JESHI LA RWANDA LAEKEKEA JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI

Kwa mara ya kwanza sehemu ya kwanza ya kikosi cha jeshi la Rwanda imeondoka mjini Kigali kuelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya kati kwa ajili ya ulinzi wa amani nchini humo.

Jeshi hilo limeelekea Jamhuri ya Afrika ya kati likiwa na zana nzito nzito za kivita kama ishara ya kukabiliana na hali yoyote ya vita.

Kikosi hicho kimesafiri kwa msaada wa helikopta ya kivita ya jeshi la Marekani.

Mwandishi aliyopo Kigali Sylvanus Karemera amefanya mahojiano na Msemaji wa jeshi la Rwanda Brigedia Jenerali Joseph Nzabamwita ambaye anaanza kwa kuthibitisha kuondoka kwa kikosi hicho na jukumu lake nchini Jamhuri ya Afrika ya kati.