa kuingia mkataba na kampuni ya Kichina (China Communication Construction Company) bila idhini ya serikali pamoja na kupandisha mshahara kwa wafanyakazi wa bodi hiyo bila idhini ya waziri anayesimamia mamlaka hiyo.

Alisema kutokana na makosa hayo wameisababishia  Bandari ya Dar es Salaam kuwa ya  mwisho kwa utendaji kati ya bandari 36 Afrika, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na DANIDA na Benki ya Dunia..
Wakati huo Dk. Mwakyembe alipofanya uamuzi huo na kumkaimisha Kipande katika nafasi ya ukurugenzi, taasisi mbalimbali za kimataifa zilionesha wasiwasi wao juu ya hali hiyo na kutahadharisha kuwa utaua uchumi wa nchi hasa katika sekta ya Bandari.

Taasisi zilizoonesha wasiwasi huo ni Umoja wa Ulaya (EU) na Benki ya Dunia (WB) ambazo kwa nyakati tofauti zilitoa maoni yao juu ya hali hiyo.

EU kwa upande wake ambayo ilifanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam na kusifia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ilihofia mafanikio hayo kupotea.


Chanzo:Tanzania Daima

Kauli ya Pinda inahitaji mjadala wa kitaifa

Mizengo Pinda atoe kauli tete Bungeni wiki iliyopita ya kulichochea Jeshi la Polisi liendeleze vipigo na mateso kwa wananchi aliodai wanakaidi sheria za nchi, wamejitokeza baadhi ya watu, wakiwamo mawaziri wakijaribu kuipaka sukari kauli hiyo ili itafsiriwe na kuonekana kama ni ya kuhimiza utiifu wa sheria.
Hatari ya kauli hiyo kwa amani na usalama wa wananchi inatokana na ukweli kwamba inaonyesha kama vile nchi yetu inatawaliwa kijeshi. Kinyume chake, nchi yetu inaongozwa na Katiba, kwa maana kwamba Serikali iliyopo madarakani ilichaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura. Haikupatikana kwa mtutu wa bunduki na mapinduzi ya kijeshi.
Kwa maana hiyo, Katiba ya Tanzania na sheria zilizotungwa na Bunge ni mwongozo kwa watawala kuhusu namna ya kuendesha Serikali kwa njia za kidemokrasia na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao. Anapotokea kiongozi wa juu wa Serikali akalichochea Jeshi la Polisi kuvunja Katiba na sheria za nchi kwa kufanya vitendo vinavyosababisha hofu na kuhatarisha amani na maisha ya raia lazima wananchi wapaze sauti, wamlaani kwa nguvu zote na wamwambie ‘hapana’.
Kauli ya Waziri Mkuu Pinda inatia hofu, hasa inapotolewa kwa Jeshi la Polisi lenye muundo uliorithiwa kutoka kwa wakoloni. Tofauti na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambalo mwaka 1964 lilifanyiwa mabadiliko makubwa kutoka jeshi la kikoloni na kuwa jeshi la wananchi, Jeshi la Polisi tulilorithi kutoka kwa wakoloni lilibakia hilohilo kimuundo na kwa kiasi kikubwa kisera.
Kimsingi ni Jeshi lililoundwa kupokea amri na kutekeleza matakwa ya watawala ya kuwakandamiza wazalendo, hata kama wazalendo hao wanadai haki zao za kiraia na kikatiba kama Jeshi la Polisi la Makaburu wa Afrika Kusini lilivyokuwa likiwaua na kuwatesa wazalendo waliokuwa wakipinga ubaguzi wa rangi. Ndiyo maana hapa nchini umekuwapo uhasama mkubwa kati ya jeshi hilo na wananchi. Watawala wanaonekana kufurahia hali hiyo ambayo tayari imesababisha vifo na mateso kwa raia wasiokuwa na hatia.
Waziri Mkuu anasema jeshi hilo lazima liwapige wananchi anaodai wanakaidi amri halali ya Polisi. Tunauliza amri halali ya Polisi ni ipi? Kupiga marufuku mikutano ya vyama vya upinzani na kuisambaratisha kwa mabomu na silaha za kivita bila sababu za msingi ni amri halali ya wapi? Tunasema hiyo siyo amri halali na inakwenda kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 inayovitaka vyama hivyo kutoa tu taarifa ya mikutano hiyo kwa Polisi ndani ya saa 24 ili vipatiwe ulinzi. Jeshi hilo sasa limejipachika madaraka ya kutoa vibali, kukataa ama kukubali kwa kutoa masharti ya ajabu. Je, hayo ni maagizo ya chama tawala na serikali yake?
Sisi tunasema kauli ya Waziri Mkuu Pinda inahitaji mjadala wa kitaifa. Ni kauli hatari. Tuikatae, kwani inalenga kuhatarisha amani na umoja wetu. Jaji mstaafu Mark Bomani juzi alionyesha njia alipotahadharisha Serikali na jeshi hilo dhidi ya kutumia nguvu kubwa kukabiliana na umma kwa kutumia silaha za moto. Alionyesha wasiwasi kama kweli Polisi wana uelewa mzuri wa sheria kuhusu matumizi ya silaha za moto au wanafanya kazi kwa kuagizwa tu. Tunahitaji sauti nyingi kama hiyo.

Chanzo: Mwananchi

Picha Ya Siku | Picture of the Day

Kutoka kwa Kipanya: Mwananchi

Marekani Yatoa onyo msafara wa Obama Dar


Dar es Salaam. Licha ya ujumbe wa Rais wa Marekani, Barrack Obama kutarajiwa kufikia katika hoteli kubwa zenye hadhi wakati kiongozi huyo atakapowasili nchini Julai Mosi mwaka huu, Ikulu ya Marekani imetoa tahadhari ya vyakula ambavyo hawatakiwi kuvigusa wakiwa nchini ikiwa ni pamoja na kutumia maji ya bomba.
Mbali na tahadhari hiyo, ziara hiyo ya Obama itakuwa na ulinzi mkubwa ambao pengine haujawahi kutokea katika historia ya viongozi wa nje wanaotembelea Tanzania kwani utahusisha idadi kubwa ya magari, ndege za kijeshi na meli kubwa ya kivita ambazo zitakuwa zikifanya doria karibu na pwani ya Tanzania.
Tahadhari za matumizi ya chakula, maji na nyinginezo zimetolewa katika nchi zote tatu za Afrika ambazo Obama atatembelea, kila moja kwa jinsi Wamarekani hao wanavyoitathmini.
Rais Obama atatembelea nchi za Tanzania, Senegal na Afrika Kusini.
Ulinzi
Vyombo vya usalama vya Marekani vimejipanga kuhakikisha ziara ya kiongozi huyo haivurugwi kwa namna yoyote ile. Tayari ndege za jeshi zilizobeba magari ya akiba 56, yakiwemo 14 aina ya ‘Cadillac One’ maalumu kwa ajili ya kiongozi huyo, yamewasili katika nchi hizo tatu za Afrika atakazotembelea.
Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post la Marekani, ndege hizo pia zimebeba malori matatu ambayo yamesheheni karatasi maalumu za kuzuia risasi kupenya kwenye vioo, zitakazobandikwa kwenye madirisha ya hoteli ambazo Rais Obama na ujumbe wake watafikia.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, mamia ya mashushushu wa Marekani tayari wako katika nchi hizo. Meli maalumu za kubeba ndege za kivita, maarufu kwa jina la ‘amphibious ship,’ ikiwa na hospitali maalumu na yenye vifaa vyote itaweka nanga baharini, jirani na nchi atakayokuwa Rais Obama, tayari kukabiliana na dharura yoyote itakayotokea. Gazeti hilo liliandika kuwa ndege za kivita za Marekani zitakuwa zikipeana zamu kufanya doria kwa saa 24, katika anga la nchi ambayo Rais Obama atakuwepo, iwapo ndege za ‘adui’ zitakaribia eneo linaloitwa ‘anga ya rais.’ Kwa mujibu wa gazeti hilo, ziara ya Rais Obama aliyoifanya hivi karibuni katika nchi za Ujerumani na Ireland Kaskazini, japo kulikuwa na gharama kwa walinzi, lakini safari za nchi za Afrika zimeelezwa kuwa na gharama kubwa zaidi.
Tahadhari
Kwa mujibu wa taarifa ya maelekezo ya Ikulu ya Marekani, ambayo Mwananchi imepata nakala yake, watu watakaokuwa kwenye msafara wa Obama wametakiwa kutotumia kachumbari. Pia imewataka kutumia maji ya chupa zaidi.
“Kutokana na mfumo wa maji uliopo, tunashauri watu wetu kutumia maji ya chupa zaidi kwa kunywa na hata kwa kupiga mswaki,” ilisema taarifa hiyo.
Kwa kuelewa fika tatizo la ugonjwa wa malaria nchini, ujumbe wa Obama umeshauriwa kutumia dawa ya mbu ya kupaka na kupuliza inayoitwa Deet.

Deet ni dawa maarufu huko Marekani na ikiwa katika aina tofauti ikiwamo ya kupaka na kupuliza na imekuwa ikitumiwa na jeshi la Marekani kwenye vita mbalimbali tangu miaka ya 1940 kabla ya kuanza kutumiwa na raia mwaka 1957.
ATM nazo noma
Pia watu watakaokuwa kwenye msafara wa Rais Obama wametakiwa kuhakikisha wanatumia mashine za kutolea fedha (ATM) zilizoko karibu na hoteli watakazofikia.
“Kuna tatizo la uhalifu kwa hiyo siyo vizuri kutumia ATM ambazo ziko katika sehemu zisizo salama. Pia katika kipindi watakachokuwa Tanzania watu wanapaswa kutumia teksi ambazo zimeidhinishwa na hoteli.
“Pia siyo vizuri kuacha kompyuta ya fedha kwenye vyumba mtakavyolala. Pia kina mama wanapaswa kuchukua tahadhari ya mabegi yao watakapokuwa wanapita mitaani,” ilitahadharisha taarifa hiyo.


Chanzo:Mwananchi

Ngono Kinyume na Maumbile zaongezeka Tanzania

Taasisi ya Kupambana na Ukimwi
Nchini (Tacaids) imesema tafiti
mbalimbali zinaonyesha kuwa
vitendo vya ngono kinyume na
maumbile vinazidi kuongezeka.
Hayo yalisemwa jana na Dk.
William Kafura, katika mkutano
wa sita wa Chama cha Wabunge
cha Kupambana na Ukimwi
(Tapac).

Alisema hiyo inatokana na
imani za kishirikina kwamba
wakifanya vitendo hivyo
watapata bahati kwa
kupandishwa vyeo.

“Lazima tukubali tatizo lipo na
tulitafutie suluhisho, utafiti upo
umefanywa na Muhimbili,
umefanywa na chuo kikuu cha Dar
es Salaam, umefanywa na Tasisi ya
Utafiti ya Ifakara,” alisema.
Alisema pia wafanyabiashara
wanaamini kwa kufanya
vitendo hivyo watajirika wakati
wanawake wanaamini kuwa
watazidi kupendwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa
TACAIDS, Dk. Fatuma Mrisho,
alisema utafiti uliofanyika nchini
unabainisha kuwa wanawake
hawana uelewa wa kutosha juu ya
kujikinga na maambukizi ya
ukimwi.

Akizungumzia suala la kujikinga
na ugonjwa wa Ukimwi Dk. Mrisho
alisema kuwa wanaume wana
uelewa mkubwa zaidi kuhusu
ugonjwa huo kuliko
wanawake.Hata hivyo, alisema
kwa sasa ipo kazi kubwa ya kutoa
elimu kwa wananchi na hivyo
kuwataka wabunge na viongozi
mbalimbali kutoa elimu juu ya
kujikinga na gonjwa hatari la
ukimwi.

Aidha Mrisho alisema kuwa kwa
sasa Mkoa wa Njombe unaongoza
kwa maambukizi ya Virusi vya
ukimwi kwa asilimia 14.8 ambapo
Unguja Kaskazini inamaambukizi
madogo kwa asilimia 0.1.
Hata hivyo alisema kuwa kuna
changamoto mbalimbali ambazo
wanakumbana nazo ni pamoja na
rasilimali za ukimwi kwa serikali,
mashirika ya Dini na sekta binafsi
kuwa pungufu kuliko mahitaji.
Alisema pamoja na kuwepo kwa
changamoto lakini nia ni kufikia
sifuri tatu ifikapo mwaka 2015 na
hiyo hipo katika ulimwenguni,
Afrika hapa hapa Tanzania.

Shomary Kapombe Kwenda Fc Twenty Kufanya Majaribio

Beki wa kimataifa wa Tanzania
na timu ya Simba, Shomari Kapombe
anatarajiwa kuondoka nchini hivi karibuni
kwenda nchini Uholanzi kwa ajili ya majaribio ya
kucheza soka la kulipwa katika klabu ya FC
Twente.

