ATEKWA, KUTESWA NA KUACHWA PORINI

Katika hali isiyo ya kawaida, kijana mmoja aliyetoweka kwa siku sita nyumbani kwao kwenye mazingiraya kutatanisha amekutwa kwenye Pori la Lumwago kijiji cha Kinyanambo wilayani Mufindi mkoani Iringa akiwa na majeraha makubwa yaliyotokana na mateso aliyoyapata baada ya kutekwa.

Chanzo cha mkasa wa kijana huyo aliyelazwa katika Hospitali ya Mafinga kinadaiwa kuwa ni kupotea kwa Pikipiki katika eneo la Mashine ya Mpunga mjini Mafinga walikokuwa wanapata kinywaji.

Akizungumzia juu ya tukio hilo la kutekwa na kisha kuteswa, ambalo limesababishia majeraha makubwa na kulazwa katika Hospitali hii ya mjini Mafinga, Ezekia Kaganga amesema tukio hilo lilitokea siku ya tarehe 18 mwezi wa pili.

Hata hivyo Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Iringa Athmani Mungi amesema tayari watu wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika katika tukio hilo, ambapo amewataja kuwa ni Alex Ludago na Steven Michael, wote wakazi wa MET Mafinga Iringa.