ARSENAL KUMENYANA NA LIVERPOOL, MAN CITY WAO KUWAKARIBISHA CHELSEA ETIHAD

Droo ya michuano ya kombe la FA imefanywa kwa mechi za mchujo wa raundi ya tano.

Chelsea wamepangiwa kucheza na Manchester City katika mchezo unaotazimiwa na ushindani wa hali ya juu.

Chelsea ambao wamefuzu kwenye raundi ya tano kwa kuiondosha Stoke City katika mchezo ambao ulimalizika kwa ushindi wa bao moja kwa bila.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akizungumza punde baada ya droo hii amesema, "Iwapo unataka kuwa bora lazima ucheze na timu bora.

"Nao Manchester City wao walijikatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo hatua ya tano kwakuiadhibu Watford kwa mabao 4-2.

Liverpool wao watakuwa wageni wa Arsenal kwenye mchezo wa raundi ya tano.

Roberto Martinez ataiongoza Everton kukutana na timu yake ya zamani ya Swansea, ilihali Sunderland wao watacheza na Southampton ikiwa ni mechi liyokutanisha timu zote za ligi ya England.

Cardiff watakuwa nyumbani kuwakaribisha Wigan na Hull watacheza na Brighton. Sheffield Wednesday watapamabana na wenzao walioko kwenye ligi ya Championship, Charlton FC.

Mechi zote zitachezwa jumamosi na jumapili ya tarehe 15 na 16 mwezi wa pili.

Mshindi wa mechi kati ya Fulhamama Sheffield United atapambana na mshindi kati ya Nottingham Forest au Preston kwenye hatua ya raundi ya tano ya kombe hilo ambalo fainal yakeitachezwa kwenye uwanja wa Wembley.


Droo kamili ni kama ifuatavyo;

Manchester City v Chelsea

Sheffield United au Fulham v Nottingham Forest au PrestonNorth End

Arsenal v Liverpool

Brighton & Hove Albion v Hull City

Cardiff City v Wigan Athletic

Sheffield Wednesday v Charlton Athletic

Sunderland v Southampton

Everton v Swansea City


*KATIKA MICHUANO YA TENIS*

Stanislas Wawrinka raia wa Uswis amefanikiwa kutwaa taji la michuano ya wazi ya Australia kwa kumchapa Mhispania Rafael Nadal katika mchezo wa fainali.

Wawrinka alimfunga Nadal aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo ya mgongo kwa seti tatukwa moja, ikiwa ni kwa matokeo ya 6-3 6-2 3-6 6-3.

Anakuwa raia wa pili wa Uswis kunyakuwa taji la Grand Slam kwa upande wa wanaume kwa mchezo wa tenesi wa mchezaji mmoja mmoja.

Pia ni mtu wa pili kunyakuwa taji kubwa kama hilo akiwa ametoka nje ya vinara wanne wa juu wa dunia wa mchezo wa tenesi, baada ya Juan Martin Del Potro kufanya hivyo kwenye michuano ya US Open mwaka 2009.

Nadal ambaye awali alisema kusumbuliwa na matatizo ya mgongo lakini hakujitoa kwenye michuano hiyo ambayo imefikia tamati huko Melbourne Park."

Sikupenda kusema kwamba sitocheza mchezo wa fainali, ni jambo ambalo nachukia sana hatakama niligundua kuwa nina maumivu ya majeraha" Alisema Nadala mwenye umri wa miaka 27." Huu sio wakati wa kuzungumzia maumivu niliyoyapata, ila ni wakati wa kumpongeza Stan.

Amecheza vizuri sana na ukweli anastahili taji hili.Ni mtu mwema, mtu mzuri na rafiki yangu, nina furaha sana kwake kuwa bingwa" Alisema Nadal.

Naye Wawrinka alimsifu Nadal kwa kuwa bingwa wa kweli na kinara wa kweli wa tenesi duniani kwa wanaume, alikiri hujisikia furaha kupambana na kumshinda bingwa kama Nadal.

Wawrinka hajawahi kushinda hata seti moja katika michezo yote 12 aliyokutana na Nadal huko nyuma, na alicheza fainal yake ya kwanza akiwa kwenye nafasi ya 19 ya ubora wa tenesi duniani.