SUDAN KUSINI KUKUTANA ETHIOPIA KWA AJILI YA MAZUNGUMZO

Pande mbili zinazopigana katika mgogoro wa Sudan Kusini zimekubali kukukatana nchini Ethiopia kwa ajili ya mazungumzo ya amani, lakini kiongozi wa waasi, Riek Machar, ameiambia BBC kuwa hata sitisha mapigano dhidi ya majeshi ya serikali.

Pia amesema majeshi yake yametwaa tena mji muhimu wa Bor kutoka majeshi ya serikali -- lakini madai haya hayajathibitishwa.

Waasi waliushambulia mji huo saa chache kabla ya kumalizika kwa muda uliwekwa na viongozi wa Afrika Mashariki, kwa kuzitakapande zinazopingana nchini Sudan Kusini kukubaliana kumaliza uhasama kati yao -- au wakabiliwe na majeshi ya nje kwa kuingilia kati mgogoro huo.

Bwana Machar awali alikaririwa akisema asingeingia katika mazungumzo ya amani hadi hapo washirika wake wa kisiasa wanaoshikiliwa na serikali watakapoachiliwa huru.

Mapigano kati ya waasi na askari watiifu kwa Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, yameenea nchini kote katika kipindi cha wiki bili zilizopit

HALI YA MICHAEL SCHUMACHER YAANZA KUIMALIKA

Madaktari wa bingwa wa zamani wa mbio za magari ya langa langa, Michael Schumacher, wamesema hali yake imeimarika kiasi baada ya kufanyiwa upasuaji kupunguza shinikizo katika ubongo wake.

Kipimo kipya cha uchunguzi kilichochukuliwa usiku kucha kimeonyesha dalili kwamba hali yake ni "nzuri zaidi kuliko ilivyokuwa jana", lakini bado hajawa salama, wamesema madaktari hao.

Bingwa huyo mara saba wa mbio za magari ya langa langa ya Formula 1 alipata majeraha ya kichwa Jumapili wakati wa mchezo wa kuruka katika theluji kwenye milima ya Alps nchini Ufaransa.

Aliwekwa katika uangalizi mkubwa wa matibabu.

Kipimo cha kwanza kilichofanyika Jumatatu usiku kilionyesha, kuimarika kwa hali yake na kutoa fursa ya kufanyika upasuaji wa pili, wamesema madaktari.

Familia walichukua uamuzi mgumu wa kuwaruhusu madaktari kuendelea na upasuaji huo, na madaktari walifanya kazi hiyo ya upasuaji kwa saa mbili.

Habari za ajali aliyopata Schumacher wakati akicheza mchezo wa kuteleza katika theluji kwenye milima ya Alps nchini Ufaransa, zilitawala katika vyombo vya habari vya Ujerumani.

Schumacher alikuwa akiteleza kwenye theluji na mtoto wake wakiume, wakati alipoanguka na kujipigiza kichwa katika mwamba.

Alikimbizwa katika hospitali ya karibu ya mji wa Moutiers.

Baadaye alihamishiwa katika hospitali kubwa ya Grenoble.

Msemaji wa Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kiongozi huyo na serikali yake, kama ilivyo kwa mamilioni ya wananchi wa Ujerumani, wameshitushwa mno na taarifa za ajali ya Michael Schumacher."

Tuna matumaini kwamba Michael Schumacher na familia yake wataweza kukabiliana na hali hii na kupona, amesema msemaji wa Chansela Angela Merkel.

Mchezaji mwenzake wa zamani katika timu ya magari la langa langa ya Ferrari, Felipe Massa, ambaye aliponea chupuchupu kupoteza maisha baada ya kupata ajali wakati wa mashindano ya Hungarian Grand Prix, ya mwaka 2009, ametuma ujumbe katika Instagram:

"Nakuombea kaka yangu! Nina matumaini kwamba utapona haraka! Mungu akubariki, Michael."

Jumatatu, baadhi ya wapenzi na mashabiki wa Michael Schumacher walikusanyika nje ya hospitali ya Grenoble.

Nuravil Raimbekov, mwanafunzi kutoka Kyrgyzstan ambaye anasoma karibu na hospitali hiyo, amemwelezea Schumacher kamakivutio.

"Nina wasiwasi, bila shaka... Lakini bado nina matumaini, na nitaomba kwa ajiliyake," amesema mwanafunzi huyo.

KAMISHNA MPYA WA JESHI LA POLISI ATEULIWA NA RAIS JK

PRESIDENT'S OFFICE,

THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu waJeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.

Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai(Director of Criminal Intelligence)katika Jeshi hilo la Polisi.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai(Commissioner for Forensic Investigations).

Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu.

Dar es Salaam.
30 Desemba, 2013

MTU MMOJA AUWA JIJINI DAR

Mtu mmoja mkazi wa kawe mzimuni jijini Dar es salaam ameuawa katika mazingira ya utata baada ya mwili wake kukutwa umetelekezwa katika chumba kimoja walichokuwa wakiishi wasichana wawili.

Huku uchunguzi wa awali ukibaini kuwa mtu huyo alichomwa na kitu chenye ncha kali na kusababisha kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha

JESHI LA DRC LAZIMA SHAMBULIO LA KIGAIDI

Jeshi la demokrasia ya Congo limesema kuwa limefanikiwa kuzima shambulio lililolenga uwanja wa ndege na kituo cha taifa cha Radio na Televisheni linalodaiwa kutekelezwa kundi lisilofahamika la kigaidi.

Waziri wa habari nchini humo Lambert Mende kwa sasa hali imedhibitiwa ambapo wamefanikiwa kuwaua watu 40 miongoni mwa waliokuwa wakiendesha mashambulizi hayo.

