AFUKUZWA UPADRE KWA UDHALILISHAJI WA WATOTO

BALOZI wa zamani wa Vatican katika Jamhuri ya Dominica, Monsinyori Jozef Wesolowski ametiwa hatiani na Mahakama ya Kanisa Katoliki kwa tuhuma za kudhalilisha watoto.


Kutokana na kutiwa hatiani huko amepokwa upadre wake. Monsinyori Wesolowski amekuwa kiongozi wa juu kuteuliwa na Papa kutiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo ya kupokwa upadri.


Taarifa ya Vatican ilisema Monsinyori Wesolowski alikutwa nahatia na Mahakama hiyo ya Usharika wa Mafundisho ya Imani katika siku za hivi karibuni: kwa adhabu hiyo ina maana hataweza kutekeleza majukumu yake kama Padre.


Wesolowski amepewa miezi miwiliya kukata rufaa. Lakini pia anakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Vatican. Kwa kuwa ni Mwanadiplomasia wa Kipapa yeye ni raia wa mji wa nchi hiyo.


Papa alimrejesha Vatican, Wesolowski ambaye ni mzaliwa wa Poland Agosti 21, 2013 na kumfutakazi baada ya Askofu wa Santo Domingo, Kadinali Nicolas de Jesus Lopez kumueleza Papa Francis kuhusu kuwepo kwa tetesi kuwa Wesolowski aliwadhalilisha watoto wa kiume akiwa Jamhuri ya Dominica.


Mamlaka za Dominican hatimaye zilianza uchunguzi lakini hazikumshtaki. Poland, pia ilianza uchunguzi dhidi ya Wesolowski.


Wesolowski ni Ofisa wa Juu Vatican kuchunguzwa kwa tuhuma za udhalilishaji watoto na kesi yake iliibua waswali iwapo Vatican, kwa kumuondoka katika mamlaka ya Dominica ilikuwa ni kumlinda na kuanzisha uchunguzi wake kabla ya mamlaka za taifa hilo la Caribbean.


Hata hivyo Vatican haijawahi kusema iwapo Wesolowski alishawahi kujitetea kuhusiana na tuhuma hizo na hajawahi kutoa mawasiliano yoyote kwa mawakili wake.


Kesi hiyo imekuwa ikichukuliwa kwa umakini kwani Wesolowski alipewa upadirisho wake na Uaskofu na Papa St John Paul 11 ambaye pia ni Raia wa Poland.

VURUGU ZAZUKA WAKIGOMBEA KUZIKA MWILI WA MTOTO

Mtafaruku mkubwa umetoke msibani katika Mtaa wa Kawajense madukani Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi baada ya ndugu wa pande mbili kugombania kuzika mwili wa mtoto aitwaye Junior Bacho mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyefariki june 26 majira ya saa saba usiku katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Tukio hilo la ambalo lilivutia hisia za watu wengi lilitokea hapo juzi katika mtaa huo baada ya marehemu huyo kufariki akiwa amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda aliko kuwa akiuguzwa na shangazi yake aitwaye Evelyne Komba


Baada ya mtoto huyo kufariki kulitokea kutoelewana baina ya ndugu wa baba wa mtoto aitwaye Joseph Bacho na ndugu wa mama wa marehemu aitwaye Anna Kizo Upande wa ndugu wa baba ulidai wao ndio wenye haki na jukumu la kuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka nyumbani kwa mama mzazi wa baba wa marehemu aitwaye Ted Francis (bibi miti) anae ishi katika mtaa wa madukani mjini hapa


Ndugu wa mama wa marehemu nao walidai hawako tayari msiba huo kwenda kwa baba wa marehemu kwani hakuwa na uhalali wakuchua mwili wa marehemu kwa kile walicho dai baba wa marehemu alikuwa ajatowa mahari hivyo wao awamtambui.


Hari hiyo iliwafanya ndugu wa pande hizo mbili kuanza kutupiana shutuma za lawama ambapo ndugu wa baba wa marehemu walimshutumu mama wa marehemu kwa kushindwa kumhudumia marehemu wakati akiwa mgonjwa na muda wote baba wa marehemu alipokuwa akifika nyumbani Anna Kiza alikuwa hamrusu kumwona mwanae kwa kumweleza amelala.


Walidai toka marehemu alipochukuliwa na baba yake hapo june 18 kwa ajili ya kumshughulikia matibabu ya ugonjwa wa ukosefu wa lishe (kashakoo) mama wa marehemu wala ndugu wa upande wake hawakuwahi kufika hata siku moja kumwangalia hari iliyofanya mtoto huyo awe anaangaliwa na shangazi Evelyne yake na bibi yake Ted Pamoja na maelezo hayo ndugu wa mama wa marehemu waliendelea na msimamo wao wa msiba kuwa kwao baada ya mabishano ya muda mrefu pande mbili hizo ziliamua kuuwacha mwili wa marehemu kwenye chumba cha kufidhi maiti katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda.

Baaada ya kurudi nyumbani kila upande uliweka msiba nyumbani kwao hali iliyofanya msiba huu kuwe kwa sehemu mbili tofauti katika mtaa mmoja.


Siku iliyofuata wazee wa mtaa huo waliingilia kati mgogoro na kufanya kikao na pande mbili hizo zilizokuwa zikivutana na kufikia uamuzi wa kuwa msiba huo uwe nyumbani kwao na baba wa marehemu Kufuatia uamuzi huo shangazi wa marehemu
Evelyne Komba aliongoza ndugu na kwenda chumba cha kuhifadhi maiti na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka kwao na baba wa marehemu kwa ajiri ya maandalizi ya mazishi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika juzi saa nane kwenye makaburi ya kawanjense msufini


Wakati huo shughuli za uchimbaji wa kaburi ulifanyika na kaburi lilikamilika ikawa unasubiliwa muda uliopangwa wa kufanyika kwa mazishi.


Baada ya muda mfupi ndugu wa baba wa marehemu walipata taarifa kuwa kaburi walilochimba kwa ajiri ya kumzikia marehemu wameonekana watu wakilifukia hari ambayo iliwafanya waelekee huko makaburini.


Ndugu hao wa baba wa marehemu walipofika makaburini walikuta dada wa mtoto wa marehemu aitwae Jane Kiza na wenzaki wakiwa ndio wanamalizia kufukia kaburi hilo ambalo halikuwa na mwili wa marehemu.

Jane na kundi lake walipoulizwa kwanini wamefukia kaburi hilo walianza kufoka na kisha kundi la ndugu wa mama wa marehemu walitokea hapo na kuanza kuwashambulia kwa kipigo ndugu wa baba wa marehemu.


Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia walikuwa wameongozwa na meja wao alijulikana kwa jina la Bahati walifika kwenye eneo hilo na kutuliza ghasia hizo na kisha walielekea eneo la msibani na kuamuru mwili huo wa marehemu urudishwe kwenye chumba cha kuifadhi maiti hadi hapo ufumbuzi wa tatizo hilo utakapo kuwa umekwisha.


Ndugu wa marehemu walikubaliana na uamuzi huo wa kuurudisha mwili wa marehemu kwenye chumba cha kuifadhi maiti.


Chanzo: Katavi yetu

MWENYEKITI WA CCM AUWA KINYAMA

Watu wanadhaniwa kuwa ni majambazi wamemuua kinyama kwa kupiga risasi moja ya kichwani mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Busambala wilayani Butiama mkoani Mara Bw Willison Opio mwenye umri wa miaka 6o huku kichwa chake kikisambaratishwa kabisa na risasi hiyo.

Mauaji hayo ya kinyama yamefanyika saa saba usiku wa kuamkia leo, baada ya majambazi hayo kuvunja milango ya nyumba aliyokuwa amelala kiongozi huyo na familia yake katika kijiji cha Kwikuba kabla ya kumshambulia kwa bapa za panga mke wamarehemu Bi Agness Wambura ambaye alilazimika kuwapa kiasi cha shilingi laki nne ambazo alizikopa kutoka katika taasisi moja ya fedha.

Afisa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Mara Acp Rogati Mlashan,akizungumza akiwa eneo la tukio, amesema baada ya majambazi hayo kuvunja milango miwili ya nyumba hiyo, walipiga risasi tatu na moja kumpata kichwani kiongozi huyo wa CCM na kufariki dunia papo hapo na kusema kuwa jeshi la polisi litafanya kila liwezavyo ili kuhakikisha wote walihusika kufanya uhalifu huo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi serikali katika kata ya Busambala,wakizungumzia tukio hilo pamoja na kuonyesha masikitiko yao baada ya kupata taarifa za kifo cha kiongozi huyo wa CCM, wameliomba jeshi la polisi kuendesha msako mkali ambao utawesha kukamatwa kwa wahusika, hatua ambayo wamesema itasaidia kuondolea wananchi hofu kubwa waliyonayo sasa.

UINGEREZA YAKABILIWA NA UHABA WA MANII

Uingereza inakabiliwa na upungufu wa shahawa hali ambayo huenda ikalazimu kiliniki za matibabu ya uzazi nchini humo kuchukua mbeguduni.

Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo hutegemea shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na mahitaji yake nchini humo.


Lakini mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan Pacey amesema kuwa ana wasiwasi j kwamba baadhi ya vituo hivyo vya matibabu sasa vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.


Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazo gharimu kiasi kikubwa cha fedha iwapo mbegu duni zitatumiwa.


Inadaiwa kuwa upungufu huo unasababishwa na kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya wanaotoa mbegu hizo sasa ni sharti yajulikane ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi walipendelea kuficha majina yao.


Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya uzazi yanawafanya wanaume wengi kutafuta watoto wao wenyewe.


Hata hivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za kiumebado upo.


Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa binaadamu zinaonyesha kuwa moja kati ya mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya kigeni.


Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu kumi mnamo mwaka 2005.

ALAZWA HOSPITALI BAADA YA KUMKANA MUNGU

Mwanamume mmoja katika jimbo la Kano, nchini Nigeria, amepelekwa katika kituo cha matibabu ya kiakili baada ya kusema kuwa hamwamini Mungu.


Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika moja lisilo la kiserikali nchini nIGERIA.


Mubarak Bala alizuiliwa kinyume na matakwa yake hospitalini baada ya familia yake kumpeleka huko kwa matibabu.


Duru katika hospitali hiyo zimesema kuwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 29 alitibiwa kwa matatizo ya kiakili na kwamba hataendelea kuzuilikwa kwa muda mrefu.


Jimbo la Kano lina idadi kubwa ya waumini wa kiisilamu, na limekuwa chini ya sheria za kiisilamu tangu mwaka 2000.


Shirika hilo la kimataifa limesema kuwa wakati ambapo Bala aliwaambia jamaa wake kuwa hamuamini Mungu, familia yake uilimpekeka kwa daktari kuuliza ikiwa akili yake iko timamu.


Licha ya kufahamishwa kuwa mwanamume huyo hana tatizo lolote la kiakili, familia ya Bala ilitafuta ushauri wa daktari mwingine aliyewafahamisha kuwa hatua yake ya kumkana Mungu, inatokana na matatizo ya kiakili.


Bwana Bala, ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu, alilazimishwa kupata ushauri wa daktari wa kiakili , ingawa alitumia simu kuwasiliana na wanaharakati wa haki za kibinadamu.


Hospitali ambako alikuwa ana pokea matibabu ilisema katika taarifa yake kuwa Bwana Bala hana tatizo lolotela kiakili na kuwa yuko sawa.


Alilazwa hospitalini kwa sababu alihitaji kuchunguwa na daktari, ilisema taarifa ya hospitali hiyo.

WATU WATATU WAFARIKI KATIKA AJARI YA NOAH

Watu watatu wamekufa na wengine kumi wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noha kupasuka tairi ya nyuma na kubingirita mara tatu katika kijiji cha Januka manispaa ya Singida.


Akithibitisha kitokea kwa vifoo hivyo mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida daktari Deogratias Banuba amesema wamepokea maiti mbili wakiwa wamesha fariki eneo la tukio akiwemo dereva wa Noha bwana Enock Mbaga, binti Ajira Juma na maiti nyingine ya Bi Tatu Bunku ambaye alikuwa herd mistres Ngimu sekondari amefia katika hospitali ya mkoa wa Singida.


