MUHONGO AAGIZA HALMASHAURI KUTOA TAARIFA ZA USHURU WA MADINI

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amezitaka Halmashauri zote Nchini ambazo maeneo yao yana migodi ya madini kuhakikisha wanatowa taarifa za fedha zinazopatikana kutokana na ushuru wa madini kwa wananchi wao.

Waziri Muhongo alitowa kauli hiyo wakati akiwahutubia viongozi wa Mkoawa Katavi na wachimbaji wa madini katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi Wa Idara ya maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wizara hiyo.

Alieleza kuwa wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini wamekuwa wakipotosha kuwa Halmashauri zimekuwa hazipatiushuru kwenye maeneo yao unaotokana na ushuru unaotokana na madini kitu ambacho sio sahihi Alisema hakikisheni mnawasomea wananchi wenu mapato yote ambayo Halmashauri zenu zinapata kutoka kwenye makampuni yanayochimba madini badala ya kuwaficha wananchi na matokeo yake yamekuwa ni wananchi kujenga chuki kwa makampuni hayo wakijua kuwa Halmashauri zao hazipati chochote kutoka kwa makampuni ya uchimbaji wa madini Pia alizitaka Halmashauri kuhakikisha fedha wanazolipwa kutokana na ushuru wa madini zinatumika kwa ajiri ya shughuli za maendeleo kwenye maeneo yote.

Profesa Muhongo alieleza zipo baadhi ya Halshauri wamekuwa wakitumia pesa hizo kwa ajili ya watumishi wao kwenda kujifundisha namna ya kuzowa taka kwenye mikoa mingine hayo siyo matumizi mazuri ya fedha alisema Muhongo Aidha alieleza kuwa serikali imeshaweka utaratibu ambao hakuna mgodi ambao unaanzishwa hapa Nchini bila kuwa na ubia na Serikali ndio utaratibu ambao umeisha wekwa na wizara hiyo kwani kama tulikosea mwanzo hatutakiwi kukosea tena Pia aliwashauri wachimbaji wadogo wadogo waanzishe vyama vyao ili iwe rahisi kwao kukopeshwa mikopo ambayo itawasaidia kununua vifaa vya kisasa.

Viongozi wa wachimbaji wawe na utaratibu wa kuwasikiliza kero za wachimbaji vijijini kuliko ilivyo sasa ambapo wachimbaji wanapiga simu mojakwa moja kwa waziri Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi DR Rajabu Rutengwe alieleza kuwa mbali ya mkoa kuwa na madini mbalimbali kama vile Dhahabu Shaba bado wachimbaji wanakabiliwa na changamoto mbalimbali Rutengwe alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwani vifaa duni wanavyotumia kuchimbia na mitaji midogo kwa wachimbaji.

Nae Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Katavi Willy Mbogo alimweleza waziri Muhogo kuwa jumla ya leseni 1035 zimeisha tolewa kwa wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Katavi.


Source: Katavi yetu

MWANAMKE MMOJA APIGWA RISASI BAADA YA KUKAIDI AMRI YA ASKARI

MWANAMKE mkazi wa PPF jijini hapa, Vailet Mathias, amepigwa risasi na polisi na kujeruhiwa eneo la Benki ya CRDB Mapato baada ya kukaidi amri halali ya Polisi na kumtishia silaha. Tukio hilo lilitokeajana saa 7 mchana katika benki hiyoya CRBD tawi la Mapato, mkabala naMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha.

Vailet alifika eneo hilo akiwa na gariaina ya Toyota Cresta namba T 888 BWW na kutaka kuliegesha katika lango la kuingilia magari ya kuchukua na kupeleka fedha katika benki hiyo.

Askari Polisi aliyekuwa akilinda eneo hilo, alimwamuru Vailet ambaye umri wake haukupatikana mara moja, kutoegesha gari eneo hilo, lakini akapuuza na kukaidi kisha akaingia ndani ya benki na hivyo askari huyo kuamua kutoa upepo kwenye matairi.

"Vailet alifika eneo hilo na kuingia ndani ya benki baada ya kupuuza amri ya askari aliyekuwa lindoni aliyemtaka atafute maegesho sehemu nyingine, lakini hakujibu kitu na kuwatazama askari waliokuwa hapo kwa dharau," alisema Kamanda wa Polisi wa Mkoawa Arusha, Liberatus Sabas alipokuwa anawathibitishia waandishi wa habari tukio hilo.

Alisema baada ya muda mfupi, Vailet alitoka nje na kukuta gari lakehalina upepo naye kwa hasira akamkabili askari Polisi aliyekuwa lindoni huku akimtolea maneno ya "hata kama una bastola nami ninayo" na kuitoa na kukoki akitaka amshambulie askari.

"Hata hivyo, askari alimwahi kwa bastola na kumpiga begani na kumfanya aanguke chini na bastola yake kumtoka mkononi," alisema Kamanda Boas huku akitoa mwito kwa wananchi kutii sheria bila shuruti. Alisema alichokifanya mwanamke huyo ni ukiukaji mkubwa wa sheria na kosa la jinai.

"Tunaomba kila mtu atii sheria, huuni ukiukwaji wa sheria na alimtishia bastola askari wetu, naye askari akamwahi maana eneo hili ni muhimu na hatujui mhusika alikuwana lengo gani," aliongeza Kamanda.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Fatma Kikuyu alidai mwanamke huyo alifanya kosa kukaidi amri ya Polisi na kuonesha ubabe kwa polisi na ndiyo maana tukio hilo likamkuta. Vailet alikimbizwa katika hospitali ya Mount Meru kwa matibabu, lakini alipofikishwa hapo alitolewa na kukimbizwa katika hospitali ya Selian.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya hospitali hiyo kutoka kwa daktari, ambaye hakutaka kutaja jina lake, Vailet alifikishwa hapo na wakati huo alikuwa akisubiri kuingizwa katika chumba cha upasuaji ili kutolewa risasi iliyompata kwenye bega la kushoto.


Source:Habari leo

KIGWANGALLA KUKUSANYA SAINI ZA KUMNG'OA MAKINDA

Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, (CCM), leo anatarajiwa kuanza kukusanya saini za wabunge akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni za Bunge.

Dk Kigwangalla aliibua hoja ya kutokuwa na imani na Spika katika kikao cha wabunge wote cha kuelezea shughuli zitakazofanywa na Bunge katika mkutano wa 13, kilichofanyika juzi jioni kwenye ukumbi wa Pius Msekwa.

Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, jana alithibitisha kuwapo kwa mjadala huo katika kikao cha wabunge, lakini hakuwa tayari kueleza kwa undani na badala yake alisema kwamba leo ataanza kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kukamilisha hoja ya kutokuwa na imani na Spika Makinda.

Chanzo chetu kutoka katika kikao hicho cha wabunge kilibainisha kuwa Kigwangalla alihoji kuhusiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bungeya Bajeti, Andrew Chenge (CCM-Bariadi Magharibi) kuteuliwa na Spika wakati katika kamati nyingine wenyeviti na makamu huchaguliwa na wajumbe wa kamatihusika.

Pia Dk Kigwangala alisema Spika Makinda alivunja kanuni kwa kuwapa posho ya Sh430,000 kwa siku wajumbe wa kamati inayoongozwa na Chenge wakati wajumbe wa kamati nyingine wamekuwa wakipewa Sh130,000.


"Anachokifanya Spika ni matumizi mabaya ya fedha za umma, inakuwaje wengine wafanye kazi hata bila posho lakini wao (Kamati ya Bajeti), walipwe posho ya Sh430,000 kwa siku?" chanzo hicho kilimkariri Dk Kigwangalla akihoji. Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah akizungumza na gazeti hili jana alisema mazingira ya kamati fulani kupata malipo ya ziada tofauti na viwango vya kawaida hutokea pale uongozi wa kamati husika unapoomba kwa Spika.

"Si kweli kwamba Kamati ya Bajeti inalipwa fedha za ziada kila wakati, hapana, ni pale tu wanapoomba malipo hayo kutokana na sababu ambazo lazima Spika aridhike nazo.

Ieleweke kuwa siyo kamati hiyo tu, kwa sasa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ambayo inachambua miswada mingi nayo imekuwa ikiomba na baada ya Spika kuridhia basi nao wanapewa," alisema Dk Kashililah.

Katibu huyo wa Bunge alieleza kuwa zaidi ya kamati nane zimewahi kuomba malipo ya ziada kwa maana ya kutaka posho zaidi, ulinzi, usafiri na hata chakula, ikiwazinakabiliwa na majukumu ya ziada pia katika mazingira tofauti nje ya utaratibu wa kawaida.


"Kimsingi, kamati nyingi zinapewa malipo tofauti, watu wanaweza kuwa na kazi mpaka saa saba au nane usiku, au wanakwenda kufanya kazi katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida, taratibu zinamruhusu Spika kama akiridhikana maelezo ya kazi husika, basi anaruhusu kutekelezwa kwa maombi hayo," alisema Dk Kashililah.

Kuhusu Serukamba Aidha, Dk Kigwangalla alinukuliwa akisema Spika amekiuka kanuni kwa kumchagua Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba (Kigoma Mjini-CCM), kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti.

"Hakuna mbunge yeyote aliyepo katika kamati mbili lakini hata kungekuwa na sababu maalumu basi wa kuteuliwa angekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Mahmoud Mgimwa (Mufindi Kaskazini-CCM) ambaye TRA (Mamlaka ya Mapato Nchini) ipo chini ya kamati yake," kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilisema Dk Kigwangalla alisema badala ya kumweka karibu katika ushiriki, Mgimwa alipokwenda katika kamatihiyo aliambulia kufukuzwa.

Akizungumzia suala hilo, Dk Kashililah alisema Serukamba pamoja na wabunge wengine kadhaa waliteuliwa na Spika kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kamati hiyo wakati wa kipindi cha Bajeti Kuu ya Serikali.

Aliwataja wabunge wengine walioteuliwa kushiriki katika Kamatiya Bunge ya Bajeti kuwa ni John Cheyo (Bariadi Mashariki-UDP), Salahe Pamba (Pangani - CCM) na Hamadi Rashid Mohamed (Wawi - CUF).

Kanuni za BungeKwa mujibu wa kanuni za Bunge katika toleo la mwaka 2007, kifungu cha 137(1), ili kumwondoa Spika madarakani, mbunge anayetaka kuwasilisha hoja hiyo atatakiwa kuwasilisha taarifa ya maandishi ya kusudio hilo kwa Katibu, akieleza sababu kamili ya kutaka kuleta hoja hiyo.

Kifungu kidogo cha pili kinasema baada ya kupokea taarifa ya maandishi ya kusudio la kumwondoa Spika kwenye madaraka, Katibu atapeleka taarifa hiyo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kujadiliwa.

Kifungu cha tatu kinabainisha kuwa endapo kamati hiyo itaridhika kuwazipo tuhuma mahususi dhidi ya Spika zinazohusu uvunjaji wa masharti ya ibara husika za Katiba, sheria au kanuni zinazoongoza shughuli za Bunge, basi kamati hiyoitaidhinisha hoja hiyo ipelekwe bungeni ili iamuliwe.

Kanuni zinasema Naibu Spika, atakalia Kiti cha Spika wakati wa kujadili hoja ya kutaka kumwondoa Spika madarakani na Spika atakuwa na haki ya kujitetea wakati wa mjadala na kwamba ili kumwondoa zinahitajika kura zisizopungua theluthi mbili ya idadi ya wabunge wote.

Source:Mwananchi

M23 WAFULUMUSHWA TOKA KWENYE NGOME YAO

Wanajeshi wa DRC wamefanikiwa kuwatimua waasi wa M23 kutoka katika ngome yao kuu katika eneo la Bunagana.

Wanajeshi hao wamekomboa mji wa Bunagana kufuatia makabiliano makali adhuhuri ya leo ambapo baadhi ya waasi walilazimika kuimbilia msituni huku baadhiwakidai waliingia Uganda baada ya kuvalia mavazi ya kiraia.

Msemaji wa serikali alisema kuwa mji wa Bunagana ulio katika mpaka wa Uganda na DRC, sasa uko chini ya wanajeshi wa serikali.

Wenyeji wa mji huo walithibitishia BBC kuwa mji huo ulikombolewa na kuwa waasiwamekuwa wakitoroka mapambano makali dhidi yao.

Hatua hii ya wanajeshi ni sehemu ya ushindi mkubwa ambao wanajeshi wamekuwa wakiupata dhidi ya waasi hao wa M23 walianza harakati zao dhidi ya serikali ya Congo mwaka jana wakidaiwa kusaidiwa na serikali ya Rwanda.

Mnamo siku ya Jumatatu mjumbe maalum wa M23 hawana tena nguvu za kijeshi kwani sio tesho tena.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa wakimbizi elfu tano wamelazimika kutoroka Bunagana na kuingia Uganda kwausalama wao.

HUKUMU YA BABU SEYA NA PAPII KOCHA YAANZA KUSIKILIZWA MAHAKAMA YA RUFAA

Hukumu ya Nguza Viking maarufu kama babu Seya imeanza kupitiwa.

Mahakama ya rufaa imeanza kupitia hukumu ya mwanamuziki maarufu nchini mwenye asili ya jamhuri ya kidemokrasia ya congo DRC Nguza Viking maarufu kama Babu seya na mwanawe Johnson Nguza maarufu kama Papii kocha.

Mapitio hayo yanafanywa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Mh Nathali Kimaro amboa ndio waliotoa hukumu Februari 2010 kwa upande wa waleta maombi wakiongozwa na wakili Mabetre Marando wamewasilisha mahakamani hapo mambo sita ambayo wangepedwa mahakama hiyo iyaangaliye kwa makini,ambapo moja ya mambo hayo ni pamoja na kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi mashahidu muhimu hawakuitwa kutoa ushaidi wao.


Aidha wanataka ushaidi wa watoto uliotolewe katika kesi hiyo uondolewe katika kumbukumbu kwa sababu haukufuta taratibu na vigezo vya matwakwa ya sheria ya ushaidi pia wamesema kuwa katika ushaidi uliotolewa ulionyesha kuwa katika nyumba ya babu seya kulikuwa na mlango wa siri lakini mahakama ilipokwenda hapo mlango huo haukuonekana.

Kwa upande wa serikali kupitia wakili wake mwandamizi jackson burashi wameiomba mahakma hiyo kutupilia mbali shauri hilo kutokana na ukweli kuwa yapo hapo kinyume na sheria na yameletwa kama rufaa na siyo mapitio.


Aidha akaongeza kuwa maombi hayo hayajakidhi viwango vya sababu za mapitio kwa kuwa maombi hayo yalipaswa kuonyesha kuwa kosa limetendeka na haki ya mleta rufaa imepotea. Baada ya maelezo ya pande zote mbili mahakama ikasema itatoa maamuazi baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili.