Kapombe mwanasoka bora wa mwaka huu
amekuwa na mafanikio makubwa tangu
alipojiunga na Simba akitokea Polisi Morogoro
miaka mitatu iliyopita kwa kuisaidia Simba
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.

Hivi sasa Kapombe anatarajiwa kwenda kufanya
majaribio katika klabu ya FC Twente, ambayo
ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uholanzi katika
msimu wa 2009-10, pia ilifanikiwa kucheza hatua
ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika
msimu huo.

Katika msimu uliopita FC Twente imemaliza
katika nafasi ya sita katika Ligi Kuu ya Uholanzi
ikiwa na pointi 62, huku Ajax wakiwa mabingwa
kwa pointi 76.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Swed
Nkwabi akizungumza na Mwananchi jana jijini
Dar es Salaam alisema,"timu atakayokwenda
kufanya majaribio Kapombe huko nchini
Uholanzi ni FC Twente, suala la ataondoka lini
kwenda kufanya majaribio tutawaambia safari
itakapokuwa tayari."

Akizungumza katika kipindi cha Spoti Leo cha
Radio One juzi, Mwenyekiti wa Simba, Ismail
Aden Rage alisema amekwishatoa kibali kwa
Kapombe kuondoka nchini siku yoyote kuanzia
sasa kwa ajili ya kufanya majaribio nchini
Uholanzi.

Alisema Kapombe alitakiwa kuondoka mapema kwa ajili ya majaribio hayo, lakini mpaka hivi sasa
amechelewa zaidi ya siku saba kutokana na kuisubiri mechi ya Taifa Stsr dhidi ya Ivory Coast ya kuwania
kufuzu Fainali za Kombe la Dunia imalizike.

Katika mchezo huo wa kusaka kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2014, dhidi ya Ivory Coast,
Kapombe alichangia kupatikana kwa bao la pili la Taifa Stars lililofungwa na Thomas Ulimwengu.

Akizungumzia safari hiyo ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka nchini Uholanzi, Kapombe
alisema mimi nimeambiwa kuhusu safari hiyo, lakini sijui ni timu gani ninayokwenda kufanya nayo
majaribio."

"Sijui ni lini nitaondoka kwa sababu hivi sasa mimi ni majeruhi, niliumia katika mchezo dhidi ya Ivory
Coast na nimetakiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki moja au mbili,"alisema Kapombe.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage alitoa ushauri kwa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) kumruhusu mchezaji huyo kwenda kwenye majaribio hayo kwani akifanikiwa itakuwa ni faida.

''Unajua kwa sasa Taifa Stars wanajiandaa na
michuano ya fainali za wachezaji wanaocheza
ligi za ndani ya Afrika (CHAN), TFF wanaweza
kumzuia mchezaji huyo kwa ajili ya maandalizi
hayo, nawaomba wasifanye hivyo,"alisema
Rage.

Hii ni mara ya pili kwa Rage kutangaza kuwa
Kapombe anatakiwa kufanya majaribio nje
baada ya kumuhusisha beki huyo na winga
Ramadhani Singano kutakiwa kufanya majaribio
katika klabu ya Sunderland ya England.

Mapema mwezi Februari, Rage alikaririwa
akisema Kapombe na Singano wataondoka
kwenda London mwishoni mwa msimu wa ligi.


Chanzo: Mwananchi.co.tz

Polisi Jamii waendeleza Kwata kwa Katavi Warriors

Timu ya Polisi jamii kutoka Mkoani mara wilayani Bunda imeendeleza ubabe kwa Katavi Warriors Kutoka Mkoani katavi baada kufanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo yake iliyopigwa nyumbani na ugenini katika ligi ya Tff hatua ya mtoano.

 Mchezo wa kwanza ulifanyika mkoani mara ambapo Katavi walikubali kichapo cha goli mbili kwa nunge. Mchezo huo uliwaweka Katavi katika mazingira magumu ambapo waliitaji ushindi wa Goli tatu bila ili kuwezesha kufuzu round inayofuata.
Polisi jamii wakishangilia
  
 Katika mchezo wa leo(Alhamisi 21 june) ulioanza kupigwa majila ya saa kumi na nusu jioni. Katavi warriors walikuwa wanahitaji ushindi wa kuanzia goli mbili, ambapo walifanikiwa kupata ushindi huo na kufanya matokeo ya jumla kusomeka (2-2), magoli hayo yaliyopachikwa kipindi cha pili cha mchezo yaliwezesha mchezo kuingia katika hatua ya kupigia penati. Ambapo walikuwa ni Polisi walioanza kupiga penati hizo.
 Ambapo piga nikupige ya penati zote tano ilikamilika kwa kila timu kuwa imepata penati 4 ya 5 ambapo iliongezwa moja kila upande, 

Walikuwa ni Polisi walioweza kutumia nafasi hiyo vizuri na kuweza kufunga, huku Mcheza wa Katavi Emmanuel akishindwa kutupia mpira kambani. kwa kipa wa Polisi kuicheza penalty kwa ustadi kama inavyoonekana pichani chini.
Kipa Akicheza Penati ya Mwisho
 Hiyo ndiyo ilikuwa safari ya mwisho ya wana katavi kuweza kusonga mbele. katika michuano hiyo ya TFF ngazi ya mtoano. Katavi mpaka kufikia hapo waliziondosha timya Ya Rukwa United na Saigon Fc kutoka mjini kigoma.

Kocha wa Katavi Warriors
Katavi wamekuwa wazuri katika uwanja wa Nyumbani Azimio, kwa kutoruhusu kushindwa katika uwanja huo. Hakika Polisi jamii wavunja rekodi hiyo kwa kuchomoza na ushindi katika uwanja huo.

Wachezaji wa Katavi wakiwa na huzuni.


Kocha Mkuu wa Polisi Jamii

Polisi Jamii wakishangilia
Mashabiki waliofulika kuja kuangalia mechi

Baada ya Mechi

                                Tazama jinsi polisi jamii walivyokuwa wakishangilia ushindi huo


Kila la heri Polisi jamii huko mbele ya safari, na Maandalizi mema kwa Katavi Warriors(AstonVilla) kwa ajili ya Ligi msimu ujao.

Picha Ya Siku | Picture of the Day

Mzee Aboud Jumbe afikisha miaka 93

Imeelezwa kuwa moja kati ya
neema alizopewa
mwanaadamu ni umri mrefu
hivyo ni wajibu wa kila mmoja
wetu kuutumia vyema uhai
wake kwa kutenda mema na
kushukuru kila siku kwani
hapaswi mwanaadamu kuwa
aasi bali anachotakiwa ni
kumuabudu Mola wake
aliyemuumba.

Kadhi mkuu wa Zanzibar
Sheikh Khamis Haji Khamis
ameyasema hayo katika dua ya
kumshukuru Mwenyezi Mungu
kutimiza miaka 93 ya kuzaliwa
kwa Rais Mstaafu wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar Alhajj
Aboud Jumbe Mwinyi
iliyofanyika Kiembe Samaki.

Sheikh Khamis Haji ametowa
ukumbusho kwa kusema kuwa
“ Ifanye dunia kama kwamba
utaishi milele kwa maana ya
kutenda mazuri na kumuabudu
Allah kama tulivyoamrishwa
katika dini pia ifanye akhera
yako kama utakufa sasa kwa
maana ya kujiandaa kwa
kutenda amali njema na
kuomba msamaha kila siku.

Katika khutba yake iliyosomwa
na Ustadh Moh’d Yoyota kwa
niaba yake Rais Mstaafu
Awamu ya Pili Alhajj Aboud
Jumbe amesema kuwa
anamshukuru Mola wake kwa
umri aliyomjaalia kwani
ameshuhudia neema nyingi
ambazo hazina kiima kisicho
kifani,kina wala mizani katika
maisha yake na kupitia nyanja
tofauti za maisha hadi M/
Mungu atakapomjaalia mwisho
wa maisha yake.

Alhajj Aboud Jumbe ameongeza
kusema kuwa anamshukuru
Mola wake kwa kumpa rehema
zake huruma na hisani pale
alipokabidhiwa dhamana ya
kuongoza baadae kumnusuru
na kumfariji na hatimae
kumuongoza pale alipoteleza
mnamo asiyoyaridhia kwani
majibu sahihi ya mithani yetu
wanaadamu yanasubiri siku
ya malipo ambayo yatupasa
tutambue kuwa kila mmoja
wetu atakutana nayo.

“Namuomba Mwenyezi Mungu
kwa unyenyekevu azidi
kuitakasa amali yangu na
kunipa khusni l khatima mimi
pamoja na waislamu wenzangu

Akitowa shukurani kwa
waalikwa waliohudhuria
katika dua hiyo kwa niaba ya
familia ndugu Mustafa Aboud
Jumbe ambae ni mtoto wake
amesema kuwa lengo la
kusoma dua hii ni
kukumbushana namna gani
tunatumia neema na kila
mmoja vipi atautumia uhai
wake na kusisitiza kuwa dua
hio ni mwenyewe baba yao
aliyetowa utaratibu juu ya
namna gani isomwe dua hio
“Tumekuwa tukipata masuala
mengi kuhusu hali ya mzee
wetu jibu ni kwamba hajambo
ila uzee tu ndio unaomsumbua,
nuru ya macho
imepotea ,kusikia kumekuwa
shida kidogo lakini anasikia
na anazungumza na hii
shughuli yake ya leo amepanga
mwenyewe”alisisitiza Mustafa
Jumbe.

Nae Sheikh Moh’d Iddi
ametowa wito kwa jamii
kufanya matendo mema kwani
kuwepo kwetu ipo historia
ambayo M/ Mungu
amewashushia waja wake na
aliyebahatika kuishi kwa
kumuabudu huyo atakuwa
amefaulu.
Miongoni mwa waliohudhuria
katika dua hio ni pamoja na
Kadhi Mkuu Mstaafu Sheikh
Habib Ali Kombo baadhi ya
Masheikh, Familia yake,
baadhi ya wanafunzi aliwahi
kuwasomesha na
kuwafundisha kazi

Chanzo:IssaMichuzi

Katavi Warriors Wakubali Kwata

Timu ya soka mabingwa na kiboko wa timu za Saigon na Rukwa United, Katavi Warriors kutoka mkoani Katavi Wamekubali kupiga kwata kutoka kwa Polisi Jamii ya mkoani Mara kwa goli mbili bila (2-0).

Katavi walikubali kichapo hicho katika kipindi cha pili cha mchezo huo. Kutokana na kufungwa huko Katavi wataitaji ushindi wa goli 3 kwa bila ili kuweza kufuzu kwa round inayofuata.

Mchezo wa marudiano unatalajia kufanyika baada ya wiki moja katika uwanja wa Azimio ambao umekuwa mgumu sana kwa timu za ugenini kuibuka na ushindi.

Aston Villa kama inavyofahamika katika mita ya Majengo, Makanyagio, kawajense na viunga vyote vya Nsemula na mpanda kwa ujumla. Wameingia katika hatua hiyo baada ya kuwaondosha Rukwa United kutoka Sumbawanga mkoani Rukwa na Saigon Fc kutoka Kigoma.

Timu zote zinashiriki ligi ya TFF ngazi ya mtoa ili kufuzu na kuingia ligi kuu. Kila la heri kwa Katavi Warriors katika mchezo wa marudiano.

Miaka 67 Jela Kwa Ujambazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi
Moshi, mkoani Kilimanjaro
imewahukumu raia wawili wa
Kenya na mwanamke mmoja
Mtanzania jela miaka 67 baada
ya kupatikana na hatia ya kula
njama na kupora Sh milioni
239 kutoka benki ya NMB tawi
la Mwanga, Kilimanjaro.

Uporaji huo ulifanyika Julai
11,2007 ambapo pia watu hao
waliiba bunduki aina ya Sub
Machine Gun (SMG) mali ya
Jeshi la Polisi nchini, na
kumuua askari Polisi Michael
Milanzi aliyekuwa lindo.
Watuhumiwa hao waliofungwa
ni Samweli Gitau maarufu kwa
jina la Saitoti na Michael
Joseph Kimani (wote kutoka
Kenya) na Mtanzania Elizabeth
Elias maarufu kwa jina la Bella
mkazi wa Kwangulelo mkoani
Arusha.

Jopo la makakimu watatu
wakiongozwa na Panterine
Kente liliwahukumu kwenda
jela miaka saba kwa kosa la
kwanza ambalo ni kula njama;
miaka 30 kila mmoja kwa kosa
la uporaji pamoja na miaka 30
kwa kosa la wizi wa silaha.

Hakimu huyo alisema kuwa
adhabu hizo zinaenda pamoja
hivyo washitakiwa
watatumikia kifungo cha
miaka 67 jela, mbali na
hukumu hiyo Mahakama hiyo
pia iliwaachia huru ndugu
watatu ni ambao ni Devotha
Elias Masenza, Ntibasana Elias
Masenza na Julian Elias
Masenza na mtu mwingine
Calist Kanje baada ya ushahidi
dhidi yao kushindwa
kuishawishi Mahakama.

