Katibu Wa Bakwata Arusha Ajeruhiwa

Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Arusha ABDULKARIM CHONJO amejeruhiwa vibaya
na amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru baada ya nyumba yake
kulipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu usiku wa kuamkia leo.

Source: ITV

JWTZ Wapita pita mitaani Kuangalia Usalama

Jeshi la wananchi wa Tanzania wakiongozwa na Jenerali Davis
Mwamunyange Wapita pita mitaa ya kariakoo kuangalia usalama yapatayo
magari makubwa matano yenye askari wapatao 20 kila gari walipita mitaa
hiyo. Huku Wafuasi wa shekh Ponda wataka kuelekea Ikulu kujisalimisha
huko, Askari wa kutuliza ghasia ndipo walipo anza kuwasambaratisha kwa
mabomu ya machozi.
Kwa sasa Askari wa JWTZ wapo maeneo ya Ikulu na wakati huu Rais Jakaya
Kikwete awasili kutoka Oman kwenye ziara yake.

JWTZ Wapita pita mitaani Kuangalia Usalama

Jeshi la wananchi wa Tanzania wakiongozwa na Jenerali Davis
Mwamunyange Wapita pita mitaa ya kariakoo kuangalia usalama yapatayo
magari makubwa matano yenye askari wapatao 20 kila gari walipita mitaa
hiyo. Huku Wafuasi wa shekh Ponda wataka kuelekea Ikulu kujisalimisha
huko, Askari wa kutuliza ghasia ndipo walipo anza kuwasambaratisha kwa
mabomu ya machozi.
Kwa sasa Askari wa JWTZ wapo maeneo ya Ikulu na wakati huu Rais Jakaya
Kikwete awasili kutoka Oman kwenye ziara yake.

Hali Si Shwari Jijini Dar Es Salaam

Hali imeendelea kuwa tete jijini dar es salaam, maeneo yote ya
kariakoo Posta maduka yamefungwa na imetangazwa kutokuwa na mkusanyiko
wa aina yoyote ule. Na inasemekana kuwa JWTZ wanaweza kuongeza nguvu
kwa polisi.

Hali Si Swari Jijini Dar Es Salaam

Hali imeendelea kuwa tete jijini dar es salaam, maeneo yote ya
kariakoo Posta maduka yamefungwa na imetangazwa kutokuwa na mkusanyiko
wa aina yoyote ule. Na inasemekana kuwa JWTZ wanaweza kuongeza nguvu
kwa polisi.

Uamsho Waamsha Tena

Vurugu kubwa zimevuka tena eneo la Darajan Visiwani zilizo sababishwa
na Kikundi chenye msimamo mkali cha Uamsho baada ya taarifa kuzuka
kuwa kiongozi wao ametekwa na watu wasio julikana, na Jijini Dar Es
Salaam polisi wamelazimika kuwatawanyisha watu waliokusanyika kituo
cha polisi jutaka shekh wao aachiwe baada ya kukamatwa jana usiku kwa
madai ya kuhusika na vurugu za hivi karibuni.

Kumbukumbu Ya Mwalimu

Tuangalie Baadhi ya hotuba za Mwalimu Nyerere alizozifanya wakati wa uhai wake.


Kumbukumbu Ya Mwalimu.

Ni miaka kumi na tatu tangu ututoke
Tuta kukumbuka kwa mambo yako yote, ulipinga ufisadi kukemea ukabila
na udini, kutoa elimu bure na mambo mengi


"Julius Kambarage Nyerere (13 April 1922 –14 October 1999) was
aTanzanian politician who served as the first Presidentof Tanzania and
previously Tanganyika, from the country's founding in 1961 until his
retirement in 1985.

Born in Tanganyika to Nyerere Burito (1860–1942), Chief of the Zanaki
Nyerere was known by the Swahili name Mwalimu, his profession prior to
politics. He was also referred to as Baba wa Taifa.


Pumzika kwa amani,

Kamanda Auwawa.