Watu hao waliokuwa na silaha 16 kati yao wameuawa katika mapambano na polisi uwanja wa ndege,16 wengine katika eneo la jeshi na nane wao waliuawa katika ofisi za Radio ya Taifa.

Amesema kuwa kulikuwa na mtukio mengine mawili ya mashambulizi katika maeneo ya uwanja wa ndege na kambi ya jeshi.

Kwa mjibu wa waziri Mende watuhao waliokuwa wakiendesha mashambulizi hayo katika televisheni ya taifa na makao makuu ya radio ya taifa walikuwa na silaha zikiwemo bunduki,visu lakini walidhibitiwa kabla ya kusababisha madhara.

Mashambulizi haya yametokea wakati rais Joseph Kabila akiwa ziarani katika jimbo la Katanga nchini humo.

Ubalozi wa Marekani umetoa tahadhali kwa raia wake kutofanya safari za ndani ya mji wa Kinsasa hadi hali itakapo dhibitiwa Zaidi.

RAIS AKABIDHIWA RASIMU YA PILI YA KATIBA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amekabidhiwa rasimu ya pili ya katiba mpya na tume ya katiba inayoongozwa na mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba.

Rais Kikwete amesema kuwa kazi iliyofanyika katika mchakato huo imewezesha makundi mbalimbalikatika jamii kuchangia mawazo yao kupitia tume aliyoiunda ili kupata mawazo ya watanzania kuhusiana na katiba wanayoitaka.

Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amekabidhiwa pia rasmu hiyo na kueleza kuwa kuwa wajumbe watakaoteuliwa katika bunge la katiba wanapswa kufanya kazi kwa bidii kama ilivyokuwa kwa kamati hii iliyomaliza kazi yakeJaji mstaafu Warioba amesema rasimu hii wanayoiwasilisha ni ndefu kuliko ile ya awali iliyokuwa na ibara 240 wakati hii ina ibara 271 ikiwa ni matokeo yatume kuzingatia maoni ya mabaraza ya katiba yaliyotoa maoni mengine mapya Ameyataja baadhi ya mambo ambayo tume imebaini kuwa yalijadiliwa kwa hisia kali katika rasmu hiyo na ile ya awali kuwa ni suala la muungano hasa kuhusu muundo wake.

Amesema wakati tume inazindua rasmi ya awali hawakupendekeza kuendelea kuwa na muundo wa serikali mbili ulihitaji ukarabati mkubwa ambao tume ilifikiri hautawezekana, hivyo mabaraza ya katiba yalitoa mapendekezo mengi yaliyoilazimu tume kufanya uchambuzi wa kina na kwamba iliwachukua muda mrefuwa tume.

Jaji Warioba amesema wananchi Zaidi ya 39,000 wa Tanzania bara waliotoa maoni yao kuhusu muungano na kati yao karibu 27,000 walizungumzia muundo na Zanzibar wananchi karibia wote waliotoa maoni walijikita katika muungano ambapo kati ya wananchi 38,000 wa Zanzibar waliotoa maoni 19,000 walizungumzia muundo wa muungano.

Tanzania bara asilimia 13 walitaka serikali moja, asilimia 24 walipendekeza serikali mbili na 61 walipendekeza serikali tatu, wakati Zanzibar asilimia 34 walipendekeza serikali mbili na asilimia 60 muungano wa mkataba ambapo asilimia 0.1 walihitaji serikali moja.

Hata hivyo Rasimu hiyo ya katiba iliyokabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeorodhesha malalamiko 10 kwa upande wa Zanzibar na manane ya Tanzania Bara Malalamiko matatu makubwa kwa Zanzibar ni Serikali ya Tanganyika kuvaa koti la serikali ya muungano hivyo kupunguza nguvu kwa Zanzibar,Ongezeko la mambo ya Muungano, kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Tanzania bara tume hiyo imeyataja malalamiko kuwa ni kuwa Zanzibar imekuwa nchi huru , ina bendera yake ya Taifa, ina serikali yake ina wimbo wake wa taifa na imebadili katika yake ili itambulike kama nchi wakati Tanzania bara imepoteza utambulisho wake, wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar wakati wenzao wanamiliki Tanzania bara.

PADRI ANG'ANG'ANIWA KORTINI

KESI inayomkabili Padri Deogratius Makuri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida kushindwa kutoa matunzo kwa mwanawe, kesi iliahirishwa tena kwa mara ya tatu baada ya mlalamikiwa kushindwa kufika mahakamani.

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Utemini mjini Singida anayesikilizakesi hiyo, Ferdinand Njau alisema Padri Makuri ametuma mtu aliyedai kuwa ni dada yake kuja kuiarifu Mahakama kuwa hataweza kutokea kutokana na kuumwa.

Hata hivyo, Hakimu Njau alimwambia dada huyo na wasikilizaji kwa ujumla kuwa ili haki itendeke ni lazima mlalamikiwa awepo mahakamani. "Kuna baadhi ya watu wanasema kwa nini labda kesi hii isingesikilizwa faragha eti kisa tunasali naye."Hoja kwamba tunasali naye haipo hapa. Ndio maana nimeamua kesi hii isikilizwe Mahakama ya wazi. Nitasimamia kwa nguvu zangu zotenikizingatia sheria hadi haki ipatikane maana nipo kwenye mtego.…. huyu ni kiongozi wangu kanisani, sawa.

Lakini pia huyu mtoto, malaika wa Mungu, anahitaji matunzo.

Nisipotenda haki, Mungu atanihukumu," Hakimu Njau alisema.

Kutokana na umuhimu huo, Hakimu Njau alisema kuwa endapo mlalamikiwa hatafika tena Januari 3, 2014, ambapo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa, atalazimikakusikiliza kesi hiyo upande mmoja.

