AFISA UPELELEZI AUAWA NEWALA

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linamsaka mtu mmoja ambaye hajatambuliwa jina kwa tuhuma ya ujambazi na mauaji mwananchi mmoja na afisa upelelezi wa jeshi hilo wilayani Newala ASP Nurdin Kassim Seif.

Mwananchi mwingine aliayeuawa katika shambulio hilo la kustukiza ametambuliwa kuwa ni Hamza Msangaluwa aliykufa hapohapo naaskari aliyetambuliwa kwa jina Robert Isaya (33) amejeruhiwa vibaya majani na amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Newala.

Taarifa lliyotolewa na jeshi hilo nakusambazwa kwa vyombo vya habari mkoani Mtwara inasema mtu huyo akiwa na siraha aina ya SMG alifika katika kituo cha kuuzia mafuta cha camel katika kijiji cha Kiduni nje kidogo ya mji wa Newala na kuwalazimisha wahudumu kutoa fedha za mauzo yote ya siku mbili kwa kuwatishia na silaha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na kaimu kamanda waPolisi wa mkoa wa Mtwara Issa Mnilota jambazi huyo alifanikiwa kupora kiasi cha zaidi ya shs 3,299,180 ndipo wananchi walipojitokeza kumfukuza hadi umbali wa kiliomita 8 kabla ya jeshi la polisi kufika katika eneo la tukio.

Taarifa inabaisha kuwa maofisa wajeshi la polisi walpofanikiwa kufika katika eneo la tukio mtuhumiwa akiwa amejificha vichakani alifyatua risasi na kuumuua raia papo hapo na baadaye kabla ya kumshambulia aliyaekuwa afisa upelelezi wa wilaya ya Newala na kusababisha kifo chake.

Mwili wa marehemu Hamza umekwisha chukuliwa na ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi wakati ule wa ASP Nurdin Kasim Seif bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Newala kusubiri taratibu zingine.

Jeshi la polisi linatoa shukrani kwa wananchi wilayani Newala kwa ushirikisno waliouonyesha na kuendelea kutoa wito kwa wananchi mkoani humo kuendelea kushirikiana katika kuwabaini na kuhakikisha wale wote waliohusika wanatiwa nguvuni.