Kabla ya kutoa hukumu hiyo ,
wakili wa Serikali Tamali
Mndeme aliomba Mahakama
kutoa adhabu kali kwa
washitakiwa ili iwe fundisho
kwa watu wengine wenye nia
ya kutenda makosa kama
hayo.

Chanzo:Habarileo

Majasusi Wajipanga Kiusalama Ziara ya Obama

Idara ya Ujasusi ya Marekani
imeweka bayana kwamba inajitegemea kwa
ulinzi katika ziara nzima ya Rais Barack Obama
kwa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika
Kusini na Senegal.

Kwa mujibu wa taarifa ya idara hiyo, katika
kuhakikisha usalama wa kutosha wakati wa
ziara ya Obama tayari maofisa wao
wameshakamilisha maandalizi ya kiusalama
katika nchi zote anazotarajiwa kutembelea.

Meli ya kivita kutua bandarini
Katika kuchukua hatua hizo, meli kubwa kabisa
ya kivita yenye hospitali maalum zipo tayari kwa
ya kambi maalumu katika bandari maalum za
nchi atakazotembelea, kwa ajili ya kukabiliana
na dharura yoyote ya kiafya ya Obama na familia
yake.

Ili kuwawezesha maofisa wa kijasusi wa
Marekani, ndege ya kijeshi ndiyo itakayobeba
magari 56 zikiwemo limousine 14 na magari
matatu maalumu ya kubeba mizigo.

Malori hayo yatakuwa yakibeba vioo ambavyo
ni vizuizi maalumu vya risasi na milipuko kwa
ajili ya kuongeza ulinzi kwenye hoteli
atakazolala yeye na familia yake.

Ndege za kivita kutawala anga
Ndege za kivita zitakuwa zikiruka kwa zamu
wakati wote muda wa sasa 24 kwa ajili ya
kuhakikisha ulinzi katika sehemu atakayokuwa
Rais Obama na kudhibiti anga yote kwa wakati
huo dhidi ya ndege yoyote ngeni itakatosogea
usawa wao.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na
Mwananchi, hakuna Maandalizi ya safari hiyo
ambayo tayari yamekamilika yanapolinganishwa na safari nyingine za aina hiyo zilizowahi kufanyika,
waraka maalumu kuhusu suala la usalama unaonesha kwamba kumekuwa na juhudi za ziada
zakuhakikisha ulinzi wa Amiri jeshi huyo Mkuu wa Marekani akiwa nje ya nchi.

Kabla ya safari yake kwa nchi za Afrika, Obama atatembelea Ireland na Ujerumani ikiwa ni sehemu ya
kuongeza changamoto inayokabili masuala ya usalama wake.

Lakini zaidi, safari ya Obama kwa nchi za Afrika inadhaniwa kuwa inayolazimisha waandaaji kuwa na
umakini wa hali ya juu na kuifanya iwe aghali zaidi katika utawala wa Obama kuliko ziara katika nchi za
ulaya, kwa mujibu wa wataalamu wa mipango.

Familia ya rais huyo inatarajiwa kutembelea nchi tatu za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini na
Senagal kuanzia Juni 26 hadi Julai 3 mwaka huu.

Chanzo:Mwananchi.co.tz

Breaking News: Bomu lalipuka Arushah

Kwa habari mpasuko kutoka jijini Arusha ni kuwa kitu kinachosadikika kuwa ni bomu kimeripuka katika Mkutano wa Chadema na kujeruhi saba(7). Watu wanne waripotiwa kufa

Habari zaidi zitafuata.

Source: ITV

Majambazi Wauwa na Kupora

Watu watano wanaosadikiwa
kuwa majambazi wakiwa na silaha
mbili bunduki  aina ya SMG
wamemuwa kwa kumpiga risasi
mbili tumboni Juma  Mabula ( 36)
mfanyabiashara wa Bariadi
Shinyanga na kumpola mamilioni
ya fedha ambazo kiasi chake
hakija fahamika  na kumjeruhi
kwa kumpiga  risasi mbili
tumboni Cosmas Michael ( 28)
mfanya biashara wa Bariadi
Shinyanga  na kumpora fedha
tasilimu milioni tatu.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa
Katavi Dhahiri Kidavashari
alisema tukio hili lilitokea  juzi
majira ya saa mbili usiku  katika
kijiji  cha Itunya  kata  ya
Kapalamsenga Tarafa ya Karema
wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi
Alisema majambazi hao  kabla ya
kufanya tukio hilo waliwavamia
Adolfu John (20 ) na kumpora
fedha  tasilimu Tsh 4, 000, 000/=
na Richard Charles (25)
alimporwa  Tsh 5,000,000/= ambao
ni wafanya biashara na wakazi
wa Kijiji cha Kakese Wilaya  ya
Mpanda
Kidavashari alieleza kuwa
wafanya biashara hao walikuwa
wamekwenda kijijini hapo kwa
lengo la kununua zao la mpunga
linalopatikana kwa wingi kwenye
kijiji hicho  na ndipo walipo patwa
na tukio hili.

Alisema katika eneo la tukio hilo
liliokotwa ganda moja la risasi
aina ya bunduki ya SMG
lililotumika likiwa karibu  na
mwili wa marehemu Juma Mabula
Baada ya jeshi la polisi kupata
taarifa lilifika katika eneo hilo la
tukio na waliendesha msako
mkali  na kuwakamata watu
wanne kuhusiana na tuhuma  za
tukio hilo
Kamanda Kidavashari aliwataja
watu hao wanao shikiliwa na
polisi kuwa ni Mussa Mathias
(36), Ngusa Tola (37),  na Shinde
Jiyaago ( 34) wote wakazi wa
kijiji cha Nkuswe Tarafa ya
Karema wilayani hapa na Doto
Kayungilo (25) Mkazi wa kijiji
cha Mnyamasi Tarafa ya Kabungu.

Alisema majeruhi Cosmas
Michael ambaye amelazwa katika
Hospital ya Wilaya ya Mpanda
anaendelea kupata matibabu na
hali yake inaendelea vizuri
Kamanda Kidavashari amewataka
wananchi wa Mkoa wa Katavi
kuwabaini wageni wanaofika
kwenye maeneo yao na kutoa
taarifa kwa Jeshi la Polisi  za
kuwaarifu watakao wabaini au
kuwatilia shaka watuhumiwa ili
waweze kukamatwa  kabla ya
kutenda tukio.

Ivory Coast Watwangana

Wachezaji wawili wa Ivory Coast
wametimuliwa kwenye kikosi
kinachojiandaa na mchezo kuwania
kufuzu michuano ya kombe la dunia
mwaka 2014 dhidi ya Tanzania
unaotarajiwa kupigwa uwanja wa
Taifa siku ya Jumapili.

Mchezaji wa zamani wa Monaco
Jean-Jacques Gosso Gosso, 30,
ambaye kwa sasa anakipiga kwenye
ligi ya Uturuki akiichezea Mersin na
kinda la miaka 20 Abdul Razack wa
Manchester City, ambaye kwa sasa
yupo kwa mkopo Charlton Athletic,
walipigana siku ya jumatano wakati
timu yao ikiwa kwenye maandalizi ya
mwisho kabla ya kuja Tanzania usiku
wa leo.

FA ya Cote D'Ivoire imesema
kwamba adhabu nyingine zinaweza
kufuatiwa kutegemea na kamati ya
nidhamu itakavyoamua.

Wakati huo huo timu hiyo ya Ivory
Coast imeshafika nchini na
wamefikia kwenye hoteli ya Bahari
Beach.

Nelson "Madiba" Mandela Aendelea Vizuri

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
amesema kuwa afya ya rais wa
zamani wa taifa hilo Nelson
Mandela imeanza kuimarika
kidogo kutokana na matibabu
anayopewa na Madaktari wake
jijini Pretoria.

Zuma amewaambia wabunge kuwa
Mandela anayefahamika kwa jina
maarufu kama Madiba ameanza
kuimarika na ni habari njema kwa
raia wa nchi hiyo ambao
wamekuwa wakikumbwa na
wasiwasi kutokana na afya yake
kuendelea kudorora.

Rais huyo ameongeza kuwa kila
mmoja anakumbuka mchango wa
Mandela ambaye alifungwa jela
miaka 27 akiwa katika harakati za
kupinga ubaguzi wa rangi nchini
humo na baadaye kufanikiwa
kuwa kiongozi wa kwanza mweusi
nchini humo mwaka 1994.

Kiongozi huyo wa Afrika Kusini
amewataka raia wa nchi hiyo na
dunia nzima kuendelea
kumwombea Mandela ili apate
nafuu haraka na kuruhisiwa
kurudi nyumbani.

Familia ya Mandela imesema kuwa
imeguswa mno na salamu za heri
njema zinazotumwa na watu
mbalimbali duniani kumtakia
kiongozi huyo wa zamani nafuu ya
haraka.

Mandela mwenye umri wa miaka
94 alilazwa hospitalini Jumamosi
iliyopita baada ya kuanza
kusumbuliwa na mapafu tatizo
ambalo limemsumbua kwa muda
mrefu.

Hii ni mara ya nne kuanzia mwezi
Desemba mwaka uliopita kwa
Mandela ambaye atatimiza miaka
95 mwezi ujao kulazwa hospitalini
na mara ya mwisho ilikuwa mwezi
Aprili mwaka huu.

Mara ya mwisho kwa Mandela
kuonekana hadharini ilikuwa
mwezi Julai mwaka 2010 wakati
wa ufunguzi wa mashindano ya
soka ya kombe la dunia nchini
humo.

Ajilipua na Moto Baada ya Kugomewa Kumuona PM

Kijana mmoja nchini Jordan
ambaye siku chache zilizopita
alikataliwa kuonana na Waziri wa
Ustawi wa Jamii wa Jordan na
kuamua kujiteketeza, amefariki
dunia hii leo kwenye hospitali ya
serikali mjini Amman.

Kijana huyo yatima aitwaye
Ahmad Rubain mwenye umri wa
miaka 23 ambaye siku ya Alhamisi
iliyopita alitaka kuonana na
Waziri wa Ustawi wa Jamii na
kumuelezea matatizo na hali
ngumu ya maisha inayomkabili,
aliamua kujiteketeza moto mbele
ya jengo la wizara hiyo baada ya
juhudi zake za kutaka kuonana na
waziri kugonga ukuta.

Msemaji wwa Hospitali ya serikali
ya al Bashir mjini Amman
amesema kuwa, asilimia 90 ya
mwili wa kijana huyo ilikuwa
imeteketea.

Hili ni tukio la tano
la kujichoma moto katika
kipindi cha miaka miwili nchini
humo.

Ni miaka miwili na nusu sasa
Jordan inakabiliwa na wimbi
kubwa la maandamano ya
wananchi wanaotaka yafanyike
marekebisho ya kisiasa, kiuchumi
na mapambano dhidi ya ufisadi
nchini humo.

Ngono Ya Mdomo Inasababisha Saratani

Saratani imeendelea
kuwa tishio hapa nchini huku hofu
ikiendelea kuikumba jamii kutokana na
wataalamu wa afya kushindwa
kufahamu tiba halisi ya maradhi hayo
hatari.

Takwimu kutoka Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road zinaonyesha ongezeko la
saratani ya mdomo na koo kwa kiasi
kikubwa kutoka kesi 167 mwaka 2006
hadi 277 mwaka 2012.

Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Ocean
road, Julius Mwaiselage anaeleza kuwa
watanzania wasipende kuiga mambo
ambayo si sahihi bila kujua madhara
yake kama kufanya mapenzi kwa njia
ya mdomo. "Saratani ya mdomo ipo,
na nyingine zinasababishwa na zinaa "
anasema Dk Mwaiselage
Tafiti mbalimbali zimewahi kufanyika
nchini na kubaini kuwepo kwa
ongezeko la saratani ya mdomo.

Utafiti
uliofanywa na Dk Innocent Mosha wa
Kitengo cha Patholojia cha Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH), umebaini
aina za saratani 1,594, kati ya hizo 509
zikiwa ni za midomo kwa mwaka 2003
pekee.

Matokeo hayo yanaonyesha kuwa kati
ya saratani 509 za mdomo, saratani
242 zilisababishwa na Virusi vya
Human Papiloma ambavyo hutokana
na zinaa.

"Ninachojua mimi ni kuwa Virusi vya
HPV husababishwa na magonjwa ya
zinaa, hivyo mtu anayeugua saratani ya
aina hiyo, imetokana na zinaa,"
anasema Dk Mosha.

Takwimu hizo ni zile zilizopatikana kwa
watu waliokwenda kufanyiwa
uchunguzi katika Mkoa wa Dar es
Salaam pekee.