Padri Makuri, ambaye pia alikuwa Katibu wa Askofu wakati huo, anatuhumiwa kushindwa kutunza mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minane aliyezaa na Maria Boniphace (26), mkazi wa eneo la Mitunduruni mjini hapa.

TAKRIBANI TEMBO 60 WAMEUAWA NDANI YA MWEZI MMOJA BAADA YA OPERESHENI TOKOMEZA

TEMBO 60 wameuawa na majangili kwenye hifadhi mbalimbali nchini katika mwezi mmoja tangu operesheni tokomeza isitishwe.

Mauaji hayo yametajwa kufanyika katika Hifadhi za Selous, Rungwa, Burigi, Katavi na Ngorongoro.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema jana kwamba idadi hiyo ni sawa na wastani wa tembo wawili kila siku, inakwenda sanjari na kuuawa, kujeruhiwa kwa watumishi kadhaa wanaofanya kazi kwenye hifadhi.

Alisema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna serikali ilivyojipanga kuhakikisha inatokomeza vitendo vya ujangili.Alitaja askari wa wanyamapori, Ramadhani Magengere (40) aliuawa na majangili na wakati huo huo, Yahya Ramadhani (34) alijeruhiwa na wafugaji walioingiza mifugo ndani ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Jumuiyan(WMA) Ukutu iliyoko Morogoro Vijijini. Matukio hayo ni ya Desemba 6 mwaka huu.

Aidha alisema Novemba 14, mtumishi wa wanyamapori, Sajid Majidi alijeruhiwa kwa kuchomwa mkuki kichwani na kuvunjwa mkonona wafugaji walioingiza ng'ombe katika eneo la Ramsar, Kilombero.Alisema wapo watumishi wa pori la akiba Mkungunero wilayani Kondoa,Dodoma, waliokuwa doria walivamiwa na kundi la watu zaidi ya 80 waliokuwa na mikuki na silahanyingine za jadi na kujeruhiwa."Kutokana na kusitishwa kwa operesheni tokomeza, matukio ya uvunjaji wa sheria za hifadhi kama vile uingizaji holela wa mifugo katika maeneo ya hifadhi, ujangili wa wanyama wakiwemo tembo pamoja na uvunaji wa miti katika hifadhi za misitu, bado yanaendelea," alisema.

Nyalandu ambaye kwa mujibu wake, vitendo vya ujangili vimeongezeka baada ya opereshenihiyo ikilinganishwa na kipindi cha opeseheni, alisema wakati wote wa operesheni tokomeza iliyodumu kwa mwezi mmoja, ni tembo wawiliwaliokuwa wameuawa.

Aliendelea kusema, "Majangili wameua tembo 60 katika hifadhi namapori ya Selous, Rungwa, Burigi, Katavi na Ngorongoro…..hawa ni takribani tembo wawili kwa siku na ikumbukwe wakati wote wa operesheni tokomeza iliyodumu mwezi mmoja ni tembo wawili tu waliokuwa wameuawa," alisema Nyalandu.

Majangili waanzisha kambi Naibu Waziri alisema serikali imegundua kambi ya majangili iliyoanzishwa katika pori la akiba la Burigi ambako vitendo vya ujangili vinaendeshwa na baada ya kukurupushwa na askari wa wanyamapori walikimbia na kuacha nyama ya nyani 30 waliokuwa wamewaua.Aidha alisema hivi karibuni, wilayani Simanjiro, lilikamatwa gari likiwa limejaa mizoga 20 ya swala. Alisema lipo ongezeko la wimbi la uvamizi na ufugaji wa mifugo ndani ya mapori ya akiba, hifadhi za misitu iliyoko Magharibi mwa nchi hususani Burigi, Biharamulo, Kimisi, Moyowosi, Katavi na Ugalla."Serikali inawakumbusha wananchi kuwa kwa mujibu wa sheria ya wanyamapori namba 5 mwaka 2009 pamoja na sheria zinazosimamia maeneo ya hifadhi za taifa na misitu kuwa hawaruhusiwi kuingiza mifugo wala kuingia kuua, kuwinda, kukamata wanyama bila kibali cha mkurugenzi wa wanyamapori," alisisitiza.

Yaliyojiri Dodoma Wakati operesheni tokomeza imegeuka kuwa mwiba baada ya wabunge kuibua kashfa ya unyanyasaji na utesaji uliofanywa nawananchi hivyo kusababisha mawaziri kadhaa kujiuzulu, Nyalandu alisema matukio hayo ya bungeni Dodoma, hayajatengua sheria yoyote ya Wanyamapori au Misitu.Aliwaagiza watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kutekeleza majukumu yao ya ulinzi wa maeneoya hifadhi za taifa, mapori ya akiba na misitu ya hifadhi bila kutetereka.

Alitaka wachukue hatua stahiki dhidiya mhalifu yeyote ilimradi wanazingatia sheria. "Ikumbukwe kuwa matukio yaliyotokea bungeni Dodoma, hayajatengua sheria yoyote…hamna maamuzi yoyote ya Bunge yaliyohalalisha ukiukwaji wa Sheria za Uhifadhi," alisema Nyalandu.

Alisisitiza kwamba wananchi wanatakiwa kutii na kufuata sheria hizo kama zilivyo.

"Tahadhari inatolewa kuwa Serikali haitasita kumchukulia hatua kali yeyote atakayekiuka Sheria ya Wanyamapori kwa makusudi. Tunawaomba wananchi wasikubali kudanganywa na mtu yeyote kuvunja sheria za nchi," alisema. "Serikali inasisitiza kuwa kwa kutumia vyombo vyake itaendelea kutimiza majukumu yake ya kusimamia ipasavyo sheria, ikiwa nipamoja na kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayeshiriki moja kwa moja au kusaidia vitendo vya ujangili ili kunusuru rasilimali za taifa," alisisitiza.