Babu Seya na mwanaye papii kocha wanaendelea kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hati ya makosa ya kunajisi na kulawiti watoto wadogo kupitia huku iliyotolewa na mahakama ya hakimu mkazi kisutu mwaka 2004 ambapo walihkumiwa kifungo cha maisha.

TANZANIA YAFIKILIA KUJITOA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Serikali ya Tanzania imesema inatafakari ushiriki wake ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na inaweza kujitoa ndani ya Jumuiya hiyo iwapo itaendelea kutengwa katika baadhi ya vikao.

Aidha imesema Tanzania haitambui vikao vinavyofanywa na nchi tatu zilizopo ndani ya Jumuiya hiyo ambazo zimekuwa zikizitenga Tanzania na Burundi.

Waziri anayehusika na masuala ya Afrika Mashariki wa Tanzania Samwel Sitta ameliambia Bunge la Tanzania kuwa makubaliano ya vikao hivyo vinavyofanywa na nchi za Kenya, Rwanda na Uganda yatatekelezwa na nchi hizo zinazofanya vikao hivyo kwa sababu vinafanyika nje ya utaratibu wa mkataba wa jumuiya hiyo.

Katika mikutano iliyofanyika hivi karibuni Tanzania na Burundi hazikualikwa kwenye vikao hivyo.

Kwa mujibu wa Waziri Sitta mikutano ya wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambayo ilianza kwa kuitenga Tanzania ilifanyika Entebbe nchini Uganda mwezi Juni mwaka huu na kufuatiwana mkutano wa pili uliofanyika Agosti mwaka huu huko Mombasa nchini Kenya ambapo nchi hizo tatu bila kuishirikisha Tanzania walizungumzia uanzishaji wa himayamoja ya forodha.

Mambo mengine waliyozungumza wakuu hao ilikuwa uanzishaji wa visa moja ya utalii kwa nchi zao na matumizi ya vitambulisho vya uraia ambavyo vitatumika kama hati za kusafiria miongoni mwa nchi hizo.

Aidha Waziri Sitta amesema ndani ya mikutano hiyo pia walizungumziakuanzisha mchakato wa kuanzisha shirikisho la nchi hizo.

Tayari Tanzania imeanza mazungumzo na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuangalia ni kwa namna gani zitaanzisha ushirikiano nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama zinavyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya.

VIJANA MILIONI 2.6 WANAISHI NA VVU NCHI

Vijana milioni 2.6 wenye umri wa miaka kati 15 na 24 nchini, wanaishi na virusi vya Ukimwi.


Takwimu hizo zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), Abdoul Coulibaly, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya elimu ya jinsia na afya ya uzazi kwa vijana katika nchi 21 za Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Alisema karibu vijana 50 katika nchi hizo huambukizwa virusi vya Ukimwi kila saa moja, huku idadi ya wasichana wakiongoza kwa maambukizi hayo.

Coulibaly alisema idadi hiyo ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa vijana kwa Tanzania, inachangiwa na kutokuwapo kwa elimu ya kutosha ya jinsia pamoja na VVU na Ukimwi, afya ya uzazi na ukuaji wa binadamu.


Alisema asilimia kubwa ya vijana hawana uelewa wa masuala ya afya ya uzazi na jinsia, jambo ambalo husababisha kujiingiza kwenye mapenzi katika umri mdogo na kusababisha kuongezeka kwa mimba za utotoni.

Pia aliiomba serikali kuweka mikakati madhubuti ya kutoa elimu ya afya na jinsia kwa vijana kwa ajili ya kusaidia kupunguza idadi ya maambukizi kwao pamoja na mimba za utotoni zinazosababishwa na ukosefu wa elimu hiyo.

Kaimu Mkurugenzi, kitengo cha masuala mtambuka kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Laetitia Sayi, alisema changamoto ya maambukizi ya VVU kwa vijana ni kubwa na kwamba serikali kwa upande wake inafanya jitihada mbalimbali za kutatua tatizo hilo.

WATU WATATU WAKAMATWA NA MKONO WA BINADAMU

Watu 3 wamekamatwa na kiganja cha mkono wa binadamu mkoani Mwanza.

Watu watatu wakiwemo waganga wawili wa jadi wamekamatwa na polisi katika eneo la Igombe Tx, jijini Mwanza wakiwa na kiganja cha mkono wa kulia unaoaminika kuwa wa binadamu.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, kamishna msaidizi wa polisi Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea eneo la kati ya ziwani na nyuma ya uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya raia wema kuwapa taarifa za siri.


Source:ITV

TANZANIA YAPUUZIA MIKUTANO INAYOITISHWA NA RWANDA, UGANDA NA KENYA

Jumuiya ya Afrika Mashariki imekumbwa na msukosuko bada ya TZ kupuuza mikutano inayofanya ikisema inakiuka utaratibu wa jumuiya.

Wakuu wa nchi za Kenya,Uganda na Rwanda baadaye leo wanatarajia kusaini makubaliano ya kuanzisha kituo kimoja cha kukusanya ushuru kinachotarajiwa kurahisisha uchukuzi wa bidhaa kutoka Mombasa Kenya -- Uganda hadi Rwanda.

Kuundwa kwa Kituo hicho pia kunatazamiwa kurahisisha shughuli nzima za uchukuzi katika maeneo hayo ya Afrika Mashariki.

Taifa la Sudan Kusini pia linataraji kuidhinishwa kama mshirika katika kikao cha wakuu wa mataifa hayo.

Mkutano huu unalenga kuimarisha maendeleo ya kikanda kupitia kwa miundo msingi bora , uchumi na biashara.

Shughuli hii inakuja baada ya mkutano uliofanyika mjini Kampala Uganda, mnamo mwezi Juni na mwengine uliofanyika mjini Mombasa mnamo mwezi Agosti ambako viongozi walipendekeza kupanuliwa kwa bandari ya Mombasa ili kuwezesha uharaka wa bidhaa kupitishiwa bandarini humo katika kuhudumia kanda nzima.

Tanzania awali ilipuuza mikutano ya Kenya ,Uganda na Rwanda ikisema kuwa ni kinyume na utaratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kando na hayo mkutano mwengine wa marais wa nchi nane utafanyika Kesho ambapo watakutana kwenye kongamano la siku nne mjini Kigali ambalo linatarajiwa kuweka kipaombele kwa uimarishwaji wa huduma za internet katika mataifa hayo.

Mkutano huo unaofanyika miaka sita baada ya Kigali kuwa mwenyeji wa kongamano la Connect Africa, mwenyeji wake atakuwa Rais Paul Kagame na Dr Hamadoun I. Toure, katibu mkuu wa muungano wa kimataifa wa mawasiliano ya kiteknolojia (ITU).

Marais hao ni pamoja na Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Salva Kiir wa Sudan Kusini Ali Bongo Ondimba waGabon, Thomas Boni Yayi wa Benin na Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso.

Mkutano huo unaanza rasmi Kesho.Nchi zengine 15 za Afrika zitashiriki kwenye mkutano huo ambao kwa mujibu wa waandalizi, zaidi ya wajumbe 1,500 watahudhuria.

WASHUKIWA WAWILI WA UGAIDI WAUWAWA TANGA

Watu wawili wanaodaiwa kuhusishwa na vitendo vya kigaidi wameuawa kwa kupigwa risasi wakati kundi hilo lilipokuwa msikitini huku wafuasi wake wakiwa na silaha za moto na baridi walipokuwa wakijibizana kwa kutumia silaha mbali mbali ndipo askari walipowahi kuwashambulia viongozi wa kundi hilo kisha kuwanyang'anya silaha zao ili kuepuka madhara makubwa zaidi.

Mkuu wa mkoa wa Tanga luteni mstaafu Chiku Gallawa amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Kimamba kilichopo kata ya Negero wilayani Kilindi wakati kundi hilo lilipokuwa limejiandaa kujibu mashambulizi ya askari msikitini kwa kuwa na silaha aina ya bunduki na mapanga ndipo viongozi hao waliposhambuliwa ambapo mmoja alifariki papo hapo huku mwingine akifariki hospitali ya wilaya.


Chanzo:ITV

CHADEMA WATUPIANA MAKONDE

Viongozi Chadema wazipiga kavukavu kwenye mkutano
Mkutano wa Baraza la Uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini juzi uligeuka ukumbi wa ngumi, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha,

Samson Mwigamba kushushiwa kipigo.
Mwigamba alishushiwa kipigo hicho na baadhi ya viongozi wenzake wa chama kwa madai ya usaliti na tayari amesimamishwa uongozi kwa muda usiojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas jana alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na viongozi hao wa Chadema kufikishana polisi.

Alikutwa na zahama hiyo mbele ya viongozi wakuu wa Chadema Taifa, Mwenyekiti, Freeman Mbowe na mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei katika Hoteli ya Coridal Spring.


Viongozi hao wamekuwa wakifanya ziara za aina hiyo nchi nzima, kuimarisha chama na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na uchaguzi mkuu ujao wa Rais na wabunge mwaka 2015.

Habari kutoka ndani ya mkutano huo zinaeleza kuwa hatua hiyo ilifuatia tuhuma kwamba Mwigamba alituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forums, unaodaiwa kukichafua chama hicho.


Tukio hilo la aina yake lilitokea wakati viongozi wote wa juu wa chama hicho, wakiongozwa na Mbowe walipokuwa wakijadili mustakabali wa chama hicho, mkutano ambao ulihudhuriwa na wabunge karibu wote wa Chadema wa kanda hiyo.

Hata hivyo, wakati mijadala ikiendelea baadhi ya viongozi wa chama hicho, akiwamo Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema walimtuhumu Mwigamba kutuma ujumbe kwenye mtandao huo, uliokuwa ukizungumzia ufisadi ndani ya chama hicho, wakidai alitaka Mwenyekiti Mbowe kukubali kuchunguzwa.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mwigamba alisema kuwa baada ya Lema kutoa tuhuma hizo aliungwa mkono na viongozi wengine na vijana waliokuwa wameimarisha ulinzi, kumvamia na kuanza kumpiga pamoja na kumnyang'anya kwa nguvu kompyuta mpakato (Laptop), aliyokuwa nayo, kisha kumpeleka Kituo Kikuu cha Polisi, mjini Arusha.

"Wamenipiga sana na kuniweka ndani, ila nashukuru Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Arusha (OCCID), alikuja na kunitoa saa 5:00 asubuhi,"alisema Mwigamba.


Alisema kuwa leo katika mkutano wake na waandishi wa habari ataeleza yote yaliyotokea na hatua atakazochukua, kwa kuwa yeye ni kiongozi wa juu wa chama.

Hata hivyo, alieleza kwamba bado anashauriana na wanasheria wake kuona kama anaweza kuwachukulia hatua waliompinga.


Kauli ya polisi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi wameona hakuna kosa la kisheria lililotokea hasa kutokana na malalamiko yaliyofikishwa kwao dhidi ya Mwigamba ya kukichafua chama kwenye mitandao.

"Hili suala la mitandao ni kubwa na lina taratibu zake sasa kusema tu umechafuliwa na iwe kesi nadhani uchunguzi unahitajika kwao, sisi tumeona haya ni mambo yao wanaweza kuyamaliza wao ndiyo sababu tulimwachia, Mwigamba,"alisema Sabas.

Kosa analodaiwa kufanya Mwigamba

Akizungumzia sakata hilo jana, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema kwamba Mwigamba alibainika kutuma ujumbe kwenye mtandao wa Jamii Forums uliokichafua chama hicho, akieleza haikuwa mara yake ya kwanza kwa kiongozi huyo kufanya hivyo na kwamba walikuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu.

"Kilichotokea ni hicho, vijana wa Red Brigade ndio waliomtoa ukumbini, baada ya kumbaini kukichafua chama, kwani laptop yake baada ya kuchunguzwa na wataalamu wetu walijiridhisha ni yeye ndiye aliyetuma ujumbe huo,"alisema Lema.

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alitaja tuhuma zinazomkabili Mwigamba kuwa ni pamoja na kusema uongo, kupotosha taarifa za chama na kuchonganisha viongozi kupitia mtandao wa kijamii ya Jamii Forums.

Katika andiko lake kwenye mtandao, Mwigamba anadaiwa kuwatuhumu viongozi wa juu wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Wilbrod Slaa kuwa wamechakachua katiba ya chama hicho kuhusu ukomo wa nafasi za uongozi ili kujinufaisha binafsi.

Golugwa alisema kuwa baada ya kubanwa kwenye kikao, Mwigamba alikiri kuandika na kurusha taarifa hizo kwenye mitandao, lakini alipotakiwa kukabidhi kompyuta yake ili ichunguzwe na wataalamu wa mawasiliano wa chama hicho aligoma, hali iliyozua tafrani kati yake na walinzi wa chama hicho (Red Brigade), waliolazimika kutumia nguvu kumdhibiti.

Purukushani zilivyotokea
Habari zaidi zinaeleza kuwa katika harakati za kutaka kumnyang'anya Mwigamba kompyuta yake, mwenyekiti huyo wa Chadema mkoani Arusha alianza kushambuliwa na baadhi ya viongozi wa Chadema, kabla ya kufanikiwa kumdhibiti.
Zinaeleza kuwa katika tukio hilo kulitokea pia kurushiana maneno na matusi ya nguoni kati yake na viongozi wengine wa chama hicho akiwamo Lema.

Baadaye Lema aliliambia gazeti hili kwamba katika purukushani hizo Mwigamba alimrushia ngumi ambayo hata hivyo aliikwepa.

Alisema kuwa wanakusudia kumfungulia kesi Mwigamba ya kukichafua chama chao katika mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, alisema kikao chao kiliendelea jana bila ya vurugu zozote na kuweka mikakati ya kushinda majimbo yote ya Kanda ya Kaskazini mwaka 2015 na kuchukua nchi katika uchaguzi huo ujao.
Adhabu kwa Mwigamba
Katika hatua nyingine Chadema, kimemsimamisha uongozi Mwigamba kwa tuhuma za kukisaliti, kukihujumu chama hicho na viongozi wake.

Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jijini Arusha jana, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Israel Natse alibainisha kuwa uamuzi wa kumsimamisha Mwigamba katika nyadhifa zote za uongozi ndani ya chama ulifikiwa na kikao cha Baraza la Uongozi wa Kanda ya Kaskazini kilichokutana juzi.


Alisema kuwa Mwigamba amesimamishwa kwa muda usiojulikana kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake na kuonya kuwa iwapo tuhuma zitathibitishwa, hatua nyingine za kinidhamu zitafuata kulingana na kanuni na katiba ya Chadema.

