WAKAMATWA WAKISAFIRISHA SILAHA YA KIVITA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu baada ya kuwa kamata wakiwa na Bunduki ya kivita Aina ya G3ikiwa na Risasi zake tisa za silaha Bunduki aina ya G3 wakati wakisafirisha Silaha hiyo kutoka Mpanda kuelekea M ji wa Tunduma Mkoa wa Mbeya.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Simoni Kasobhile maarufu kwa jina la Kamwela 42 Mkazi wa Ileje Mkoa wa Mbeya Bilau Rashid maarufu kwa jina la Maftah 44 Mkazi wa Sumbawanga Mkoa wa Rukwa na Martine John 32 Mkazi wa Tunduru.

Tukio la kukamatwa kwa watu hao watatu lilitokea mnamo January 10 mwaka huu majira yasaa mbili usiku huko katika kitongoji cha Matandalani Kata ya Sitalike Wilaya ya Mlele wakiwa na Silaha bunduki ya kivita Aina ya G3 yenye namba FMP 061283B3,67 ikiwa na Risasi tisa za Bunduki aina ya G3.

Kwa mujibu wa Kidavashari watu hao walikamatwa wakiwa wanasafiri kwa gari aina ya Toyota Cruiser ii Prado lenye namba za usajiri T 564 ABW lililokuwa likiendeshwa na dreva anaeitwa George Kiluli Mkazi wa Mpanda gari hilo lilikuwa likitoka Mpanda kuelekea Sumbawanga.

Alisema dreva wa gari hilo alikuwa anampeleka mdogo wake aitwaye Gabriel Samwel shule ya Sekondari Laela Sumbawanga alipofika kwenye eneo linaloitwa City Mjini Mpanda Dreva alisimamisha gari na kupakia abiria na miongoni mwa abiria waliokuwepo na hao watuhumiwa waliokuwa na silaha.

Alieleza jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi lilipata taarifa kutoka kwaraia wema kuwa kunawatu wenye silaha wamepanda gari lenye Namba tajwa wanaelekea Sumbawanga wakiwa na Silaha hiyo na ndipo mawasiliano yalifanyika kati ya Polisi na Idara ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi TANAPA na ndipo askariwa Hifadhi ya Katavi waliweka kizuizi katika eneo la Matandalani.

Kidavashari alisema Askari hao waliweza kulisimamisha gari hilona kisha kwa kushirikiana na Polisi kufanya upekuzi na kufanikiwa kukuta silaha aina ya G3 ikiwa imehifadhiwa kwenye turubai ikiwa ndani ya mfuko wa salufeti Baada ya kuhojiwa watu hao walikana kuwa mzigo huo sio mali yao lakini dereva wa gari hilo George Kiluli aliutambua mzigo huo kuwa ni mali ya watuhumiwa hao watatu Kamanda Kidavashari alieleza kuwa baada ya watuhumiwa kupekuliwa kwenye maungo yaondipo mtuhumiwa Simoni Kasobhile.


Chanzo: Katavi Yetu blog