Katika mkutano huo wa jana, Naibu Waziri asisitiza serikali ina maadili na miiko ya utendaji kazi kwa watumishi wake wakiwemo askari wa wanyamapori.

Alisema serikali itaendelea kuwakumbusha watumishi maadili na miiko kila wakati kupitia mafunzo na mbinu nyingine.

Kujiuzulu mawaziri Operesheni Tokomeza ilisitishwa Novemba mosi kabla ya wabunge kuibua kashfa ya unyanyasaji na utesaji unaodaiwa kufanywa na waliokuwa wakiiendesha na hivyo kusababisha mawaziri wanne kuachia nyadhifa zao.

Ripoti ya kamati ndogo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyoundwa kuchunguza operesheni hiyo, ilieleza kuwa athari zilizotokana na operesheni hiyo zilisababishwa na wizara nne zilizokuwa zikiongozwa na mawaziri hao.

Mawaziri walioachia nyadhifa zao ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki aliyejiuzulu na wengine wanne ambao kwa pamoja, Rais Jakaya Kikwete alitengua nafasi zao.

Wengine ambao uteuzi wao ulitenguliwa ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Ulinzi na Jeshila Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.

JUHUDI ZA KUKWAMUA MELI, WAOKOAJI WA CHINA WAKWAMA

Meli ya Australia imo njiani kuelekea Mashariki wa Antarcticakwa ajili ya kukwamua meli ya wanasayansi iliyokwama kwenye theluji tangu siku ya jumanne.

Awali juhudi za uokoaji zilifanywana wavuja theluji wa Uchina na Ufaransa lakini walikwama kutokana na unene wa theluji.

Hata hivyo mwandishi wa habari wa BBC aliyepo kwenye meli ya utafiti ya Urusi anasema tayari theluji imeanza kupasuka na kuongeza matumaini ya meli hiyo iliyonasa kujikwamua yenyewe na kuanza kuondoka.

Wanasayansi wapatao sabini na nne, watalii na wafanyakazi wa meli wapo kwenye meli hiyo iliyokwama inayoitwa.

Meli hiyo imekuwa ikitumiwa na taasisi ya Australasian Antarctic Expedition kufuatilia njia mtafiti Douglas Mawson aliyesafiri kwenye njia hiyo karne iliyopita.

Shokalskiy imejaa chakula cha kutosha na hakuna hatari hii ni kwa mujibu wa timu ya uokoaji.

Pamoja na kunasa, wanasayansi wanaendelea na majaribio ya kisayansi, kupima nyuzi joto kuzunguka theluji iliyoanza kupasuka.

Mamlaka ya Usalama wa Majini ya Australia ambayo ndio inayoratibu uokoaji imesema kikosi cha uokoaji cha Aurora Australis kilitarajiwa kuwasili katika eneo meli hiyo iliponasa siku ya jumapili majira ya saa 9 kwa saa za Afrika Mashariki.

Mitambo mikubwa ya kukata theluji ina uwezo wa kukata theluji yenye unene wa mita 1.6 na uwezo wa kuzoa theluji ya ukuta wa mita tatu kuzunguka eneo la Shokalskiy.

Kama operesheni hiyo ya uokaji itashindikana itabidi helkopa zitumike kuwaokoa.

RADI YAUWA WATU WANNE

Watu wanane wamekufa nchini Malawi wakati radi ilipopiga kanisa katika mji mkuu, Lilongwe.

Walioshuhudia wanasema kulitokea mtafaruku katika kanisala Sabato baada ya jengo la kanisakupigwa na radi Jumamosi jioni.

Wakuu wa afya wanasema mtoto mmoja ni kati ya watu waliokufa.

Wameeleza kuwa watu 40 wengine wanatibiwa katika hospitali kuu.

Vyombo vya habari vya Malawi vinaripoti kuwa radi iliuwa watu watatu wengine katika matukio mbali-mbali tangu majira ya mvua kuanza mwezi uliopita.

WABUNGE 15 MATATANI

Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewaanika wabunge 15, waliobainika kuchukua posho za safari bila kusafiri huku wengine wakikatisha safari zao.

Akizungumza katika mahojiano maalumu jana na mwandishi wa gazeti hili, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashililah, alisema tayari fedha hizo zimesharejeshwa kwa kukatwa kwenye mishahara yao.

Dk Kashililah alisema baadhi ya wabunge waliomba wasikatwe fedha hizo kwenye mishahara yao, badala yake wazirejeshe wao wenyewe.

Hata hivyo, Katibu huyo wa Bunge alisema wabunge hao walishindwa kusafiri kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kuwa na ugeni wa viongozi wa chama na matatizo ya kifamilia.

"Kwa mfano Komba (Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba) alishindwa kwenda kwa sababu ya kutembelewa na ziara ya Katibu wake wa Chama (Abdulrahman Kinana) muda wa safari ukamalizika hivyo akashindwa kusafiri na taarifazilikuwepo ofisini," alisema Dk Kashililah na kuongeza.

Akizungumzia safari ya Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani, Freeman Mbowe nchini Uingereza, Dk Kashililah alisema Bunge halina uwezo wa kumzuia mbunge yeyote kufanya shughuli zake safarini baada ya kumaliza jukumu lililompeleka.

Dk Kashililah alisema Mbowe alikamilisha ziara yake ya Bunge nakwamba baada ya hapo aliendelea na shughuli za chama chake nchini humo.

