Kufuatia ufichuzi wa aliyekuwa mchambuzi wa maswala ya ujasusi nchini marekani, Edward Snowden, Rais Obama ameweka viwango vya utumizi wa data ya simu za watu.
Lakini afisa anayesimamia mswala ya sheria katika kampuni ya Google David Drummond ameiambia BBC kwamba Rais Obama anapaswa kutoa maelezo kuhusu viwango vya udukuzi huo katika mtandao.
Bwana Drummond amesema kuwa Marekani haifai kuchukua habari kwa wingi bali inafaa kutoaombi la kupewa habari hizo kupitia agizo la mahakama.
Amesisitiza kuwa kampuni ya Google haina ushirikiano wowotena shirika lolote la ujasusi.
Bwana Drummond aliongeza kwamba serikali zote duniani zinapaswa kubuni sheria za kimataifa kuhusu udukuzi wa taarifa binafasi za watu kwenye internet.