Dk Mosha anasema kuwa wanaume
ndiyo huathiriwa zaidi na saratani ya
mdomo ambapo kwa hapa nchini,
asilimia 53 ya wanaume waliofika MNH
kwa ajili ya vipimo, walibainika kuugua
saratani hiyo, huku wanawake wakiwa
ni asilimia 47.

Utafiti kama huo ulifanywa pia na Dk
Amos Mwakigonja, mkuu wa Idara ya
Patholojia katika Chuo Kikuu cha Tiba
cha Muhimbili (MUHAS).

Dk Mwakigonja alifanya utafiti wa
saratani ya mdomo aina ya Kaposi's
Sarcoma ambapo wagonjwa 78
walibainika na saratani hiyo kuanzia
mwaka 1990 hadi 2003.
"Saratani za
mdomo zipo za aina nyingi na
zimetofautiana kulingana na
visababishi vyake," anasema Dk
Mwakigonja.

Katika utafiti wake Dk Mwakigonja
alibaini kuwa wanawake wengi
walikuwa na saratani ya mdomo aina
ya Kaposi's Sarcoma kuliko wanaume.

Hata hivyo, utafiti huo ulionyesha kuwa
asilimia 50 ya wanaume walikuwa na
saratani ya mdomo hatari zaidi
(systemic) kuliko wanawake ambao ni
asilimia 37.

Mapenzi kwa mdomo husababisha
maradhi
Dk Mwakigonja anasema kuwa
mapenzi yoyote kwa njia ya mdomo
lazima yasababishe maradhi ya zinaa
iwapo mmoja ameambukizwa.

Pia anasema kwamba sampuli nyingi
za wanaume wanaojihusisha na
mapenzi na wanaume wenzao
(mashoga) zilibainika na saratani ya
mdomo.

Utafiti huo ni sehemu ya utafiti wa
Shahada ya Uzamivu ambao
ulionyesha kuwa wagonjwa wengi wa
saratani ya mdomo walikuwa ni
wanaume wenye umri wa miaka kati ya
38 na kuendelea na wanawake ni 31.

Ufatiti wa WHO Tanzania

Shirika la Afya Duniani (WHO) pia
lilifanya utafiti mwaka 2010 nchini kwa
kushirikiana na Kituo cha Taarifa za
HPV, ambapo ilibainika kuwa asilimia
20 ya saratani za koo na mdomo nchini
zinasababishwa na ufanyaji wa
mapenzi kwa njia ya mdomo.

Taarifa hizo za WHO zinaeleza kuwa
wanaume 747 hugundulika na saratani
ya mdomo kila mwaka wakati
wanawake 472 hubainika na saratani
hiyo pia.

Wakati huohuo, wanaume
wanaopoteza maisha kutokana na
saratani hiyo ni 444, kwa mwaka na
wanawake ni 270, kwa mwaka.

Utafiti wa WHO umebaini kuwa saratani
ya mdomo inashika nafasi ya sita katika
aina 24 za saratani 24 zinazoisumbua
zaidi Tanzania.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa wanaume
wanaoathirika zaidi ni wenye umri wa
kati ya miaka 15 na 55, ambao tayari
wameshaanza kujihusisha na ngono.

Kama maradhi mengine ya
kuambukiza, Virusi vya HPV
huambukizwa kwa urahisi zaidi kutoka
kwa wanawake kwenda kwa wanaume
kuliko kutoka kwa wanaume kwenda
kwa wanawake.

Utafiti huo uliodhaminiwa na mfuko wa
Bill na Melinda Gates na Kituo cha
Saratani na Mpango wa Utafiti wa
Taasisi ya ICO unaeleza kuwa mitandao
ya kijamii na picha za ngono ndiyo
chanzo cha watu wengi kuiga ufanyaji
wa mapenzi ya aina hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la The New York
Times, tafiti zimefanyika na kubaini
kuwa asilimia 70 ya wagonjwa
wanaobainika na saratani ya koo na
mdomo duniani, husababishwa na
Virusi vya Human Pappiloma
vinavyotokana na magonjwa ya zinaa.

Tafiti hizo zinaonyesha kuwa wagonjwa
wengi wanaogundulika na saratani
hiyo ni wanaume wenye umri wa kati,
wenye uwezo wa kifedha, wasiovuta
sigara wala siyo walevi waliokubuhu.

Utafiti huo ulibaini kuwa wanaume
wapo hatarini zaidi kupata saratani ya
koo inayosababishwa na Virusi vya
HPV.

Miaka ya 80, idadi ndogo ya watu
waliougua saratani ya koo
walihusishwa na maambukizi ya Virusi
vya HPV.

Kihistoria, watu waliobainika na
ugonjwa huo, ni wenye umri wa miaka
70 kwenda juu ambao walikuwa ni
wale walevi waliokubuhu na wavuta
sigara.

Ilielezwa kuwa Virusi vya HPV vipo kwa
wingi kiasi ambacho watu wazima
wanaojihusisha na ngono ya aina
yeyote ile, huweza kupata maambukizi
ya zinaa hata kama siyo saratani.

Hata hivyo ilibainishwa kuwa saratani
isababishwayo na virusi vya HPV ni
rahisi kuitibu kuliko saratani ya koo
isababishwayo na tumbaku au pombe
kali.

Virusi vya HPV ni nini?
Kwa jina la jumla, saratani ya koo au
mdomo huitwa saratani ya kichwa na
shingo. (Neck and Head Cancer)
HPV ni miongoni mwa virusi hatari zaidi
duniani visababishwavyo na magonjwa
ya zinaa na vinaweza kuathiri sehemu
mbalimbali za mwili.

Zipo aina zaidi ya 120 za HPV, baadhi
huweza kuzalisha usugu (warts)
ambazo si saratani katika sehemu za
siri, mikononi na miguuni.

Maambukizi ya HPV hufanyika kwa
urahisi, hata kwa kugusana ngozi au
majimaji, huku maambukizi mengine
yakisababishwa na ngono.

Virusi hatari na vinavyosababisha
saratani ni HPV-16, HPV-18, HPV-31 na
HPV 45.

Aina hii ya Virusi vya HPV husababisha
saratani ambapo uvimbe waweza
kujitokeza kwa ndani na unaweza
usionekane ukilinganisha na vivimbe
vingine vya saratani.

Wataalamu wanasema HPV-16 na
HPV-18 inahusishwa zaidi na saratani
ya shingo ya kizazi na endapo mapenzi
kwa njia ya mdomo yatafanywa na mtu
mwenye uambukizo huu ni rahisi
kuambukizwa.

Jela Miaka Mitatu Kwa Kumuuma Nyeti Mumewe

MAHAKAMA ya Wilaya ya Iramba
mkoani Singida umemhukumu
mwanamke mmoja mkazi wa kijiji
cha Kisana wilayani humo, Sayuni
Ramadhani (42) kwenda jela miaka
mitatu baada ya kukiri kosa la
kumng’ata mumewe sehemu
zake za siri.

Mwendesha mashitaka mkaguzi
wa polisi, Vincent Ndasa alidai
mbele ya hakimu mfawidhi wa
mahakama ya wilaya ya Iramba,
Kariho Mrisho kuwa Juni 4 mwaka
huu saa 12.00 jioni katika kijiji cha
Kisana, mshitakiwa kwa
makusudi alizing’ata kwa meno
sehemu za siri za mume wake,
Onesmo Nathania (42) na
kumsababishia maumivu.

Ndasa alidai kuwa siku ya tukio,
wanandoa hao waliporejea
nyumbani kutoka kwenye klabu
cha pombe ya kienyeji kijijini
hao, kulitokea kutokuelewana
na hivyo kuanza kugombana.

Alidai wakati wanaendelea
kupigana, Onesmo alizidiwa nguvu
na kuangushwa chini na mkewe
ambaye alifungua zipu ya suruali
na kufanikiwa kuzitoa sehemu za
siri za mumewe na kuzing'ata
nusura azitenganishe.

Mwendesha mashitaka aliendelea
kudai kuwa mlalamikaji Onesmo
alipiga yowe na majirani walifika
mara moja na kumkimbiza katika
zahanati ya kijiji kwa ajili ya
matibabu.

Mshitakiwa alipoulizwa iwapo ni
kweli alikiri kosa na akaiomba
mahakama imwonee huruma kwa
kumpa adhabu ndogo kwa kuwa
hilo lilikuwa ni kosa lake la
kwanza na kwamba anahitaji
kuwa na mumewe ili waendelee
kulea idadi kubwa ya watoto wao
kwa pamoja.

Naye mwendesha mashitaka,
Ndasa aliiomba mahakama kumpa
adhabu kali mshitakiwa ili kuwa
fundisho kwake na pia kuogofya
wanawake wanaotarajia
kuwafanyia unyama wa aina hii ya
kung’ata sehemu nyeti za waume
zao.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu
Mfawidhi Mrisho, alisema
mahakama yake imezingatia kwa
makini maombolezo ya
mshitakiwa na kufikia uamuzi wa
kutoa adhabu ya kutumikia jela
miaka mitatu.

Source:habari leo

Paul Kagame Aonesha Dharau Ushauri wa Kikwete

DHARAU za Rais wa Rwanda Paul
Kagame kwa Rais wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania na Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
na Usalama Jakaya Mrisho Kikwete
zimewagawa Watanzania na
kuwafanya wawe na mitazamo
tofauti.

Wapo wanaomuunga mkono
Rais Kagame na wapo pia
wanaompinga kwa kauli yake...

Rais Kagame alimkejeli Rais
Kiwete kwa kuuita ushauri wake
ni ushauri wa kijinga kwa
wanyarandwa,awali Rais Kikwete
alizishauri nchi za Rwanda na
Congo DRC kukutana na kumaliza
tofauti zao kwa njia ya amani.

Rais Kikwete alitoa ushauri huo
wakati wa mkutano wa kujadili
amani na mpango wa ulinzi nchini
Congo DRC uliofanyika katika
Makao Makuu ya AU mjini Addis
Ababa Ethiopia.

Katika ushauri huo Rais Kikwete
alisema kwamba ni vyema Rais
Kagame akakaa katika meza ya
mazungumzo ya amani na Rais wa
Congo DRC Joseph Kabila ili
kumaliza tofauti zao badala ya
kutumia nguvu ya kijeshi.

"Nimekaa kimya kwa kipindi
kirefu na kwa jinsi nilivyoweza
kwa sababu nilifikiri kwamba
mazungumzo ya kipuuzi
yaliyozungumzwa na watu
wajinga yamemalizika "alisema
Rais Kagame.

Katika hatua nyingine Rais Kagame
alisema kwamba ushauri huo wa
Rais Kikwete ni sawa na
kuwachezea wanyarandwa mbele
ya mataifa.

Rais Kagame aliyasema hayo
katika sherehe ya kuhitimu
mafunzo ya maofisa wa jeshi
wapatao 45 katika kituo cha
mafunzo ya kijeshi siku ya Juma
Tatu nchini Rwanda.


NB:
RAIS WETU SIYO MJINGA...
HILO NI TUSI , JK ALIWAPA
USHAURI WA BURE...MLIKUWA
HURU KUUTUMIA AU KUUACHA

Katavi Warriors Kukipiga na Polisi Jamii

Mechi za kwanza za hatua ya tatu ya
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL)
kuwania nafasi tatu za kupanda Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao
zitachezwa Jumamosi (Juni 15
mwaka huu) wakati za marudiano
zitachezwa Jumatano ya Juni 19
mwaka huu.

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imekutana leo (Juni 11 mwaka huu)
jijini Dar es Salaam kupitia ripoti za
michezo iliyopita na kufanya uamuzi
mbalimbali ikiwemo mechi ya
marudiano kati ya Mpwapwa Stars
na Machava FC ambayo
haikuchezwa.

Machava FC ambayo ilishinda mechi
ya kwanza iliyochezwa mjini Moshi
kwa mabao 2-0 inaendelea katika
hatua ya tatu kwa vile haikuhusika
katika kukwamisha mchezo wa
marudiano uliopangwa kuchezwa
Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Dodoma (DOREFA) kiliuhamishia
mchezo huo kwenye Uwanja wa
Mgambo mjini Mpwapwa kinyume
na maelekezo ya Kamati ya
Mashindano ya TFF.

Kamati katika
kikao chake cha awali iliekeleza kuwa
mechi zote za RCL zitachezwa makao
makuu ya mikoa isipokuwa kwa
Morogoro ambapo timu ya Techfort
FC iliruhusiwa kutumia Uwanja wa
CCM Mkamba mjini Ifakara.

Hivyo timu nane zilizofuzu kucheza
raundi hiyo ni Friends Rangers ya
Dar es Salaam, Kariakoo ya Lindi,
Katavi Warriors ya Katavi, Kimondo
SC ya Mbeya, Machava ya
Kilimanjaro, Njombe Mji ya Njombe,
Polisi Jamii ya Mara na Stand United
FC ya Shinyanga.