"Suala hili lilikuwa limebeba hisia za kisiasa, baada ya kusikika tu bungeni basi vyombo vya habari vikaanza kuwahukumu wabunge ni mafisadi bila hata kutafuta ufafanuzi kutoka wetu. Sisi taarifa hizo tulikuwa nazo kabla ya hata ya kuibuka bungeni, lakini lilivyotafsiriwa sikupenda," alisema Dk Kashililah.

Dk Kashililahb alisema, "Bunge lilikuwa limeratibu jumla ya safari mbalimbali zilizokuwa zimependekezwa na Kamati 16, lakini hazikufanikiwa kwenda zote kwa pamoja.

Alisema ziara zote za kamati huandaliwa kwa mujibu wa kanuni ya 117 ambayo inazipatia mamlaka Kamati hizo kuandaa ziara inazooana zina manufaa kwa ajili yakuboresha utendaji wake.

MWANAMKE AUAWA KIKATILI NA MUME WAKE

MWANAMKE mkazi kitongoji cha Tulieni kijijini Tumaini wilayani Mlele, Rehema Lubinza (47) ameuawa kikatili kucharangwa na mapanga na mumewe kisha mwili wake kufungiwa ndani ya nyumba yake kwa siku tatu.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kamishna Dhahiri Kidavashari alisema mauaji hayo yalifanyika mkesha wa Sikukuu ya Krismasi , Desemba 24 katika kitongoji hicho cha Tulieni, Kata ya Itenka.

Kidavashari alimtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa Mathias Mashini "Igoka' (46) mkazi wa kitongoji cha kijiji hicho cha Tulieni ambaye anadaiwa kuishi na mkewe huyo kwa miaka mingi bila kujaliwa watoto.

Akisimulia mkasa huo Kidavashari alidai kuwa kwa siku kadhaa wanandoa hao walikuwa wakishutumiana ambapo mke alikuwa akimshutumu mumewe kwa kushindwa kumpatia mahitaji muhimu ukiwemo unyumba kwa muda mrefu.

Inadaiwa kuwa baada ya kuoana mke alimkaribisha mumewe nyumbani kwake Tulieni na kufanya makazi.

Kwa mujibu wa Kidavashari, mke baada ya kuona mume haeleweki alimtaka mumewe huyo atoke nyumbani kwake (Rehema) kwa madai kuwa ameshindwa kumpatia mahitaji muhimu ukiwemo unyumba kwa muda mrefu kauli ambazo zilimkasirisha mume huyo ambaye inadaiwa hakuwa tayari kuachana na mkewe.

Inadaiwa mwanamke huyo alimfukuza mumewe huyo nyumbani hapo akisisitiza lazima aondoke ndipo mume huyo akishirikiana na mkazi wa kitongoji hicho aliyetambuliwa kwa jina la Ngussa Masengwa (39) walimshambulia mwanamke huyo kwa mapanga akiwa amelala nyumbani kwake hapo na kumjeruhi vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia umauti kisha waliufungia mwili wa marehemu ndani ya nyumba yake hiyo.

Kwa mujibu wa Kidavashari Siku ya Desemba 25 majirani baada ya kutowaona wanandoa hao huku nyumba yao ikiwa imefungwa mchana kutwa, waliamua kuwasiliana na Mathias kwa simu yake ya mkononi ambaye aliwaeleza kuwa wako Mpanda mjini wakila Sikukuu ya Krismasi.

Inadaiwa siku iliyofuata majirani wa wanandoa hao walianza kusikia harufu mbaya ikitokea ndani ya nyumba ya wanandoa hao ndipo walipolazimika kuvunja mlango wa nyumba hiyo na kushuhudia mwili wa marehemu ukiwa sakafuni.

MAPIGANO BADO YAKIENDELEA SUDAN KUSINI

Wakati juhudi zikizidi kuendelea za kujaribu kumaliza mapigano Sudan Kusini, Msemaji wa Jeshi la Sudan Kusini amesema kuna matumaini madogo ya kusitishwa kwa mapigano.

Kiongozi wa waasi Riek Machar amesema wapiganaji wake bado wanashikilia eneo kubwa la Kaskazini mwa nchi, huku majeshi ya serikali yakisema yameukomboa mji wa Malakal na wamezingira eneo la Bentiu , mjimkuu wa jimbo la Unity.

Rais Salva Kiir amesema yupo tayari kusitisha mapigano mara moja, lakini hasimu wake Bwana Machar amesema mazungumzo zaidi yanahitajika kukubaliana kusitisha mapigano na kwamba yupo tayari kufanya mazungumzo iwapo serikali itakuwa tayari kuwaachia huru wanasiasa 11 wanaomuunga mkono ambao walikamatawa wakati vurugu zilipotokea.

Machar aliyasema hayo baada ya serikali kusema ipo tayari kusitisha mapigano makubaliano yaliyopokewa kwa mikono miwili na viongozi wa Afrika Mashariki mjini Nairobi.

Mapigano yaliendelea siku ya ijumaa katika mji wa Makalal, katika jimbo la Upper Nile.

Tayari askari zaidi wa Umoja wa Mataifa wa kuongeza nguvu wamekwisha wasili nchini Sudan Kusini.

WANAJESHI WA MAREKANI WAACHIWA LIBYA

Makao Makuu ya Ulinzi nchini Marekani, Pentagon imesema wanajeshi wake wanne waliokuwa wakishikiliwa kwa saa kadhaa nchini Libya wameachiwa.

Wanajeshi hao wanne waliripotiwa kukamatwa wakati alipokuwa wakiangalia nji za kuwaondoa wafanyakazi wa Ubalozi wa nchi hiyo nchini Libya.

