Katika eneo la tukio mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaaam Bwana Saidi Mecky Sadiki amesema kuwa moto huo inaaminika kuwa ulisababishwa na moja ya cheche zilizoruka wakati mafundi wakiendelea na ukarabati katika ghala hilo.
Katika eneo hilo vikosi vya uokozi vya serikali na watu binafsi vilijitahidi kuokoa moto huo lakini kutokana na miundo mbinu hasa ya wamiliki wamajengo hayo kutokuwa rafiki katika uokozi ambapo zoezi hilo lilikuwa gumu kwa vikosi hivyo.
Naye meneja usambazaji wa dawa aina ya Coatem inayo tibu Maralia bwana Godson Muro, amesema kuwa kiasi kikibwa cha dawa kimeteketea katika tukia hilo, na kudai kuwa hawajui kiasi kamili cha dawa hizo ila huwenda kukawa na upungufu wa dawa hiyo nchini.
Eneo hilo lililopo karibu kabisa na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ambapo kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam, amesema kuwa walisimamisha kwa muda kutua na kuruka ndege, ambapo mpaka ITV inaondoka katika eneo la tukio ndege zilikuwa zimeanza kuruka na kutua katika uwanja huo.
Chanzo:ITV