WATU 20 WAHOFIWA KUFA KUTOKANA NA MLIPUKO

Watu 20 wanahofiwa kufariki kutokana na mlipuko katika ghalala silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa nchini humo, vimesema kuwa nyumba nyingi ziliharibiwa wakati wa mlipuko huo katika kambi moja ya kijeshi karibu na soko kuu la Mbuji-mayi.

Mlipuko huo uliotokea katika mji wa Mbuji-Mayi inasemekana ulisababishwa na radiKwa mujibu wa taarifa za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa Monusco, zaidi ya watu 50pia walijeruhiwa huku nyumba kadhaa zikiharibiwa.

Lengo la Monusco nchini humo nikupokonya makundi yanayopigana silaha.

DRC inajaribu kutokamana na vita vilivyo sababisha mamilioni ya vifo kati ya mwaka 1998 na 2003.'Nimewaamrisha maafisa wetu walio mjini Mbuji-Mayi kushirikiana na wenyeji ili kusaidiana kukabiliana na hali,'' alisema Martin Koble mkuu wa kikosi hicho cha Monusco.

Mbuji-Mayi ni mji wa tatu kwa ukubwa DRC, na ndio kitovu cha uchimbaji wa madini ya Almasi.