"Kwa sasa Mwigamba anatuhumiwa kuvunja sura ya kumi, kifungu cha 10.1 kifungu kidogo cha 8, 9 na 10 ya katiba ya Chadema inayozungumzia maadili ya uongozi,"alisema Natse.

Akifafanua zaidi alisema kuwa sura na vifungu hivyo vinakataza kiongozi wa chama hicho kutoa tuhuma dhidi ya viongozi wenzake bila kufuata vikao halali vya kikanuni na kikatiba.

MASHABIKI WA DORTMUND WAVUNJA VITI EMIRATES

Kama ulizani tatizo lipo kwa watanzania tu kung'oa viti uwanja wa taifa basi ondoa mawazo hayo.

Mashabiki wa Borussia Dortmund kutoka Ujerumani wamevunja na kung'oa viti(Pichani) katika uwanja wa Emirates unaomilikiwa na klabu ya Arsenal kutoka Uingereza.

Tukio lilitokea siku ya jumanne wakati timu hizo zilipokutana katika mchuano wa ligi ya klabu bingwa ulaya ambapo Dortmund waliondoka na ushindi wa goli 2 kwa 1.

Magoli katika mchezo huo yalifungwa na H. Mkhitaryan wa Borussia Dortmund katika dakika ya 18 ya michezo kabla ya mfungaji wa Arsenal Olivier Giroud kusawazisha katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza.

Alikuwa ni Roberto Lewandowski aliyepigilia msumari wa mwisho katika dakika ya 85 na kufanya ubao wa matangazo kusomeka Arsenal 1-2 B. Dortmund na kuharibu furaha ya kocha Arsene Wenger ambae ilikuwa siku yake ya kuzaliwa na kufikisha miaka 64.

Arsenal bado wanashikilia usukani wa kundi huku wakiwa pointi sawa na Dortmund pointi 6 tofauti ya magoli imeibeba Arsenal. Baada ya Dortmund wanafuata Napol kutoka Italy wakiwa na pointi 6 kisha Marseille ya Ufaransa ikiwa haina kitu.

MALAWI YACHUKIZWA NA MATAMSHI YA ZUMA

Serikali ya Malawi imeghadhabishwa na matamshi ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Kusini yaliyoonekana kudharau miundo msingi nchini Malawi.

Malawi sasa imemtaka balozi mkuu wa Afrika Kusini nchini humo kuelezea matamshi ya kusikitisha yaliyotolewa na Rais Jacob Zuma kuhusu nchi hiyo.

Balozi huyo, Cassandra Makone alitakiwa na serikali ya Malawi kufafanua matamashi ya Zuma yaliyotafsiriwa na wengi kumaanisha kuwa Malawi bado iko nyuma sana alipokuwa anazungumzia miundo msingi ya Afrika Kusini.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Quent Kalichero aliambia shirika la habari la AFP kuwa Makone aliitwa na serikali ili kueleza alichomaanisha Rais Zuma.

Balozi huyo alifanya mkutano na afisaa mkuu katika wizara ya mambo ya nje George Mkondiwa ingawa Kalichero inaarifiwa alikataa kutoa maelezo ya mkutano.

Mnamo siku ya Jumatatu, Zuma alizua utata alipokuwa anawashawishi madereva wa nchi hiyo kukubali kutozwa kodi za barabarani mjini Johannesburg.

''Tuko mjini Johannesburg, na hii ni Johannesburg. Sio kama barabara ovyo ya kitaifa nchini Malawi,'' alinukuliwa akisema Zuma.

Hata hivyo msemaji wa Zuma Mac Maharaj alisema kuwa taarifa hiyo ilitafsiriwa visivyo.

Aliongeza kuwa Zuma alikuwa tu anasisitiza kuhusu mfumo mzuri wabarabara Afrika Kusini ikilinganishwa na nchi zengine katika kanda ya Afrika Kusini.

Hata hivyo, Maharaj aliomba radhi kwa matamshi hayo akisema kuwa watu wengi wameghadhabishwa nchini Malawi.

MABAKI YA MOBUTU SESEKO KUZIKWA DR CONGO

Serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, imesema itahamisha mabaki ya mwili wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mobutu Sese Seko kufuatia makubaliano na familia yake. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya rais wa nchi hiyo, President Joseph Kabila.

Hayati Mobutu alizikwa nchini Morocco, alikofariki mnamo mwaka 1997 baada ya kuondolewa mamlakani kutokana na uasi ulioongozwa na baba yake Rais Joseph Kabila.

Alikuwa mtu aliyechukiwa sana na wengi nchini Congo, lakini nchi hiyo imekumbwa na migogoro tangu alipong'olewa mamlakani.

Hatua ya Kabila inaonekana na wengi kama mpango wake wa kuwapatisha watu wa nchi hiyo.

Kabila alishinda uchaguzi wa mwaka 2007 bila ya pingamizi na anakabiliana na uasi Mashariki mwa nchi.

Rais Kabila ametoa tangazo hilo la kipekee katika hotuba yake kwa bunge ambapo aliahidi kuunda serikali ya pamoja.

''Serikali hii itajumuisha wanachamawa chama tawala na wale wa upinzani pamoja na viongozi kutoka mashirika ya kijamii,'' alisema katikahotuba yake.

Mtaalamu wa maswala ya Afrika Ibrahima Diane anasema kuwa huenda Kabila alishauriana na mwanawe Mobutu, Nzanga Mobutu, kabla ya kutangaza kuwa mabaki ya hayati Mobutu yatazikwa nchini Congo.

Mobutu Sese Seko angali anawakumbuka wengi hasa wafuasi wake wanaoamini kuwa moja ya mambo mazuri aliyoyafanya ni kuunganisha nchi hiyo.

Nzanga Mobutu ni mbunge ambaye sasa ni mshirika wa karibu wa Rais Kabila.

Mobutu Sese Seko alitoroka DR Congo wakati waasi walioongozwa na Laurent Kabila, kuzingira mji mkuu Kinshasa, mnamo mwaka 1997.

Wakosoaji wake wanamtuhumu kwakuwa mkatili na kiongozi mfisadi aliyekandamiza upinzani na kuponda maliasili ya DR Congo.

Pia alitumia mamilioni ya dola kuijengea kasri yake ya Gbadolite, iliyo ndani ya misitu ya DRC ambayo ilifanyiwa msako mkubwa alipotoroka DR Congo.

Aliingia mamlakani kupitia kwa mapinduzi na kuitawala DR Congo, iliyokuwa inajulikana kama Zaire, kwa zaidi ya miaka 30.

Hata hivyo alifariki akiwa na miaka 66 miezi michache tu baada ya kuikimbia nchi yake.

MOSHI WA KIWANDA CHA OK PLASTIC WAZUA TAHARUKI

Moto uliowaka eneo la kiwanda cha OK Plast Ltd wasababisha hali ya taharuki.

Moto uliowaka katika eneo la Jalala la kiwanda cha OK Plast Ltd kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam umesababisha hali ya taharuki ikiwemo watu kukimbia ovyo na kuacha ofisi na mali zao kwa kuhofia maisha yao baada ya Moshi mzito uliotokana na moto huo kutanda angani.

Tukio la moto huo umetokea katika eneo la wazi la kiwanda cha OK Plast Ltd inayohusika na utengenezaji wa vitu mbalimbali ikiwemo viatu aina ya kandambili pamoja na mikeka, ambapo kwa mujibu wa wenyweji wa eneo hilo wamedai kiwanda hicho cha OK Plast Ltd walikuwa wakitumia eneo hilo kutunzia mabaki ya mali gafi yao ambapo ghafla kijana mmoja amedaiwa kwenda katika eneo hilo na kuwasha moto ikisemekana alikuwa akitafuta asali kutokana na kuwepo kwa nyuki waliokuwa wakiishi kwa muda mrefu katika eneo hilo.

Moto huo ulisababisha moshi mzito kutanda angani huku vikosi vya zimamoto na baadhi ya wafanyakazi wa makampuni ya jirani na eneo la tukio wakijitahidi moto kuenea katika viwanda na makampuni mengine ambayo kwa wakati huo tayari yalikuwa yapo tupu baada ya watu kutimua mbio kuokoa maisha yao ambapo mkurugenzi wa Pb Investment bwana Mushtack Fazar aliyethibitisha kununua eneo hilo kutoka kwa kiwanda cha Ok Plast Ltd anaeeleza tukio ilivyokuwa.

Licha ya tukio hilo la moto kutokea katika eneo hilo lakini wakazi wa maeneo wamesema kiwanda hicho kinaongoza kwa kuchafua mazingira na kwamba tukio kama hilo si la kwanza ambapo afisa utawala wa kiwanda cha OK Plast Ltd bwana Martin Msamba alipofuatwa kujibu malalamiko hayo amesema ni tukio la kwanza na kwamba kijana aliyehusika kuwasha moto ameshikiliwa na polisi tayari.

KAMPUNI YA SIGARA KOREA YADAIWA KUFANYA UBAGUZI WA RANGI

Kampuni kubwa ya Tumbako nchini Korea Kusini, imeahidi kubadilisha tangazo lake la kibiashara ambalo limekosolewa kwa kuonekana kuwa la kibaguzi.

Mabango yenye tangazo hilo la aina mpya ya sigara ya kiafrika, yalikuwa na picha za Tumbili waliovalia kama waandishi wa habari wakitangaza kuwa ''Afrika inakuja!" Sigara hizo ni bidhaa mpya ya kampuni ya 'This Africa line'.

Aidha kampuni hiyo inasema kuwa sigara hizo zimetengezwa kwa Tumbako ya kiafrika na ambayo imekaushwa kwa njia za kitamaduni.

Paketi za Sigara zina picha zinazoonyesha Tumbili wakichoma tumbako hiyo.

Kejeli kwa Afrika

"tumeudhiwa sana na picha hii ya kejeli iliyotumiwa na kampuni hiyo ikionyesha Tumbili na kuwahusisha na Afrika,'' alisema, ilisema taarifa ya baraza kwa kudhibiti biashara ya Tumbako ya Afrika ikisema kuwa sharti tangazo hilo liondolewe haraka iwezekanavyo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, ''kukejeli Afrika ili kuongeza mauzo ya bidhaa ambazo husababiha vifo na maradhi sio jambo linalokubalikana wala hatutakubali. ''Tangazo hilo la biashara limewekwa katika maeneo ya maduka kote nchini humo.

Hata hivyo msemaji wa kampuni hiyo ameelezea kuwa tangazo hilo litaondolewa madukani mwezi ujao.

Amesema kuwa kampuni imejutia utata uliosababishwa na tangazo hilo na kusema kuwa kampuni hiyo ingependa kuondoa wasiwasi wowowte ulioibuka kutokana na tangazo hilo kuhusu ubaguzi wa rangi Alisema hawakuwa na nia yoyote yakuwa kejeli waafrika na kuwa walichagua kutumia tumbili kwa sababu ni wanyama wazuri wanaowakumbusha watu kuhusu Afrika.

Kampuni hiyo inasema kuwa kwa sababu bidhaa hii ina majani ya tumbako kutoka Afrika, nia ya kampuni ilikuwa tu kufananisha bidhaa hiyo na Afrika.

DIWANI ACHEZEA KICHAPO HUKU MTU MMOJA AKIUWAWA KWA RISASI MKOANI KATAVI

Diwani wa Kata ya Majimoto Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Nyasongwe (45) amejeruhiwa vibaya na kulazwa hospitalini baada ya kupigwa na askari wanaofanya oparesheni kimbunga katika Mkoa wa Katavi wakati akiwa msibani kwa mwanakijiji aliye uwawa kwa kupigwa risasi na Askari wanaofanya oparesheni kimbunga baadaya kutokea vurugu baina yao na wanakijiji cha Luchima kata ya Majimoto Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.

Akiongea kwa taabu na waandishi wa habari Diwani huyo wa Kata ya Majimoto ambae amelazwa katika wodi namba moja huku akiwa chini ya ulinzi wa Polisi katika wodi namba moja katika hospitali ya wilaya ya Mpanda ambako amelazwa Alisema tukio hilo na kupigwa na kujeruhiwa lilitokea hapo oktoba 13 mwaka huu majira ya saa sita mchana wakati akiwa msibani kijijini hapo alipokuwa amekwenda kwenye msiba wa mwanakijiji ambae alikuwa ameuwa muda mfupi kwa kupigwa risasi na askari wanaofanya opuresheni Kimbunga.

Alieleza kuwa siku hiyo ya tukio yeye wakiwa na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mamba Lyoba Juma Shomari walipata taarifa kuwa kumetokea vurugu baina ya wanakijiji cha Luchima na Askari wanaofanya opuresheni Kimbunga na kusababisha kifo cha mwanakijiji mmoja na kushambuliwa na kujeruhiwa kwa mkuu wa kituo cha kutuliza ghasia wa Mkoa wa Katavi ASP Mafie Diwani huyo ambae ameumia vibaya sehemu yamatako.

Alisema ndipo walipokubaliana na afisa tarafa huyo na kuelekea kwenye eneo la tukio ambapo walikuta wanakijiji wakiwa wameweka tayari msiba wa mwanakijii mwenzao ambae alikuwa ameuwawa kwa kupigwa risasi Alifafanua kuwa kifo cha mwanajijiji huyo kilitokana na vurugu zilizotokana na wanakijiji hicho kutoridhishwa kuona mwenzao mmoja nyumba yake ikipekuliwa na kikosi cha opareshen kimbunga ndipo walipoamua kumshambulia kwa fimbo ASP Mafie na kujeruhi kichwani na kumfanya kupoteza fahamu.

Pia wanakijiji hao walilishambulia kwa mawe gari la polisi lenye namba PT 0985 na kulivunja kioo ndipo askari hao wa opuresheni kimbunga walipo amua kufyatua risasi ambayo ilimuuwa mwanakijiji huyo na kumjeruhi mguuni mwakakijiji mwingine ambae amepelekwa Katika hospitali ya Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ajiri ya matibabu Serengeti alieleza kuwa wakati wakiwa bado wako hapo msibani ghafla lilitokea kundi la askari wa opuresheni kimbunga na kuanza kuwashambulia waombolezaji wote waliokuwepo hapo bila kujali jinsia ingawa yeye na afisa Tarafa hiyo waliweza kujitambulisha lakini waliendelea kupokea kipigo bila huruma kutoka kwa askari hao.