Walikamatwa katika katika kituo cha uchunguzi wa magari karibu na Sabratha, mashariki mwa mji mkuu wa Tripoli. Na baadae walikabidhi kwenye wizara ya mambo ya ndani.

Wanajeshi hao wanne wanasemekana walikuwa wamebeba silaha, na moja kati ya magari yao yanaripotiwa kuchomwa moto.

Picha za wanajeshi hao wakionyesha hati mbili za kusafiria pamoja na vitambulisho zilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Maafisa Ubalozi wa Marekani walikuwa wakifanya kazi zao nchini Libya chini ya ulinzi mkali baada ya shambulio la mwaka jana kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa eneo la Benghazi ambalo lilisababisha kifo cha Balozi wa Marekani nchi Libya.

MUSLIM BROTHERHOOD WACHOMA MOTO VYUO VIKUU JIJINI CAIRO

Kundi la Muslim Brotherhood kilichopigwa marufuku nchini Misri wamechoma moto majengoya vyuo vikuu viwili katika mji mkuu wa Cairo.

Wanafunzi walikuwa wakiwapiga polisi katika eneo la Chuo Kikuu cha al-Azhar , mjini Cairo.

Watu watatu waanarifiwa kufa siku ya ijumaa wakati polisi walipokuwa wakipambana na wafuasi wa Muslim Brotherhood katika eneo la Minya ya Kusini na Nile Delta.

Mamlaka nchini Misri imekuwa ikiwasaka kundi la Muslim Brotherhood tangu mwezi julai, wakati aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi ambaye ni mfuasi wa kundi hilo alipoondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo.

Tayari kundi hilo limeshatangazwa kuwa ni kundi lakigaidi tangu jumatano.

WATU WATANO WAMEKUFA BAADA YA KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI WENYE HASIRA

Watu watano wamekufa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za kuiba rambirambi ya shilingi elfu 65.

Tukio hilo limetokea mchana huu majira ya saa saba na nusu katika kitongoji cha Nyantolotolo A nje kidogo ya mji wa Geita.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa Mzee Luhemeja alifiwa na mjuukuu wake na baada ya kuisha msiba huo hapo jana watu wote walisambaa wakiwepo pia watuhumiwa waliouawa hao na kurudi makwao.

Mashuhuda wameongeza kuwa usiku huo watu wanaosadikiwa wanaodaiwa kuwa 8 walifika Nyunbani kwa mzee huyo na kuingia ndani ambapo walimkuta mtoto mdogo na kumpiga kofi baadae wakamfuata mzee wakampiga na kumuonba awapatie fedha kwa usalama wake.

Baada ya kumpiga mzee huyo walifanikiwa kuchukua shilingi elfu 60 zinazodaiwa kuwa ni pesa za rambirambi zilizotolewa wakati wa msiba baada ya mzee huyo na kufiwa na mjukuu wake.

Imeelezwa kuwa baada ya kuchukua pesa kwa mzee watuhumiwa hao na kumfata mke wake ambaye jina lake halijafahamika naye wakampiga na kumuumiza kisha kuchukua kiasi cha shilingi elfu 5 kisha wakatokomea kusikojulikana.

Baada taarifa kusambaa kuwa kuna uvamizi umetokea jeshi la jadi sungusungu lilianza msako na kufanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa akiwa na damu kwenye nguo zake na kumhoji juu ya tukiohilo, mtuhumiwa aliwataja wenzake mmoja baada ya mwingine na jeshi hilo kuwatia mbaroni wote watano.

Baada ya watuhumiwa kutiwa mbaroni wananchi wenye hasira kali walianza kuwashushia kipigo kisha kuwachoma moto hapo hapo huku mmoja kati ya hao watano akikatwa panga kwenye mguu nakudumbukizwa kwenye kisima na kufia humo humo.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya Geita Dkt Adam Sijaona amekiri kupokea miili ya marehemu majira ya saa nane na nusu mchana wa leo na gari la polisi waliofika muda mfupi baada ya tukio wakiwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoawa Geita kamishina msaidizi mwandamizi Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio na kuwataja majina yao kuwa ni Juma Patrick Kigara,Marwa,Chacha Kigara, na wawili waliofahamika kwa Eze na Shija na wa tano akiwa hajafahamika jina lake.

Kamanda Paulo amesema tayari watu watatu akiwemo kiongozi wa jeshi la jadi wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi huku jeshi likiendelea kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukiohilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwandishi wa habari hizi kutoka mkoani Geita Valence Robert asilimia kubwa ya wanaumme wamekimbia miji yao kutokana na msako mkali unaofanywa na jeshi la polisi kubaini wahusika wa tukio hilo.

JESHI LA POLISI LAONYA UPIGAJI FATAKI NA BARUTI

Jeshi la polisi katika kanda maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku ulipuaji wa mafataki kwa mtu ama taasisi yoyote katika mkesha wa mwaka mpya kutokana na kuwepo tishio la vitendo cha kigaidi katika nchi za Afrika ya mashariki.

Kamishina wa kanda hiyo Suleiman Kova amesema wameamua kufanya hivyo ili kuzuia fursa kwa magaidi kutumia uwepo wa milio ya mafataki na wao kulipua mabomu.

MATOKEO YA WANAFUNZI WALIYOMALIZA DARASA LA SABA 2013 KUJIUNGA NA SEKONDARI YATANGAZWA

Watahiniwa 411,127 wafaulu kujiunga sekondari Jumla ya watahiniwa 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2013 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule za Serikali.

Hata hivyo, kwa mujibu wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, wanafunzi 16,484 watashindwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa wakati muafaka kutokana na uchache wa madarasa.

