MORSI KUSHITAKIWA KWA KUPANGA NJAMA KUTOROSHA WAFUNGWA

Aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa shitaka la kupanga njama ya kuwatorosha wafungwa wakati wamapinduzi ya Hosni Mubarak 2011.

Kosa jengine ni pamoja na kuwaua maafisa wa polisi wakati wa tukio hilo.

Hii ni miongoni tu mwa kesi nne zinazomkabili bwana Morsi.

Zaidi ya walalamishi wengine 130 wakiwemo viongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood watawekwa kizimbani na Morsi.

Bwana Morsi hajakuwa huru tangia jeshi limuondoe madarakani mwaka mmoja baadaya kuchaguliwa kama rais.

Wakati huohuo, wizara ya mamboya ndani imesema kuwa afisaa mmoja wa wizara hiyo Generali Mohammed Saeed, alipigwa risasi akielekea kazini.

Mauaji hayo yanatokea wakati mashambulizi dhidi ya maafisa wa usalama katika siku za hivi karibuni na masaa kadhaa baada ya jeshi kumuunga mkono mkuu wake Field Marshal Abdul Fattah al-Sisi kugombea urais.

Hali ya usalama imeimarishwa nje ya ya jengo la wizara hiyo , lakini hakuna hata mfuasi mmojawa Mohammed Morsi amejitokeza.

Vuguvugu la Muslim Brotherhood, limeharamishwa na kutajwa kama kundi la kigaidi na pia wameifanya hatia uungwaji mkono wa kundi hilo.

Makabiliano kati ya wafuasi wa Brotherhood pamoja na vikosi vya usalama, yaliripotiwa kutokeakatika eneo la Ramses mjini Cairo.

Morsi anatuhumiwa kwa kosa la kupanga njama ya kuwatorosha wafungwa kutoka katika gereza laWadi al-Natrun wakati wa ghasia za mwaka 2011.

Mara ya kwanza alipofikishwa mahakamani mwezi Novemba, Morsi alikataa kutambua uhalali wa mahakama wala kuvalia vazi lagerezani.