Alieleza kuwa kisha walipakiwa kwenye roli la jeshi wakiwa na kundi la watu waliokuwa wanaomboleza msibani hapo kwa kudaiwa kumshambulia mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia wa Mkoa wa Katavi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alipotakiwa kutowa ufafanuzi kuhusiana na tukio hili alisema kuwa opuresheni hiyo Kimbunga mhusika ambae anatakiwa kutowa taarifa za tukio hili ni mkuu wa Hifadhi ya wanyama pori ya Katavi Kwa upande wake mkuu wa Hifadhi ya Katavi Ignasi Gara alishindwa kutowa kabisa ushirikiano kwa waandishi wa habari na kuatupia jeshi la wananchi kuwa wao ndio wasemaji wakuu.


Chanzo:Katavi Yetu blog

MADIWANI WAGOMA KUJADILI TAARIFA YA KAMATI YA FEDHA

Mpanda Katavi

Madiwani wa Halimashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi wamekataa kujadili taarifa ya kamati ya fedha na mipango ya Halmashauri hiyo iliyo wasilishwa kwenye kakao cha Baraza la madiwani kilichofanyika juzi kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha Mkoa wa Katavi.

Baraza hilo la madiwani lilikataa kupitisha taarifa hiyo kufuatia hoja mbalimbali zilizotolewa na Madiwani ambao walidai kuwa taarifa hiyo iliyoletwa mbele ya kikao hicho haikuwa imejitosheleza.

Miongoni mwa kasoro zilizodaiwa kuwemo kwenye taarifa hiyo ni kutokuwemo kwa viambata vinavyo onyesha namna ya mapato yandani yalivyo kusanywa na sehemu yaliko tokaDiwani wa kwanza kipinga taarifa hiyo kwenye kikao hicho cha Baraza la madiwani kilicho kuwa kinaongozwa na makamu mwenyekiti wa Halimashauri ya mji wa Mpanda Yusuph Ngasa.

Alikuwa ni Diwani wa Kata ya Shanwe Abel Kapini Diwani Kapini alidai kuwa taarifa hiyo inamapungufu ambayo yatawafanya madiwani kama wataamua kuijadili washindwe kuijadili kitaalamu kwani haina mchanganuo ambao utawawezesha madiwani kuhoji taarifa hiyo ya kamatiya fedha na mipango Kwa upande wake diwani wa Kata ya Ilembo Wensilaus Kaputa alilieleza Baraza hilo kuwa taarifa hiyo haiko wazi kwani inaonekana taarifa zake zimefichwa kwa hari hiyo ni vizuri irudishwe ikaandaliwe upya.

Mwenyekiti wa kikao cha baraza la madiwani baada ya kutolewa hoja hizo aliwashauri madiwani wapige kura ili kujua ni madiwani wangapi wanao unga mkono hoja hiyo ya kuikataa taarifa hiyo.

Kufuatia uamuzi wa mwenyekiti madiwani walipiga kura ambapo kulikuwa na madiwani kumi kwenye kikao hicho na madiwani wanane waliunga mkono kuikataa taarifa hiyo na madiwani wawili waliikubali Nae Mkugenzi wa Halimashauri ya Mji wa Mpanda Selamani Lukanga alihaidi kuwa kikao kijacho cha Baraza hilo watasomewa taarifa ikiwa na viambatanisho na mchanganuo kama ambavyo walivyo hitaji madiwani.


Source:Katavi Yetu

RENAMO YAFANYA SHAMBULIO HUKO MSUMBIJI

Ripoti kutoka Musumbiji zinaarifu kuwa wanaharakati waliojihami kutoka kundi la upinzani la Renamo, wameshambulia kituo kimoja cha polisi katika mji wa kati wa Maringue.

Kisa hicho kinajiri siku moja baada ya Renamo kusema kuwa inajiondoa katika mazungumzo ya amani ya mwaka 1992 yaliosababisha kusitishwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Renamo ilikaidi makubaliano hayo baada ya vikosi vya serikali kushambulia kambi iliokuwa na kiongozi wake Afonso Dhlakana na kumlazimu kutoroka.

Hali ya wasiwasi kati ya serikali na Renamo imeongezeka katika siku za hivi karibuni huku mapigano yakiripotiwa katika maeneo mbalimbali.

Inakadiriwa kwamba zaidi ya watu milioni moja waliuawa katika vita hivyo vya miaka 16 vilivyo sababisha mazungumzo ya amani huku Renamo ikibadilika kutoka kundi la wanamgambo hadi chama cha kisiasa.

SIMBA, YANGA WAINGIZA SH. MILIONI 500

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ya watani wa jadi Simba na Yangailiyochezwa jana (Oktoba 20 mwakahuu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar esSalaam na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3 imeingiza sh. 500,727,000.Washabiki 57,422 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 63kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000na sh. 30,000.Ni tiketi 131 tu ndizo hazikuuzwa ambazo ni 90 za VIP A, 40 za VIP B namoja ya VIP C. Tiketi zilizochapwa kwa ajili ya mechi hiyo ni 57,558 ambayondiyo idadi ya viti vilivyopo kwenye uwanja huo.

Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,025,564.32 wakati Kodi ya Ongezeko laThamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,382,084.75.


Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 62,555,371.69, tiketi sh. 7,309,104, gharama za mechi sh. 37,533,223.01, Kamati ya Ligi sh. 37,533,223.01, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.18,766,611.51 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.14,596,253.39.

WASHAMBULIWA WAKATI WAKITOKA KANISANI

Waumini walishambuliwa wakiwa wanatoka kanisaniWatu watatu akiwemo msichana mdogo mwenye umri wa miaka 8 aliuawa wakati watu waliokuwa wamejihami wakiwa kwenye pikipikikushambulia sherehe za ndoa nje ya kanisa la Kikopti mjini Cairo.

Takriban wengine 9 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo mjini Giza.

Hata hivyo hakuna taarifa zozote kuhusu nani aliyehusika na shambulizi hilo.

Jamii ya wakristo wa kikopti wamekuwa wakishambuliwa na baadhi ya waisilamu wanaotuhumu kanisa kwa kuunga mkono jeshi katika kumpindua aliyekuwa Rais Mohammed Morsi mwezi Julai.

Washambuliaji hao ambao hawakutambuliwa, waliwafyatulia risasi kiholela watu waliokuwa wanaondoka kanisani.

Mwanamume mmoja na mtoto huyo waliuawa nje ya kanisa hilo wakati mwanamke mmoja akifariki akipelekwa hospitalini. "Tulisikia mlio mkubwa sana mfano wa kitu kilichokuwa kinaanguka,'' alisema shahidi mmoja.

"Nilimkuta mwanamke mmoja akiwa ameketi kwenye kiti chake, akiwa amejeruhiwa kwa risasi. Watuwengi walikuwa wameanguka kandoyake akiwemo mtoto mdogo.

''Kasisi wa kanisa hilo Thomas Daoud Ibrahim alisema kuwa alikuwa ndani ya kanisa hilo, wakati, milio ya risasi ilikuwa inasikika.

"Kilichofanyika ni kitu kibaya sana na sio waksristio wakopti waliolengwa pekee yao , tunaharibunchi yetu,'' alisema kasisi huyo.Kasisi mwingine aliambia vyombo vya habari kuwa kanisa hilo liliachwa bila polisi wala mlinzi tangu mwishoni mwa mwezi Juni.

Kanisa hilo ni moja ya makaisa ya zamani ya kikristo iliyoanzishwa mjini Alexandria mapema miaka ya 50 AD.

Idadi ya wakristo nchini Misri ni asilimia 10 ikiwa waumini milioni 80, na wamekuwa wakiishi kwa amani na waisilamu wa kisunni kwa miaka mingi.

Hata hivyo, kuondolewa mamlakani kwa Morsi kijeshi, kumefuatiwa na mashambulizi mabaya dhidi ya makanisa na rasilimali za waumini hao kwa miaka mingi.

Wakati mkuu wa majeshi Generali, Abdul Fattah al-Sisi, alitangaza kwenye televisheni kuwa rais Morsi aliondolewa mamlakani baada ya maandamano makubwa yakimtaka ajiuzulu aliandamana na papa Tewadros.

Tewadros alisema kuwa mkakati uliofikiwa na Al-asisi ulitokana na mawazo ya viongozi waheshimiwa ingawa hakuwataja.

WANAJESHI WA KENYA WALIENDA KUPORA AU KUOKOA WESTGATE?

Picha za wanajeshi wa Kenya waliokwenda katika jumba la Westgate katika juhudi za uokozi na kisha baadaye kuonekena kwenye kamera za CCTV wakiondoka na mifuko ya plasitiki yenye bidhaa za madukani, bila shaka zimewashangaza wengi.

Picha hizo mwanzo zimeonyesha wanajeshi wakiingia ndani ya jengo hilo wakiwa wamebeba silaha kukabiliana na wanamgambo walioshambulia jengo hilo wiki nne zilizopita na baadaye wakitoka wakiwa wamebeba mifuko hiyo wakiwa na silaha zao kwa wakati mmoja.

Hata hivyo haijulikani walichokuwa wamekibeba kwenye mifuko hiyo.

Pamoja na picha za wanajeshi wakiwa wamebeba mifuko, pia kulikuwa na picha zengine zilizoonyesha mashine ya pesa zikiwa zimeporwa ndani ya mikahawa huku picha za alama za risasi kwenye maeneo ya kuhifadhiapesa, pia zikionekana.

Inaarifiwa ilikuwa jaribio ya kufungua hifadhi hizo ambalo halikufanikiwa.

Madai haya ya wanajeshi kufanya uporaji wa maduka katika jingo hilo, yalikanushwa vikali na jeshi la Kenya kiasi cha kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya waliokuwa wanatoa madai hayo, lakini haijulikani jibu lao litakuwa nini hasa kwa picha hizo za CCTV zilizoonyesha wanajeshi hao wakifanya uporaji.

Wamiliki wa maduka waliorejea kwenye maduka yao baada ya shambulizi , walidai kuwa maduka yao yaliporwa ingawa jeshi lilikanusha madai hayo baadhi ya taarifa zikisema kuwa ilikuwa njamaya wafanyabiashara kudai fidia kwa mali zao zilizoharibika.

Sio wanajeshi pekee waliotuhumiwakwa uporaji, kwani polisi mmoja naye alifikishwa mahakamani kwa kosa la uporaji baada ya kupatikana na pochi la mtu liliokuwa na damu.

Wangambao wa Al Shabaab walitekanyara jengo la Westgate kwa siku nne na kusababisha vifo vya watu 60 pamoja na kuwajeruhi zaidi ya watu miamoja.

WAKAMATWA NA SHEHENA YA BUNDUKI NA NYARA ZA SERIKALI

WAKAZI tisa Wilaya ya Handeni na Kilindi mkoani Tanga wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka kwa kosa la kukutwa na bunduki zaidi ya 25 na nyara nyingine za Serikali kinyume cha sheria.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa Jeshi la Polisi, Nzagalila Kikwelele mbele yaHakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Handeni, Patrick Maligana kuwa, Oktoba 11, mwaka huu katika nyakati tofauti wilayani Handeni na Kilindi, Jeshi la Polisi, maofisa wanyamapori na misitu walifanya msako wa kutafuta wawindaji haramu katika maeneo hayo na kufanikiwa kuwakama watu hao.

Alidai kuwa, katika msako huo watu tisa walikamatwa wakiwa na nyara mbalimbali za Serikali ikiwemo ngozi za pongo, tandala na nyati, pembe za nyati, meno matano ya ngiri na vifaa vya kutengenezea magobore, pia walikamata magobore zaidi ya 25 yakiwa katika makazi yao.

Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa, hadi sasa upelelezi kuhusu watu hao umekamilika na kwamba, mahakama inaweza kuendelea na mchakato wa usikilizaji wa shtaka hilo.

Akitoa hukumu kwa mtuhumiwa wa kwanza, Iddi Abdalah (51), Hakimu wa mahakama hiyo, Patrick Maligana alidai kuwa, anamtia hatiani kwa kosa la kukutwa na ngozi tatu za tandala zenye thamaniya zaidi sh. milioni 25 na bunduki aina ya gobore ambazo ni nyara za Serikali.

Alipotakiwa kujitetea kabla ya kupewa hukumu, mtuhumiwa alidaikuwa, anaomba kupunguziwa adhabu kwani ana watoto watano wadogo na kwamba, hawana mlezi.

Baada ya utetezi huo, hakimu alisema anamhukumu kwenda jela miaka 20 ama alipe faini ya zaidi ya sh. milioni 125, ambapo mtuhumiwa alisema hana fedha hizo. Wengine waliohukumiwa ni Muya Kidundo (63), ambaye amehukumiwa miaka mitano jela kwa kosa la kukutwa na meno matano ya ngiri na ngozi ya swala.

Mwingine ni mkazi wa Negero, Bakari Mwikalo (50), ambaye alihukumiwa miaka saba jela kwa kosa la kukutwa na silaha bila kuwa na kibali. Pia, alimhukumu Selemani Mzimba (45), kwenda jela miaka sita kwa kosa la kukutwa na silaha kinyume cha sheria.


HakimuMaligana alimuachia Hamza Msami (70), kutokana mazingira ya kosa lake kuwa dogo na umri wake mkubwa, kwani hakuisumbua mahakama katika kujua ukweli wa kesi yake na kwamba, watuhumiwa wengine wapo nje dhamana.

Watu hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika operesheni okoa maliasili inayoendeshwa nchini koteambapo katika Wilaya ya Handeni na Kilindi, watu tisa walikamatwa.


Chanzo:Jambo leo

P-NESTA KUKIMBIZA SAN NSIRO

Yule star wa Jini kisirani na raha mustarehe kutoka Mpanda Katavi na kundi zima la Katavi for Real anakumua show yake siku ya jumapili tarehe 20 Oktoba kuanzia saa saba mchana, kiingilio ni bure.

Njoo utoe support yako kwa P-Nesta wakati akishambulia jukwaa, Na timu nzima ya Clouds fm katika shindano la Fiesta Super Nyota ni pale pale San Nsiro Sinza Jijini Dar es salaam.

Wote mnakaribishwa, Utamcheki akikamua Jini kisirani aliyoshirikiana na Sabria kutoka Mjomba Band, Raha Mustarehe aliyopiga na marehemu Ngwair na Nyingine kibao, atasindikizwa na wasanii kadhaa ya ndani ya Dar

KATI YA VIJANA 10, 6 WANAPIGA PICHA AU VIDEO YA NGONO NA KUISAMBAZA

Sita kati ya vijana 10 wanasema kuwa wameombwa picha au video za kingono. Hii ni kwa mujibu wa utafiti a kitengo kuhusu maslahi ya watoto Uingereza ambao BBC iliweza kuuona

Kati ya waliohojiwa , asilimia arobaini walisema kuwa walijipiga picha au kunasa video wakiwa katika vitendo vya ngono na karibu robo yao walimtumia mtu picha hizo kwanjia ya SMS au ujumbe mfupi.