Wakati timu nyingine zimefuzu kwa
kushinda mechi zao za raundi ya
mbili, Njombe Mji imeingia hatua
hiyo kwa kuwa timu yenye uwiano
mdogo wa kufungwa (best looser)
katika hatua ya pili.

Katika hatua hiyo mechi ni ifuatavyo;
Kariakoo vs Friends Rangers,
Machava FC vs Stand United FC,
Polisi Jamii vs Katavi Warriors, na
Kimondo SC vs Njombe Mji. Timu
zilizoanza kutajwa ndizo zinazoanzia
nyumbani.

Vilevile Kamati ya Mashindano
imeagiza Kamishna wa mechi ya
marudiano kati ya Mpwapwa Stars
vs Machava FC, Mwijage Rugakingira
wa Tanga ambaye alikwenda Uwanja
wa Mgambo badala ya Uwanja wa
Jamhuri kinyume na maelekezo ya
TFF aondolewe kwenye orodha ya
makamishna.

Pia waamuzi wa mechi hiyo ambao
nao walikwenda Mpwapwa badala
ya Dodoma Mjini wamepelekwa
Kamati ya Waamuzi ya TFF kwa ajili
ya kuchukuliwa hatua kutokana na
tukio hilo.

Kamati ya Mashindano
imekumbusha kuwa RCL ni
mashindano yanayosimamiwa na
TFF, hivyo maelekezo yoyote
kuhusiana na mashindano hayo pia
yatatoka TFF na si mahali pengine
popote. Hivyo, msimamizi wa kituoa
hana mamlaka ya kubadili uwanja.

Hatua ya nne ya RCL itachezwa kati
ya Juni 23 na 23 mwaka huu wakati
mechi za marudiano zitachezwa kati
ya Juni 29 na 30 mwaka huu.

Aliyetoa Siri za CIA Ajificha

Mwanamume aliyefichua habari za
ujasusi za Marekani, akiwa Hong
Kong, sasa ametoweka hotelini
mwake.

Edward Snowden aliambia
waandishi wa habari kuwa ameishiwa
na pesa na alisema ana hakika kuwa
maafisa wa usalama wa Marekani
watamtafuta kokote aliko.

Mfanyakazi huyo wa zamani wa CIA,
mwenye umri wa miaka 29, aliyekuwa
akifanya kazi na CIA alisema kuwa
maafisa wa kijasusi wa Marekani
walitumia mitambo maalumu
kupekua simu, barua pepe na aina
nyingine za mawasiliano kote duniani.

Alisema kuwa alifichua njma hiyo kwa
sababu aliamini ilikuwa kinyume cha
demokrasia.

Ikulu ya White House haijasema iwapo
itatoa amri ya Edward Snowden
kurudishwa nchini ili kushtakiwa kwa
kosa hilo.

Msemaji wa Ikulu, Jay
Carney, alikataa kufafanua ila akaeleza
tu kuwa uchunguzi unaendelea na
akakariri kuwa kitendo cha Snowden
kimehatarisha usalama wa Marekani.

Ingawa kuna wale ambao wamtaja
Snowden kama msaliti kwa taifa, kuna
wale waliomshangilia kama shujaa wa
kitaifa.

Maelfu ya watu wametia sahihi
katika mtandao wa Ikulu ya White
House wakitaka asamehewe kwa
makosa yo yote ambayo huenda
ameyafanya kisheria.

Huku mjadala ukiendelea iwapo
Snowden alifanya kosa au la ni
dhahiri sasa kuwa idara ya ujasusi ya
Marekani itatafuta njia nyingine ya
kukusanya habari zake za kijasusi.

Itabidi wajue iwapo kuna watu wengi
kuliko inavyodhaniwa wanaofahamu
siri za Serikali, ambao wanaweza
kuzifichua kwa umma wakati wo wote.

Misri Watoa Onyo kwa Ethiopia

Rais wa Misri Mohammed Morsi
amesema kuwa taifa lake litatumia kila
mbinu kuhakikisha kuwa Ethiopia
inasitisha ujenzi wa bwawa la maji
katika mto Nile.

Idadi kubwa ya raia wa Misri millioni
84 imekuwa ikitegemea mto huo kwa
maji safi.

Akishangiliwa na wafuasi wake ,Morsi
amesema kuwa ijapokuwa Misri
haitaki vita haitokubali usalama wake
wa maji kuingiliwa kivyovyote.

Tayari kiongozi huyo anapanga
kumtuma waziri wake wa maswala ya
kigeni nchini Ethiopia ili kuanzisha
mazungumzo kuhusiana na swala
hilo.

Misri ina wasiwasi kuwa maji ya mto
Nile huenda yakapungua kwa kiwango
kikubwa iwapo bwawa hilo litajengwa.

Inasema kuwa, kwa mujibu wa sheria
zilizowekwa na mkoloni, ndio taifa
linalopaswa kufaidika pakubwa na
maji hayo swala linalopingwa na
Ethiopia ambayo inasema sheria hiyo
imepitwa na wakati.

Mbunge Mtwara Adakwa na Polisi kwa Uchochezi.

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata
mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji
likimtuhumu kuchochea vurugu za kupinga
mradi wa bomba la gesi kutoka mkoani humo
kwenda jijini Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na
Msemaji wa Jeshi la polisi nchini, Advera Senso
zinaeleza kuwa Murji alikamatwa jana jioni
nyumbani kwake maeneo ya Shangani mjini
Mtwara.

Kukamatwa kwa mbunge huyo kunakuja ikiwa
zimepita siku tano tangu viongozi wanne wa
vyama vya upinzani mkoani Mtwara,
kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Mtwara, Juni 4, mwaka huu wakikabiliwa na
mashtaka matatu ikiwamo kula njama, kufanya
uchochezi na kuamsha hisia mbaya kwa wakazi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Washtakiwa hao ni Katani Ahmed Katani (33)
na Saidi Kulaga (45) wa CUF, Hassan Uledi (35)
wa NCCR Mageuzi na Hamza Licheta (51) wa
TLP, wote wakazi wa Mtwara.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa baada ya polisi
kumkamata mbunge huyo, walifanya upekuzi
katika nyumba yake kwa saa kadhaa na baada
ya kujiridhisha walikwenda kupekua na ofisi
yake.

"Amekamatwa kwenye saa 11:00 jioni, hata
hati ya kukamatwa kwake imeeleza kuwa
anatuhumiwa kuchochea vurugu za
kupinga gesi inayopatikana mkoani Mtwara
kwenda Dar es Salaam," alisema Katibu wa
Mbunge huyo, Meckland Millanzi.

Katika ufafanuzi wake Senso alisema
kukamatwa kwa mbunge huyo ni jambo la
kawaida na kwamba hivi sasa unaandaliwa
utaratibu ili faili lake lipelekwe kwa
Mwanasheria wa Serikali.

"Acheni polisi ifanye kazi yake kama
kutakuwa na la ziada tutawaeleza ila kwa
sasa tunaandaa utaratibu wa suala hili
kwenda kwa mwanasheria wa Serikali,"
alisema Senso.

Murji amekamatwa ikiwa zimepita siku 16
tangu kutokea vurugu kubwa mkoani Mtwara
zilizodumu kwa siku mbili, ambapo polisi
walipambana na makundi ya vijana
wanaopinga mradi wa bomba la gesi kujengwa.

Vurugu hizo zilizosababisha baadhi ya watu
kupoteza maisha huku wengine wakiachwa
majeruhi na mali nyingi kuharibiwa, ziliibuka
baada ya hotuba ya bajeti ya wizara ya nishati
na madini kusomwa bungeni.

Mvutano kuhusu mradi wa bomba la gesi
ulianza Novemba 16, mwaka jana baada ya
Serikali kutuma kamati inayoratibu maoni ya
sera ya gesi "The Natural Gas Policy of Tanzania
-2013" ambayo ilifika mkoani Mtwara
kukusanya maoni ya wananchi.

Katika mikutano yake mjini Mtwara, wananchi
wengi hawakukubaliana na wazo la
kusafirishwa gesi nje ya Mtwara kwa njia ya
bomba.

Hali hiyo ndiyo iliyowasukuma
viongozi wa vyama kuhamasisha wananchi
kuhusu suala hilo.

Mtikila: Nitakwenda kwenye mahakama za Kimataifa

Mchungaji Dr. Christopher Mtikila amesema atakwenda kwenyd mahaka za kimataifa kupinga rasimu ya katiba mpya kwa kutoitambua Tanganyika.

Ikiwa zimepita siku chache tu tangu kuzinduliwa kwa rasimu ya katiba mpya Mtikila amesema atakwenda hata kwenye mahakama za kimataifa kupinga Rasimu hiyo kwa kutoitambua Tanganyika ambapo katika rasimu hiyo kumependekezwa serikali tatu Zanzibar, Serikali ya shirikisho na Tanzania Bara.

Dr. Mtikila anapinga uwepo wa Tanzania bara Badala ya Tanganyika.

Uingereza Kuwafidia Mau Mau

Serikali ya Uingereza inatarajiwa
kuomba msamaha pamoja na
kuwalipa fidia manusura wa harakati
za ukombozi wa Uhuru wa Kenya
Mau Mau.

Waliokuwa wanachama wa vuguvugu
hilo waliwasilisha kesi mahakamani
kwa mateso na dhuluma walizodai
kutendewa na uliokuwa utawala wa
ukoloni miaka ya 50.

Waziri wa mambo ya nje wa
Uingereza William Hague, anatarajiwa
kutangaza kiwango cha pesa ambazo
serikali ya Uingereza iko tayari kutoa
kama fidia, duru zikisema kuwa
huenda ikawa dola milioni 20
Zaidi ya wakenya 5,000, waliteswa
baadhi wakinyanyaswa na waliokuwa
wakoloni wa Uingereza.

Uingereza ilipigana vita vikali dhidi ya
Mau Mau, waliokuwa wanadai ardhi
na kuondoka kwa utawala wa kikoloni.
Manusura wa vita hivyo wamekuwa
wakiidai Uingereza kuwalipa fidia kwa
miaka mingi.

BBC ina habari kuwa bwana Hague
atawaomba radhi waathiriwa wa vita
vya Mau Mau, wakati akitangaza
kiwango cha pesa watakazotoa kama
fidia kwao.

Serikali ya Uingereza awali ilikuwa
imesema kuwa madai yote ya vitedno
walivyofanya wakoloni ni juu ya
serikali ya Kenya tangu kuipa uhuru
mwaka 1963 na kuwa kwa sasa
haiwezi kutakiwa kulipa.

Lakini mwaka 2011, mahakama
iliamuru kuwa, wanaodai fidia, Paulo
Muoka Nzili, Wambuga Wa Nyingi na
Jane Muthoni Mara, walikuwa na haki
ya kudai fidia kutoka kwa Uingereza .

Mawakili wao wanasema kuwa Nzili
alihasiwa , huku Bwana Nyingi
akichapwa vibaya wakati Bi Mara
akiteswa kimapenzi katika kambi za
mateso ambako waliokuwa
wanapinga ukoloni walikuwa
wakifungwa.

Baada ya uamuzi wa kesi hiyo,
ilirejeshwa katika mahakama kuu ili
kuamua pesa watakazolipwa na ofisi
ya jumuiya ya madola.

Duru zinasema kuwa serikali
ilikumbwa na wakati mgumu kupata
mashahidi na stakabadhi muhimu
kuweza kuelezea ukweli katika kesi
hiyo.

Lakini Oktoba mwaka jana, mahakama
iliamua kuwa waathiriwa
waliowasilisha kesi hiyo mahakamani
walikuwa na haki ya kufidiwa kwani
walikuwa na kesi nzito dhidi ya serikali
ya Uingereza.

Watatu hao walikuwa wamesema
kuwa wangekubali wahusika wa kesi
kuafikiana nje ya mahakama lakini pia
walikuwa wanataka kufuata sheria
kwani waliona wangepata haki katika
mahakama.


Kutoka:BBC

Mtoto Wa Michael Jackson Ajaribu Kujiua

Bintiye marehemu Michael Jackson,
Paris, mwenye unmri wa miaka 15,
amelazwa katika hospitali moja mjini
Carlifornia baada ya kujaribu kujiua.

Msemaji wa familia ameeleza kuwa
anaendelea kupata nafuu na kuwa
madaktari wanamshughulikia vilivyo.

Inasemekana, Paris Jackson, ambaye
babake alifariki mwaka 2009,
amekuwa katika hali ya kusononeka
kwa muda sasa.

Msemaji wa familia hiyo amesema
kuwa usiku wa kuamkia leo binti huyo
alikimbizwa hospitalini baada ya
kujaribu kujiua lakini anaendelea
kupata nafuu.

Msemaji alifafanua kuwa hali yake si
mbaya sana ya kupelekwa kwa wadi
ya wagonjwa mahututi.

Paris Jackson ametajwa kama mmoja
wa familia ya Michael Jackson
anayetaka kulipwa mamilioni ya Dolar
kutoka kampuni ya AEG ambayo
ilimwajiri daktari aliyempa madawa
Michael ambayo yaligunduliwa
baadaye kuwa yalimwua.
Kesi inayohusiana na madai hayo
imeendelea kwa majuma sita sasa.

