Ajali hiyo imetokea ikihusisha lori lenye namba za usajili t 417
ABF, mali ya kampuni ya Camel oil ambalo lilikuwa likisafirisha lita
35,000 za mafuta aina ya diesel kutoka jijini Dar es salaam kwenda
nchini Congo DRC ambalo linadaiwa kugongwa na lori linguine.
Baadhi ya wananchi ambao wameshuhudia ajali hiyo wameitaka
serikali kuwalazimisha wamiliki wa malori kuhakikisha magari yao
yanakuwa na madereva wa akiba kwa kuwa wanaamini kuwa ajali hiyo
imesababishwa na dereva wa lori moja wapo kusinzia wakati akiendesha
gari kutokana na uchovu wa safari ndefu.
Mpaka ITV inaondoka katika eneo hilo la ajali, bado lori hilo
lilikuwa likiendelea kuteketea huku kukiwa hakuna msaada wowote wa
kuuzima moto huo.
Chanzo; ITV