Mkuu wa kitengo hicho, Peter Wanless, alisema kuwa "sexting" au jambo la vijana kutuma ujumbe wenye mada ya ngono limekuwa la kawaida miongoni mwa vijana Uingereza.

Matokoe haya yanaonyesha kuwa tabia hii inafanyika sana miongoni mwa vijana na ni moja ya mambo ambayo vijana hufanya katika mahusiano yao.

Katika utafiti huu vijana 450 walihojiwa kuhusu tabia hiyo kote nchini.

Miongoni mwa wale waliohojiwa kuhusu kutuma picha zao za ngono au video kwa njia ya simu asilimia hamsini walisema kuwa waliituma picha hiyo kwa wapenzi wao wanaume au marafiki zao wa kike, lakini thuluthi moja wakasema kuwa walimtumia mtu wasiyemjua kwenye mtandao wa internet.

Lakini wataalamu wanasema kuwa watu wanawadhalilisha vijana kwa kuwataka wawatumie picha zao kwa kutumia vitisho.

Miongoni mwa wale waliosema kuwa walimtumia mtu picha yao, , asilimia 20 walisema kuwa waligundua watu walichangia picha zao wakati wengine wakisema hawajui zilikokwenda picha zao.

Kulingana na sheria za Uingereza ni halali kujihusisha na ngono ukiwa na umri wa miaka 16 lakini ni kinyume na sheria kupiga picha za ngono au kuchangia picha za ngono za kijana walio chini ya umri wa miaka 18.

Hata hivyo, ilisemekana kuwa vijana hawawezi kuchukuliwa hatua kwa kutuma picha zenye mada ya ngono miongoni mwao.

MAMA YAKE UFOO SARO ALIPIGWA RISASI TANO

TAARIFA zaidi za kusikitisha kuhusumauaji ya kinyama, yaliyofanyika katika familia ya Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, UfooSaro zimeendelea kutolewa, ambapo imebainika mama mzazi wa mtangazaji huyo, Anastazia Saro(58), aliuawa kwa kupigwa risasi tano.

Msemaji wa familia hiyo, Idd Lemaalisema hayo jana wakati wa ibada ya kumuaga Anastazia, iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibwegere, Dar es Salaam.

Awali, taarifa zilizokuwepo, zilidai Anastazia alipigwa risasi mbili kifuani, lakini Lema alisema baada ya uchunguzi wa mwili huo uliofanywa na Polisi, ilibainika kuwa alipigwa risasi tano na si mbili.

Akizungumza wakati wa ibada ya kumuaga Anastazia, ambayo mwanawe wa pekee Ufoo hakuweza kuhudhuria, Mwinjilisti wa Kanisa hilo, Margaret Shekoloa alisema Anastazia atakumbukwa kwa mambo mengi, aliyoyafanya katika Kanisa hilo katika nafasi mbalimbali alizokuwa nazo ukiachaya muumini.

Alisema siku moja kabla ya kifo chake, Anastazia alikwenda kanisani na kupanda maua katika bustani ya kanisa na kupamba madhabahu.

"Alipomaliza kupamba madhabau pamoja na kupanda maua katika bustani, aliniaga na kuniambia mchungaji tutaonana katika ibada ya kesho bila kujua kuwa siku hiyo hataiona," alisema Mwinjilisti Shekoloa.

Alisema matukio ya ukatili, kwa sasa yamezidi kuongezeka nchini na chanzo chake ni watu kutokuwa karibu na Mungu wao. Alisema matukio hayo, yanayowagusa watu wengi wasio na hatia, pia yamekuwa yakichangia uvunjifu waamani.

"Anastazia alikuwa na malengo makubwa na Kanisa hili, aliwaunganisha wanawake wote kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali," alisema Shekoloa.

Alisema hata pale alipohitajika na kanisa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana, aliitikia mwito bila tatizo lolote.

Ibada ya kuaga mwili huo ilimalizika saa 11.30 jioni na mwili huo kusafirishwa kwenda kijiji cha Shali, Machame mkoani Kilimanjaro.

WARUHUSIWA KULA PAKA NA MBWA

Wengi wamenaswa katika vitongoji vinavyokumbwa na vita na kukosa chakula kwa muda mrefuKikundi cha viongozi wa dini nchini Syria kimetoa Fatwa inayowaruhusuwatu wanaoishi katika vitongoji vya mji mkuu Damscus vinavyokumbwana vita kula nyama ambayo kwa kawaida huwa imeharamishwaKwenye kanda ya video, viongozi hao walisema kuwa watu wanaokumbwa na njaa wanaweza kula nyama ya Paka,Mbwa na Punda.

Fatwa hiyo imetolewa huku kukiwa na ripoti za watu kukumbwa na njaa katika kitongoji cha Muadhamiya mjini Damsacus moja ya vitongoji vilivyotekwa na waasi Mashirika ya misaada yameitaka serikali kuruhusu misaada ya kibinadamu kupelekwa katika eneo hilo , ambako wenyeji wamekwama.

Mamia ya raia , hata hivyo walifanikiwa kutoroka maeneo hayomwishoni mwa wiki baada ya vita kusitishwa kwa muda.

Katika ujumbe wao wakati wa sherehe za Eid al-Adha viongozi wa kidini waliwashauri wenyeji wa eneo la Ghouta kula nyama ambazokwa kaiwada huwa haziliwi katika dini ya kiisilamu.

Viongozi hao walisema huu ni wito kwa dunia nzima na kuongeza kuwa ikiwa hali itaendelea ilivyo, watu wanalio hai watalazimika kula wafu.Sio mara ya kwa fatwa kama hii kutolewa kwenye mzozo wa Syria.

Fatwa sawa na hii iliwahi kutolewa mjini Homs na Aleppo wakati mapigano yalikuwa mabaya zaidi katika miji hiyo.Mashirika ya misaada ambayo yamekuwa yakitoa msaada wa chakula katika maeneo ya vita yamesema kuwa lazima jambo hilo liwe muhimu kama ilivyo kuharibu silaha za kemikali za Syria.

WIZARA YA AFYA YATANGAZA UWEPO WA HOMA YA UTI WA MGONGO MKOANI RUKWA

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma juu ya kuwepo kwa Ugonjwa wa Homa ya Uti wa Mgongo mkoani Rukwa. Ugonjwa umedhibitika kuwepo baada ya Vipimo vya Maabara kuonyesha uwepo wa vijidudu vya homa ya uti wa mgongo kwenye sampuli za wagonjwa waliolazwa kwenye Hospitali ya Mkoa Sumbawanga. Hadi kufikia tarehe 08/10/2013 jumla ya wagonjwa 21 wameripotiwa katika hospitali ya Mkoa na kati yao wanne (4) wamefariki dunia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi wote, katika mikoa yote yaTanzania hususani mikoa iliyo mpakani na mkoa wa Rukwa na vilevile wasafiri wanaotarajiwa kwendamkoani Rukwa.

Homa ya Uti wa Mgongo

Homa ya Uti wa Mgongo inasababishwa na bakteria aitwaye Neisseria meningitidis. Bakteria huyu ndiye anayeleta milipuko mikubwa ya Homa ya Uti wa mgongo.

Ugonjwa huu hatari unaathiri zaidi meninji na husababisha athari kubwa kwa ubongo. Ugonjwa huu unapatikana kwa binadamu tu. Asilimia 50 za wagonjwa hupoteza maisha iwapo matibabu hayataanzishwa mapema.

Dalili kuu ni Kukakamaa kwa shingo, Homa kali, Kutokupenda mwanga mkali, Kuchanganyikiwa, Kichwa kuuma pamoja na Kutapika.

Ugonjwa huu unaweza kuathiri ubongo na kupelekea kupoteza uwezo wa kusikia au kupoteza kabisa uwezo wa kuelewa na kunyambulisha vitu mbalimbali. Iwapo ugonjwa huu utaathiri ubongo na meninje kwa kiasi kikubwa, umauti hutokea.

Dalili za ugonjwa ni kati ya siku 2 hadi 10 baada ya kupata maambukizi.

Ugonjwa huu unaenezwa kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu kwa njia ya hewa au kwakugusa majimaji/mate kutoka kwa mtu ambaye tayari ni mgonjwa. Ugonjwa huu unaenea kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine kwa urahisi na kwa kasi sana iwapo mtuatakuwa karibu na mgonjwa mwenye maambukizi kwa muda mrefu. Uambukizo unaweza kutokana iwapo mgonjwa atapiga chafya au mate ya mgonjwa huyu kuguswa. Aidha kasi ya maambukizi pia inatokea iwapo mtu ataishi kwa karibu ndani ya nyumba moja na mgonjwa na kushirikiana naye kwa kula chakula kwenye chombo kimoja.

Ugonjwa huu unatibika iwapo mgonjwa atawahi hospitalini na kupewa dawa.

Hatua zinazochukuliwana WizaraKutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania Bara hususan mikoa inayopakana na Rukwa.

Aidha taarifa hii pia imewakumbusha waganga wakuu warejee miongozo yao ya kudhibiti Ugonjwa wa Homaya Uti wa Mgongo yaani namna ya utambuzi wa mgongwa na, uchukuaji wa sampuliKuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na maeneo ya mipakani.

Kutuma Timu ya Taifa ya Maafa ambayo imeenda kuungana na timu za Mkoa na Wilaya za Rukwa katika kukabilana na ugonjwa huu.

Aidha timu hiyo imeondoka tarehe 10.10.2013.

Kutuma chanjo pamoja na dawa na vifaa Kinga kwa mkoa wa Rukwa ili kuweza kukabilana na ugonjwa huu Elimu ya Afya inaendelea kutolewa katika maeneo ambayo yamekumbwa na mlipuko na pia mashuleni, vyuoni, magerezani, nakwenye mikusanyiko na msongamano wa watu.

Aidha wananchi wanashauriwa kujenga nyumba bora zenye madirisha yanayoingiza hewa na mwanga wa kutosha.

Kufungua kambi maalamu mkoani Rukwa kwa ajili ya wagonjwa wa Homa ya Uti wa Mgongo.

Wananchi wanashauriwa kutoa taarifa pindi kutoa taarifa kwenye kituo cha huduma za afya kilicho karibu mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huu.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Wadau wengine wanaendelea na mikakati ya kuhakikisha ugonjwa huu unathibiwa mkoani Rukwa na kwa mikoa mengine.

KESI YA BABU SEYA NA MWANAE KUSIKILIZWA OKTOBA HII

MAHAKAMA ya Rufaa Oktoba 30 mwaka huu inatarajiwa kufanya kusikiliza marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viki maarufu kama Babu seya na wanawe. Baada ya hukumu hiyo, Babu Seya na mwanawe pamoja na wakili wao Mabere Marando waliomba marejeo ya hukumu hiyo.

Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati. Katika hukumu hiyo iliyotolewa Februari 2010, mahakama hiyo iliridhia hukumu ya kifungo cha maishakwa Babu Seya na mwanawe, Papii Nguza huku ikimuwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu, na Francis Nguza.

Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, iliwatia hatiani Babu Seya na wanawe Papii Nguza 'Papii Kocha', Nguza Mbangu na Francis Nguza kwa kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti.

Januari 27 mwaka 2005, Jaji waMahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa nayo Juni 25 mwaka 2004.

Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam.


Chanzo: Mpekuzi

TUNAENDELEA KUMKUMBUKA MWALIMU NYERERE KWA MENGI ALIYOYAFANYA

WAKATI taifa linaadhimisha miaka 14 ya kifo cha mwasisi wa taifa, na rais wa kwanza wa Tanzania, kizazi kinahitaji kujua Nyerere alikuwa mtu gani na alianzia wapi.

Nia yetu ni kutaka kumuezi na kujikumbusha.

Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 , katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara. Alikuwa mmoja kati ya watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabilala Wazanaki.

Alipokuwa mtoto, Nyerere alichunga mifugo ya babake. Katika umri wa miaka 12, aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi katika shule ya msingi ya Mwisenge, iliyoko Musoma Mjini.

Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki iliyoko Tabora. Katika umri wa miaka 20, Nyerere alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.

Kutokana na ujasiri na nia ya kuwa mwelewa wa kila kitu, mapadre wa Kanisa katoliki waliona akili yake na nia yake nzuri ya kutaka kujifunza , wakamsaidia kusoma kozi ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.

Akiwa katika Chuo cha Makerere, Nyerere alianzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia aliamua kujihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).

Baada ya kumaliza masomo yaualimu, Nyerere alirudi Tabora nakuanza kufundisha shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria (St.Mary´s). Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti / Uingereza , akasoma Shahada ya Uzamili ya historia na uchumi... Kwa hatua hiyo Mwalimu alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania.

Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam, (siku hizi Pugu Sekondari).

Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika huo kikuu cha Makerere.

Mwaka 1954, alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA.

Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinacho ongoza Tanganyika.

Uwezo wa mwalimu uliwashitua viongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.

Aliamua kujiuzulu ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru.

Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Mkutano wa Baraza la udhamini (Trusteeship council) ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.

Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuumwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na Desemba 9,1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuuwa Tanganyika huru na mwakammoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa jamhuri ya Tanganyika.

Nyerere alikuwa kiungo muhimu sana katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964, yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.

Hayati Mwalimu Nyerere mnamo Februari 5, 1977, aliongoza chama cha TANU katika tendo la kuungana na chama tawala cha Zanzibar ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake.

Nyerere aliendelea kuongoza Taifa hadi 1985 alipong'atuka na kumwachia nafasi rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi.

Aliendelea kuongoza Chama cha CCM hadi 1990 na kuwa makini na mfuatiliaji huku akionya katika mambo kadhaa katika siasa za Tanzania hadi kifo chake.

Baada ya kustaafu kazi ya ukuu wanchi, Nyerere alikaa muda mwingi kijijini kwake alikozaliwa Butiama akilima shamba lake la mahindi.

Pamoja na hayo, Nyerere alianzisha taasisi yenye jina lake inayojulikana kama "Mwalimu Nyerere Foundation", mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.

Mwishoni mwa maisha yake Mwalimu aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama Mwalimu alianza kujisikia vibaya mwezi Augost mwaka 1999, akaanza kupata matibabu ya kila mara, baadae alihamishiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas huko Uingereza. Oktoba 14, 1999 aliaga dunia katika hospitali hiyo ambapo madaktari walisema kuwa alikuwa akisumbuliwa na kansa ya damu (leukemia).


Mafanikio na kasoro

Kitendo kikubwa ambacho Mwalimu alikifanya na dunia inakumbuka ni kuchanganya ardhi ya Zanzibar na Tanganyika ambapo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulizaliwa rasmi na hadi leo upo.

