Mikopo ya Wanafunzi Elimu Ya Juu Wiki hii Kutolewa na HESLB


   Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) itaanza kupeleka fedha za wanafunzi katika vyuo kuanzia wiki hii.
   Ahadi hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, George Nyatega, alipozungumza na NIPASHE.
   Nyatega alisema jumla ya wanafunzi 29,113 wa elimu ya juu nchini kutoka vyou mbalimbali waliochaguliwa kupata mkopo, fedha zao zitaanza kupelekwa kuanzia wiki hii.
   Nyatega alisema baada ya kutoa majina hayo,bodi ya wakurugenzi ilitarajiwa kukutana Jumamosi kufanya tathmini kisha fedha zao zianze kupelekwa vyuoni.
   Hata hivyo alisema kwa mwaka huu idadi ya walioomba mikopo imeongezeka tofauti na mwaka jana na kuongeza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ufinyu wa bajeti.
   Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandara, jana aliiambia NIPASHE kuwa chuo hichi kimekubaliana na HESLB kwamba kuanzia Alhamisi wiki hii fedha zitapelekwa.
Chanzo:NIPASHE
chuotanzania.blogspot.com

Shilole Achafua Mashabiki Wake

Hii ndiyo post ya Shilole
Comment ya moja wa mashabiki wake
Jibu alilotoa Shilole
Katika pita pita zangu leo kwenye mitandao ya kijamii leo nimekutana
na kali ya Msanii Shilole kutukana mashabiki wake katika Facebook.
Swali lilibaki kwangu kuwa ile account ya Shilole Facebook ni yake au?
Lakini baada ya mashabiki kumjibu alijaribu juomba ladhi.
Kweli ni Kioo cha jamii????????????

Serengeti Fiesta 2012

Na hatimae Rick Ross kutua Bongo kuja kukamua show ya Fiesta 2012 Dar
es salaam Viwanja vya Leaders tarehe 6 October 2012
Kiingilio: Tsh 20,000 Ukiwahi tiketi yako mapema na Tsh 25,000 Mlangoni
Bhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaas!

Pamoja FM

Neema yazidi kuufikia mkoa wetu wa Katavi na Sasa Pamoja Fm imeanza
kurusha matangazo yake Rasmi kwa masafa ya fm 98.5 Tune radio Yako
mpaka hapo kwa Wakazi wa Mpanda uweze kusikiliza Radio ya nyumbani.
Kuongezeka kwa Radio ya Tano (5) Pamoja Fm baada ya hapo mwanzo kuwa
na RFA, TBC Taifa, TBC fm na Radio Maria. Sasa kutazidi kufungua
mianya ya uwekezaji na Kufahamika kwa Mkoa mpya wa katavi
Ni Pamoja FM 98.5

Wananchi Wa Rukwa na Katavi Kukutana

Kwa Wale Wananchi wote wenye asili au wanaotokea Mkoa Wa Rukwa na mkoa
Mpya wa Katavi ambao wanaishi Dar na mikoa ya Karibu, Kutakuwa na
mkutano katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Dar Es Salaam Ili kupanga
mikakati ya Uzinduzi wa Mkoa mpya wa Katavi. Kikao hicho kitafanyika
siku ya Jumapili tarehe 23/9/2012 Muda ni kuanzia Saa nane mchana
mpaka saa Kumi Jioni
Fika bila kukosa.

TCU yatoa Majina Ya Waliochaguliwa kujiunga na vyuo viwango vyao vya mkopo pamoja na Waliokosa

SELECTED APPLICANTS FOR THE 2012/2013ADMISSIONSThe Tanzania Commission
for Universities(TCU) in Collaboration with the NationalCouncil for
Technical Education (NACTE) isannouncing the names of Applicants who
were seleted into various programs forthe 2012/2013 Admissions.
However, weshall announce the list of  someapplicants who were
selected into variousprograms but obtained no loan,applicants who were
returned by some institutions, and selected applicants whoasked for
transfer, will be announcedbefore 21 September 20121.

1. To view selectedApplicant with no loan/Waliochaguliwa wakakosa
mkopo http://www.tcu.go.tz/uploads/file/SELECTED%20APPLICANTS.pdf

2. To view selected Applicant with loan but subject to verification
with heslb/ Waliochaguliwa wakapata mkopo
http://www.tcu.go.tz/uploads/file/LOANS%20SUBJECT%20TO%20VERIFICATION.pdf

Source: www.heslb.go.tz

Waandishi wa Habari wafanya Maandamano.

Waandishi wa Habari jijini Dar-es-salaam leo wanafanya maandamano
asubuhi hii kuonesha masikitiko yao kwa kuuwawa kwa Mwandishi wa
habari Daudi Mwangosi aliyeuwawa na polisi mjini Iringa

Picha:EARadio

Kifo Cha Mwandishi wa Habari

Vurugu kubwa zilizuka jana katika eneo la Nyororo wilayani Mufindi
kati ya polisi na wafuasi wa Chadema, baada ya askari hao
kusambaratisha mkutano wa chama hicho nakusababisha kifo cha mwandishi
wa habari na watu kadhaa kujeruhiwa.
Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi
anadaiwa kuuawa kwa bomu lililorushwa na polisi katika vurugu hizo.
Awali, inadaiwa kuwa mwandishi huyo alishambuliwa kwa marungu na
Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kabla ya bomu hilo
kumjeruhi vibaya tumboni na kusababisha kifo chake.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio, alisema wakati mwandishi huyo
akishambuliwa na polisi, mmoja wa askari wa jeshi hilo aliwazuia
wenzake kuendelea kumpiga akiwaeleza kuwa anamfahamu kuwa ni mwandishi
wa habari, huku akimkumbatia.
Shuhuda huyo alidai kwamba jitihada za askari huyo hazikusaidia, kwani
baada ya kutupwa kwa bomu hilo lililosababisha utumbo wa mwandishi
huyo kutoka nje, polisi huyo naye alijeruhiwa mguu.
Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alikana polisi
kumuua mwandishi huyo akidai kwamba kilichosababish a kifo chake
nikitu kilichorushwa na wananchi ambapo alisema polisi inakichunguza.
Vurugu hizo ziliibuka baada ya polisi kufika Nyororo na kuwataka
viongozi wa Chadema pamoja na wafuasi wao kutawanyika kwa kuwa
walikuwa hawaruhusiwi kufanya mkusanyiko wowote kutokana na amri
iliyotolewa na jeshi hilo awali.
Polisi mkoani Iringa jana asubuhi walilipiga marufuku kufanyika kwa
maandamano na mikutano yote ya halaiki ya kisiasa mpaka hapo Sensa ya
Watu na Makazi itakapokamilika baada ya kuongezwa wiki zaidi.
Hata hivyo, pamoja na amri hiyo Chadema kilifanya mkutano wilayani
Mufindi kitendo ambacho polisi walisema ni kinyume cha sheria.

Source: Star Tv