Bi Valleeie alilazwa hospitalini Ijumaa kwa maagizo ya daktari iliaweze kupumzika , baada ya jarida la Closer kuchapisha picha za Rais Hollande na mwanamke anayedaiwa kuwa na uhusiano wakimapenzi naye Julie Gayet.
Bwana Hollande hakukanusha madai hayo ingawa aliteta vikali kuhusu vyombo vya habari kuingilia maisha yake binafsi.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Conservative, Jean-Francois Cope amesema kuwa taarifa hiyo imeharibu sifa ya Ufaransa kimataifa.
Bi Trierweiler anatarajiwa kuondoka hospitalini baadaye Jumatatu.
Hii leo Rais Hollande alitarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu uchumi wa nchihiyo ingawa mambo yanaonekana yatabadilika kutokana na taarifa hizi kuhusu kashfa ya mapenzi inayomwandama Hollande.
Trierweiler na Hollande walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1988 akiwa mwandishi wahabari wakati huo naye Hollande akiwa mbunge wa chama cha kisosholisti.
Kura za maoni zinaonyesha ushawishi wa Hollande kudidimiana kwamba ni 25% pekee ya watu nchini humo wana Imani naye.