Mengine ni Kujenga umoja wa kitaifa na utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vitadhidi Nduli Idi Amin Dadaa wa Uganda.

Watu walimuita mwalimu kuwani mwanamapinduzi wa afrika, kiongoizi wa bara nzima kutokana na nia yake ya kutaka kila Mwafrika kuwa huru na kuwa na amani.


Mwalimu pia alifanikiwa kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za kusini ya Afrika kama; Zimbabwe {ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo) Kutofanikiwa kwake Kitu ambacho kilimuumiza mwalimu na kumfanya akose raha mara nyingi ni juu ya kutofanikiwa kwa nia yake ya kuanzisha siasa za Kijamaa.
Siasa zake za ujamaa zilishindwa baada ya mwaka 1976.

Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa za kijamaa na kutoweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa ambazo yeye hakuwa muumini, Nyerere kwa maamuzi yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais baada ya uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani rais Mwinyi aliyetawala kwa siasa za uchumi wa soko huria.

Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere alitamka katika tafrija ya kumuaga juu ya siasa yake kiuchumi :
"Nimefeli. Tukubali hivyo."


Alikosolewa pia

Kutokana na hali hiyo na kufikia yeye kukubali kushindwa , Mwalimu Nyerere analaumiwa kwa siasa zake za kiujamaa kuwa zilichelewesha maendeleo ya uchumi wa Tanzania, pamoja na kwamba hata leo kuna makundi ya watanzania kwa mtazamo waoyanazitamani siasa hizo.

Mbali na hayo, kuna makundi ya waislamu wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa siri vita dhidi ya uislamu na upendeleo wa elimu na madaraka kwa wakristo. Kutangazwa mwenye HeriKwa taratibu za Kanisa Katoliki,mchakato wa kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu ulianza mwaka 2005,na tayari kanisa hilo kwa kibali rasmi kutoka Roma makao ya Baba Mtakatifu, limeshamtangaza kuwa mwenyeheri.

Kuwa mwenyeheri ni hatua ya kwanza ya kuingia utakatifu. Wakristo wakatoliki wameanzisha sala maalumu na kufanya maombi kwa nia yamaombezi yake ili aweze kutangazwa kuwa mtakatifu. Ibada ya kwanza ilifanyika katika kanisa kuu la Jimbo la Musoma, na kuongozwa na aliyekuwa askofu wa Jimbo hilomarehemu askofu Justine Samba.

Alikuwa mwana michezo Licha ya Kuwa mwalimu na mwanasiasa hususani kiongozi mkuu wanchi, pia Nyerere alikuwa mwanamichezo.

Alianzisha mchezo wa Bao, akiwa Butiama alicheza bao nyumbani kwake na majirani zake, wakati mwingine alipotembelewa na wafuasi wake wa kisiasa alikuwa akishiriki nao kucheza bao.

Kutokana na maisha yake aliyoishi ambayo yalijaa uvumilivu, unyenyekevu na uadilifu bado anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake zakujali utu na ubinadamu.

Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.

Taifa linamkumbuka kwa hayo na mengine mengi ambayo aliyafanya, ameacha machapisho mengi ambayo pia yamekuwa hazina ya maarifa kwa watanzania.

ODINGA AELEZEA JINSI MWALIMU NYERERE ALIVYOMSAIDIA KUSOMA

Waziri Mkuu wa zamani waKenya, Raila Odinga ameeleza kuwabila ya Pasipoti ya Tanzania aliyopewa kwa msaada na MwalimuJulius Nyerere asingeweza kwenda Ujerumani kusoma baada ya Idara ya Uhamiaji ya Kenya kumnyima hati hiyo ya kusafiria.

Odinga ambaye hivi sasa ni kiongozi mkuu wa Muungano wa Cord ameeleza hayo katika kitabu chake kiitwacho The Flame of Freedom, ambamo ameelezea historia yake na familia yake katika mambo mbalimbali.

Idara ya Uhamiaji ya Kenya ilimnyima Odinga hati hiyo kutokana na Serikali ya kikoloni kuzuia hati ya baba yake, mzee Jaramogi Odinga kwa sababu alitembelea nchi za Urusi na China zilizokuwa maasimu wakubwa wa nchi za Magharibi.Hata hivyo, Mzee Jaramongi aliamua kusafiria hati ya kimataifa alizopewa na Kwame Nkurumah waGhana, pamoja na Gamel Abdel Nasser wa Misri.

Odinga alihitaji hati hiyo kwa kuwa baba yake alitaka amalizie masomoyake nchini Ujerumani baada ya kukatishwa masomo akiwa kidato cha pili mwaka 1962 katika Shule ya Maranda.

Katika kitabu hicho, Odinga alisemahakushangaa kunyimwa hati hiyo.Katibu wa baba yake aitwaye Olwande K'Oduol alimpeleka kwa Ofisa Afya wa Halmashauri ya Jiji la Nairobi, Rading Omolo ambapo alipigwa chanjo ya homa ya manjano.

"Nilipopata cheti cha chanjo hiyo tulirudi nyumbani kwa K'Oduol ambapo nilikuta vijana wengine wawili Mirulo na Oudia ambao nao walikuwa wakisafiri nje kusoma, hivyo tukaungana katika safari moja," alisema Odinga katika kitabuhicho.Alisema siku iliyofuatia waliamka mapema ili wawahi basi la kwenda Dar es Salaam ambapo walifika kituoni saa 12 asubuhi na waliondoka Nairobi saa 1:30 asubuhi kwa kutumia basi la kampuni ya Overseas Transport Company (OTC).

Wakati huo, barabara ya lami ya Nairobi ilikuwa inaishia njiapanda ya Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta na kuanzia hapo hadi Namanga barabara ilikuwa ni mbaya, anaeeleza Odinga.

"Utaratibu wa kuvuka mpaka ulikuwa rahisi, tulipata kifungua kinywa katika eneo hilo na kuondoka baada ya muda ambapo kituo kingine kilikuwa ni Arusha. Basi hilo lilipakia abiria wengine kabla ya kufika Moshi na kupata chakula cha mchana," anasema Odinga na kuongeza; "Tulipitia Korogwe, Handeni hadi Morogoro ambapo barabara ya lami ilianza kuonekana tena na tulifika Dar es Salaam saa 1:30 asubuhi baada ya safari ya saa 24 na tulipokelewa na Dola Osman ambaye alikuwa ni Katibu wa KatibuMkuu wa TANU, Oscar Kambona.

"Odinga anaeleza katika kitabu hichokuwa Osman aliwapeleka hotelini na kuwaacha kwa kuwa walikuwa wachafu na wenye njaa kutokana nasafari ndefu. Walioga na kubadilisha nguo kisha kupata kifungua kinywa, ndipo Osman aliporudi na kuchukua picha tatu ndogo kwa kila mmoja ambazo walitakiwa kuwa nazo. "Haikuchukua muda mrefu kwani kabla hata hatujamaliza chakula chamchana, Osman alirudi na hati zetuza kusafiria akitueleza kuwa kila kitu kimeshakamilika;

"Siku moja kabla ya kuondoka kwetu, Osman alituchukua saa 3 asubuhi na kutupeleka ofisini kwa Waziri Mkuu, Mwalimu Julius Nyerere ambapo Mwalimu alifurahi sana kutuona na kunielezakuwa Jaramongi ni rafiki yake wa karibu, pia alitueleza kuhusu safari yake ya Kisumu mwaka uliopita alipohudhuria mkutano wa Pan African," anasema.

Baada ya hayo waliingia kwenye gari la Nyerere hadi nyumbani kwake ambapo walipata chakula chamchana, kisha Mwalimu aliwatakia safari njema na masomo mema.

KATAVI KUNUFAIKA NA NYUMBA ZA NHC

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), limeingiza sokoni nyumba 406 katiya 2,000 zilizopo kwenye awamu ya kwanza ya nyumba za gharama nafuu huku likihadharisha umma kuhusu uwepo wa matapeli wanaotumia jina lao kama madalalikuwarubuni watu wawape fedha ili wawapatie nyumba kwa urahisi.

NHC imesema hakuna dalali katika uuzaji wa nyumba hizo zinazoanza kuuzwa leo katika mikoa 10 kati ya 11 inayohusika na awamu hii kupitia kampeni iitwayo "Nyumba Yangu-Maisha Yangu".

Meneja wa Biashara na Maendeleowa NHC, David Shambwe aliyasema hayo na kutoa hadhari hiyo jana, Dar es Salaam alipozindua uuzaji wa nyumba hizo 406 za awali ambazo gharama ya chini ya nyumba ni Sh milioni 33 hadi Sh milioni 49 bila Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Akifafanua, alisema katika mradi wa uuzaji nyumba Kibada Kigamboni shirika hilo lilitangaza kuzuia wananchi wasitumie madalali.

Alisema mhitaji afike ofisi za NHC matawi yote nchini ama kutumia mtandao wao au simu namba 0754444333 kwa maelezo zaidi.

Alisema ili kuondoa watu kujimilikisha, NHC itauza nyumba moja kwa mtu mmoja katika mkoa wowote husika na ikiwa watu wa familia moja wana uwezo wa kununua nyumba zaidi ya moja kwa kila mtu, hawazuiwi.

Alitaja maeneo zilipo nyumba hizo na mikoa kwenye mabano ni Bombambili (Geita), Ilembo na Mlele (Katavi), Kongwa (Dodoma) na Mkinga (Tanga).

Mengine ni Mkozo mkoani Ruvuma, Mlole (Kigoma), Mrara (Manyara), Mtanda (Lindi), Mvomero (Morogoro) na Unyankumi(Singida).

Kwa mujibu wa Shambwe kila Mtanzania anaruhusiwa kununua nyumba moja kati ya hizo kwa kulipia asilimia 10 ya gharama kupitia akaunti namba 01500250887500 iliyopo benki ya CRDB Kariakoo na kutakiwa kukamilisha malipo ya nyumba husika ndani ya siku 90 kupitia mkopo wa benki zinazoshirikiana na NHC au fedha binafsi.

ZITTO ATAJA MSHAHARA WA RAIS

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analipwa sh milioni 384kwa mwaka, sawa na sh milioni 32 kwa mwezi pasipo kukatwa kodi. Hii ni mara ya pili kwa Zitto kutangaza hadharani mishahara ya viongozi wakuu wa serikali, akiwa ameanza na ule wa Waziri Mkuu, aliyesema analipwa takribani sh milioni 26 kwa mwezi.

Akiwahutubia wananchi mjini Igunga jana, ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama Kanda ya Magharibi, Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema kuwa sababu ya kutaka mishahara ya viongozi wakuu wa nchi ijulikane, ni kuzuia mianya ya watu wachache kuiibia nchi kutokana na usiri wa jambo hilo.

Zitto alisema hoja ya msingi si kiasi wanacholipwa viongozi hao walioajiriwa na wananchi, bali ni usiri unaofanywa juu ya kiwango hicho jambo alilosema kuwa linaweza kutumiwa na wajanja kuendelea kuinyonya nchi.

Alisema ni jambo la kusikitisha kuona mwalimu anayelipwa mshahara wa sh 220,000 kwa mwezi akikatwa kodi, huku viongoziwa kuchaguliwa wakiwa wanapokea mishahara mikubwa pasipo kukatwakodi licha ya kuhudumiwa kila kitu na serikali.

Aliongeza kuwa katiba ya sasa Ibara ya 43(1), inaeleza kuwa rais atalipwa mshahara pamoja na malipo mengine, huku ibara hiyo hiyo kifungu cha pili ikizuia mshahara na marupurupu kupunguzwa, hali aliyoelezea kuwa ni muhimu katiba mpya ikabadilisha sheria hizo kwa manufaa ya nchi. "Kwa hiyo hata kesho kama Dk. Willibrod Slaa akiwa rais na akataka kupunguza mshahara wake, kwa katiba hii hawezi na hili jambo si sahihi kwani viongozi wa ngazi hizi wanapata kila kitu bure kutoka serikalini," alisema Zitto.

Akiwa katika Kata ya Choma, Zitto alikagua kilichokuwa kiwanda cha kuchambulia pamba cha Giner ambacho kimeacha kufanya kazi tangu mwaka 1998.

Alisema kufa kwa viwanda vingi vya uzalishaji nchini kumechangiwa kwakiasi kikubwa na Serikali ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akidai kuwa alishindwa kutofautisha suala la uwekezaji na biashara huru.


"Ni serikali ya Mkapa ndiyo ilitufikisha hapa katika kupotea kwa viwanda nchini, wao walidhani biashara huru ni kuwapa wawekezaji viwanda vyetu na serikali kujiweka pembeni, sasa nchi imebaki kutegemea uchumi wauchuuzi badala ya uzalishaji," alisema.

Alisema sera ya uwekezaji katika Serikali ya CCM ilichukuliwa kama fursa ya viongozi wa chama hicho kujinufaisha na mali za serikali pasipo kujua wataendeleza vipi.

Zitto alisisitiza kuwa kila mara CHADEMA imekuwa ikisisitiza bungeni juu ya kupiga marufuku usafirishaji wa pamba kwenda nje kama malighafi, na badala yake wakitaka viwanda vifufuliwe kwa ajili ya kutoa ajira kwa Watanzania.

Alirejea kusisitiza sera ya hifadhi yajamii kwa wakulima akisema imefikia wakati serikali kupitia SSRA ione umuhimu na ulazima wa kuhakikisha wanaongeza Watanzaniawenye hifadhi ya jamii kwa kuanza mfumo maalumu wa hifadhi ya jamii kwa wakulima (Supplementary scheme for social security to small holder farmers).

"Ninapendekeza serikali ichangie nusu kwa nusu na mkulima ili kuvutia uwekaji akiba katika nchi nakuwa na sera ya uwekezaji katika maeneo yatakayomwinua mkulima kama miundombinu ya umwagiliaji, mikopo nafuu kwa wakulima kwenye pembejeo na nyumba na bima ya afya.

"Nimezungumzia umuhimu wa uwazi katika matumizi ya fedha za umma ikiwemo malipo ya watumishi na viongozi wa umma. Nimewaeleza wananchi wa Nzega kuwa siku ya Jumanne kamati yanguya Hesebu za Serikali (PAC) itaanza kukagua mahesabu ya vyama vya siasa nchini," alisema.

Zitto alisema vyama vya siasa vinatumia fedha za umma takribanish bilioni 20 kila mwaka kama ruzuku, kwamba ni haki ya wananchi kujua fedha zinatumika namna gani.

Alisema kuwa wananchi wa Nzega wana changamoto nyingi sana.

Kwamba wakulima wa pamba walipewa madawa feki ya kuua wadudu, michango ya hovyo hovyo ni mingi mno na unyanyasi wa wana-CHADEMA ni mkubwa vijijini.