Daktari Banubasi amesema majeruhi kumi wamepatiwa huduma ya kushonwa sehemu mbalimbali za miili yao na wanaendelea na matibabu ,pia hakuna majeruhi ambaye atapatiwa rufaa.


Mmoja wa majeruhi akiongea kwa shida huku akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida bwana Ramadhani Mlenga amesema gari halikuwa katika mwendo wa kasi na gafla likaacha njia na kupinduka mara tatu.

SUPER EAGLES WAGOMEA MAZOEZI

Kikosi cha Nigeria katika kombe la dunia kimesusia kikao cha mazoezi kama ilivyopangwa kwa sababu ya kukosa kulipwa fedha zao za ziada.


Kitengo cha michezo cha BBC kimeelezwa kuwa wachezaji hao wanaamini kuwa wamelipwa kiasi cha dola 15,000 (pauni 8,800), chini ya pesa wanazopaswa kulipwa baada ya kufika katika mkondo wa pili wa kombe la dunia, huko Brazil.


Wachezaji hao wamesusia mazoezi katika uwanja wa Campinas na baadaye maafisa wakadai kwamba mazoezi hayo yalikuwa yametupiliwa mbali.

Nigeria inachuana na Ufaransa katika mechi ya muondowano siku ya Jumatatu baada ya kuchukua nafasi ya pili katika kundi lao la F.


Shirika la habari la BBC michezo limeelezwa kuwa shida imetokea katika ufafanuzi wa njia itakayotumika kuwalipa wachezaji hao pesa hizo za ziada.


Wachezaji hao wanaamini kuwa watapokea dola 10,000 kwa ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Bosnia-Hercegovina na dola 5,000 kwa sare yao dhidi ya Iran.


Wachezaji hao pia wanadhania kuwa wanapaswa kulipwa dola 30,000 kwa kufuzu katika kundi hiyo.


Hata hivyo, inaaminika kuwa ahadi hiyo ya shirikisho la soka la Nigeria kwa wachezaji wake ilijumuisha malipo ya ushindi na kutoka sare na pia asilimia 30 ya pesa watakazolipwa na Fifa kwa kufika katika raundi ya muondowano.


Inaaminika kuwa kitita hicho kinatarajiwa kupanda hadi asilimia 40 kama fedha watakazolipwa na Fifa ikiwa Nigeria watashinda mchuano wao wa raundi ya muondowano, aslimia 50 kwa ushindi wa robo fainali, asilimia 60 kwa ushindi katika nusu fainali na asilimia 70 kwa kushinda kombe hilo la dunia.


Huku Wahusika wote wakifanya juhudi za kupata suluhu ya mtafaruko huo , mkufunzi, Stephen Keshi anasisitiza kuwa swala hilo halitakuwa na madhara yoyote katika timu hiyo.


BBC pia imethibitishiwa kuwa wachezaji hao watasafiri kwenda Brasilia siku ya Ijumaa kama ilivyoratibiwa na kufanya mazoezi yao jioni itakayofuata.

Si mara ya kwanza timu ya Super Eagles kuchukua msimamo kama huo kuhusu fedha.


Mwaka uliopita walichelewa kufika katika michuano ya kombe la mashirika huko Brazil.

MORAVIAN WAPINGA HUDUMA YA WACHUNGAJI MASHOGA

HALMASHAURI Kuu ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Misheni Mashariki, limetoa tamko la kutounga mkono maazimio ya Kanisa la Moravian Jimbo la Marekani ya Kaskazini lililoruhusu huduma ya wachungaji mashoga na wasagaji.


Juni 22 mwaka huu, Sinodi ya Kanisala Moravian Jimbo la Amerika ya Kaskazini imeruhusu watu wenye uhusiano wa jinsia moja kubarikiwa katika daraja takatifu la uchungaji pamoja na kuruhusu viapo vya ndoa za jinsia moja kufungwa kanisani.


Katibu Mkuu wa Jimbo hilo, Mchungaji Emmaus Mwamakula alisema kuwa kanisa lake haliungi mkono maazimio hayo kutokana na kuwa vitendo hivyo ni kinyume na misingi, imani na mafundisho ya Kanisa la Moravian."


Kanisa limepata mashangao mkubwa taarifa za Sinodi ya Kanisa Moravian Jimbo la Amerika ya Kasikazini, ya kuruhusu huduma ya wachungaji mashoga na wasagaji na ndoa za jinsia moja kufungwa kanisani.


"Biblia Takatifu inatamka wazi vitendo vya ushoga na usagaji ni chukizo mbele za Mungu na watu wanaotenda hawataurithi ufalme wa Mungu na pia ni kinyume na tamaduni na imani ya kikristu na kuwa mamlaka ya mwisho kuhusu imani ni neno la Mungu (Biblia),"alisema.


Alisema kuwa kutokana na maazimio hayo ambayo ni chukizo mbele za Mungu, kanisa lake linasitisha uhusiano na Jimbo ya Amerika ya Kaskazini na kuwaombea ili viongozi wake wafikie hatua ya kufikiria toba.


Mwamakula alitoa wito kwa wakristo wa Mashariki na majimbo mengine ya kanisa hilo hapa nchini, kukataa kwa namna zote ushoga na usagaji pamoja na kuwakataa viongozi wanaoshikana na watu waliohalalisha ushoga katika majimbo yao.

KOBE WAZUA TAHARUKI DAR

HALI ya taharuki ilizuka jana katika eneo la Tabata Mawenzi jijini Dar es Salaam baada ya kobe wadogo zaidi ya 300 kuonekana katika maeneo hayo huku wakiwa hawajulikani walipotokea.


Kobe hao walikutwa katika shamba la Hassan Msumi wakiwa wametapakaa eneo zima la shamba hilo kana kwamba kuna mtu alifika na kuwamwaga eneo hilo.


Akizungumzia tukio hilo, Msumi alisema jambo hilo linastaajabisha kwani ameishi katika maeneo hayo tangu miaka ya 1980 lakini hakuwahi kuona kobe hata mmoja.


"Inashangaza sana kwa sababu tangu tumeanza kuishi katika maeneo haya hatujawahi kuona kobe, tunajiuliza hawa wametokea wapi lakini hatuna jibu," alisema Msumi.


Msumi alisema asubuhi ya jana wakati baadhi ya watu wakienda kuchota maji katika kisima kilichopo ndani ya shamba hilo, mdogo wake wa kike aliwaona kobe hao na ndipo alipomuita ili aje kushuhudia.


Alisema wakati akijiandaa kutoka kuna muokota chupa za plastiki alikuwa anapita jirani na shamba hilo, baada ya kuwaona alimwaga chupa na kuanza kuwaokota kobe hao.


"Kuna 'teja' alikuwa anaokota chupa lakini alipowaona hawa kobe alimwaga machupa yake yote akaanza kuwaokota na wakati mimi natoka ndani alikimbia," alisema.

Alisema mtu huyo alifanikiwa kuondoka na kobe hao wakiwa wamefikia nusu ya kiroba hicho alichokuwa amekibeba.


Aliongeza kuwa walianza kuwakota kobe waliobaki na kuwakusanya sehemu moja ambapo idadi yao ilifikia 338 huku aliokimbia nao mtu huyo idadi yake ikiwa haijulikani.

Inasemekena alioondoka nao idadi yake inaweza kufikia 300.

Msumi alisema baada ya kuwakusanya kobe hao alichukua hatua ya kutoa taarifa kwenye Idara ya Wanyamapori ili waje kuwachukua baada ya baadhi ya vijana kuanza kuwapiga kwa mawe.


Hata hivyo Msumi alisema baada ya kobe hao kuchukuliwa, wengine walianza kuonekana mmoja mmoja ambapo watu wa eneo hilo walikuwa wakiwakusanya.


Wakazi wengi wa eneo hilo walikusanyika kuwashangaa kobe hao na kujiuliza walipotokea bila kuwa na majibu.


Ofisa mmoja wa Idara hiyo ya Maliasili ambaye alikataa kunukuliwa kwa kuwa si msemaji alisema, kitendo kilichofanywa na watu hao ni cha kiungwana kwani wangeweza kuwaficha na kutafuta wateja kwa ajili ya kuwauza.

Alisema kwa mujibu wa Sheria za nchini hairuhusiwi mtu kumiliki kobe ila ni mali ya serikali.


Kwa kawaida kobe jike huchimba kiota na kutaga mayai ndani yake nyakati za usiku na kufunika kwa udongo, mchanga au vitu vya organi ambapo hukaa kwa siku 60 hadi 120 na kutotolewa.


Kobe mmoja anaweza kutaga mayai kati ya moja hadi 30, na inasemekana kuwa kobe anaishi maisha marefu kuliko wanyama wengine, wapo wanaoishi maisha zaidi ya 150 .

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA ASKARI NA MGAMBO AKAMATWA ZANZIBAR

MAKACHERO wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wamefanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa hatari wa mauaji ya askari Polisi mmoja na askari mgambo katika kituo cha polisi Kimanzichana Mkuranga Mkoani Pwani.


Mtuhumiwa huyo ni Hamisi Othman Mzee maarufu kwa jina la Hamisi Mabunduki(44), Mkazi wa Zanzibar na Dar es Salaam.


Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba, Juma Yusuf Msige alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kijiji cha Matale wilaya ya Chakechake akiwa mafichoni.

Kamanda Msige alisema Polisi inawasiliana na wenzao wa Mkoa wa Pwani kwa upelelezi zaidi.


Katika uvamizi wa kituo na mauaji, majambazi hayo yaliwaua Koplo Joseph Ngonyani na Mgambo Venance Mushi aliyekuwa akisaidia ulinzi kituoni hapo kabla ya kupora silaha zaidi.


Kamanda Msige alisema taarifa za kiintelijensia zinaonesha kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni hatari amekuwa akikabiliwa na kesi lukuki za matukio ya ujambazi wa kutumia silaha na alitoka rumande Mei 28 mwaka huu.


Tangu wakati huo mtuhumiwa huyo na genge lake amekuwa akiendeleza matukio ya kihalifu yakiwemo ya uporaji na mauaji katika mikoa mbalimbali.


Kamanda Msige alisema polisi wanaendelea na upelelezi ikiwa ni pamoja na kupata taarifa muhimu za watuhumiwa wengine wanaojificha ili watiwe mbaroni kukabili mkono wa dola.

KATIBU MKUU AMTISHIA KAFULILA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi ameibuka na kuzungumzia sakata la kuitwa Mwizi na Mbunge wa Kigoma Kusini,David Kafulila (NCCR –Mageuzi )na kumtaka kama ana ubavu azungumzie nje ya Bunge.


Akizungumza na Waandishi wa habari jana kuhusu Serikali kupitisha Mkakati na Mwelekeo wa Sekta Ndogo ya Umeme (ESI), alisema wabunge wamekuwa wakizungumzia masuala hayo ya kashfa bungeni kutokana na kuwa na kinga.

"Kama ana uhakika wa jambo hilo kuwa mimi ni mwizi aje aseme hadharani kama ilivyo hapa na siyo ndani ya Bunge, aone kama sijamfikisha mahakamani, kwani akiwa ndani ya Bunge anajifanya mwanaume kweli kumbe m***'," alisema.


Alisema kuwa kuna unafiki umejaa na unaenezwa kwa vipeperushi na kushabikiwa na baadhi ya waandishi wa habari wakidai kuwa anahusika na ufisadi wa zaidi ya Sh bilioni 200 katika akaunti ya Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).


Maswi alisema yeye binafsi anajiamini hachukui rushwa hivyo anaruhusu yeyote anayetaka kupata uhakika amfuatilie na yeye atawaonyesha jinsi alivyopata mali zake zote .

"Njooni nitawaonesha nilivyopata mali zote nilizonazo na yeye Kafulila kama mwanaume kweli aseme nje ya bunge kwani atanitambua nitakavyo mshughulikia, t***i kweli yule,"alisema.


