WAASI SYRIA KUSHIRIKI MAZUNGUMZO

Baada ya mjadala mkali, kundi la upinzani nchini Syria limekubali kuhudhuria mazungumzo ya amani mjini Geneva wiki ijayo.

Uamuzi huo ulipokelewa vyema na wafadhili wake wa Magharibi waliosema ni hatua muhimu huku wakionyesha matumaini katika mazungumzo hayo.

Mataifa ya magharibi yenye uwezo mkubwa yamekuwa yakiushinikiza upinzani huo kushiriki katika mazungumzo hayo ambayo pia yatashirikisha serikali ya syria.

Swala la iwapo kuna umuhimu wakuhudhuria mazungumzo hayo yaliugawanya upinzani huo huku wengi wa wanachama wa kundi hilo wakiamua kujiondoa.

Mwandishi wa BBC amesema kuwa kutakuwa na maswala mengi kuhusu vile wawakilishi waupinzani huo walivyo jitayarisha.

Wakati huohuo, waziri wa mamboya nje wa Marekani, John Kerry amepongeza uamuzi wa upinzani wa Syria kwenda kwa mazungumzo nchini Switzerland.

Lengo la mkutano ni kuona ikiwa inawezekana kuunda serikali ya mpito, ili kumaliza mzozo wa Syria.

Mgogoro huo wa miaka mitatu, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 100,000