Chanzo: Tanzania Daima

SHERIA YA NDOA KUFUMULIWA NA KUANGALIWA UPYA

SERIKALI imesema inaangalia uwezekano wa kubadili sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ambayo inaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 15 badala yake iruhusu umri wa kuolewa uanzie miaka 18.Aidha imeeleza kuwa ndoa za utotoni kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikirudisha nyuma maendeleo ya watoto wa kike, kutokana na wengi wao kuachishwashule na kuozeshwa.

Hayo yameelezwa jana jijini Dar esSalaam na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe wakati akizungumza katika majadiliano ya ngazi ya juu kuhusiana na ndoa za utotoni, ambapo jana ilikuwa ni Siku ya Mtoto wa Kike Duniani.

Waziri Chikawe alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya sasa mtoto wamiaka 15 anaruhusiwa kuolewa kwa idhini ya wazazi wake, jambo ambalo amewataka wadau wote kushirikiana kuhakikisha sheria itambue umri wa ndoa uwe ni miaka 18 na si vinginevyo. Hata hivyo, Waziri Chikawe alisema suala la kubadili sheria hiyo linatarajiwa kuchukua zaidi ya miaka mitatu, ili kukomesha kabisandoa za utotoni.

"Serikali inatambua uwepo wa ndoa za utotoni na hili ni tatizo kubwa sana, hivyo mbali na kurekebisha sheria lakini pia tunahitaji kuwapa wananchi wetu elimu zaidi kuhusiana na ndoa za utotoni ili hata wao wajue madharayake," alisema Waziri Chikawe.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Valerie Msoka alisema suala la ndoa za utotoni bado ni changamoto kwa nchi zote za Afrika, ambapo Tanzania inaonekana kuwa ni ya 20, jambo ambalo alisema ni lazima serikali iungane na taasisi mbalimbali kulitetea jambo hilo.

"Kikubwa ni elimu iendelee kutolewa kwa wananchi wote, pia tunafarijika kuona kuwa sasa serikali itaenda kubadilisha sheria ya ndoa kutoka miaka 14 kwenda miaka 18, japo napo ni bado ingekuwa hata miaka 21 lakini kwa kuanza si mbaya" alisema Msoka.


Chanzo:Habari leo

WAZIRI MKUU WA LIBYA ATEKWA NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA

Libyan PM Ali Zeidan has been seized by armed men in the capital, Tripoli.

Mr Zeidan was taken from his hotel before dawn "by gunmen to an unknown place for unknown reasons", said a government statement.

A former rebel group loosely allied to the government said it had arrested him following a prosecutor's warrant.

The government has denied this.

The government has been under pressure after US commandos seized senior al-Qaeda suspect Anas al-Liby in Libya.

Mr Liby was snatched on Saturday in Tripoli. He is wanted in the US over the 1998 bombings of US embassies in Kenya and Tanzania. On Monday, Libya demanded an explanation from the US ambassador over the incident.

The government is also struggling to contain rival tribal militias and Islamist militants who control parts of the country, two years after the revolt which overthrew Muammar Gaddafi.

Cabinet summoned

The BBC's Rana Jawad, in Tripoli, says the details of Mr Zeidan's capture remain unclear, but that he was taken by armed men from a hotel he resides in in the early hours of the morning.

The government website said he had been taken "to an unknown place for unknown reasons by a group thought to be from the Tripoli Revolutionaries Control Room and the Committee for Fighting Crime".

The government statement did not name the hotel, but a womanat the Corinthia Hotel - where the prime minister lives - confirmed the incident happenedthere when armed men entered the building.

She said no-one had been killed. Our correspondent says there are a number of militia groups operating in Libya which are nominally attached to government ministries but often act independently.

One of them - the Operations Cell of Revolutionaries - said it was acting on the orders of the prosecutor general in accordancewith Libya's penal code. However, state-run National Libyan TV quoted Justice MinisterSalah al-Marghani as saying that the prosecutor general had issued no such order.

Libya's cabinet has been summoned for an immediate meeting under the leadership of the deputy prime minister.

UK Foreign Secretary, William Hague condemned the capture and called for Mr Zeidan's immediate release.

"It is vital that the process of political transition in Libya is maintained. The government andpeople of Libya have our full support at this concerning time," he said.

'Act of sabotage'

In an interview with the BBC on Monday, Mr Zeidan had said Libya was being used as a base toexport weapons throughout the region, and called on the West tohelp stop militancy in Libya. Last month Mr Zeidan visited theUK and appealed for British help to remove weapons from the country amid fears of increased arms smuggling to Syria.

In April he urged Libyans to back their government in the face of "people who want to destabilise the country".

He also complained at that time of other attacks and "acts of sabotage" carried out by separate groups, against the interior ministry and national TV headquarters.


Chanzo:BBC

WASTAAFU WA SMZ NA JESHI WATAKA UNGUJA, PEMBA WAJITAWALE

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Waziri wa zamani na wafanyakazi wastaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wametoa wito wakitaka visiwa vya Unguja na Pemba vijitawale. Wastaafu hao ni waliokuwa wanajeshi wastaafu, askari wa vikosi vya SMZ, wafanyakazi wa wizara na idara za mbalimbali za umma.

Katika kongamano lililofanyika siku chache zilizopita kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo eneo la Kikwajuni, walisema ipo haja ya kufanyika 'mapinduzi ya heshima na adabu', baada ya yale ya 1964.

Kongamano lilikuwa chini uenyekiti wa Ali Hassan Khamis, ambapo mbali ya wastaafu, pia lilihudhuriwa na wakulima na wafanyakazi wa SMZ.

Miongoni mwa walioshiriki ni aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Awamu ya Pili Zanzibar), Aboud Talib Aboud. Yeye aliondolewa madarakani pamoja na Rais Aboud Jumbe mwaka 1984, baada ya hali ya kisiasa kuchafuka visiwani humo.

Aboud alisema watu kutoka Oman walifika Zanzibar kama walowezi na kuigeuza ardhi mali yao hadi yalipofanyika Mapinduzi yaliyorejesha hadhi, utu na ukombozi wa wananchi wanyonge 1964.

"Jueni kwamba Zanzibar haitatawaliwa tena na wageni. Wanaosema 'Zanzibar kwanza', nawaeleza kuwa ni 'wananchi kwanza' na Mapinduzi ndio yaliyowakomboa Waafrika wanyonge, hatutakubali ng'o kuwa chini ya ukoloni mamboleo," alisema Aboud.

Mbunge wa zamani wa Kikwajuni, Parmuk Hogan Sing, aliiponda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar akidai haikutokana na ridhaa ya Wazanzibari wengi na kudai wameingizwa viongozi wapinga sera za umoja, Mapinduzi na Muungano, hivyo inakosa uzani wa uhalali na kuaminiwa.

Mshiriki wa kongamano hilo, Ali Machano Khamis, alisema matatizo yanayokikumba kisiwa cha Unguja ni kitendo cha kuchaguliwa wagombea urais ambao si chaguo la Wazanzibari.

Alisema wagombea hao wasiofaa ndio chanzo na kiini cha kuanza kulegelega kwa utetezi wa misingi ya Mapinduzi, na kuwataka wazee kuanza kujirekebisha kuhakikisha wanaoteuliwa lazima wawe na uchungu wa nchi, si wasaka maslahi binafsi.

Akizungumzia mchakato wa kuundwa SUK, Suleiman Omar Suleiman, alisema ulifanyika kibabe na kwa hila bila kuwaweka vituoni mawakala wa kusimamaia kura za maoni kujua idadi ya waliosema "hapana" na "ndiyo".

Alisema hakuna kigezo halisi cha kuwapo Muungano wa visiwa vya Unguja na Pemba tangu asili na jadi, na kwamba muda umefika sasa kwa visiwa hivyo kujigawa, kila upande uwe na mamlaka yake kamili.

"Ni vipi Pemba iwe ya Wapemba, Unguja iwe ya wote? Viwanja vya Unguja wamepewa Wapemba wakati Pemba hakuna Muunguja anayeishi na kujenga nyumba. Jamani, Waunguja tumechoka! Tunataka mamlaka yetu haraka," alisema Suleiman.

Kuibuka kwa madai hayo wakati huu huenda kukaiweka Serikali ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein katika taharuki na kuitikisika SUK iliyopatikana baada ya mazungumzo kusaka muafaka, na kubadilishwa kifungu cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, hivyo kufanyika kwa kura za maoni ambapo asilimia 66 ya Wazanzibari waliikubali SUK.

Khamis Mwinyishehe Suleimna alisema Pemba haikushiriki katika harakati za Mapinduzi ya Zanzibar na hata walipotakiwa na Waingereza wakapigane Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1939 hadi 1945), walikataa kwa madai kuwa wao walikuwa chini ya Wareno.

Alisema kati ya waasisi 14 wa Mapinduzi hakuna hata mmoja kutoka Kisiwa cha Pemba, hivyo suala la visiwa hivyo kujitenga halihitaji mapatano wala mazungumzo ya suluhu mezani.

Mzee Younus Haji alisema jambo hatari lililofanyika katika uundwaji wa SUK ni kuingizwa viongozi wenye itikadi za vyama vya zamani vya Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) na Zanzibar Nationalist Party (ZNP), na kwamba sasa ni wakati muafaka wa kufanya tathmini kuhusu Serikali hiyo na kutafuta Katiba mpya ya Zanzibar.

Wastaafu wengi waliozungumza walionekana kusikitishwa na kuvunjwa kwa miiko ya Mapinduzi ya Zanzibar wakisema waliomrithi Rais Abeid Amani Karume, walipuuzia wosia ulioachwa na viongozi wa Afro Shiraz Party (ASP) na waasisi wake.

"Kama watu hawa wangependa umoja na maridhiano tangu awali hata Mapinduzi ya mwaka 1964 yasingetokea, kwani kiongozi wa ZPPP, Mohamed Shamte Hamad, angeunganisha viti vyake vitatu na ASP basi," alisema Mzee Kheir.

Madai yao mengine ni kwamba wazee wa Pemba wamewahi kwenda hadi Ofisi za Umoja wa Mataifa Dar es Salaam mwaka 2000 wakitaka wapewe mamlaka, na kwamba ni heri wakapewa sasa kuepusha shari.

Ahmed Khamis Mcheju alisema kitendo chochote cha kuyapuuza Mapinduzi ya Zanzibar hakivumiliki kwa Waafrika waliobaguliwa na kudharauliwa tangu kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa Kiafrika, Mwinyimkuu, na Waarabu kutoka Oman mwaka 1804.

Madai hayo mazito ni kama ishara ya kutimia kwa utabiri Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyewahi kusema nje ya Muungano kutajitokeza Uzanzibari na Uzanzibara, kisha Uunguja na Upemba na Taifa halitabaki salama.

Chanzo: Jamii Forum

MAREKANI KUPUNGUZA MISAADA YAKE MISRI

Marekani inabana sehemu kubwa ya dola bilioni 1.3 ambazo hutolewa kwa Misri kama msaada wa kijeshi.

Kutolewa kwa zana za kijeshi pamoja na msaada wa kifedha kwa serikali ya Misri itabanwa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya mambo ya nje ya Marekani.

Imesema kuwa hatua lazima zichukuliwe katika kuhakikisha kuna uchaguzi huru na wa haki kama kikwazo cha kupata msaada huo tena.Hataua hii inatokana na Marekani kudurusu hali nchini Misri baada ya maafisa wa utawala kumwondoa mamlakani Morsi na kusababisha idadi kubwa ya vifo miongoni mwa wafuasi wake.

"Tutatendelea kuzuia msaada mkubwa wa kijeshi kwa Misri hadi itakapochukua hatua za kuhakikisha kuna serikali halali mamlakani na ambayo imechaguliwa kihalali na kwa njia ya kidemokrasia,'' alisema msemaji wa idara ya mamambo yandani wa Marekani Jen Psaki.Maafisa walisema kuwa kubanwa kwa msaada huo, kutakosesha Misri kupata mamilioni ya dola pamoja na ndege aina yaApache helikopta, pamoja na makombora ya Harpoon na sehemu za vifaru vya kijeshi.

Serikali pia inapanga kubana dola milioni 260 kwa serikali ya Misri pamoja na mkopowa dola milioni 300.

Hata hivyo wadadisi wanasema kuwa hatuahii sio kali sana kwa Misri na kuwa ilitarajiwa hasa kutoipa Misri zana za kijeshi, na mafunzo ambayo pia hayatatolewa hadi masharti yatimizwe.

Aidha itaendelea kutoa msaada wa kiafya na elimu pamoja na kuakikisha kuwa usalama unadhibitiwa katika rasi ya Sinai.

MSHUKIWA WA UGAIDI ADAKWA LIBYA

Waziri mkuu wa Libya Ali Zeidan amezitaka nchi za Magharibi kuisaidia kukomessha kuenea kwa makundi ya wapiganaji wenye ikitadi kali nchini humo.

Kwenye mahojiano na BBC Bwana Zeidani alisema kuwa Libya inatumika kama sehemu ya kusambazia silaha katika kanda nzima.

"Hizi silaha zinapelekwa kwa wingi katika nchi jirani kwa hivyo lazima pawepo ushirikiano wa kimataifa kukomesha jambo hilo,'' alisema bwana Zeidan.

Mnamo siku ya Jumatatu serikali ya Libya ilimhoji balozi wa Marekani nchini humo kuhusu kukamatwa kwa mshukiwa wa ugaidi na mmoja wa viongozi wa kundi la al-Qaeda mjini Tripoli.

Anas al-Liby, alikuwa anasakwa kwa kuongoza mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 na baada ya zaidi ya miaka kumi aliweza kukamatwa mjini Tripoli na makomando wa Marekani.

Marekani imetetea hatua ya kukamatwa kwa gaidi huyo ikisema kuwa kilikuwa kitendo halali kuambatana na sharia za kimataifa.

Lakini bunge la Libya Jumanne lilitaka al Liby kurejeshwa nchini humo likitaja kukamatwa kwake kama kitendo cha utekaji nyara na kupuuza utawala wa Libya.

Rais Barack Obama aliambia waandishi wa habari Jumanne kuwa Marekani ina ushahidi wa kutosha kuonyesha kua Al Liby alipanga na kusaidia katika kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani na kuwaua watu wengi sana.

Obama aliongeza kuwa Al Liby atafikishwa mbele ya vyombo vya sharia.

11 WADAKWA MSITUNI WAKIJIFUA KIJESHI

SIKU chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka Watanzania kujiandaa na uvamizi wa kigaidi, vijana 11 wenye umri kati ya miaka 18 na 39, wametiwa mbaroni mkoani Mtwara, wakidaiwa kuwa katika mafunzo ya kijeshi msituni, yaliyotajwa kuwa ya kutisha na hatari.