Alipoulizwa anadhani ni kwa nini Kafulila amekuwa na nguvu za kumtaja hadharani kama anahusika na tuhuma hizo, Maswi alimtaka Kafulila na wabunge wengine kutotumia bunge kusema uongo kwa kuwa wana kinga bali watoe ushahidi wa wizi wanaoujua.


Maswi alisema pia anamjua Kafulila na hawezi kusimama na kusema hadharani anayotamba bungeni kwani kutokana na kuwa sio mwanasiasa na amelelewa na anajua maadili.


"Kama hakulelewa vizuri, atalelewa na dunia kama wahenga walivyosema kwani nina usongo naye sana kwa kuwa najua ana makaratasi ya kufungia vitumbua na kudai ni ushahidi jambo ambalo serikali haitishiwi,"

alisema Maswi alikuwa akijibu hoja za Kafulila, baada ya kuulizwa na waandishi wa habari ni jinsi gani watakabiliana na matumizi mabaya ya fedha katika wizara hiyo wakati wa uboreshaji wa sekta ya umeme.

ISRAEL YAONYWA KUHUSU KUWATAFUTA VIJANA WA 3 WALIOTEKWA

Umoja wa Mataifa umeishauri Israel ijizuie wakati inapowatafuta vijana 3 raia wa nchi hiyo waliotoweka tangu Juni 12 Ukingo wa Magharibi. Afisa wa umoja huo ameonya juu ya kutokea mapinduzi mapya dhidi ya Israel.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya siasa, Jeffrey Feltman, amelionya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba msako unaofanywa na Israel katika maeneo ya Wapalestina yumkini ukazusha machafuko zaidi katika eneo hilo. Feltman amesema, na hapa namnukuu, "Wakati Israel ikiwatafuta vijana hawa tunahimiza ijizuie katika kufanya operesheni zake za usalama kwa kufuata sheria za kimataifa," mwisho wa kumnukuu.
Akilihutubia baraza la usalama Jumatatu (23.06.2014) wakati wa mkutano wa kila mwezi kuhusu Mashariki ya Kati, Feltman amesema, "Ongezeko la vifo kutokana na operesheni ya usalama ya Israel katika eneo la Ukingo wa Magharibi linatisha. Tunalaani mauaji ya raia na tunataka kufanyike uchunguzi. Tunaitaka Israel ijiepushe kuwaadhibu watu kwa makosa ambayo kibinafsi hawajayafanya."
Feltman pia amesema hali ni mbaya mno na anahofia huenda kukazuka mapinduzi ya tatu ya intifada dhidi ya Israel.
Bildergalerie Israel Konflikte Wazazi wa mmoja wa vijana wanaotafutwa, Gil-Ad
Hatua ya Israel kuwaadhibu Wapalestina wakati wa zoezi la kuwatafuta vijana hao katika Ukanda wa Gaza imezua ghadhabu miongoni mwa Wapalestina, ambao wameonya tukio hilo linatumiwa kwa masilahi ya kisiasa.

Operesheni yaibua wasiwasi
Hani al-Masri, mwandishi wa habari wa Kipalestina na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, anasema, "Kuendelea kuratibu operesheni ya usalama kati ya Wapalestina na Waisraeli katika mazingira haya kunaifanya mamlaka ya ndani ya Wapalestina kuwa mshirika na dola inayoyakalia maeneo yake. Na ni mbaya sana kwa uaminifu na uhalali wa mamlala hiyo.
Mzozo huo umeibua hali ya wasiwasi katika Ukingo wa Magharibi, ambao pamoja na Jerusalem Mashariki na Ukanda wa Gaza, Wapalestina wanataka liwe taifa lao la siku za usoni. Msemaji wa kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza, Mushir al Masri, ameonya dhidi ya msako wa Israel kutumika kusababisha uhasama kati ya kundi hilo na chama cha Fatah.
"Tunachotakiwa kufanya sasa ni kuendelea mbele na mchakato wa maridhiano kati ya pande hizi mbili bila kujali ushawishi mbaya kutoka kwa Israel. Tuna matumaini Fatah na Hamas hawatazuiwa na Israel na hawatoacha kabisa mchakato huo wa maridhiano."
Israelische Militäraktion im Westjordanland Wapalestina mjini Nablus na maiti ya kijana aliyeuwawa na Israel katika operesheni
Jeshi la Israel limesema limewatia mbaroni Wapalestina wengine 37 usiku wa kuamkia leo huku ikiwatafuta vijana hao na kutanua harakati yake dhidi ya kundi la Hamas, ambalo limeknusha kuwa na taarifa kuwahusu vijana hao wasiojulikana waliko. Jeshi la Israel aidha limesema linawazuia watu 361 tangu wanafunzi hao walipotoweka Juni 12, na limetuma vikosi zaidi vya wanajeshi kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi tangu Juni 13 kuwatafuta vijana hao watatu wa Kiisraeli waliotoweka karibu na mji wa Hebron.

TRAFIKI MARUFUKU KUVIZIA

SERIKALI imepiga marufuku tabia ya askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, kuvizia magari katika barabara kuu wakiwana kifaa cha kupima mwendo kasi wa magari.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Peraira Silima, alisema tabia hiyo ya trafiki ni kinyume chasheria na zinaweza kusababisha ajali.


Hata hivyo, Silima aliwataka madereva kutii Sheria za Barabarani ikiwemo kupunguza mwendokasi na kufafanua kuwa, wakati mwingine askari hutafuta kivuli na hatua hiyo isichukuliwe kuwa wanavizia magari.


Katika swali lake, Ngoye alitaka Serikali ieleze ni hatua gani zimekuwa zikichukuliwa kuhakikisha madereva wanafuata sheria zilizowekwa kama inavyofanyika katika nchi nyingine.


Ngoye pia alitaka Serikali ieleze kwa nini madereva wameendelea kutumia magogo, mawe na majani yenye miba barabarani kuashiria kuwa kuna gari limeharibika, na wakiondoka wanayaacha na wengine wameendelea kuendesha magari huku wakisikiliza simu.


Naye Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema), alihojikama ni sahihi kwa trafiki kuvizia magari na kifaa cha kupima mwendo kasi.

ARFI: JIMBO KWANZA, CHADEMA BAADAE

SIKU moja baada ya Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Amour Arfi (Chadema) kushangaza kambi ya upinzani kwa kupiga kura ya kuunga mkono Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015, mwenyewe amesema amefanya hivyo kwa ajili ya jimbo lake na si kutanguliza maslahi ya Chama chake kama wafanyavyo wabunge wengine.


Arfi aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa na nafasi hiyo kujiuzulu mwaka huu, aliunga mkono bajeti hiyo akiwa ni miongoni mwa wabunge wanne waupinzani na kusababisha kushangiliwa kwa nguvu na wabunge wa CCM.


Wengine waliounga mkono Bajeti hiyo ambapo hata bajeti hii ya mwaka 2013/2014 inayomalizika waliiunga mkono na vyama vyao kwenye mabano ni Mbunge wa Vunjo Augustino Mrema(TLP), John Cheyo wa Bariadi Mashariki(UDP) na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed(CUF).


Katika bajeti hiyo inayoanza kutekelezwa Julai mwaka huu, wabunge 234 walipiga kura ya Ndiyo na wabunge 66 wakiikataa bajeti hiyo ya Sh trilioni 19.8. Wabunge 54 hawakuwepo bungeni.

Idadi kamili ya wabunge ni 357.


Akizungumza na gazeti hili jana baada ya kuulizwa sababu ya kwenda kinyume na kambi ya upinzani na kuwa Mbunge wa kwanza kuunga mkono Bajeti ya serikali, alitoa sababu kadhaa ambazo ni pamoja na kuridhishwa na serikali katika kutatua kero nyingi za jimboni kwake pamoja naWaziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum kutatua kero za muda mrefu.


"Nikiwa kama Mwakilishi nina mambo matatu makuu ya kusimamia pamoja na kuwasemea watu, la kwanza ni Jimbo langu, pili Nchi yangu na tatu Chama changu (Chadema).

Katika haya matatu kwa bajeti hii niliamua kwa ajili ya jimbo langu tofauti na wengi wanaotanguliza vyama vyao kuliko majimbo na nchi yao,"alitetea uamuzi wake wa kuunga mkono Bajeti hiyo.


Arfi ambaye anaamini kitendo cha kuunga mkono bajeti hiyo ni kudumisha utamaduni wa demokrasia kuchukua mkondo wake wa kukubaliana na kutokubaliana, alisema ameridhishwa na majibu yaliyotolewa na Waziri wa Fedha kwa maana alivyoweka bayana katika yale anayoamini ikiwemo misamaha ya kodi ambayo imekua kero ya muda mrefu.


"Pia utayari wake(Waziri) wa kujipunguzia mamlaka ya kutoa misamaha jambo ambalo watangulizi wake walishindwa. Pia kwa namna alivyohimiza ukusanyaji wa mapato na nidhamu ya Bajeti na hususan kukabiliana nawakwepa kodi na wale ambao wanadhani hawawezi wafunge biashara zao,"alifafanua.


Sababu nyingine ambazo ni majibu ya matatizo mengi ya jimbo lake lauchaguzi ni kuendeleza na kukamilisha mradi mkubwa wa Maji wa Ikolongo ambao tayari mabomba katika kilometa 46 yametandi kwa jambo ambalo anaamini litamaliza kabisa tatizo la Maji jimboni kwake na kuingizwa katika mpango wa serikali wa ujenzi wa barabara za lami kufungua Mkoa wa Katavi yaani Mpanda-Tabora na Mpanda-Kigoma.


Majibu ya matatizo mengine ni kuwepo kwa fedha za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa Mpanda Mjini, kuondoa tatizo la Umeme Mpanda kwa kupeleka jenereta mbili mpya na kupeleka umeme katika vijiji vyote katika jimbo lake pamoja na kuwepo kwa fedha kwa ajili ya reli ya Kaliua hadi Mpanda na mpango wa kuendeleza kazi hiyo hadi Karema.


Arfi alisema "utatuzi mwingine wa kero ni Mji wa Mpanda kuwemo katika Mpango wa Maendelezo ya Miji ambapo tutapata fursa nyingi, Mji kupimwa vyema na uwepo wa miundombinu bora katika Mji wa Mpanda".


Chanzo: Habari Leo

MUNTARI NA BOATENG WATIMULIWA TIMU YA TAIFA

Wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana Sulley Muntari na Kevin Prince Boateng wamefukuzwa katika timu hiyo kwa ukosefu wa nidhamu.

Taarifa kutoka mtandao wa shirikisho la soka nchini humo imesema kuwa wawili hao wametimuliwa mara moja.

Boateng anayechezea kilabu ya Schalke 04 amefukuzwa kwa kutoa matamshi machafu yaliomlenga mkufunzi wa timu hiyo Kwesi Appiah wakati timu hiyo ilipokuwa katika mazoezi katika eneo la Maceio.

Naye mchezaji wa AC Milan Sulley Muntari ameadhibiwa kwa kumshambulia afisa mmoja wa kamati kuu ya timu hiyo.

Shirikisho la soka nchini Ghana limeongezea kwamba kisa kinachomuhusu Muntari kilitokea siku ya jumanne na kumtaja Moses Armah, mwanachama wa usimamizi wa timu hiyo kamamtu aliyeshambuliwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.

Wakati huohuo Boateng amedaiwa kutojali matamshi aliyoyatoa.

Habari hizo zinajiri siku moja baada ya serikali ya Ghana kutuma dola millioni 3 nchini Brazil ili kuwalipa wachezaji wa timu hiyo nchini Brazil fedha zao za kushiriki katika michuano ya kombe la dunia.

Timu hiyo inayojulikana kama Black Stars ilikuwa imetishia kususia mechi kati yake na Ureno iwapo haitapewa fedha hizo swala lililoilazimu serikali kuingilia kati.

Ghana ina nafasi ya kufuzu katika michuano ya mchujo iwapo itaishinda Ureno na iwapo mshindi wa kundi G atakuwa Ujerumani.

