POLISI WAWAFYATULIA RISASI WANAOTAKA MASHOGA KUNYONGWA

Maafisa wa ulinzi Kaskazini mwa Nigeria wamefyatua risasi hewani kuwatawanya waandamanaji, waliokuwa wakishinikiza adhabu ya kifo kwa wanaume saba ambao wametuhumiwa kuwa wanachama wa shirika moja linalohimiza mapenzi ya jinsia moja.

Wanaume hao walikuwa wakishtakiwa chini ya sheria za Kiislamu maarufu kama Sharia, mjini Bauchi Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kesi hiyo ilivurugwa na mamia wa vijana waliokuwa wamejawa na hasira ambao walirusha mawe nje ya mahakama hiyo.

Polisi waliwatawanya waandamanaji hao ili kupata nafasi ya kuwarejesha washukiwa hao gerezani.

Nchini Nigeria, vitendo vyote vyote vya mapenzi ya jinsia moja ni haramu chini ya sheria za Kiislamu na hata sheria zingine zakidini na kitamaduni.

Sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja nchini Nigeria, ilifanyiwa marekebisha hivi majuzi ili watakaopatikana na hatia kupewa adhabu kali.