Uwasilishwaji wa rasimu ya katiba uliokuwa ufanywe na mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Mh jaji Joseph Warioba umeshindwa kufanyika baada ya baadhi ya wajumbe ambao ni wanachama wa umoja wa katiba ya wananchi kusimama na kuanza kuzomea, kupiga makofi na kuzungumza bila ya utaratibu wa kipinga kuwasilishwa kwa rasimu hiyo kwa kile walichodai kuwa kanuni zimekiukwa.
Siyo kwamba ni sokoni bali ni wajumbe wa bunge maaalum la katiba ambao wanapinga kuwasilshwa kwa rasimu hiyo ambapo licha ya mwenyekiti wa bunge hilo Mh Samweli Sitta kumtaka jaji Warioba kuendelea haikuwezekana.
Baada ya hali hiyo wabunge ambao wanaunga mkono kitendo kilichofanyika cha kuzuia kuwasilishwa kwa rasimu hiyo ambapo wali kilaani vikali.
Aidha kwa upande wa wabunge ambao wanaunga mkono kilichotokea bungeni wamesema mwenyekiti ameanza kwa kukiuka kanuni kana kwamba wakati zinapitishwa hakuwepo na hivyo hawawezi kamwe kukubali kuburuzwa.
Hata hivyo licha ya kusitishwa kwa bunge hilo wajumbe waliendelea kukaa ndani ya ukumbi huo wakipiga soga hatua ambayo pia ilipelekea kutolewa kwa tangozo lingine la kuwataka watoke nje.