GAVANA WA LAMU KENYA AKAMATWA



Polisi nchini kenya wamemtia mbaroni gavana wa jimbo la Lamu lililokumbwa na mapigano hivi majuzi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 65.
Polisi walimshika Issa Timamy,kufuatia tuhuma za kuhusika na mashambulizi yaliyotokea Mpeketoni mapema mwezi huu.
Timamy anatarajiwa kufikishwa mahakamani mjini Mombasa alhamisi.
Punde baada ya tukio hilo rais Uhuru Kenyatta alikatalia mbali madai kuwa ilikuwa shambulizi la kigaidi lililotekelezwa na kundi la waislamu la Al shabab.


Rais Kenyatta alisema kuwa hilo lilikuwa shambulizi lenye misingi ya kikabila na kisiasa.
Kundi la wapiganaji kutoka Somalia Al shabab lilidai kutekeleza shambulizi hilo.
Bwana Timamy ni Gavana wa pekee kutoka chama cha UDF .


Rais Kenyatta alipinga kuhusika kwa Al shabab kwani wengi waliouawa walikuwa wa jamii ya wakikuyu jamii anayotoka rais Kenyatta .
Aidha wavamizi waliwalenga wanaume ambao hawakuwa waislamu na kuwataka kukariri shahada ama aya za Quran,wale walioshindwa walikuawa .
Siku ya jumatano maafisa wa utawala katika jimbo hilo la Lamu walidai kuwa wamewakamata watu 13 waliokuwa wakipanga njama ya kufanya uvamizi zaidi.

JESHI LA POLISI KAGERA LAUWA MAJAMBAZI

Jeshi la polisi mkoani Geita limefanikiwa kuwauwa watu wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi baada ya kupora na kufanya mauaji ya mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Gosbert Walwa katika eneo lake la biashara.

Ni majira ya saa kumi na mbili kasoro robo watu wanaosadikika kuwa ni majambazi walivamia duka la wakala wa vinywaji ambapo walipora fedha kiasi cha shilingi millioni moja na laki nane na bastola moja aina ya piyutro bereta yenye namba h 04788 yenye usajili wa namba 5808 iliyokuwa inamilikiwa na Ignas Athanas na hatimaye kwenda katika vibanda vya huduma za fedha kwa njia ya simu majira ya saa kumi na mbili na kupora fedha kiasi ambacho hakijafahamika na kufanya mauaji.

Baada ya masaa mawili kwa ushirikiano wa wananchi na jeshi la polisi, majambazi waliuwawa katika msitu wa miyenze kilomita hamsini na nane kutoka Geita mjini,mafanikio ya kuwadhibiti wahalifu hao yamewafurahisha wananchi na kuahidi kutoa ushirikiano, barabara za mji zilifurika watu mbalimbali wakishangilia vifo vya majambazi hao na kulipongeza jeshi la polisi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Acp Joseph Konyo amewataka wananchi kuendeleza ushirikiano uliopo kwa jeshi la polisi ambapo baadhi ya wananchi wameahidi kutoa pikipiki mpya kumi na mbili na zaidi ya shilingi millioni tatu kama sehemu ya kulipongeza jeshi hilo.

FIFA KUMSHITAKI SUAREZ KWA KUMNG'ATA CHIELLINI

FIFA imemshitaki Luis Suarez kwa kumng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini kwenye mechiya Kombe la Dunia, suala ambalo linaweza kumsababishia mchezaji huyo wa Uruguay kufungiwa kucheza mashindano ya kimataifa kwa miaka ipatayo miwili.
Siku ya Jumatano, chombo hicho kinachosimamia mpira wa miguu kilisema kuwa kamati yake ya nidhamu imefungua jalada dhidi ya Suarez, ikiwa ni masaa machache baada ya kuisha kwa mechi mjini Natal.
Maafisa wa Uruguay wameombwa kuwasilisha ushahidi wao saa 2 usiku leo Jumatano.
Suarez, ambaye ameshawahi kusimamishwa mara mbili kwa kung'ata wachezaji, alipigwa picha hivi karibuni akimng'ata Chiellini begani, kabla hajajiangusha chini na kupiga uso wake.
Mwamuzi Marco Rodriguez wa Mexico hakuona tukio hilo na hakufanya chochote.

Hatahivyo, FIFA wana uwezo wa kulishughulikia, "ufunjwaji sheria ambao haukuweza kuonekana kwa maafisa wa michezo", ilieleza taarifa ya FIFA.
Suarez anaweza kufungiwa kwa miaka miwili kama atakutwa nakosa akimshambulia mpinzani.
Uamuzi utatangazwa kabla ya Jumamosi, ambapo Uruguay itacheza na Colombia kwenye hatua ya mtoano kwenye uwanja wa Maracana.





WALIO MUUA SISTER KUSAKWA KILA KONA

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imeanzisha msako mkali, kuwatafuta watu waliohusika na mauaji ya Mhasibu wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makoka jijini Dar es Salaam, Sista Cresencia Kapuri (50), ambao utahusisha vikosi vyote vya Polisi. Vikosi hivyoni Usalama Barabarani, askari wa doria wanaotumia pikipiki na magari, wapelelezi na askari Polisi wa kawaida.


Mauaji ya mtawa huyo, yalitokea juzi mchana katika eneo la UbungoRiverside, jijini humo, ambapo alipigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi na kumpora Sh milioni 20 pamoja na nyaraka mbalimbali za ofisi.


Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliwaambia waandishi wa habari ofisi kwake jana kuwa Sista Cresencia wakati anapigwa risasi, alikuwa ameongozana na wenzake, ambao ni Sista Brigita Mbaga (32) na dereva wao Mark Mwarabu, aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Hilux Pick-Up, yenye namba T213 CJZ.


Kova alisema wakati watawa hao, wakitoka katika Benki ya CRDB Tawi la Mlimani City, walipofika Ubungo Riverside kulipa deni la chakula katika duka la Thomas Francis, ndipo walitokea watu hao wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa na pikipiki, ambayo haikusomeka namba, hukummoja akiwa na bunduki aina ya SMG.


"Yule dereva wa gari la masista walimpiga risasi katika kidole gumba cha mkono wa kulia na kisha kumpiga mtawa huyo risasi ya kifuani na kupora kiasi hicho chafedha na nyaraka hizo," alisema Kova.

Alisema kuwa jambo kubwa walilogundua ni kuwa matukio mengi ya ujambazi, hasa unaohusisha wananchi kuporwa kiasi kikubwa cha fedha, yanaanzia katika mabenki, hivyo kuna uwezekano wa watu ambao si waaminifu, wanafanya uhalifu huo.


Alisema kuwa katika matukio ya aina hiyo, majambazi huwafuatilia wateja wanapoingia au kutoka katika benki mbalimbali.

Alisema imeonekana kwamba mara nyingi benki, zinapohitaji kusafirisha pesa nyingi, hutumia askari au taasisi nyingine za usalama kusafirisha fedha zao."

Tunawaomba mameneja wa benki zote, kuhakikisha yanawahimiza wateja wake kutumia njia mbadala za kusafirisha pesa nyingi, kama vile matumizi ya hundi, kufanya miamala bila kadi, matumizi ya kadi za kutolea fedha (ATM) na njia nyingine ambazo ni salama.


"Matukio kama haya, yanaonesha ni wazi huu utaratibu wa watu kutoa pesa nyingi kutoka benki na kwenda kufanya malipo si salama. Kuna baadhi ya huduma, kwa mfano kuna baadhi ya nchi ambazoni sheria mtu haruhusiwi kutembea na fedha nyingi, kwa hiyo ni muhimu kwa sisi wenyewe tukajielewa kwanza," alisema Kova.

Alisema pia wanaomba mameneja wa benki, kuhakikisha benki zao zinakuwa na kitengo maalumu cha ushauri wa masuala ya usalama kwa wateja wao.


Alifafanua kuwa kama mteja atafika katika benki zao na akahitaji kutoa fedha nyingi ni vyema wakamshauri ;na kama atakaidi, benki ichukue hatua ya kutaarifu Polisi.


Aidha, alitaka wafanyabiashara na taasisi mbalimbali, zisitumie njia za mkato katika usafirishaji na uhifadhi wa pesa zao kwa faida ya usalama wa maisha na mali zao.Aidha, Kova alisema katika kukabiliana na uhalifu wa aina hiyowa kutumia pikipiki, wamezikamata pikipiki 668, ambazo wanazitilia shaka na wanazifanyia ukaguzi zaidi.

Pia, zipo ambazo zimekamatwa kuhusiana na makosa mengine ya barabarani.

BENKI YA DUNIA YAONYA ONGEZEKO DENI LA TAIFA

BENKI ya Dunia imeonesha wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa deni la taifa kutokana na Serikali kuendelea kukopa mikopo ya biashara ya ndani hadi kuzidi kiwango kilichowekwa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa asilimia 1.2 ya Pato Halisi la Taifa (GDP).

Hali ya uchumi wa Tanzania iliyotolewa jana na taasisi hiyo, imeonesha nchi imefanya vibaya zaidi katika maeneo ya mauzo ya nje, kushuka kwa nakisi ya fedha yajumla, kushindwa kwa Serikali kukusanya mapato pamoja na ongezeko la ukosefu wa ajira kwa vijana.


Ripoti hiyo iliyobatizwa jina la 'Nanianataka kazi? Nguvu ya Mvutano wa Majiji' imeeleza kuwa Tanzania imeonesha utendaji mbovu zaidi wa mauzo ya nje tangu mwisho wa miaka ya 1990.

Jambo lingine la kutia wasiwasi zaidi ambalo limetajwa na ripoti hiyo ni kwa nakisi ya fedha ya jumla kushuka hadi viwango vilivyosawa na asilimia 6.8 ya GDP katika mwaka 2012/13.

Ripoti hiyo inasema huo ulikuwa niupungufu mkubwa zaidi tangu mdororo wa uchumi wa dunia mwaka 2008/9.


Katika eneo la mikopo, ripoti hiyo ilieleza kuwa thamani ya mikopo ilikuwa juu zaidi kwa asilimia 1.2 ya GDP kuliko lengo lililokubaliwa na Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Mikopo hiyo ripoti inaeleza kuwa haikutosha kuziba pengo la fedha kutokana na deni kubwa la nyuma ambayo thamani yake ni karibu asilimia 4 ya GDP hadi ilipofika Juni 2013.


Ripoti hiyo pia imeeleza kuwa roboza mwanzo za mwaka 2013/14 Serikali ilikusanya mapato yake kwa asilimia 82 tu ya lengo la mapato hali iliyosababisha Serikali kupunguza au kuahirisha utekelezaji wa baadhi ya programuza uwekezaji, manunuzi ya bidhaa na huduma.

Pamoja na kuchukuliwa hatua hizo, ripoti imebainisha kuwa thamani ya deni la taifa iliendelea kukua hadi kufikia karibu asilimia 5 ya GDP mwishoni mwa Machi 2014.


Deni hilo halijumuishi malimbikizoya taasisi za Serikali ikiwemo Tanesco na wagavi wake. Ripoti hiyo inasema iwapo madeni hayo yatajumuishwa inaweza kuongeza hesabu ambayo ni sawa na asilimia2 ya GDP kwenye jumla ya thamani ya deni la Serikali.

Uchumi na Ajira Ripoti hiyo imebainisha kuwa idadi ya watu ambao hawana kazi zinazowapatia kipato cha kutosha kuweza kujikimu juu ya mstari wa umasikini inazidi kuongezeka.


"Hatari kubwa ni kwamba wafanyakazi wengi wa mashambaniwanazidi kukimbia kutoka kwenye kilimo kwenda katika biashara za kujikimu zilizoko mijini," inasema ripoti hiyo.

Pia imebainisha kuwa wakati kuna kampuni kubwa zenye mafanikio katika maeneo ya mijini, kiwango kikubwa cha ajira katika maeneo hayo hutolewa na biashara ndogo ndogo zisizokuwa za kilimo ambazohazina tija ambazo zinakosa uwezo wa kupanuka na kuwa shindanishi.


Kuhusu biashara, ripoti ilisema biashara nyingi za mijini ni zile ndogo ndogo ambazo sio rasmi na sio za kitaalamu na huendeshwa nawenye mali ambao wana ujuzi mdogo.