Mengi ya kusikitisha juu ya Michael
Jackson yamekuwa yakitajwa na
inadhaniwa kwamba yamechangia
pakubwa kupandisha huzuni na
simanzi kwa msichana Paris.

Inadhaniwa kuwa Paris amejaribu
kadiri ya uwezo wake kumwomboleza
baba yake lakini angali anasononeka
kutokuwepo kwake.

Mlezi wake
kisheria ni nyanya yake Catherine
lakini hata hivyo siku chache zilizopita
amekuwa akiishi na mamake mzazi.

Kesi ya Ruto Kuhamishiwa Tanzania au Kenya

Kesi inayomkabili
makamu wa Rais wa Kenya, William
Ruto kwenye Mahakama ya
Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huenda
ikahamishiwa nchini Tanzani au
Kenya.

Hiyo inatokana na uamuzi
unaotajwa kufikiwa na majaji wa ICC
ambao wametoa mapendekezo
wakimtaka Rais wa ICC aangalie
umuhimu na kutoa ruhusa ya kesi
hiyo kusikiliziwa nchini Kenya au
kama ikishindikana basi isikiliziwe
nchini Tanzania.

Uamuzi huo unaweza pia
kusababisha athari za kuichochea
mahakama hiyo kuhamisha pia kesi
ya aina hiyo inayomhusu Rais
Uhuru Kenyatta ambaye pia
mawakili wake wameomba kesi
dhidi yake ihamishiwe nchini Kenya
au Tanzania.

Ruto pamoja na mtuhumiwa
mwenzake, aliyekuwa mtangazaji wa
Redio, Joshua Arap Sang
wanakabiliwa na mashtaka kadhaa
ya uhalifu dhidi ya ubinadamu
wakidaiwa kuhusika kuchochea
vurugu za baada ya uchaguzi mkuu
wa mwaka 2007 zilizosababisha vifo
vya zaidi ya watu 1,000.

Mapendekezo hayo yametokana na
ombi hilo lililotumwa Januari 24
mwaka huu ambalo lilikuwa bado
likiendelea kujadiliwa n amamlaka
zinazohusika kwenye mahakama
hiyo.

Februari mwaka huu, Mwendesha
mashtaka mkuu wa ICC, Fatou
Bensouda aliieleza mahakama hiyo
kwamba hana pingamizi iwapo
itakubalika kesi hiyo isikiliziwe
Tanzania au Kenya.

Hata hivyo mahakama hiyo ilieleza
kuwa mapendekezo hayo bado
yanaendelea kujadiliwa kwa mujibu
wa taratibu zilizowekwa na
mahakama hiyo.

Hata hivyo, jana ICC ilitoa taarifa
ikisema kesi dhidi ya Ruto
anayetuhumiwa kufanya makosa ya
uhalifu dhidi ya binadamu itaanza
Septemba 10 mwaka huu.

Taarifa hiyo imesema majaji
wameamua kupanga tarehe ya
kusikilizwa kesi hiyo mapema zaidi
kuliko ilivyopangwa awali.

Rais Kenyatta na naibu wake
wanahitajika kupandishwa kizimbani
ili kujibu mashtaka yanayowakabili
ya uhalifu dhidi ya ubinadamu,
makosa ambayo waliyafanya wakati
wa vurugu zilizotokea baada ya
uchaguzi mkuu wa Rais wa mwaka
2007/08.

Tanzania Yasaini Mkataba wa Kudhibiti Biashara ya Silaha

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imekuwa miongozi mwa nchi za
kwanza kutia sahihi Mkataba wa
Kimataifa wa Kudhibiti Biashara ya
Silaha Duniani ( ATT)
Utiaji sahihi wa tukio hilo la kihistoria
umeziduliwa jana jumatatu ( Juni 3)
hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa. Ukishuhudiwa na viongozi
mbalimbali akiwamo Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon.

Katika tukio hilo Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania iliwakilishwa na Balozi
Ramadhan M. Mwinyi, Naibu
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa.

Utiaji sahihi wa mkataba huo
unafanyika ikiwa ni takribani miezi
miwili kupita tangu Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa lilipoupitisha kwa
kuupigia kura 154 za ndiyo na hivyo
kuhitimisha majadiliano ya uundwaji
wa mkataba yaliyodumu kwa takribani
miaka sita.

Kutiwa sahihi kwa Mkataba huo sasa
kunafungua fursa ya kuanza kufanya
kazi rasmi baada ya siku 90, kwa
sababu zilikuwa zikihitajika sahihi 50 ili
upate baraka ya kuanza rasmi. Lakini
idadi hiyo imepitiliza katika siku ya
kwanza ya utiaji wa sahihi na kufikia
nchi 67.

Dhumuni kuu la mkataba pamoja na
mambo mengine ni kusimamia na
kuratibu biashara ya silaha za aina
mbalimbali zikiwamo, mizinga ya kivita,
magari ya deraya, ndege za kivita,
helkopta za mashambulizi, meli za
kivita, makombora pamoja na silaha
ndogo ndogo na nyepesi.

Aidha Mkataba pamoja masuala
mengineyo hautaingilia uhuru wa nchi
kununua silaha kwa matumizi yake ya
ndani na haki ya kujilinda na kulinda
mipaka yake, vilevile mkataba hauzui
nchi kufanya biashara ya kusafiri aina
yoyote ya silaha ilimradi inazingatia
sheria na taratibu zilizomo ndani ya
mkataba ikiwa ni pamoja na taratibu
ambazo nchi yenyewe imejiwekea.

Matumaini ya Jumuiya ya Kimataifa ni
kwamba utekelezaji wa mkataba na
kama utaekelezea ipasavyo utasaidia
sana kudhibiti silaha zisiangukie
mikononi mwa makundi mbalimbali ya
kihalifu yakiwamo ya kigaidi.

Akizungumza mara baada ya kutia
sahihi, Balozi Ramadhan Mwinyi
aliungana na wasemaji wengine katika
kukaribisha hatua hiyo muhimu. Huku
akieleza kwamba kwa Tanzania kutia
sahihi ni uthibitisho wa utayari wake
wa kuutekeleza kwa kuzingatia
masharti na matakwa yanayoendeana
na mkataba huo.

Akasema Tanzania imekuwa miongoni
mwa nchi za mwanzo kutia sahihi
mkataba huo kwa kuwa ilikuwa moja
kati ya nchi zilizodhamini Azimio la
Kuanzishwa kwa Mkataba na pia
ilishiriki kikamilifu katika majadiliano
yote yaliyozaa mkataba huo.

Balozi Mwinyi akaeleza pia kuwa
kufanya kazi kwa Mkataba huo
kutachangia katika amani ya Kimataifa,
amani na usalama wa Kikanda na pia
utachangia sana katika kupunguza
madhara yatokanayo na biashara
haramu na holela ya silaha lakini pia
utasaidia katika kukuza na kuimarisha
uhusiano mzuri miongoni mwa nchi
wanachama.

Katika hatua nyingine Muwakilishi huyo
wa Tanzania amesisitiza haja na
umuhimu wa uwepo wa fursa sawa
kati ya wasafirishaji wa silaha na
waagizaji wa silaha na kwamba
Mkataba huo usidhibiti au kuzuia
biashara ya silaha ambayo ni halali na
kwamba mkataba haupashwi kuingilia
au kwa namna yoyote ile au kuadhiri
uhuru na haki ya nchi kujilinda na
kulinda watu wake.

Tanzania pia imekaribisha misaada ya
kiufundi katika maandalizi ya utekelezaji
wa mkataba huo hasa kwa nchi
zinazoendelea.

Nchi hizo 67 ambazo zimetia sahihi ni ,
Albania, Antigua and Barbuda,
Argentina, Australia, Austria, Bahamas,
Belgium, Belize, Benin, Brazil, Burkina
Faso, Burundi, Chile, Costa Rica, Cote
D' Ivoire, Croatia, Cyprus, Czech
Republic , Denmark, Djibout, na
Dominica Republic.
Nyingine ni Estonia, Finland, France,
Germany, Greece, Grenada, Guyana,
Hungary, Iceland, Italy, Jamaica, Japan,
Latvia, Liechtenstein, Lithuania,
Luxembourg, Mali, Malta, Mauritania,
Mexico na Montenegro.
Mataifa mengine ni Mozambique,
Netherlands, New Zealand, Norway,
Palau, Panama, Portugal, Republic of
Korea, Romania, Saint Lucia, Saint
Vincent and the Grenadines, Senegal,
Seychelles, Slovenia, Spain, Suriname,
Sweden, Switzerland, Togo, Trinidad
and Tobago, Tuvalu, United Kingdom
of Great Britain and Northern Ireland,
United Republic of Tanzania na
Uruguay.

Rasimu ya Katiba Mpya

1. UTANGULIZI

Ndugu Wananchi,
Awali ya yote namshukuru
mwenyezi mungu kwa
kutuwezesha kufikia hatua hii ya
leo ya kuzindua Rasimu ya
Katiba. pia, niwashukuru ninyi
nyote mliohudhuria halfa hii
ikiwa ni mwendelezo wa
mchakato muhimu wa
Mabadiliko ya Katiba ya nchi
yetu.

Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
ilipitishwa Bungeni Novemba,
2011 na kufanyiwa mabadiliko
Februari, 2012. Tume ya
Mabadiliko ya Katiba iliundwa
kwa mujibu wa Kifungu 6(1) cha
sheria hiyo (Cap.83). Wajumbe 34
wa Tume waliteuliwa na
kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete, mwezi Aprili,
2012. Kwa mujibu wa Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba, Tume
imepewa miezi kumi na minane
kukamilisha kazi yake kuanzia
siku ilipoanza kazi rasmi ambayo
ilikuwa Mei 2, 2012.

Tume iliandaa ratiba ya
utekelezaji wa majukumu yake.

Kufuatana na ratiba hiyo Tume
ilijipanga kukusanya maoni ya
wananchi katika kipindi cha miezi
mitano kuanzia Mwezi Julai hadi
Disemba, 2012. Kazi hiyo
ilifanywa kama tulivyopanga.

Tume ilijigawa katika makundi na
ilitembelea mkoa yote
thelathini.
Tume ilifanya mikutano 1,942
ambayo ilihudhuriwa na
wananchi wapatao 1,365,337
ambao kati ya hao wananchi
333,537 walitoa maoni ama kwa
mazungumzo ya ana kwa ana au
kwa maandishi. Tume pia ilipata
maoni ya wananchi wengi, wa
ndani na nje ya nchi kwa njia
mbali mbali kama vile; Mikutano
ya hadhara, Fomu maalum za
Tume, barua kupitia Masanduku
ya Barua ya Tume, Mitandao ya
Kijamii ya barua pepe; facebook
ya Tume, Tovuti ya Tume; Makala
mbalimbali kutoka kwenye
magazeti na ujumbe mfupi wa
simu.

Tume ilitumia mwezi Januari,
2013 kukusanya maoni ya
makundi mbali mbali katika
jamii, ikiwa ni pamoja na vyama
vya siasa, taasisi za Serikali,
taasisi za dini, wakulima,
wafugaji, wafanyakazi, asasi za
kiraia na kadhalika. Makundi
zaidi ya 160 yalikutana na Tume
na kutoa maoni. Tume pia ilipata
maoni ya viongozi wa juu wa
Serikali walioko madarakani na
waliostaafu. Kwa jumla viongozi
43walitoa maoni.

Tume ilipanga kutumia miezi
mitatu ya Februari, Machi na
Aprili kuchambua maoni ya
wananchi na kuandaa Rasimu ya
Katiba. Lakini tuligundua
kwamba maoni tuliyopata
yalikuwa mengi sana, na pamoja
na matumizi ya teknolojia ya
kisasa, tulitambua umuhimu wa
kuongeza muda hadi mwisho wa
mwezi Mei, Maoni ya wananchi
yaligusa mambo yote yanayohusu
Katiba na mengi ya maoni hayo
yalikinzana. Aidha, baadhi ya
maoni yaligusia masuala ya
Kisera, Kisheria na Kiutendaji.

Tulifanya uchambuzi makini na
wa ndani wa maoni hayo na kazi
hiyo tumeikamilisha na rasimu
imeandaliwa na Tume na leo
tupo hapa kwa ajili ya kuizindua,
ambapo Wananchi watapata
nafasi ya kuisoma. Kwa leo, kwa
niaba ya Tume, napenda kutaja
maeneo machache tu ambayo
tunayapendekeza.

IBARA ZINAZOPENDEKEZWA
KWENYE RASIMU YA KATIBA

Ndugu Wananchi,
Katiba yetu ya sasa ina ibara 152.

Tume ilifanya jitihada kubwa
sana kuandaa rasimu ambayo
siyo ndefu. Lakini katika hali
halisi haikuwezekana. Rasimu ya
Katiba tunayopendekeza ina
ibara 240.