Vijana hao wanadaiwa kukutwa katika mlima wa Makolionga wilayani Nanyumbu, wakiwa katika maficho wakitumia CD zipatazo 25 zenye mafunzo mbali mbali. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen alielezeatukio hilo kuwa si la kawaida na kutaja aina ya CD zilizokuwa zikitumika.

Kwa mujibu wa Zelothe, CD hizo zilihusu Al -Shabaab, mauaji ya Osama bin Laden, Zindukeni Zanzibar, kuandaa majeshi, mauaji ya Idd Amin na Mogadishu sniper.

"Pamoja na CD hizo, watuhumiwa walikuwa na zana nyingine na vyakula," alisema.

Alitaja zana hizo ni DVD player moja, Solar panel moja yenye wati 30, mapanga mawili, visu viwili, tochi moja na betri ya pikipiki namba 12. Pia, wanatuhumiwa walikutwa na simu tano za viganjani, vyombo mbalimbali vya chakula, jiko la mkaa, jiko la mafuta ya taa, taa ya chemli, baiskeli tatu, ndoo nne za maji na vitabu vya dini ya Kiislamu.

Vitu vingine walivyokutwa navyo niunga wa mahindi kilogramu 50, mbaazi kiroba kimoja chenye kilogramu 50, mahindi viroba vitatu sawa na kilogramu 150, virago vya kulalia na mfuko wa kijani, unaosadikiwa ni wa kijeshi wenye nembo ya nanga ya meli yenye mistari kulia na kushoto na nyoka katikati.

Kamanda Zelothe alitaja waliokamatwa kuwa ni Mohamed Matete (39), mkazi wa kijiji cha Sengenye ambaye anadaiwa kuwa kiongozi wa kundi hilo na Hassan Omary, maarufu kama Ajili (39), mkazi wa Nalunyu.

Wengine ambao wote ni wakazi wa Likokona ni Rashidi Ismail (27), Abdallah Hamis (32), Salum Bakari maarufu Wadi (38), Ramadhan Rajabu (26), Fadhil Rajabu (20), Abbas Muhdini (32), Ismaili Chande (18), Said Mawazo (21) na Issa Abed mwenye umri wa miaka 21.

"Watuhumiwa hao wote tayari wamefikishwa mahakamani na wakati huo Polisi mkoani hapa inaendelea na upelelezi wa kina kuhusu tukio hili ambalo si la kawaida.

"Tunasaidiwa na Makao Makuu ya Polisi pamoja na kushirikisha mikoa mingine kuwanasa watu wote ambao wanatajwa kuhusishwana tukio hilo la mafunzo ya kutishana hatari," alisema Zelothe katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Jeshi la Polisi limetoa rai kwa wananchi wote wenye taarifa, inayohusu tukio la aina hiyo, watoetaarifa mapema iwezekanavyo ili watu hao wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.


Chanzo: Habari Leo

MGOGORO NA RWANDA UMEKWISHA

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ametangaza kuwa mgogoro baina yaTanzania na Rwanda sasa umemalizika rasmi.

Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi kwa raia wa nchi hiyo Rais Kikwete amesema hatua hiyo inafuatia mazunguzo baina ya viongozi hao wawili yaliyofanyika hivi karibuni nchini Uganda.

Kwa miezi kadhaa Tanzania na Rwanda zimekuwa katika mgogoro wa kidiplomasia baada ya Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuishuri Rwanda pamoja na Uganda kuzungumza na waasi wa nchi zao waliopo nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Japo hajataja ni kwa namna gani mgogoro huo uliokuwa umefukuta baina ya Tanzania na Rwanda na vipiumepa afumbuzi, Rais Jakaya Kikwete amesema hatua ya mazungumzo baina yake na Rais wa Rwanda Paul Kagame ndio chanzo cha mafanikio hayo yote.

Tanzania na Rwanda ziliingia katika mgogoro wa kidiplomasia hadi kufikia hatua ya kutunishiana misulikisiri siri baada ya Rais Jakaya Kikwete kushauri nchi ya Rwanda naUganda kuzungumza na waasi wa nchi zao waliopo nchini Jamuhuiri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jambo lililopingwa vikali na Rwanda kwa madai kwamba Rais Kikwete aliingilia mambo ya ndani ya Rwanda kwa kuwashauri kufanya mazungumzo na watu walioua raia wa nchi hiyo.

Mgogoro huu ulipamba moto na hata kukolezwa na zaidi na vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.

Sasa Rais anavyoomba vyombo vya habari Wanasiasa pamoja na mitandao ya kijamii kusaidia kwa upande mwingine kuziba ufa wa uhusiano uliobomolewa.

Aidha katika hotuba Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa opereshi ya kuwaondoa wahamiaji haramu nchini humo iliyofanyika hivi karibuni ambapo amesema kuwa operesheni hiyo iliendeshwa kwa haki na hakuna uvunjifu wa haki za binadamu uliofanyika katika operesheni hiyo.

Hata hivyo Rais Kikwete ametoa agizo kama kuna mtu aliyenyanyaswa katika operesheni hiyo atoe taarifa kwa viongozi wa serikali.

Kuhusu wahamiaji waliokaa nchini Tanzania muda mrefu Rais Kikwete amesema watu hao sasa watapewa uraia rasmi wa Tanzania ili wafuate uratibu.

Mbali na suala la uhusiano wa Tanzania na Rwanda Rais Kikwete pia alizunguzia masuala mengine yaliyojitokeza hivi karibu ikiwa ni pamoja na muswada wa sheria ya katiba mpya kuhusu uundwaji wa bunge la katiba uliozua mtafaruku hivi karibuni ambapo alivialika vyama vya upinzani vilivyokuwa vikipinga sheria hiyo wakae naye katika meza ya mazungumzo kumaliza mgogoro huo.

50 WAUWAWA MISRI

Takriban watu 50 wameuawa kwenye makabiliano kati ya polisi na wafasi wa Rais aliyeondolewa mamlakani Mohammed Morsi.

Zaidi ya wanachama wengine miambili wa vuguvugu la Muslim Brotherhood walikamatwa mjini Cairo,ambako vifo vingi zaidi viliripotiwa.

Wafuasi wa Morsi waliandamana katika miji kadhaa kote nchini Misri,huku jeshi likiadhimisha miaka 40 ya vita vya mwaka 1973 katika ya waarabu na waisraeli.

Wafuasi wa Morsi wanasema kuwa aliondolewa mamlakani na jeshi mwezi Julai mwaka huu.

Kipindi muhimu

Mamia ya watu walikusanyika katikamedani ya Tahrir kuadhimisha siku hiyo.

Ndege za kijeshi zilionekana zikipaa angani huku jeshi likionyesha uwezowake wa kulinda nchi.

Baadhi ya waliokuwa wamekusanyika mjini humo walishangilia wakiwa wamebeba mabango yenye picha za mkuu wa ulinzi Generali Abdel Fattah al-Sisi.

Baadhi wanamtaka agombee urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Lakini mwandishi wa BBC Quentin Sommerville mjini Cairo anasema kuwa wafuasi wa Morsi pia waliandamana kwa wingi wakijaribu kuingia Tahrir kwa lazima huku wakimuita Generali Sisi muuaji.

Askari wa usalama walitumia moshi wa kutoza machozi na kufyatua risasi hewani kuwazuwia wafuasi wa Morsi kufika medani ya Tahrir mjiniCairo.

Maelfu ya watu walishiriki Tahrir katika shughuli zilizotayarishwa na jeshi kuadhimisha siku hiyo.

Ghasia piya zilizotokea katika maandamano kama hayo kwenye miji kadha mengine ya Misri

MADEREVA WA MALORI WAGOMA MIZANI YA KIBAHA

Magari yanayongia na kutoka DSM yamekwama Kibahamizani baada ya madereva wa Malori kugoma kwa madai ya kutofautiana kwa uzito kati ya bandarini na mizani Kibaha

WATU 60 WANUSURIKA KIFO

Watu zaidi ya 60 waliokuwa wakisafiri wamenusurika kifo huku wengine wakijeruhiwa baada ya basi la Mtei Express Coach kuyagonga magari matatu katika eneo la kijiji cha Mawemairo Wilayani Babati Mkoani Manyara kilichopo katika barabara kuu inayotoka mjini babati kuelekea mkoani Arusha.

Ajali hiyo imelihusisha bus hilo lenye namba za usajili T 729 bes wakati lilipokuwa likitokea mjini Babati kuelekea mkoani Arusha na kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa wakisafiri wamesema lilipofika katika eneo hilo,dereva wa basi hilo alishindishwa kulimudu wakati alipopewa ishara na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi wa barabara ya serikali ya china(Chico) kusubiri lori lililokuwa likishusha matofali kwa ajili ya ukarabati wa karavati na hatimaye kuyagonga magari yaliyokuwa yakisubiri lori hilo.


Nae mganga mfawidhi katika hospitali ya Halmashauri ya mji wa Babati Bw Mosses Mollel amesema amepokea majeruhi wanane na mpaka sasa amebaki majeruhi mmoja huku wengine wamepata ruksa baada ya kupatiwa matibabu.

Chanzo:ITV

RWANDA YAPUUZA VIKWAZO VYA MAREKANI

Jeshi la Rwanda limepuuzilia mbali hatua ya Marekani kuiwekea vikwazo kuhusiana na madai ya watoto kutumiwa kupigana kama wanajeshi katika vita ambavyo Rwanda inadaiwa kuunga mkono waasi wa M23 ndani ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.Shirika la habari la AFP lilimemnukuu msemaji wa jeshi la Rwanda akisema kuwa sio haki kwa Rwanda kuadhibiwa kwa mambo ambayo hayafanyiki ndani ya mipaka yake wala kutekelezwa na jeshi la Rwanda.

Joseph Nzabamwita alisema kuwa hatua ya kujumlisha Rwanda kuwa miongoni mwa nchi zinazotumia watoto kama wanajeshi haina misingi hata kidogo.

Umoja wa mataifa unatuhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasiwa M23 katika harakati zao dhidi ya serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo madai ambayo Rwanda imekana.

Mnamo siku ya Alhamisi naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani kuhusu maswala ya Afrika Linda Thomas-Greenfield alisema kuwa Marekani inatumia sheria ya kuwalinda watoto ya mwaka 2008 katika kuiwekea Rwanda vikwazo ili ikome kujihusisha na vita ndani ya DRC hususan katika kuwasajili watoto kama wanajeshi.

Kwa mujibu wa afisaa mkuu katika idara ya mambo ya nje alisema kuwa hatua hiyo itaifanya Rwanda kunyimwa msaada wa kijeshi katika mwaka 2014.

Nzabamwita alinukuliwa na AFP akisema kuwa Marekani inafahamu fika kuwa Rwanda haijawahi kuunga mkono utumiaji wa watoto kama wapiganaji na kuwa licha ya vikwazo hivyo Rwanda itaendelea kushirikiana na Marekani.

Kundi la waasi la M23 lilianzishwa na waliokuwa waasi wa Tutsi waliojiunga na jeshi la DRC chini ya mkataba wa amani wa mwaka 2009 Mwaka 2012 mwezi Aprili waasi wa M23 waliwageuka waliokuwa wanajeshi wenza na kuanza uasi Mashariki mwa nchi ambako kuna utajiri mkubwa wa madini.

SHEKHE AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI USIKU WA KUAMKIA LEO

Kiongozi mmoja wa dini ya kiisilamu ameuawa kwa kupigwa risasi pamoja na watu wengine mjini Mombasa, Pwani ya Kenya.

Haijulikani aliyetekeleza mauaji hayo ya usiku wa kuamkia leo huku kukiendelea kuwa na hali ya wasiwasi miongini mwa waisilamu na maafisa wa usalama mjini humo.

Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa muhubiri katika msikiti alipokuwa akihubiri marehemu Sheikh Aboud Rogo ambaye pia aliuawa kwa kupigwa risasi.

Aliuawa na watu wengine watatu walipokuwa wanrejea nyumbani Alhamisi usiku baada ya kuhubiri.

Sheikh Rogo alishutumiwa kutoa mafunzo yenye itikadi kali yaliyowashawishi vijana kujiunga na makundi ya kigaidi kama Alshaabab.

Marehemu Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al ShabaabMauaji haya ni sawa na ya marehemu Aboud Rogo Mohammed mwaka jana na ambayoyalisababisha ghasia mjini humo.

Yanakuja wiki mbili tu baada ya shambulizi la kigaidi lililofanywa dhidi ya jumba la maduka la Westgate ambapo watu 67 waliuawaKundi la kigaidi la al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi hayo ya kigaidi.

Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Shabab na baadhi ya waisilamu walioshutumu polisi waliomuua walisema kuwa yalikuwa madai tu wala.Ibrahim Rogo alionekana kama mrithi wa marehemu Aboud Rogo, alipohutubu katika msikiti huo.

WATUPWA JELA NA KUCHAPWA MIJELEDI 1200 KWA KUCHEZA UCHI

Mahakama nchini Saudi Arabia, imewahukumu wanaume wane vifungo jela na dhabu ya maelfu ya mijeledi baada ya mmoja wao kunaswa kwenye video akicheza dansi juu ya gari akiwa uchi.Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo, wananume hao walishtakiwa kwa kosa la kucheza dansi juu ya gari hadharani na kukiuka maadili ya umma.Hata hivyo wamepewa ruhusa ya kukata rufaa.

Saudi Arabia inafuata sharia kali za kiisilamu, ambazo zinaweka vikwazovingo vya kijamii na hata kuharamisha maeneo ya hadhara yakujitumbuiza.

Tukio hilo lilitokea katika eneo lijulikanalo kama Borayda, mji mkuu wa mkoa wa al-Qasseem Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu Riyadh, na kanda ya vitu walivyovifanya kuwekwa kwenye mtandao.

Mwanamume aliyepatikana na hatiaya kucheza dansi akiwa uchi alipokea adhabu kali kuliko wote ya kifungo cha miaka kumi jela , kuchapwa viboko 2,000 na kutozwa faini ya dola 13,000.

Mshukiwa mwingine alipatikana na hatia na kufungwa jela miaka saba pamoja na kupokea mijeledi 1,200 wakati wengine wawili wakifungwa jela kwa miaka mitatu kila mmoja na kupokea adhahbu ya mijeledi miatano, kila mmoja.

Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, mwendesha mashtakaya umma, alipinga kile alichokiita adahabu nyepesi.

Duru zinasema kuwa Mkoa wa al-Qasseem unafuata sharia kali sana za kiisilamu na polisi wa kidini ndio wakali zaidi kuliko wote.