Wamiliki wa biashara hizo, ripoti imewataja kuwa ni wajasiriamali wasio na ari na wanaendesha biashara hizo kwa kuwa tu hawana njia nyingine ya kujikimu kutokana na biashara hizo kutokuwa na faidakubwa.


Pinda azungumza ajira Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo kuwa idadi ya watu wanaoishi mijini inaongezeka hadi kufikia watu milioni 13.3 wengi wao wakiwa vijana ambao wanaenda kusaka ajira.

Pinda alisema hata hivyo vijana hao ambao asilimia 78 hawana elimu yenye ujuzi wanakosa ajira.


Alisema sababu kubwa ya vijana kwenda mijini ni kutokana na kilimo kutowapatia tija hivyo kuamini kuwa mijini kuna maisha mazuri zaidi.

Alisema Serikali inashughulikia tatizo hili la kuhakikisha vijana wanaohitimu shule za msingi na sekondari wanakuwa na ujuzi utakawawezesha kuendesha shughuli halali za kuwapatia kipato.


Alisema licha ya kuwepo vyuo vya ufundi lakini wanafunzi wanaosoma kwenye vyuo hivyo bado ni wachache.

Waziri Mkuu alikiri kuwa takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu zinaonesha kuwa jumla ya watu milioni 2.4 hawana ajira na wengi wao ni vijana ambao wamekimbilia mijini.


Alisema Serikali inazo changamoto za kuweka miji yake iweze kukidhi mahitaji ya ajira, lakini akasema bado Serikali inashughulikia suala hilo.

Benki ya Dunia yaasa Mtunzi Mkuu wa ripoti hiyo Jacques Morisset, alisema kuna haja ya haraka kwa Serikali kushughulikia changamoto wanazokabiliana nazo wajasiriamali wadogo katika miji ya Tanzania.


Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi na Uganda, Philippe Dongier alisema licha ya uchumi wa Tanzania kukua;lakini umeshindwa kutengeneza ajira za kutosha zenye tija kwa nguvu kazi inayokua kwa haraka.

"Leo hii kuna Watanzania milioni 23 ambao wako katika soko la ajira, watafikia milioni 45 ifikapo mwaka 2030 wakiwa na matumainimakubwa ya kazi zenye heshima na maisha mazuri," alisema Dongier.


Chanzo: Habari Leo

CHADEMA WAMKALIA KOONI SILAA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimempa siku 21 Diwani wa Ukonga, Jerry Silaa, kutoa maelezo ziliko fedha za ujenzi wa ofisi ya kata zaidi ya sh. milioni 175.

Chama hicho kimesema endapo Silaa ambaye pia ni Meya wa Manispaa yaIlala hatafanya hivyo, kitaungana na wananchi na kufanya maandamano kuelekea Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ilala kudai haki yao.


Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Katibu wa CHADEMA Jimbo la Ukonga, Juma Mwipopo, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Stendi, Gongolamboto.

Alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa katika kipindi cha miaka miwili haijulikani fedha hizo zimepelekwa wapi huku kata hiyo ikiendelea kupanga kwenye nyumba ya watu.


"Ni jambo la kushangaza kusikia ofisi inajengwa, lakinisisi tunajua hata kiwanja kwa ajili ya ujenzi huo hakipo, ndiyo maana tunamtaka Silaa atuambie unafanyika katika kiwanja kipi au fedha hizo wamezipeleka wapi," alisema.

Mwipopo, alisema akiwa Mwenyekiti wa Maendeleo wa Kata, meya huyo, amekuwa mstari wa mbele katika uvunjaji wa kanuni ya majukumu ya udiwani inayomtaka kutoa taarifa kwa wapiga kura kuhusu fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

WASAKWA KWA MAUAJI NA KUFUKIA MAITI

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kadavashari, amesema jeshi hilo linawasaka watu watatu kwa tuhuma za kumuua na kumfukia Mbaya Lukondia (36), mwanakijiji wa Kabunde, Kata ya Mamba wilayani Mlele, Mkoa wa Katavi.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ubakila Kidakira, Jimon Dogi 'Lala' na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Omary, wakazi wa Kijiji cha Kabunde.

Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari,kabla ya kifo hicho Lukondia alitoweka nyumbani kwake Aprili mwaka huu hadi Juni 19 mwili wake ulipogundulika ukiwa amefukiwa aridhini huku ukiwa umeharibika.

"Baada ya kufukuliwa na kufanyiwa uchunguzi, ilibainika kwamba kabla ya kufa alipigwa na kitu kizito kichwani na ubavuni… watuhumiwa wa mauaji hayo walikimbia kijijini hapo na mpaka sasa hawajulikani walipo,"

alisema kamanda huyo huku akisisitiza kwamba wanatafutwa kwa kuwa walikimbia baada ya mwili huo kuonekana.


Chanzo: Tanzania Daima

AL SHABABU WASHAMBULIA TENA

Takriban watu watano wameuawa katika shambulizi lengine katika eneo la pwani ya Kenya.

Mauaji hayo yametokea karibu na eneo ambako mashambulizi mengine yalifanyika wiki jana na kusababisha vifo vya watu zaidi ya sitini.


Maafisa wanasema kuwa kundi la watu waliokuwa wamejihami walivamia kijiji cha Witu ambacho kiko umbali wa kilomita 15 kutoka mji wa Mpeketoni.

Hakuna aliyedai kufanya mashambulizi hayo hadi kufikia sasa.

Kundi la wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia, al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi ya wiki jana katika mji wa Mpeketoni karibu na Lamu.


Rais Uhuru Kenyatta, hata hivyo aliwalaumu wanasiasa kwa mauaji hayo.

Mkuu wa jimbo la Lamu, Stephen Ikua, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo usiku wa kuamkia leo.


Al-Shabab, lilisema kuwa mashambulizi yao yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa kuwendelea kuwepo wanajeshi wa Kenya nchini Somalia.

Ndege za kivita za Kenya zilifanya mashambulizi mengine dhidi ya kambi za wapiganaji wa Al Shabaab na kuwaua wapiganaji 80 mapema wiki hii.

TBS WAKAMATA SHEHENA YA NGUO ZA NDANI

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekamata shehena ya marobota ya nguo za ndani za mitumba ambazo thamani yake haijajulikana kwa kuwa zimechangaywa na nguo za watoto.
Mkaguzi wa TBS, Donald Manyama alisema wamefanikiwa kukamata nguo hizo juzi bandarini zikiwa kwenye kontena mbili ambapo walilazimika kuongozana na wahusika ambao ni Kampuni ya Dema ili kuufanyia ukaguzi zaidi mzigo huo.
“Katika ukaguzi wetu , tumebaini kwamba marobota haya yanaonekana kama ni nguo za watoto lakini ndani kuna nguo nyingi za ndani za kike na za kiume za wakubwa na watoto za mitumba ambazo zimepigwa marufuku kuingizwa au kuuzwa nchini,” alisema.
Akiwa katika ghala za kampuni hiyo eneo la Mwenge, Dar es Salaam, Manyama alisema kazi ya kuzichambua na kuzitenganisha inaendelea ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
Mfanyabiashara Mussa Kassim wa Kampuni ya Dema katika utetezi wake amedai  kusikitishwa kwake na hali hiyo hasa kwa kuwa wao waliagiza nguo za watoto na siyo za ndani kama ilivyotokea.
“Mitumba hii sisi tunaiagiza kutoka Ujerumani. Hatukuagiza nguo za ndani kwa kuwa siyo kusudio letu wakati Serikali imepiga marufuku. Nafikiri zimechangaywa kwa bahati mbaya,” alisema Kassim. 

MABOMU YATIKISA TARIME

POLISI Kanda maalumu ya Tarime na Rorya Mkoa wa Mara, imelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya wananchi wenye hasira wa mji mdogo wa Sirari.


Wananchi hao walikuwa wakiandamana barabarani kwenda kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Sirari(OCD), huku wakichoma matairi ya magari wakidai polisi kituo cha Sirari wamemuua kwa kipigo mkazi mmoja wa Kitongoji cha Sokoni katika mdogowa Sirari.

Mkazi aliyeuawa alifahamika kwa jina Tandeka Mserega (25), ambaye niyatima.


Maandamano ya wananchi hao yalizimwa jana saa 7 mchana, ambapo maandamano yalianza saa 12 asubuhi.

Maandamano hayo yalisababisha shughuli mbalimbali za kimajii na kiuchumi kusimama kwa muda.

Wakizungumzia maandamano hayo,baadhi ya wananchi jana, walisema yametokana na tukio la Juni 17, mwaka huu, ambapo polisi wa Kituo cha Sirari walimkamata kijana huyo ambaye ni dereva wa bodaboda.


Walisema baada ya kumkamata walimpandisha kwenye kwenye gari la polisi na kuondoka naye kwenda kwenye kituo cha Polisi cha Sirari bila kujua tuhuma yake.


Mmoja wa ndugu zake marehemu,Mariam Kirigiti, alisema kuwa,walifuatilia kituo cha polisi asubuhi sikuya pili, lakini walimkosa ndugu yao.

"Hivyo, tuliamua kwenda Kituo Kikuu cha Polisi cha Tarime nagereza la Tarime, baada ya kushindwa kumpata,"alisema.


Aliongeza kuwa, walifanikiwa kupata taarifa kutoka kituo cha Polisi cha Sirari kwa askari mmoja kuwa, ndugu yao alifariki dunia na mwili wake ulihifadhiwa chumba cha maiti katika Hospitali ya Tarime.

Ndugu hao walitaka kujua kifo chandugu yao, kwani wakati akikamatwa na polisi, alikuwa mzima na hakuwa na tatizo lolote kiafya.


Walidai kuwa, hawakupata majibuya kuridhisha kutoka kwa polisi wakituo hicho, Hivyo waliamua kuweka msimamo hadi waelezwe ukweli.


Msimamo huo, uliwafanya wananchi wa Sirari kuamua kufanya maandamano kwa jazba ya kufunga barabara, kuchoma matairi na kurusha mawe yaliyosababisha baadhi ya polisi akiwamo mkuu wa upelelezi wa kituo hicho kukutana na adha ya mawe hayo.

HAKIMU ALIYEMHUKUMU SADDAM KUNYONGWA NAE ANYONGWA

Hakimu ambaye alimhukumu kifo kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein amekamatwa na kunyongwa na wanamgambo wa ISIS, inadaiwa hivyo.


Raouf Abdul Rahman, ambaye alimhukumu kifo dikteta huyo kwa kunyongwa mwaka 2006, aliripotiwa kuuawa na waasi kwa kulipiza kisasi kwa kuhukumu kunyongwa kwa kiongozi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 69.

Kifo chake hakijathibitishwa na serikali ya Iraq, ila maafisa hawajakataa taarifa za kuhusu kukamatwa kwake na waasi wiki iliyopita.

Anaaminikia kuwa alikamatwa Juni 16, na kuuawa siku mbili baadae.

Mbunge wa Jordan Khalil Attieh aliandika kwenye ukurasa wakewa Facebook kwamba Hakimu Rahman, ambaye aliiongoza Mahakama ya Jinai wakati wa kesi ya Saddam, alikamatwa na kuhukumiwa kifo.


"Wanamapinduzi wa Iraq walimkamata na kumhukumu kifo kwa kile kinachodaiwa kulipiza kisasi kutokana na kifo cha Saddam Hussein", alisema, kulingana na Al-Mesyroon.

Attieh pia alisema kwamba Jaji Rahman alishindwa kutoroka Baghdad akiwa amevaa nguo zamcheza muziki.

NACTE WAFUNGUA OFISI TANO ZA KANDA

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ( NACTE), imefungua ofisi tano za kanda, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa wizara ya kuwekeza katika eneo la usimamizi wa sekta ya elimu nchini kuongeza ufanisi na kufikia Matokeo Makubwa Sasa (BRN).Ofizi hizo na makao yake makuu kwenye mabano ni Kanda ya Kaskazini (Arusha), Kanda ya Ziwa (Mwanza), Kanda ya Kusini (Mbeya),Kanda ya Kati (Dodoma) na Zanzibar.