MISINGI MIKUU YA TAIFA

Utangulizi wa Katiba ya sasa ndio
unaobeba misingi mikuu ya Taifa
ambayo ni Uhuru, Haki, Udugu na
Amani. Tume inaamini kwamba
misingi hii ni mizito na inastahili
kubaki kwenye Katiba mpya.
Hata hivyo, Tume imeona ni
busara kuongeza misingi mingine
mitatu ya Usawa, Umoja na
Mshikamano. Hivyo, Tume
imependekeza Katiba iwe na
Misingi Mikuu saba ya
Taifa;yaani; Uhuru, Haki, Udugu,
Usawa, Umoja, Amani na
Mshikamano.

TUNU ZA TAIFA

Katiba yetu ya sasa haina sehemu
inayoelezea tunu za Taifa
(National Values). Wananchi
wengi walitoa maoni kwamba
Katiba itaje Tunu za Taifa.

Tume
imependekeza Tunu zifuatazo
zitajwe ndani ya Katiba.

Tunu
hizo ni;- Utu, Uzalendo, Uadilifu,
Umoja, Uwazi, Uwajibikaji na
Lugha yetu ya taifa ya Kiswahili.

MALENGO YA TAIFA

Tume ilipozunguka nchi nzima
wananchi walizungumzia sana
kuhusu malengo ya taifa.
Walitaka Katiba ionyeshe dira ya
taifa. Wananchi wanayo ndoto
yao ya Tanzania ya kesho na
kesho kutwa. Kwa kuzingatia
maoni ya wananchi, kuna sura
nzima inayohusu Malengo
mahsusi na ya msingi ya
mwelekeo wa shughuli za
Kiserikali na Sera za Kitaifa.

Rasimu ya Katiba inaeleza kuwa
Malengo ya Kitaifa yaliyoainishwa
ndani ya Rasimu yatakuwa ni
Mwongozo kwa Serikali, Bunge,
Mahakama, Vyama vya Siasa,
Taasisi na Mamlaka nyingine, na
kwa kila mwananchi katika
matumizi au kutafsiri Masharti ya
Katiba au Sheria nyingine za
Nchi.

Kwa msingi huo, Tume
imependekeza malengo makuu
ya taifa yapanuliwe kwa
mpangilio wa kuonesha malengo
ya kisiasa, kiuchumi, kijamii,
kiutamaduni, kimazingira na sera
ya mambo ya nje. Malengo hayo
yameingizwa kwenye Rasimu ya
Katiba.

VYOMBO VYA KIKATIBA

Wananchi walizungumzia suala la
kubainishwa kwa vyombo vya
Kikatiba na kuingizwa kwenye
Katiba ili viwe na nguvu ya
Kikatiba katika utekelezaji wa
majukumu yao. Tume
imependekeza baadhi ya vyombo
vifuatavyo viwe vya Kikatiba;

Tume ya Uhusiano na Uratibu wa
Serikali, Baraza la Mawaziri,
Kamati Maalum ya Makatibu
Wakuu na Sekretarieti ya Baraza
la Mawaziri; Baraza la Ulinzi na
Usalama la Taifa, Tume Huru ya
Uchaguzi, Tume ya Utumishi wa
Mahakama, Tume ya Utumishi wa
Umma, Tume ya Maadili ya
Uongozi na Uwajibikaji, Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala
Bora

MAADILI YA VIONGOZI NA
MIIKO YA UONGOZI

Wananchi wengi pia
walizungumzia kwa upana sana
kuhusu maadili na miiko ya
Viongozi, kwa kuzingatia maoni
ya wananchi Tume inapendekeza
maadili ya viongozi wa umma,
pamoja na miiko ya uongozi
yawekwe kwenye Katiba. Tume
pia imependekeza kuwa
Sekretariati ya Maadili
ibadilishwe kuwa Tume yenye
mamlaka makubwa ya kusimamia
maadili ya viongozi wanaovunja
miiko ya uongozi.

HAKI ZA BINADAMU

Kuhusu haki za binadamu
wananchi walitaka haki hizi
ziimarishwe na kusiwe na
vikwazo visivyo vya lazima.

Tume
imependekeza mabadiliko katika
baadhi ya haki za binadamu kwa
madhumuni ya kuziimarisha.

Moja ya mabadiliko hayo ni
kuhusu uhuru wa mwananchi
kushiriki shughuli za umma.

Tume inapendekeza kwamba
vikwazo vilivyowekwa kuzuia
mgombea huru viondolewe. Kwa
maana nyingine Tume
inapendekeza mgombea binafsi
aruhusiwe.

Tume pia, inapendekeza haki
mpya ziingizwe kwenye Katiba
ikiwa ni pamoja na haki ya
wafanyakazi, , haki ya mtoto,
haki za Watu wenye Ulemavu,
Haki za Wanawake, Haki za
Wazee, Haki za Makundi Madogo
katika Jamii, Haki ya Elimu na
Kujifunza, Haki ya kupata habari,
Haki na uhuru wa habari na
vyombo vya habari na kadhalika.

URAIA

Wananchi wengi walipendekeza
kuwa suala la Uraia libainishwe
wazi kwenye Katiba. Tume
imependekeza kwa kutaja Raia
wa Jamhuri ya Muungano na haki
zake.

MIKOPO NA DENI LA TAIFA

Ndugu Wananchi,
Wananchi walizungumzia suala la
uwepo wa Ukomo wa nchi
kukopa na uwepo wa utaratibu
wa kulipa Deni la Taifa ili
kuilinda Nchi isiwe na deni
kubwa. Kwa kuzingatia maoni ya
Wananchi, Tume imependekeza
kuwa, Serikali itawajibika kutoa
taarifa Bungeni kuhusu Mikopo
kwa kuainisha kiasi cha deni
lililopo, riba yake na matumizi ya
fedha za Mikopo na utaratibu wa
kulipa Madeni ya Taifa.

MFUMO WA UTAWALA

Kuhusu utawala, Tume
inapendekeza Tanzania iendelee
na mfumo wa Jamhuri kwa maana
ya nchi inayoongozwa na Rais
Mtendaji ambaye ni Mkuu wa
nchi, Kiongozi wa Serikali na
Amiri Jeshi Mkuu.

UCHAGUZI WA RAIS

Umri wa kugombea Urais
Tume ilipokea maoni
yanayokinzana kuhusu umri wa
mwananchi kugombea Urais.

Baadhi walipendekeza mtu
akishakuwa na sifa ya kupiga
kura awe pia na sifa ya
kugombea Urais. Umri wa mtu
kuruhusiwa kupiga kura ni miaka
18.

Wengine walipendekeza umri
uliopo kwenye Katiba wa mtu
kugombea Urais, yaani kuanzia
miaka 40 na kuendelea,
uendelee kubaki kama ulivyo.

Wengine walisema Umri wa mtu
kuruhusiwa kugombea Urais uwe
miaka 35 au miaka 50 na
kuendelea.

Tume imeyachambua maoni yote
hayo, ikafanya utafiti kwa kupitia
Katiba za Nchi zingine na uhalisia
wa watu wanaogombea na
kuchaguliwa kuwa Marais katika
Nchi mbalimbali Duniani ambazo
zingine zimeruhusu wagombea
wa nafasi ya Urais kuwa na umri
chini ya miaka 40.

Wengi walioomba kugombea
nafasi hiyo walikuwa na umri wa
miaka 40 au zaidi.

Kwa kuzingatia maoni ya
wananchi, utafiti na hali halisi,
Tume inapendekeza Rais
aendelea kuchaguliwa na
wananchi na pamoja na sifa
nyingine, mtu anayeomba urais
asiwe chini ya miaka 40.

Uchaguzi wa Rais itakuwa kama
ilivyo sasa, yaani mgombea Urais
atakuwa na mgombea mwenza
kwa utaratibu kama ilivyo sasa.

Isipokuwa, Tume imependekeza
Mgombea Urais anaweza
kupendekezwa na Chama cha
Siasa au kuwa Mgombea Huru.

Mgombea wa nafasi ya Rais
atatangazwa kuwa mshindi iwapo
atakuwa amepata kura zaidi ya
asilimia hamsini ya kura zote
zilizopigwa.

Hata hivyo, matokeo ya uchaguzi
wa Rais yanaweza kulalamikiwa
Mahakamani, lakini siyo kila mtu
anaweza kufungua kesi.

Wanaoweza kufungua kesi ni
wagombea Urais. Aidha, ni
Mahakama ya Juu pekee ndiyo
itakuwa na Mamlaka na uwezo
wa kusikiliza malalamiko kuhusu
matokeo ya uchaguzi wa Rais na
shauri lazima liamuliwe ndani ya
mwezi mmoja, yaani siku
therathini.
Rais aliyeshinda ataapishwa siku
thelathini tangu alipotangazwa
kuwa mshindi au kuthibitishwa
na Mahakama.

MADARAKA YA RAIS

Ndugu Wananchi,
Tume inapendekeza kwamba,
Rais abaki na madaraka ya uteuzi
wa viongozi wa ngazi za juu. Hata
hivyo inapendekezwa Rais
ashirikiane na taasisi na vyombo
vingine katika uteuzi. Kwa
mfano:
Uteuzi wa Mawaziri na Manaibu
Waziri, Rais atateua na Bunge
litathibitisha.

Kuhusu Jaji Mkuu na Naibu Jaji
Mkuu Rais atawateua kutokana
na majina ya watu
waliopendekezwa na Tume ya
Uutumishi wa Mahakama na
baada ya hapo Bunge
litathibitisha.

Kuhusu Wakuu wa vyombo vya
Ulinzi na Usalama
inapendekezwa kianzishwe
chombo kipya kitakachoitwa
Baraza la Ulinzi na Usalama la
Taifa, ambalo kati ya majukumu
yake itakuwa ni kumshauri Rais
kuhusu uteuzi wa Wakuu wa
vyombo vya ulinzi na usalama.

Kuhusu Makatibu Wakuu na
Naibu Makatibu Wakuu
watateuliwa na Rais kutokana na
mapendekezo ya Tume ya
Utumishi wa Umma.

KINGA YA RAIS

Tume baada ya kupitia maoni ya
Wananchi, inapendekeza Rais
abaki na kinga kama ilivyo sasa
na anaweza kushitakiwa na
Bunge kama ilivyo Katiba ya sasa.

IDADI YA MAWAZIRI

Inapendekezwa Rais aunde
Serikali ndogo iliyo na Mawaziri
wasiozidi kumi na tano na
mawaziri hao wasiwe wabunge.

Mawaziri hawatahudhuria vikao
vya Bunge isipokuwa kama
watahitajika kutoa ufafanuzi
kwenye kamati za Bunge.

BUNGE

Ndugu Wananchi,
Kuhusu Bunge kutakuwa na
wabunge wa aina mbili

Kutakuwa na Wabunge wa
kuchaguliwa na wabunge watano
wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha
Watu wenye Ulemavu.

Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na
Wabunge Wawili mmoja
mwanamke na mwingine
mwanamume.

Tume inapendekeza kwamba,
Mbunge akifukuzwa na Chama
cha Siasa abaki kuwa Mbunge
lakini akihama Chama atapoteza
Ubunge wake.

Inapendekezwa ukomo wa
Ubunge uwe vipindi vitatu vya
miaka mitano mitano. Hata hivyo,
wananchi wanaweza kumwondoa
mbunge wao kabla ya mwisho wa
kipindi chake.

Inapendekezwa pia kusiwepo na
uchaguzi mdogo isipokuwa kama
nafasi inayokuwa wazi inatokana
na Mbunge huru ndipo
utafanyika uchaguzi mdogo
kujaza nafasi hiyo, lakini kama
nafasi ikiwa wazi kutokana na
Mbunge wa Chama cha Siasa basi
nafasi hiyo, ijazwe na mtu kutoka
Chama hicho.

Inapendekezwa Spika na Naibu
Spika wasitokane na Wabunge na
wasiwe Viongozi wa vyama vya
Siasa.

TUME YA UCHAGUZI

Tume imefanya uchambuzi wa
maoni ya wananchi kuhusu Tume
ya Uchaguzi. Tume inapendekeza
jina la tume liwe Tume Huru ya
Uchaguzi.

Tume pia
inapendekeza sifa za wajumbe wa
Tume Huru ya Uchaguzi ziwekwe
kwenye Katiba. Wajumbe wa
Tume Huru ya Uchaguzi
watapatikana kutoka miongoni
mwa watu wenye sifa
zilizoainishwa ndani ya Katiba
kwa kuomba. Majina ya
waombaji yatachambuliwa na
Kamati ya Uteuzi ambayo
Mwenyekiti wake atakuwa Jaji
Mkuu na wajumbe wengine sita
ambao ni Majaji Wakuu wa nchi
Washirika, Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano, Maspika
wa Mabunge wa nchi Washirika
na Mwenyekiti wa Tume ya Haki
za Binadamu.

