PAUL KAGAME AZUSHIWA KIFO

Kwa masaa kadhaa Ijumaa nyakati za asubuhi, kulikuwa na fununu kuwa Rais wa Rwanda,Paul Kagame ameaga dunia na taarifa hizo zilienea hadi mji wa Goma Mashariki mwa Congo. Wengi walisherehekea baada ya kupata habari hizo.

Lakini taarifa hiyo inasemekana kutokana na ujumbe bandia kwenye Facebook.

Hapana shaka kuwa kuna uhasama kati ya DR Congo na Rwanda hasa katika eneo la Mashariki mwa DRC ambako Rwanda imekuwa ikituhumiwa kwa kuchochea ghasia zinazoendelea huko.

Kwa hivyo fununu zilipoanza kuenezwa kuwa Kagame amefariki, walikuwa na furaha sana.

Mamia ya watu waliandamana kwenye barabara za mji wa Goma kuelekea katika mpaka wa Rwanda kusherehekea kile ambacho baadaye kilijuliakana kuwa tu tetesi na fununu za uongo kuwa Kagame kafariki. Hata walibeba jeneza bandia na msalaba.

Madereva barabarani walishaniglia kwa kupiga honi.

Tetetsi hizo zilipingwa vikali na serikali ya Rwanda kupitia Twitter.

Waziri mkuu wa Rwanda alijibu kwa kusema , kuwa taarifa hizo ni za kipuuzi sana huku mshauri mkuu waKagame pia akisema ni mambo ya kipuuzi.

Punde baada ya fununu hizo, maafisa wa serikali walichapisha picha ya Kagame kwenye Twitter akiamkiana na wanafunzi wageni waliotembelea nchi hiyo kutoka Marekani, ishara ya kuwa Kagame yuko hai.

Chuo hicho kimethibitishia BBC kuwa picha hiyo ni ya kweli na kuwa Kagame kweli alikutana na wanafunzi hao.

Sasa kwa kuwa Kagame yuko hai na anaendelea na kazi zake za kawaida, fununu hizo zilitoka wapi na zilianzavipi? Wakazi wa Goma wanasema kuwa zilitokana na ujumbe kwenye facebook ambao ulitolewa kwenye mtandao bandia kuhusu taarifa za vifo. Ujumbe huo ulichapishwa na kuanza kusambaziwa watu wa Goma.

Christoph Vogel, mtaalamu wa maswala ya Goma, anasema kuwa alianza kusikia kelele za watu asubuhi na kisha kuona baadhi ya ujumbe wa Facebook ukichapishwa katika mkahawa mmoja.

Na hapo ndipo maji yalizidi unga kwani watu walianza kukusanyika wakishangilia Na hivyo ndivyo taarifa huibuka na kuenea ziwe na kweli au za uongo