Katika uzinduzi wa kanda hizo, uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema kanda hizo zitaongeza ufanisi na usimamizi wa elimu ya ufundi nchini.


Alisema Wizara itaendelea kutekeleza mikakati iliyojiwekea kuhakikisha ubora wa elimu unasimamiwa vema na unalindwa hiyo ikiwa ni pamoja na kukabili watoa huduma kwenye sekta ya elimu wasiokuwa makini.


Mkurugenzi Mtendaji wa NACTE , Dk Primus Nkwera alisema ofisi hizo za kanda, zitakuwa na majukumu ya kusimamia na kutekeleza mipango na mikakati ya Baraza na Wizara kwa ujumla katika sekta ya elimu ya ufundi nchini ikiwemo udhibiti na usimamizi wa vyuo vya elimu ya ufundi.

WAWILI KUMKABILI LIPUMBA UCHAGUZI WA CUF

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, na Katibu Mkuu wa chama hicho, Seif Sharif Hamad bado wanahitaji kuendelea na nafasi hizo za uongozi kitaifa baadaya kuchukua fomu kuzitetea katika uchaguzi utakaofanyika wiki hii.

Katika mkutano huo mkuu wa sita wa chama hicho utakaofanyika jijiniDar es Salaam, viongozi hao, Lipumba na Hamad wataachia ngazi kupisha uchaguzi mkuu kufanyika.


Katika hafla maalumu ya kuagana na wajumbe wa Baraza Kuu na watendaji wengine wa ngazi mbalimbali za chama hicho, Lipumba aliahidi kukubaliana na matokeo, iwapo atashindwa na kwamba ataendelea kuunga mkonochama hicho kwa kutoa kila msaada unaostahiki.

"Nilikuwa mwanachama wa kawaida kwa kipindi kirefu ndipo ikafika wakati chama kikaniteua kugombea na kuchaguliwa Mwenyekiti hadi leo, kwa hivyo haki hii anaweza kuwa nayo mwanachama yeyote", alisema Lipumba katika hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwake.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu waCUF, Hamad, alisema kila mwanachama ana wajibu wa msingi wa kukijenga chama bila kujali wadhifa alionao.

Katika hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Profesa Lipumba, Hamad alipongeza wajumbe wa Baraza kwa ushirikiano katika kipindi chote cha miezi 64, hali ambayo alisema imeleta mafanikio makubwa ndani ya chama.

Akizungumza na HabariLeo, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari na Uenezi wa chama hicho, Salim Biman, alisema Lipumba anatetea nafasi ya uenyekiti, aliyoishika kwa zaidi ya miaka 10 sasa akipambana na wenzake wawili.


Alitaja wagombea wengine wa nafasi hiyo ni Chifu Yemba kutoka Shinyanga na M'bezi Adam Bakar kutoka Temeke, Dar es Salaam. Katika nafasi ya Ukatibu Mkuu, Hamad ni mgombea pekee wa nafasi hiyo huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, ikiwaniwa na Juma Duni Haji ambaye pia ni mgombea pekee.

Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Machano Khamis Ali, amesema ameamua kwa hiari yake kutogombea tena, kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo za kiafya Aidha, alisema katika uchaguzi huo, pia kuna nafasi 45 zaujumbe wa Baraza zinazowaniwa.


Kati ya hizo, 20 ni wajumbe kutoka Zanzibar na 25 wajumbe kutoka Tanzania Bara na uchaguzi wa Viti Maalumu.

"Kesho (leo) tunatarajia kuanza mkutano mkuu wa sita wa chama ambao kikatiba ndio mkubwa wenye maamuzi makuu ya mwishoya mambo mbalimbali ndani ya chama, ikiwemo kupitisha wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa ndani wa chama," alisema Bimani.

Alisema mkutano huo wenye wajumbe zaidi ya 800 kutoka sehemu mbalimbali Bara na visiwani, utafanyika kwa siku tano kuanzia leo hadi Ijumaa, jijini Dar es Salaam.

KIKUNDI CHA KATAVI NDIO HOME WATEMBELEA HOSPITALI YA WILAYA YA MAPNDA

Kikundi cha Katavi/Mpanda ndio home kutoka mkoa wa katavi wilayani Mpanda kwa umoja wao ambao pia ni mashabiki wa Manchester United na Arsenal wamefanya jambo la kijamii kwa kutoa msaada kwa wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa kuwasaidia maji, Sabuni, Matunda na Biskuti katika wodi tatu za wanawake, mbili za wanaume na moja ya watoto katika Hospitali hiyo.
Picha ya Pamoja Hospitali

   
Abdillazaq na Rajabu Katika Wodi ya Wanawake
 Katika mchakato huo wanakikundi wamejiwekea kila mwaka kutembelea maeneo mbalimbali hususa ni hospitali, magereza na kukutembelea vivutio vya utalii pamoja na kufanya Bonanza la michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, kuvuta kamba, kukimbiza kuku na kadharika.

Katika mahojiano ya mtandao huu Katibu wa Kikundi bwana Michael Mazalla na Mwenyekiti Ndugu Dickson Kashura wameeleza kuwa mwaka wa tatu mfululizo sasa Katavi/Mpanda Ndio Home wameweza  kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi, Hospitali ya wilaya Mpanda na kuongeza kuwa katika kuwa karibu zaidi na jamii wamepanga msimu ujao wataweza kutembelea maeneo mengine ikiwamo na Gereza kuu la Mpanda.

Katibu Michael Mazalla akisaini kitabu cha wageni katika Hospitali ya Wilaya

Ndugu Alex SoCksea akimpatia mgonjwa Sabuni.

"Katika kuendeleza utalii wa ndani kikundi kimepanga kutembelea fukwe za ziwa Tanganyika mkoani hapa katika maeneo ya Ikola na Karema mwishoni mwa mwezi June pia katikati ya mwezi July kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi" alisema Katibu
Katibu Michael Mazalla akitoa salam fup kwa wagonjwa katika wodi ya wanawake

Wanakikundi wakielekea katika wodi ya Wanaume
 Katika hari ya kujiweka sawa kimwili wanakikundi walimalizia wikiend kwa mpambano wa mpira wa miguu uliofanyika katika uwanja wa Azimio mjini hapa na Mashabikiwa Manchester united kuibuka na ushindi kwa kuwachabanga wenzao wa Arsenal kwa magoli Manne kwa moja ambapo Mchezaji wa man U Khalid aliweza kufunga goli tatu(Hat trick) peke yake huku lile la kufutia machozi la Arsenal likifungwa na Abdillazaq Osman kwa mkwaju wa penati.
Johnson & Michael

Kikosi cha arsenal kikiongozwa na Kapteni Mike Mertesacker

Kikosi cha Man U kikiongozwa na kapten Hussein  

Picha ya Pamoja
 Mwenyekiti bwana Dickson kashura aliweza kuongelea matitizo yaliyotokea katika kipindi hiki ikiwa ni pamoja na mwanakikundi ndugu Omary Zozi (Picha Chini) kuvunjika mguu eneo la paja baada ya kuanguka mzoezi, pia changamoto nyingine ni uchache wa watu kujitoa katika kutekeleza mkakati wote wa bonanza, akisema kuwa tofauti na mwaka jana ambapo watu walijitokeza kwa wingi.

Omary zozi wkibadilishana mawazo na wanakikundi walipomtembelea.
Kwa upande wa mwanakikundi na Katibu wa kamati ya Usafirishaji bwana Joseph Mtitimya amewataka wananchi wa mkoani hapa kupenda kujitolea na kujumuika na wananchi wengine ilikuweza kusaidiana katika mambo ya kijamii na kiuchumi kwani kwa kujitoa huko kunaongeza upendo, urafiki a undugu kwa ujumla. Aliongeza kwa kuwataka wananchi wa maeneo yote kujitokeza kwa wingi katika safari ya kutembelea maeneo ya Karema, Ikola (Beach) na Katavi National park.
Ndugu frank akigawa sabuni kwa mgonjwa.



Unaweza kuangalia video hapa chini jinsi mchakato mzima ulivyokuwa katika Hospitali ya wilaya ya mpanda.

PUTIN AANDA MAJESHI YAKE

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameviweka vikosi vyake vilivyoko nchini humo katika hali ya "tahadhari kamili ya vita" na kuwaamuru wanajeshi 65,000 katika eneo hilo kufanya luteka za kijeshi za wiki moja kuwa tayari kwa vita.


Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu, amesema mazoezi hayo ya kijeshi ya angani na ardhini katika maeneo ya milima ya Volga na Ural yatafanyika kuanzia Jumamosi Juni 21 hadi Juni 28.

Jumuiya ya Kujihami ya NATO imesema mapema wiki hii kwamba Urusi imerudia tena kurundika wanajeshi wake kwenye mpaka na Ukraine ambapo waasi wanaotaka kujitenga wamekuwa wakipambana na vikosi vya serikali kwa wiki kadhaa katika mzozo uliogharimu maisha ya watu 300 na kuwapotezea makaazi wengine 34,000.


*Kusitisha uhasama

Hatua hizo za kijeshi zinakuja siku moja baada ya Rais Petro Poroshenko wa Ukraine kutangaza wiki moja ya usitishaji wa mapigano na waasi wanaoiunga mkono Urusimashariki ya nchi hiyo ikiwa ni sehemu ya mpango wa amani wa vipengele vinne ambao pia unajumuisha msamaha na ahadi ya kufanyika kwa marekebisho ya katiba.

Serikali ya Urusi imeishutumu mpango huo wa Poroshenko kuwa ni "amri" ambao hautopelekea kupatikana kwa ufumbuzi wowote ule na waasi wameukataa wito wake wa kuwataka wasalimishe silaha zao.


Chanzo:DW SWAHILI

ZANZIBAR WATEKETEZA BIDHAA ZA CHAKULA TANI 25

Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi imeangamiza bidhaa mbalimbali za chakula zipatazo tani 25 baada ya kubainika kuwa hazifai kwa matumizi ya Binadamu.


Bidhaa hizo ni pamoja na maziwa ya kopo aina ya NAN tani 7.4 soda za kopo, chama tani tano, tende tani 10, mchele tani 1.1 na vyakula mchanganyiko tani moja ambapo uangamizaji huo ulifanyika katika Maeneo ya Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.

Mkuu wa ukaguzi wa Bodi hiyo,Aisha Suleiman alisema kuwa Bidhaa zote hizo zilizoangamizwa ni kufuatia ukaguzi unaofanyika kila siku kupitia Bandarini, Madukani pamoja na maghala yanayohifadhia bidhaa hizo.


Alifahamisha kuwa soda hizo zimeingizwa nchini zikiwa na tarehe iliyotengenezwa na hazina tarehe ya kumaliza muda wa matumzi jambo ambalo linaweza kuhatarisha afya za watumiaji.

Alisema kwa upande wa mchele ulioangamizwa umebaki kutokana kwa mchele huo kurejeshwa ulikotoka nchini Pakistan ambao ulikua tani 26 na uliobaki kuangamizwa.


Alisema gharama zote za uangamizaji wa vyakula hivyo kwa mujibu wa sheria ya Bodi ya chakula Dawa na Vipodozi mwenye mali yake ndio anaegharamia uangamizaji huo.

Amewataka wananchi kutoa taarifa kwa bodi hiyo endapo watatilia shaka bidhaa za aina yoyote ile kama vile za chakula, Dawa pamoja na vipodozi kwa lengo la kufanyiwa uchunguzi na kuepuka madhara kwa watumiaji.


Kwa upande wa wafanya biashara wametakiwa kuleta bidhaa zenye ubora kwa wananchi na kuepuka udanganyifu ambao unaweza kuleta madhara yanayopelekea kuleta athari kubwa kwa jamii.

WAPIGANAJI WA JIHAD WAZIDI KUTEKA MIJI

Wapiganaji wa Jihadi wameendelea kuyateka maeneo zaidi nchini Iraq, baada ya kuliteka eneo moja la kivuko karibu na mpaka wa Syria, na sasa wanalekea mjini Baghdad kupitia bonde la Euphrates.

Mwandishi wa BBC nchini Iraq amesema kuwa hatua hiyo inawafungulia njia wapiganaji wengine wa ISIS nchini Syria.