Kamati ya uteuzi itapendekeza
majina ya watu wanaofaa kwa
Rais ambaye atateua Mwenyekiti,
Makamu Mwenyekiti na
Wajumbe wengine. Bunge
litathibitisha uteuzi wao.

Wabunge na viongozi wa aina
hiyo hawatakuwa na sifa za kuwa
wajumbe wa tume ya uchaguzi.

Inapendekezwa Tume huru ya
Uchaguzi isimamie masuala ya
uchaguzi, kura ya maoni na
Usajili wa Vyama vya Siasa.

MAHAKAMA

Kuhusu Mahakama
inapendekezwa kuanzishwa kwa
Mahakama ya Juu (Supreme
Court) Majaji wa Mahakama ya
Juu na Mahakama ya Rufani
watateuliwa na Rais baada ya
kupendekezwa na Tume ya
Utumishi wa Mahakama.

MUUNDO WA MUUNGANO

Ndugu Wananchi,
Suala la muundo wa Muungano
ndilo lililokuwa gumu kuliko
masuala yote. Tume ilitumia
muda mwingi kuchambua maoni
ya wananchi.

Pamoja na kwamba
hadidu za rejea zilielekeza Tume
kuzingatia uwepo wa Muungano,
baadhi ya wananchi walitoa
maoni kwamba Muungano
uvunjwe na Tume iliyapokea
maoni hayo. Licha ya kwamba
waliotaka kuvunjwa muungano
walikuwa wachache sana, Tume
ilichambua sababu walizotoa na
kuridhika kwamba hazikuwa na
uzito.

Wananchi walio wengi walitaka
Muungano uendelee. Kati yao
wapo waliopendekeza Muungano
wa Serikali moja, Serikali mbili,
Serikali tatu, Serikali nne na
muungano wa mkataba.

Sababu
za wale waliopendekeza Serikali
nne hazikuwa na uzito, kwa hiyo
Tume ikaamua kutopendekeza
muundo huo.

Wananchi waliopendekeza
Serikali moja walikuwa wachache
lakini sababu zao zilkuwa na
uzito. Hata hivyo, Tume kwa
kuzingatia hali halisi iliona ni
changamoto kubwa kuwa na
Muungano wa Serikali Moja.

Wananchi waliopendekeza
Muungano wa Mkataba walikuwa
wengi (hasa wananchi wa
Zanzibar) na sababu zao zilikuwa
na uzito. Lakini uchambuzi wa
Tume ilionekana wazi kwamba ili
kupata mkataba lazima kwanza
kuwe na nchi mbili huru kabisa
lakini hakukuwa na mazingira ya
uhakika ya kupata mkataba wa
muungano. Tume iliona kuna
changamoto ya muungano
kuvunjika ingawa waliotoa maoni
walisisitiza muungano ubaki.

Hivyo, Tume iliamua
kutopendekeza muundo huo.

Wananchi waliopendekeza
Tanzania iendelee na Muundo wa
sasa wa Serikali mbili walikuwa
wengi na sababu zao zilikuwa
nzito. Hata hivyo, wananchi
katika kundi hili walipendekeza
mabadiliko mengi na makubwa.

Tathmini ya Tume ilionyesha
kwamba isingewezekana kufanya
mabadiliko yote
yaliyopendekezwa.

Wananchi waliopendekeza
muundo wa Serikali tatu
walikuwa wengi kuliko makundi
yote. Sababu zao zilikuwa nzito
lakini pia kulikuwa na
changamoto nyingi na nzito.

Pamoja na maoni ya wananchi
Tume ilirejea sababu za
kupendekeza muundo huu
zilizotolewa na Tume zilizopita na
Tafiti zilizofanywa na Tume
kuhusu aina mbalimbali za
Muungano. Baada ya yote hayo
Tume ilifikia uamuzi wa
kupendekeza mfumo wa Serikali
tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho,
Serikali ya Tanzania Bara na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

ORODHA YA MAMBO YA
MUUNGANO

Ndugu Wananchi,
Tume imependekeza katika
Rasimu ya Katiba kuwa orodha ya
Mambo ya Muungano yawe 7
badala ya 22 yaliyopo sasa.

Mambo ya muungano
yanayopendekwa ni:

1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
3. Uraia na Uhamiaji
4. Sarafu na Benki Kuu
5. Mambo ya Nje
6. Usajili wa Vyama vya Siasa
7. Ushuru wa bidhaa na mapato
yasiyo ya Kodi yatokanayo na
Mambo ya Muungano.

BENKI KUU

Kwa kuwa Tume imependekeza
Muungano wa Shirikisho
kutokana na uzito wa maoni ya
wananchi. Hivyokutakuwa na
Benki Kuu ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
itakayokuwa na wajibu wa
kusimamia masuala ya Sarafu na
Fedha za Kigeni na Benki za
Washirika wa Muungano.

BENKI ZA SERIKALI ZA
WASHIRIKA

Kutokana na pendekezo la
kuwepo kwa Serikali ya
Shirikisho la Nchi tatu,
inapendekezwa kuwepo kwa
Benki zitakazokuwa na jukumu la
kutunza akaunti ya fedha za
Serikali za kila Mshirika wa
Muungano na kuzisimamia benki
za biashara katika mamlaka zao.

BAADHI YA MAMBO AMBAYO
HAYAMO KWENYE RASIMU YA
KATIBA

Serikali ya Majimbo
Ndugu Wananchi,

Tume ilipokea maoni kuhusu
mambo mengine muhimu
ambayo hayamo katika rasimu
hii. Moja ya mambo hayo ni
Serikali za Majimbo. Tume
ilichambua maoni na sababu za
wananchi kupendekeza Serikali
za Majimbo lakini Tume ilibaini
changamoto nyingi na ikaamua
kutopendekeza muundo huu.

Kwanza, baada ya kuamua
kupendekeza Muundo wa
Muungano wa Serikali Tatu,
ilionekana ni dhahiri kuongeza
ngazi nyingine ya Serikali
ingeleta gharama kubwa. Serikali
nyingine kumi zingekuwa na
Wakuu wa Majimbo, Mabaraza ya
Mawaziri na Mabunge na
gharama yake ingekuwa kubwa.

Pili, katika kutembelea nchi
Tume ilishuhudia dalili za wazi za
mivutano ya Udini,
ukanda,malalamiko ya
upendeleo wa baadhi ya maeneo
na ukabila. Dalili zilikuwa wazi
kwamba utawala wa majimbo
ungeirudisha nchi kwenye
utawala utakaoigawa nchi kwa
misingi ya ukabila, udini na
ukanda na kuzigawa rasilimali za
taifa kikanda na hivyo kuleta
tofauti kubwa ya kimaendeleo
katika nchi.

Mahakama ya Kadhi

Ndugu wananchi,
Jambo la pili ni mahakama ya
kadhi. Tume ilipokea maoni
mengi kuhusu suala hili.

Baadhi
ya wananchi walitaka mahakama
ya kadhi iingizwe kwenye Katiba
na wengine walipinga.

Baada ya
kuamua kuwa Muundo wa
Muungano uwe wa Serikali Tatu,
Tume iliona kuwa Mahakama ya
Kadhi siyo suala la Muungano na
imeliacha ili lishughulikiwe na
Washirika wa Muungano.
Hata hivyo ilionekana kuwa suala
siyo kuwapo au kutokuwapo kwa
mahakama ya kadhi. Mahakama
hizo zinaweza kuwapo bila ya
kuwa katika Katiba.

Zanzibar
kuna mahakama ya kadhi bila
kuingizwa kwenye Katiba ya
Zanzibar. Kwa kutumia uzoefu
huo hata Tanzania Bara inaweza
kupata ufumbuzi wa suala hili.

Wakuu wa Mikoa na Wakuu
wa Wilaya

Jambo la Tatu ni Kuwepo au
kutokuwepo kwa Wakuu wa
Mikoa na Wilaya. Baadhi ya
Wananchi walitaka Wakuu wa
Mikoa na Wilaya wasiwepo,
wengine walitaka Wakuu wa
Mikoa na Wilaya waendelee
kuwepo lakini wachaguliwe na
wananchi na waengine wakasema
wawepo na waendelee kuteuliwa
na Rais kama ilivyo sasa. Tume
ilitafakari kuhusu suala hili na
kuamua kwamba siyo suala la
Muungano na kwa kuwa Muundo
wa Muungano imependekezwa
uwe wa Serikali Tatu, Tume iliona
suala la uwepo au kutokuwepo
na namna ya upatikanaji wa
Wakuu wa Mikoa na Wilaya
lishughulikiwe na Washirika wa
Muungano.

Serikali za Mitaa
Kuhusu Serikali za Mitaa, Tume
ilipokea maoni kutoka kwa
wananchi kuhusu kuziimarisha
Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa
kuzipatia uhuru kamili wa
kujiamulia mambo yao bila
kuingiliwa na Serikali Kuu.

Tume
ilitafakari suala hili na kuamua
kwamba siyo jambo la Muungano
na hivyo, litashughulikiwa
kwenye Katiba za Washirika wa
Muungano.

Uraia wa Nchi mbili
Ndugu Wananchi,
Jambo la tatu ni Uraia wa Nchi
mbili. Tume ilipokea maoni
kutoka kwa wananchi mbalimbali
kuhusu kuwekwa kwenye Katiba
suala la Uraia wa nchi mbili.

Baada ya kufanya uchambuzi kwa
kutengenisha mambo yapi ni ya
Kikatiba na yapi yanaweza
kutekelezwa bila kuingizwa
kwenye Katiba bali kwenye
Sheria inayohusu jambo husika,

Tume imependekeza kuwa suala
la Uraia wa nchi mbili linaweza
kuwekwa kwenye Sheria badala
ya kuwekwa kwenye Katiba. hii
ni kwa sababu kutokana na utafiti
uliofanywa na Tume, suala hilo
linaweza kubadilika wakati
wowote na hivyo likiwa kwenye
Katiba linaweza kuifanya Katiba
kubadilishwa mara kwa mara.

MWISHO

Naomba nichukue fursa hii kwa
niaba ya Tume kuwashukuru
Watanzania wote kwa kushiriki
kikamilifu katika mchakato wa
Mabadiliko ya Katiba, kuanzia
hatua ya kutoa maoni na
kuwachagua wawakilishi wenu
watakaopata fursa ya kuipitia,
kuijadili na kuitolea maoni
Rasimu ya Katiba.

Ushirikiano
huu ulikuwa muhimu sana kwa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba
hasa ukizingatia kuwa lengo ni
kupata Katiba Mpya ambayo
itaakisi ndoto na matakwa ya
Wananchi wa Tanzania.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
inatoa shukrani za dhati kwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar:

1. Kwa kuipatia vifaa afisi na
mahitaji ya lazima
2. Kwa kuiwezesha Tume
kutekeleza majukumu yake
kwa ukamilifu,
3. Kwa kutokuingilia Uhuru wa
Tume wakati wa Utekelezaji
wa Majukumu yake na
4. Kutoa Wataalam wenye
Weledi, Mahiri, Makini na
Waadilifu ambao wameunda
Sekretarieti ya Tume.

Ndugu Wananchi,
Shukrani za pekee ziwaendee:
1. Wakuu wa Mikoa,
2. Wakuu wa Wilaya,
3. Wakurugenzi / Makatibu wa
Mamlaka za Serikali za Mitaa,
4. Makamanda wa Polisi wa
Mikoa na Wilaya,
5. Watendaji wa Kata, Vijiji,
Mitaa na Masheha.
Kwa kuisaidia Tume kutekeleza
Majukumu yake kwa ufanisi.

Aidha, tunazishukuru Asasi za
Kiraia, Taasisi, Jumuiya za Kidini,
Vyama vya Siasa na Makundi
mbalimbali kwa namna
walivyoshiriki katika
kuhamasisha wananchi kushiriki
katika kutoa maoni.

Mwisho ingawa siyo kwa
umuhimu, Tunawashukuru
Wanahabari wote kwa kazi nzuri
waliyoifanya ya kuisaidia Tume
kufikisha taarifa mbalimbali za
Tume kwa Wananchi na katika
kuhamasisha Wananchi kushiriki
katika mchakato wa Mabadiliko
ya Katiba.

Nachukua nafasi hii kuwaomba
Wananchi kupitia Mabaraza ya
Katiba ya Wilaya, Mabaraza ya
Katiba ya Asasi, Taasisi na
Makundi ya Watu wenye
Malengo yanyofanana kushiriki
vyema, kwa umakini, utulivu na
kwa amani katika hatua hii ya
kuipitia, kuijadili na kuitolea
maoni Rasimu ya Katiba.
Tume imekuwa ikithamini na
itandelea kuthamini mawazo na
maoni kutoka kwa Watanzania
wote.

Rasimu ya Katiba itapatikana
kwenye tovuti ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba ya
www.katiba.go.tz