OBAMA ATOA HOTUBA KWA TAIFA

Rais Obama ametumia hotuba yake ya kila mwaka kwa taifa kuelezea jinsi atakavyotumia madaraka yake kujaribu kuimarisha uchumi wa marekani na pia kukabiliana na bunge la Congress ambalo linashuhudia mgawanyiko.

Bwana Obama ameutaja mwaka 2014 kuwa mwaka wa mafanikio kwa Marekani na kusema kuwa China sio tena mahali bora pa kuekeza bali ni marekani. ''Haya ndiyo matokeo ya juhudi zenu: kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira kwa kiwango kikubwa zaidi katika kipindi cha miaka mitano. Sekta ya nyumba na makaazi iliyofufuka.

Sekta ya utengenezaji bidhaa inayobuni nafasi za ajira kwa mara ya kwanza tangu miaka ya tisini. Mafuta zaidi yanazalishwa hapa nyumbani ikilinganishwa na yale tunayonunua-hili limetokea kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka ishirini.

Nakisi katika bajeti yetu ilipungua kwa zaidi ya nusu. Na kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja, viongozi wa kibiashara kote duniani, wametangaza kuwa China haiongozi tena kama eneo bora la kuekeza duniani bali ni marekani,'' amesema rais Obama.

Kadhalika bwana Obama amesema licha ya kushuhudia miaka minne ya ukuaji wa uchumi na faida kubwa iliyovunwa na makampuni, ukosefu wa usawa umezidi kukitamizizi nchini marekani.

Amesema ametoa mapendekezo ya kuimarisha ukuaji.

Bwana Obama amesema:
''leo, baada ya ukuaji wa uchumi kwa kipindi cha miaka minne, faida za makampuni ya bei ya hisa zimekuwa juu, na zilizokuwa juu zimezidi kuwa bora. Lakini mishara ya wastani bado iko palepale. Ukosefu wa usawa umezidi kukita mizizi.''

Kuhusu usumbufu wa bunge la Congress, bwana Obama amesisitiza kuwa yuko tayari kuendelea kufanya kazi na wabunge wa Congress kurekebisha baadhi ya mambo, lakini hatasita kutumia fursa nyingi zitakazojitokeza kadri iwezekanavyo kuchukuwa hatua za kurekebisha mambo hata bila marekebisho ya sheria kupitia Congress.