Wapiganaji hao vilevile wameiteka miji zaidi katika mkoa wa Anbar ambapo mwandishi huyo anasema kuwa lengo lao ni kuitumia kuvamia mji mkuu wa Baghdad.


Waasi hao wanasema kuwa waliiteka miji hiyo bila kumwaga damu kupitia majadiliano na makabila ya kisunni.

Wanamgambo wa Kishia hapo jana walifanya gwaride mjini Baghdad, na kuzua wasiwasi kuhusu tofauti inayozidi kuibuka kati ya watuwa dhehebu la kishia na walewa Kisunni.

WATU 6 WAFARIKI KATIKA AJARI NA WENGINE 12 WAJERUHIWA

Watu sita wamepoteza maisha na wengine kumi na mbili wakijeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea eneo la Makongo barabara ya Bagamoyo jijini Dar-es-salaam,ikiyahusisha magari manne mawili kati ya hayo yakiwa ni ya abiria maarufu kama Daladala,zifanyazo safari zake kati ya Ubungo,Mwenge,Makumbusho na Tegeta.

Vilio na simanzai vilitawala kwenye maeneo yanayozunguka hosipitali kuu ya jeshi la wanachi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo jijini Dar-es-salaam,ambapo mashuhuda wa ajali hiyo wanadai kuwa,dereva aliyekuwa akitokea tegeta kwenda mwenge alikuwa katika mwendo wa kasi ya ajabu.

Mganga mkuu wa hosipitali ya jeshi lugalo iliyopokea majeruhi na maiti hao,Brigedia Jenerali Dkt Makere Josiah, amethibitisha kupokea majeruhi kumi na wawili na maiti sita, huku wengine hali zao zikiwa ni mbaya na kukimbizwa kwenye hosipitali ya taifa ya rufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

UTEKELEZAJI HUKUMU YA MGOMBEA BINAFSI UTATA

Utata wa kisheria umeibuka kuhusu utekelezaji wa amri ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu kuhusu nafasi ya mgombea binafsi nchini.

Juni 14, 2013, Mahakama hiyo ilitoa amri ya kuitaka Serikali ya Tanzania kutoa taarifa ndani ya miezi sita kuhusu hatua ilizochukua kulingana na hukumu hiyo.
Wakati wanasheria wakieleza kuwa kitendo cha Serikali kushindwa kutekeleza amri hiyo kunaweza kuifanya nchi iwekewe vikwazo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema amri hiyo haiwezi kutekelezeka mpaka mchakato wa Katiba Mpya utakapokamilika.
Akizungumza jana, Jaji Werema alisema nchi haiwezi kuwekewa vikwazo vyovyote kwa kuwa tayari suala hilo lipo kwenye mchakato wa Katiba Mpya na kama ikishindikana iliyopo itafanyiwa marekebisho.
“Hakuna cha vikwazo wala nini… hilo suala kwa sasa liko kwenye mchakato wa Katiba unaoendelea, hatuwezi kurekebisha Katiba tena kwa hilo. Mnapaswa kuelewa hizi Mahakama za kimataifa, utekelezaji wa hukumu unategemea pia uwezo wa nchi husika. Sisi tuko kwenye mchakato wa Katiba, hadi ipatikane, isipopatikana ndipo tutaleta marekebisho. Mbona kuna marekebisho mengi tu yaliletwa lakini yanasubiri?”
Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia alisema: “Nchi haiwezi kutumia sababu zake za ndani ya nchi kama kisingizio cha kutotekeleza masharti ya mkataba iliyoridhia yenyewe kwa hiari na kwa nia njema.”
Mwanasheria kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Steven Msechu alisema japo Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu haina jeshi la kuilazimisha Serikali kutekeleza hukumu hiyo, bado itabanwa katika vikao vya nchi za Umoja wa Afrika... “Mahakama hiyo itapeleka ripoti kwenye Baraza la Marais wa Umoja wa Afrika kuonyesha kuwa Tanzania imeidharau... Baraza la Mawaziri wa Afrika nalo litapewa taarifa kama hiyo, hivyo marais na mawaziri husika watahojiwa kwa nini wameshindwa kutekeleza.”
Hata hivyo alisema Serikali inaweza kujitetea kuwa imeshaliweka suala hilo kwenye Rasimu ya Katiba hivyo liko kwenye mchakato.
Mchungaji Mtikila, TLS na LHRC walishinda kesi hiyo waliyofungua katika Mahakama hiyo baada ya kushindwa katika rufaa iliyofunguliwa na upande wa Serikali kupinga suala la mgombea binafsi.
Katika hukumu iliyosomwa na Rais wa Majaji wa mahakama hiyo, Sophia Akuffor Arusha hivi karibuni, Serikali italazimika kutekeleza kwa vitendo hukumu hiyo.

KISIMA KINGINE CHA GESI CHAGUNDULIWA

Kampuni ya Statoil ya Norway na mshirika wake ExxonMobil wamegundua kiasi kingine kikubwa cha gesi katika Bahari ya Hindi nchini Tanzania.

Kiwango hicho kinakadiriwa kufikia futi za ujazo trilioni mbili mpaka tatu (sawa na lita trilioni 56.6 hadi trilioni 84.9).
Ugunduzi huu unafanya jumla ya ujazo wa gesi iliyogunduliwa na washirika hao kufikia takriban futi za ujazo trilioni 20 (lita trilioni 566.25) kwenye Kitalu Namba 2, ambako washirika hao wanafanya shughuli za utafiti na uchimbaji.
‘’Tangu mwaka 2012 tumekuwa tukipata mafanikio ya asilimia 100 nchini Tanzania na eneo hilo limekuwa kitovu cha utafiti ndani ya muda mfupi. Ni kwa haraka tulitoka kwenye kuchimba kisima kimoja hadi kuwa na mkakati wa kuchimba visima vingi,’’ alisema Makamu wa Rais wa Shughuli za Utafiti za Statoil Ukanda wa Magharibi, Nick Maden.
Ugunduzi huo mpya katika Kisima Piri-1 umefanyika katika eneo lenye kiwango kidogo cha mawe ya mchanga kama ilivyokuwa wakati ilipogunduliwa gesi katika Kisima cha Zafarani-1 mwaka 2012.
Ugunduzi katika kisima hicho unakuwa wa sita katika Kitalu Namba 2.
Uchimbaji wa gesi katika kisima hicho ulifanywa na meli ya Discoverer Americas, usawa wa mita 2,360 za kina cha maji. Meli hiyo sasa inachimba kisima kingine cha Binzari katika Kitalu namba 2.
“Eneo lingine la utafiti limeshaandaliwa na litajaribiwa ndani ya mwaka 2014 na 2015. Tunatarajia kuchimba visima zaidi na tunatumaini kuwa matokeo ya visima hivi yataongeza kiasi cha ujazo wa gesi kwa ajili ya miundombinu ya mradi mkubwa wa gesi hapo baadaye,’’ alisema Maden.
Statoil ambayo imekuwapo nchini tangu 2007, inatafiti na kuchimba gesi katika kitalu namba mbili kwa niaba ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ikiwa na hisa ya asilimia 65 katika kitalu hicho wakati ExxonMobil Exploration and Production Tanzania Limited ina asilimia 35.



Chanzo: Mwananchi

IRAQ YAOMBA MSAADA


Majeshi ya angani ya MArekani kutumwa Iraq

Iraq imeomba rasmi usaidizi wa Marekani kushambulia kwa ndege wapiganaji wa kiislamu walioteka miji kadhaa nchini humo wiki hii.
"Tumepokea ombi kutoka kwa serikali ya Iraq kutumia ndege zetu huko,'' alithibitisha kamanda mkuu wa jeshi la Marekani Jenerali Martin Dempsey mbele ya baraza la senate.

ISIS waendeleza harakati zao

wapiganaji wa ISIS wameilemea serikali ya Iraq

Awali wapiganaji hao wa madhehebu ya Sunni walishambulia kiwanda kikubwa zaidi cha kusafishia mafuta nchini Iraq katika mji wa Baiji kaskazini mwa Baghdad.
Katika taarifa yake kwa taifa, waziri mkuu Nouri AL Maliki alitoa wito kwa raia wa Iraq waungane dhidi ya wanamgambo.
Vikosi vya jeshi vinajitahidi kuwakabili na kuwasukuma nje wanamgambo wa ISIS pamoja na washirika wao wa Ki-sunni kutoka mikoa ya Diyala na Salahuddin baada ya waasi hao kuteka mji wa Mosul wiki iliyopita.

Obama ataka kuisaidia Iraq

Na hapo Jumatano, rais Barack Obama alifanya kikao cha dharura na baraza la Congress kujadili mzozo wa Iraq.
Duru za ikulu ya White house zinasema kuwa Bwana Obama ''amependekeza kuongezwa juhudi zetu nchini Iraq na kusaidia majeshi ya serikali hiyo katika kukabiliana na wanamgambo wa ISIS ikiwemo uwezekano wa kuongeza usaidizi wa kiusalama''.

Baadhi wanapinga

Lakini kabla ya kufanyika mkutano huo, kinara wa baraza la Senatae wa Marekani Harry Reid, kutoka chama cha Demokrats alisema kuwa hakubaliani kamwe na wazo la kuihusisha Marekani katika ''vita vya ndani vya Iraq''.
Marekani imekuwa katika ubishi mkubwa katika mabunge ya Senate na Congress juu ya kuondolewa majeshi yao ndani ya Iraq na Afghanistan.

JWTZ NA POLISI WAFANIKIWA KUHARIBU BOMU

Jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kushirikiana na jeshi la wananchi wa Tanzania wamefanikiwa kuharibu bomu lililokuwa limetelekezwa katika kijiji cha Mdui kata ya Mbawala wilaya ya Mtwara vijijini baada ya kuonekana likichezewa na watoto.

jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kushirikiana na jeshi la wananchi wa Tanzania wamefanikiwa kuharibu mlipuko wa bomu katika kijiji cha Mdui kata ya Mbawala wilaya ya Mtwara vijijini baada ya kuonekana likichezewa na watoto.
Akizungumza na ITV kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Maisha Maganga amesema taarifa hizo wamezipata kutoka kwa raia wema baada ya kuonekana likiwa eneo la makaburi.

Amesema baada ya kupata taarifa juu ya bomu hilo lenye kilo nne jeshi hilo lilichukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kuomba kikosi maalum cha kutegua mabomu kutoka jeshi la wananchi wa Tanzania.
Amesema bomu hilo linaonyesha ni la siku nyingi mahali hapo na liliachwa enzi za vita ya Msumbiji.

Chanzo: ITV



TANZANIA KUBADILISHA SHERIA KUHUSU SHISHA

Waziri wa afya nchini Tanzania, amesema kuwa Tanzania inapanga kutathmini sheria ya sasa kuhusu matumizi ya Sisha ili kufanya mageuzi au kubadili sheria hiyo matumizi ya Shisha.

Dkt Seif Rashid Selemani amesema kuwa sheria hiyo italenga kulinda afya ya watanzania hasa walio na uraibu wa Shisha na pia kuhakikisha kuwa wanaotumia Shisha katika sehemu zengine duniani wanapata kubadili mfumo wamaisha ili kulinda afya zao.

Hii ni baada ya taarifa ya awali kuwa serikali ilikuwa tayari imechukua hatua kupiga marufu bidhaa hiyo ambayo inaenziwa sana hasana vijana.


Uraibu huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye ladha tofauti tofauti ambayo hutiwa ndani ya chupa kubwana kuvutwa kwa mirija, umeshika kasi sana Tanzania hasa miongoni mwa vijana mjini Dar Es Salaam.

Baadhi ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya kiafya ikilinganishwa na uvutaji wa Sigara.


Lakini wataalamu wanaamini kuwa uvutaji wa Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta sigara miamoja.

Madaktari walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha wakisema kuwa waraibu wanakabiliwa na tisho la kuugua Saratani sawa na hatari inayowakabili wavutaji wa sigara.

SHEKHE WA MKOA MAHAKAMANI

SHEHE wa Mkoa wa Tabora, Salum Shaban na waumini wengine watano wa dini ya Kiislamu, wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka ya kutishia kufanya fujo.


Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Tabora, Issa Magoli, ilidaiwa na Wakili wa Serikali, Juliana Changalawe kwamba watu hao walitenda kosa Juni 14 mwaka huu katika Msikiti Mkuu wa Mkoa, ulioko eneo la Gongoni, mjini Tabora.

Washitakiwa wengine ni Mgude Ahmed, Said Maganga, Kassim Shomary, Abubbakar Ludenga na Kassim Rajab, wanaodaiwa kwamba siku hiyo mchana, walimtoa sehemu ya ibada Shehe Ibrahim Mavumbi.

Washitakiwa hao ambao wanawakilishwa na Mwanasheria Mussa Kwikima wa mjini Tabora, walikana mashitaka. Kesi iliahirishwa hadi Juni 30 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kutokana na upelelezi kukamilika.


Wote walipata dhamana. Kukamatwa hadi kufikishwa mahakamani kwa watu hao, kunatokana na mgogoro uliokuwa ukiendelea na kusababisha Mufti wa Tanzania, Shehe Mkuu, Issa Shaban bin Simba kutangaza kumuengua Shehe wa Mkoa wa Tabora, Shaban (mshitakiwa); kitendo ambacho kinapingwa na baadhi ya waumini.


Katika mgogoro huo, baadhi ya Waislamu wanapinga uamuzi wa Mufti kumtangaza Shehe Mavumbi Ally kuwa Kaimu Shehe wa Mkoa, wakidai alishindwa kwenye uchaguzi.

MRAMBA APUNGUZA SHAHIDI MMOJA

WAZIRI wa Fedha wa zamani, Basil Mramba, anayekabiliwa na kesiya matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara yash bilioni 11.7, ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa anamuondoa shahidi wake wa tatu ambaye alikuwa ni Naibu Kamishna wa Income Tax, Felisian Busigala (67), katika orodha yamashahidi ambao awali alikuwa anataka wamtetee.

Kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya jopo la majaji watatu, John Utamwa, Sam Rumanyika na Sauli Kinemela kutoa uamuzi wa pingamizi lililowasilishwa na upande wa jamhuri ambalo liliomba mahakama hiyo, imuondoe Busilaga katika orodha ya mashahidi wa Mramba.


Hatua hiyo ni kutokana na ushahidi alioanza kuutoa Septemba 20, mwaka2013, kuonyesha amefika mahakamani hapo kama mtaalamu wa masuala ya kodi na siyo shahidi ambaye anastahili kuzungumzia mashitaka yanayomkabili Mramba.


Wakili wa Mramba, aliwasilisha ombi hilola kuomba mahakama imuondoe shahidi huyo katika orodha yamashahidi, ombi ambalo lilikubaliwa na Jaji Utamwa, na wakili Swai aliomba kesi hiyo ihairishwe hadi Agosti 21, mwaka huu.

Alisema sababu ya kufanya hivyo ni kutokuwapo na shahidi, ombi ambalo lilikubaliwa na jopo hilo.


Septemba 20, mwakajana, mawakili wa serikali waandamizi; Shadrack Kimaro na Oswald Tibabyekomya, waliweka pingamizi hilo wakiomba shahidi huyo asiendelee kutoa ushahidi wake kwa sababu alionyesha kuwa alifika mahakamani hapo kutoa ushahidi wa kitaalamu na sio wa mashitaka yanayomkabili Mramba.

Mapema jana, Busigala akiwa kizimbani alijibu maswali ya wakili Nyange ambayo yalimtaka afafanue maana ya 'Net of all taxes' kwa sababu kwamujibu wa mkataba ulioingiwa na Benki Kuu na Kampuni ya Alex Stewart inaonyesha benki hiyo kwa niaba ya serikali iliridhia kampuni hiyo ichukue asilimia 1.9 ya dhahabu yote atakayokuwa ameishaikagua.


Busigala alianza kufafanua kuwa 'Net of all taxes' katika mkataba ule maana yake Kampuni ya Alex Stewart itaondoka na asilimia 1.9 baada ya kumaliza ukaguzi wa dhahabu na hiyo asilimia 1.9 ni baada ya kodi yote kukatwa na serikali na kwamba kama kisinge kuwepo hicho kipengele kwenye ule mkataba, ni kwamba Kampuni ya Alex Stewart ingelipwa fedha zaidi na serikali ili mwisho wa siku kampuni hiyo iweze kulipa kodi husika kwa serikali.


Kwamba tatizo hapo siku zote kodi zimekuwa zikibadilika kwani zinapanda na kushuka na hivyo ingelikuwa ni vigumu kwa serikali kuweza kutekeleza matakwa ya mkataba ambao usingekuwa na kipengele hicho cha kumlipa moja kwa fedha kampuni na kisha kampuni ije ilipe kodi husika kwa serikali.


Maelezo hayo ndiyo yalisababisha mawakili wa upande wa jamhuri kuwasilisha pingamizihilo ambalo lilisababisha mahakama kumtaka shahidi huyo asindelee kutoa ushahidi wake hadi watakaposikiliza pingamizi hilo kwa njia ya maandishi na watalitolea uamuzi Oktoba 25, mwaka huu.


Novemba 2008 ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Mipango naUchumi, Gray Mgonja wanakabiliwa na makosa mbalimbali ya matumizi mabaya na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7.

CARE INTERNATIONAL WATIMULIWA MTWARA

MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile, amelipa siku 14 Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Kimataifa la Care International Tanzania, kuondoka katika wilaya hiyo baada ya kubainika kuwa wanasambaza mbegu 'feki' za ufuta kwa wakulima.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mwishoni mwa wiki, Ndile alisema Care International walifika Mtwara kwa lengo la kufanya kazi na wanawake na wakulima vijijini, wakidai wanaongeza kipato cha wakulima kupitia ufuta.

Ndile alisema amechukua uamuzi huo baada ya kubaini kwamba shirika hilo linasambaza mbegu za ufuta aina ya Lindi 2003 ambazo ni feki, na tayari amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), kuwafuatilia nyendo zao."

Nawapa siku 14 hatutaki kuziona ofisi zao hapa kwa sababu hawana mchango kwawana Mtwara… siwataki Care International katika wilaya yangu, nimepokea malalamiko ya wakulima wa Tarafa ya Mayanga na Mpapura wakisema kwenye mashamba yao kuna mbegu za ufuta zilizosambazwa mwaka 2013/2014 zinastawi vizuri, lakini hazitoi mavuno.


"Niliwaita wasaidizi wangu Idara ya Kilimo nikawauliza kuhusu Care, wakasema hawakushirikishwa, tumewauliza kituo cha Utafiti wa Mazao na Maendeleo Kanda ya Kusini, Naliendele nao hawakuambiwa… tumeliona suala hili ni zito, wanarudisha nyuma jitihada za maendeleo ya kilimo," alisema.

Mratibu wa Mradi wa Care International, Ofisi ya Mtwara, Morine Kwilasa, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alikuja juu akiwataka waandishi wa habari wampatie majina yao na vyombo wanavyofanyia kazi huku akibainisha kwamba si msemaji wa shirika hilo.

LOWASSA, MBOWE WAIKOSOA SERIKALI

KIONGOZI Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wameikosoa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, wakisema kuwa ajira kwa vijana ni bomu linalofanyiwa mzaha.

Hii si mara ya kwanzakwa Lowassa kuinyooshea kidole Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), japo mara zote amekuwa akibezwa kuwa anatumia turufuhiyo kujijenga kisiasa wakati suala hilo si kubwa kiasi hicho.


Katika kampeni za kuingia madarakani mwaka 2005, Rais Kikwete aliahidi kutengeneza ajira milioni mbili kwa vijana, ahadi ambayo hadi sasa utekelezaji wake unatia shaka, kutokana na muda wake kufikia ukingoni.

Akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15 bungeni juzi, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, alisema suala la ajiralinapaswa liwe hoja maalumu bungeni kwa kuwa serikali imeshindwa kulipa kipaumbele.


Alisema ukosefu ajirani janga la kitaifa, serikali haionekani kushitushwa nalo na badala yake imekuwa ikifanya mikatati inayoishia ngazi za juu.

Mbowe alifafanua kuwa jambo hilo linatakiwa liwekewe mikakati kuanzia ngazi za halmashauri, mikoa na serikali kuu.

Alibainisha kuwa kuongeza ajira si suala la kufumania bali ni mkakati maalumu unaoandaliwa na serikali.


Alisema tukio lililotokea hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwa vijana 11,000 waliokwenda kufanya udahili wa kupata nafasi 70 za ajira za Idara ya Uhamiaji, ni ishara mbaya kwa mwelekeo wa taifa.

"Serikali haipo makinina ukosefu wa ajira, na sisi wabunge hatulichukulii jambo hilo kwa ukubwa wake, vijana 11,000 wanawania nafasi 70! Hii ni hatari," alisema.


Aliongeza kuwa suala hilo limezungumzwa na watu wengi, akiwemo kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM, lakini akaelezwa si kubwa kama anavyolizua.Mbowe alisema tatizola ukosefu wa ajira limechangiwa na mfumo uliopo sasa wa kila kitu kurundi kwa kwenye Serikali Kuu.

Alisema tatizo hilo lingepungua kama halmashauri zingekuwa na mkakatiwa kuzitengeneza kwenye mazingira wanayofanyia kazi.

"Sioni haja ya kuwa nawataalamu wa uchumi na wakurugenzi katika halmashauri kama hawawezi kutengeneza ajira…. Tutengeneze mfumo wa ajira kuanzia ngaziza chini, serikali itoe agizo kwa halmashauri kutengeneza ajira," alisema.

Kwa mujibu wa Mbowe, miradi ya ushirikiano kati ya sekta binafsi na sekta ya umma (PPP) inaweza kulifanya taifa litengeneze kati ya sh bilioni 500 hadi 800.


*Madeni ya serikali

Kuhusu madeni, Mbowe alisema baadhi ya madeni ya taifa yanatokana na uzembe wa mawaziri na watendaji serikalini.

Kauli hiyo ameitoa juzi jioni bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015.


Mbowe alisema serikali imeliingiza taifa hasara ya sh bilioni tano kutokana na kushindwa kuilipa kwa wakati kampuni inayojenga bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.

Alisema ana barua za kutoka katika kampuni ya kujenga bomba la gesi ambayo inakwenda katika Shirika la Umeme na Wizara ya Fedha inayodai sh bilioni 5 kama riba na mkopo.

Kwa mujibu wa Mbowe, serikali haijailipa kampuni hiyo tangu Januari mwaka huu, kama mkataba unavyosema, hivyo kuzua hofu ya kukamilika kwa wakati kwa mradi huo."

Jamani madeni mengi ni ya kujitakia tu… ni uzembe tu hapa, tumeingizwa kwenye deni la sh bilioni tano kwa sababu ya wizara imeshindwa kuilipa kampuni hii.

"Tuna kila sababu kuangalia deni hili la taifa linasababishwa na nini ili tuangalie namna bora ya kulishughulikia na kuwashughulikia wale wote wazembe," alisema.


*Lowassa aibuka

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli kupitia CCM, katika mchango wake alisema mara kwa mara alikuwa akitahadharisha kuwa ajira ni bomu, lakini watu hawakumuelewa.

Alisema sasa bomu hilo linaanza kupasuka taratibu na kuwa serikali inatakiwa kutengeneza ajira kwa vijana.


Kwa mujibu wa Lowassa, idadi ya Watanzania ni milioni48 na kila mwaka wahitimu wa vyuo vikuu wanafikia zaidi ya 40,000, lakini hakuna ajira.

Alisema ni lazima taifa liwe na mkakati wa kitaifa wa kuwasaidia vijana kwa kutengeneza ajira.


Lowassa aliongeza kuwa ujenzi wa kiwanda chochote ni vema ukaangalia utazalisha ajira kwa kiwango gani.

Alibainisha kuwa Rais Barak Obama wa Marekani, ni miongoni mwa viongozi walioingia madarakani kwa awamu ya pili baada ya kutengeneza ajira.


Chanzo: Tanzania Daima