Kamanda wa mkoa wa Mwanza Ndugu Liberatus Barlow auwawa na majambazi
usiku wa kuamkia leo. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi

Zurugu za Mbagala Kizuiani

Mkuu wa Dar Es Salaam,Said Meck Sadick,Kamanda wa Polisi kanda maalum
ya Dar Es Salaam Suleiman Kova na Sheikh wa Mkoa wa Dar Es Salaa,Alhaj
Musa Salum,wamewatak a waislam Jijini Dar Es Salaam kuacha Vurugu
zisizokuwa na tija kwakosa lililosababishw a na ubishani wa watoto
kuhusu Quran takatifu, jambo ambalo limesabaisha vurugu huko eneo la
Chamazi Mbagala ambapo magari yalivunjwa vioo na kuvunjwa kwa makanisa
Matatu.
Swali linakuja Makanisa yanausika na nini hapa?

Fujo Zazuka Mbagala

Fujo za zuka Mbagala na Polisi walazimika kutumia mabomu ya machozi
kutawanya wananchi Mbagala baada ya mtoto mmoja kumnyang'anya mwenzake
kitabu cha Dini ya kiislamu na kukikojolea.

Dr. Ulimboka Anena

Dk Ulimboka aibuka ajipanga kuanika waliomteka
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania,

Dk Steven Ulimboka ameibuka na kusema yuko imara na anajiandaa kuanika
waliomteka, kumtesa na kisha kumtupa katika Msitu wa Pande, nje kidogo
ya Jiji la Dares Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Dk Ulimbokaalisema kamwe hajanunuliwa
na kwamba ukimya wake wa muda mrefu umetokana na kufuatilia kwa karibu
masharti ya matibabu yake na si vinginevyo.

Rick Ross Ndani Tanzania The Land Of Kilimanjaro

Msanii kutoka Marekani Rick Ross a.k.a the Boss amefika Tanzania kwa
ajili ya Kutumbuisha a.k.a kukamua katika show ya Serengeti Fiesta
2012 ambayo yafanyika katika Viwanja vya Leaders Club hapo kesho
tarehe 6/10/2012. Na amethibitisha kufika kwake kwa kupitia account
yake ya Twitter


Picha: www.shaffihdauda.com

Ajali Jijini Mbeya

Ajali imetokea Jijini Mbeya eneo la Mbalizi na watu kumi wafari na
wengine 25 wajeruhiwa akiwamo mbunge wa viti maalum Mary Mwanjelwa,
ajali hiyo imesababishwa na lori la mafuta lililokata break na kuanza
kugonga magari mengine na mwisho kulipuka. Mungu azilaze mahali pepa
peponi roho za marehemu wote na awaponye majeruhi wote

Ajari Ni Popote

Kweli Ajari ni popote hii ilitokea katika Mto Katuma eneo la Sitalike
Darajani Mkoani Katavi Wilaya ya Mlele, kama Unaingia hifadhi ya Taifa
ya Katavi
Dereva wa gari dogo(pichani) alilielekezea gari mtoni ambako wamejaa
Viboko ili kuepusha kugongana na Lori lililokuwa likipita darajani kwa
wakati huo kutokana na ufinyu wa daraja kutoruhusu gari zaidi ya moja
kupita kwa wakati. Hakuna mtu aliyefariki kulikuwa na majeruhi tu

Auric Air Yaanza Safari za Mpanda

AURIC AIR SERVICES LTD.

ITAFANYA SAFARI ZAKE KATIKA MAENEO HAYA.
NEW SCHEDULE OCTOBER2012. MBEYA: 10 FLIGHTS A WEEK. SONGEA: 5 FLIGHTS
A WEEK. SUMBAWANGA: 3 FLIGHTS A WEEK. MPANDA: 2 FLIGHTS A WEEK.
KIGOMA: 9 FLIGHTS A WEEK. BUKOBA: 9 FLIGHTS A WEEK. IRINGA: 7 FLIGHTS
A WEEK. RUBONDO: 7 FLIGHTSA WEEK. SERENGETI: 7 FLIGHTS A WEEK.

WOTE MNAKARIBISHWA