Akitangaza idadi ya wanafunzi walichoguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katibu Mkuu Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Jumanne Sagini amesema kutokana na tatizo la upungufu wa madarasa ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zina kamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa hadi ifikapo machi mwaka mwakani.

Aidha, Sagini anaeleza takwimu zawanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.

Amesema idadi ya ufaulu kwa mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana na hivyo kusababisha kuwepo cha changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 412.

Jumla ya wanafunzi 867,983 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 455,896 sawa na asilimia 52.52 na wavulana 412,087 sawa na asilimia 47.48.

KOCHA MKUU WA ITALIA CESARE PRANDELI KUSHUHUDIA UFUNGUZI WA MAPINDUZI CUP

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya Italia, Cesare Prandeli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano ya soka ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kutimua vumbi Januari mosi.

Mechi ya ufunguzi itakayoshuhudiwa na kocha Prandelini kati ya Simba na FC Leopard ya Kenya itakayochezwa saa mbili usiku kwenye Uwanja wa Amaan.

Kabla ya mechi hiyo, jioni ya siku hiyo kutakuwa na mechi kati ya wenyeji KMKM na KCC ya Uganda. Hayo yamebainishwa na Msemaji wa Kamati ya michuano hiyo, Farouk Kareem alipozungumza na waandishi wa habari jana.

Alisema kuwa uamuzi wa kumualikakocha huyo kuwa mgeni rasmi, umefikiwa kwa pamoja na viongozi wa kamati hiyo waliokutana juzi visiwani Zanzibar.

Alisema maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo yamekamilika na timu zote kutoka nje ya Zanzibar zinatarajiwa kuwasili Desemba 30.

Alisema kuwa Kamati imeamua kumuita kocha huyo kuwa mgeni rasmi kutokana na mafanikio yake makubwa katika soka nchini kwake ambayo yanaonekana ulimwenguni kote.

Aidha alisema kuwa pamoja na kumteua kocha huyo kuwa mgeni rasmi pia kamati hiyo imefanya marekebisho ya michezo ya uwanja wa Gombani ambayo yalionekana kuzibana sana timu katika michezo yao.

Alisema kuwa katika marekebisho hayo michezo yote ya Pemba itachezwa mmoja kwa siku ambapo siku ya kwanza kutakuwa na mchezokati ya Clove Stars na Mbeya City nasiku itakayofuata Chuoni atacheza na URA ya Uganda.

Jumla ya timu 12 zinatarajiwa kushiriki katika michuano hiyo ambayo itachezwa katika vituo viwili, huku bingwa mtetezi ni AzamFC ya Dar es Salaam.

JELA MIAKA 30 KWA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA

WAKAZI wawili wa vijiji vya Nyabisaga Kata ya Pemba wilayani Tarime mkoani Mara, Mhoni Chacha Ng'wena (25) na Isack Magawi Meng'anyi (30), wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Wilaya ya Tarime.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Adrian Kilimi alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka,ukiongozwa na Inspekta Usu, George Lutonja kwamba washitakiwa walitenda kosa la unyang'anyi wa silaha.

Alisema Mahakama imeridhika na ushahidi, ulioambatana na vielelezovya mlalamikaji, vilivyokamatwa kwa watuhumiwa hao, vikiwemo baiskeli, simu ya mkononi, viatu na tochi.

Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Usu Lutonja alidai kuwa washitakiwa hao pamoja Januari 3, mwaka huu saa 12 alfajiri, wakiwa na silaha za jadi za mapangana marungu walivamia na kuingia ndani ya nyumba ya Selestin Omahe, mkazi wa Sirari na kumshambulia na familia yake na kupora vitu vya ndani, vikiwemo baiskeli aina ya Phoenix, simu ya mkononi, viatu na tochi, vyote vyenye thamani ya Sh 284,000.

Alidai baada ya tukio hilo, mlalamikaji Omahe alipiga yowe, kuomba msaada na majirani, ambao walitokea pamoja na polisi, waliokuwa doria eneo hilo. Hata hivyo, hawakufanikiwa kukamata washitakiwa hao wakiwa na mali za mlalamikaji.

Lakini, baada ya kukamatwa, washitakiwa walifikishwa kwenye vyombo vya sheria, ambapo upandewa mashitaka ulileta mashahidi wanne na vielelezo, vilivyokamatwakwa washitakiwa wakati wa tukio hilo. Washitakiwa hao waliomba wasamehewe.

Mwendesha Mashitaka aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa. Hakimu Kilimi alisema anawahukumu kwenda jela miaka 30 kila mmoja ili iwe fundisho kwa watu wenye tamaa ya kupora mali za watu.

WALAJI WA KITIMOTO HATARINI KUPATA KIFAFA

CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) kimehadharisha walaji wa nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa.

Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.

Hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya, zimebaini nguruwe wengi wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark(DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.

"Majibu ya sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii. "Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamojawa tatizo hili kati ya watafiti na Serikali," alisema Profesa Lekule.

Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha binadamu.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao.

Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri, minyoo hiyohumwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.

Alisema athari za kuenea kwa maambuziki hayo inaweza kutokea katika miji mikubwa ikiwamo Dar esSalaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo.

"Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu, hivyo ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara, Serikali na wataalamu wa afya katika kufikia hatua ya kumaliza changamoto hii unahitajika," alibainisha Profesa Lekule.

MWANAMKE WA KITANZANIA AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYEVA.

Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao.

Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.

Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.

Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau.

Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013

MOSHI WALETA TAFRANI KATIKATI YA JIJI

Taharuki na hofu ya moto imewakumba wakazi wa jiji la Dar es Salaam maeneo ya katikati ya jiji kufuatia Moshi mkubwa uliokuwa ukitoka katika mojawapo ya majengo ya benki kuu ya Tanzania na kusababisha baadhi ya wakazi hao pamoja na jeshi la polisi akiwemo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa kipolisi wa Ilala kufika haraka katika eneo la tukio kutokana na hofu ya kuungua kwa benki hiyo.

Taarifa za awali ambazo zilianza kusambaa zilikuwa zikidai kuwa ni hoteli ya Kilimanjaro Kempisk ndio iliyokuwa ikiungua na kusababisha waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wakazi wa jiji kufika katika eneo hilo na baadae kubaini moshi mkubwa ukifuka kutoka katika mojawapo ya majengo ya benki kuu ya Tanzania ambapo baadhi ya askari wa jeshi la polisi pamoja na wananchi wamekusanyika kuishuhudia hali hiyo.
Kitambo kidogo baada ya wananchi kukusabyika baadae kikosi cha zimamoto nacho kikawasili katika eneo la tukio tayari kabisa kukabiliana na hatari ya moto ambapo hata hivyo walilazimika kuondoka katika eneo la tukio huku kiongozi wa msafara huo aliyejitambulisha kwa jina la sifuri simba akidai kuwa wamepata taarifa ya uwepo wa tukio la moto katika benki kuu.

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Ilala Marietha Minangi ameviambia vyombo vya habari kuwa hakuna tukio lolote la ajali ya moto bali ni jenereta la benki hiyo lilikuwa likijiwasha mara baada ya kukatika kwa umeme wa Tanesco.

Hata hivyo maelezo ya kamanda huyo yanatofautiana na maelezo ya mmoja wa walinzi wa benki hiyo ambaye hakutaka kupigwa picha wala kutaja jina lake kuwa moshi huo umesababishwa na zoezi la kawaida la kusafisha mtambo ambao hata hivyo alikataa kuutaja mtambo huo uliokuwa ukisafishwa ni wa shughuli gani.

PINDA APOKEA PIKIPIKI 44 KUTOKA UBALOZI WA CHINA

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amepokea pikipiki 44 zikiwa ni msaada kutoka Ubalozi wa China na Kampuni ya Fu-Tang ya kutoka China.

Alikabidhiwa msaada huo jana mchana mbele ya viongozi wa Wilaya ya Mlele katika hafla fupi iliyofanyika kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele, mkoani Katavi na kushuhudiwa na wakazi wa kijiji hicho.

Akizungumza na viongozi wa wilayahiyo pamoja na wakazi wa kijiji hicho kabla ya kukabidhi msaada huo, Balozi wa China hapa nchini, Dk Lu Youqing alisema anaamini kupatikana kwa pikipiki hizo kutasaidia kuleta maendeleo ya haraka ya wilaya hiyo."Tunataraji matumizi ya pikipiki hizi yatasaidia kuleta maendeleo ya haraka na hatimaye kuongeza kipato cha wakazi wa wilaya hii," alisema Balozi Lu ambaye ofisi yake imekabidhi pikipiki 20.

Alisema wakazi wa nchi yake wanafikia bilioni 1.3 na yeye anatamani kuona walau kila raia wa China akinunua walau kilo moja ya chakula kutoka hapa nchini ili waweze kuongeza soko kwa mazao yanayozalishwa na wakulima wa Tanzania.

Naye Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza pikipiki cha FEKON ambayo ni kampuni tanzu ya Fu-Tang, Zheng Bing alisema mara taratibu zitakapo kamilika, wana lengo la kujenga kiwanda cha kutengeneza pikipiki na kompyuta ili kuongeza ajira kwa Watanzania. Kampuni hiyo ilikabidhi pikipiki 24.

Akipokea msaada huo, Waziri Mkuu alimshukuru Balozi Lu na kampuni ya Futang kwa msaada huo na kuahidi kuzigawa ili ziwasaidie watendaji kusimamia kazi na hivyo kuharakisha kuleta maendeleo kwa wakazi wa wilaya hiyo.

"Tuna kata 24 kwenye wilaya yetu kwa hiyo kila kata itapewa pikipiki moja. Hiyo pikipiki si ya Katibu Kata binafsi bali ni ya Kata, kwa hiyo Katibu Kata atakuwa ndiyo msimamizi...," alisema.

Waziri Mkuu ambaye yuko kijijini kwake Kibaoni kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka, alisema pikipiki saba zitapelekwa kwenye vituo vitano vya afya vya Mamba, Usevya, Inyonga, Katumba na Kanoge na Zahanati za Nsimbo na Kasansa.

"Pia tutapeleka pikipiki nyingine nane katika Shule za Sekondari za Sitalike, Machimboni, Magamba, Nsimbo na Mtapenda. Nyingine ni Utende, Inyonga na Kasokola," aliongeza.

Mbali na hao, wengine watakaofadika na mgao huo ni watendaji wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mlele ambao watapatiwa pikipiki moja, jumuiya za chama katika wilaya hiyo zitapatiwa pikipiki tatu na moja iliyobakia itagawiwa kwa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi.

Kuhusu uzalishaji wa chakula cha kutosha wakazi bilioni 1.3 wa China, Waziri Mkuu alisema itabidi Tanzania izalishe magunia milioni 13 ya nafaka ili iweze kufikisha lengo alilolisema Balozi Lu.

Waziri Mkuu Pinda alishapokea msaada wa pikipiki 23 kutoka kwa wafadhili wengine na kugawa pikipiki sita kwa Jeshi la Polisi, pikipiki 13 kwa vikundi vya vijana na zilizobakia nne alizigawa kwa shule za sekondari.

TMA YAHADHARISHA WAKAZI WA PWANI YA BAHARI YA HINDI

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imehadharisha juu ya kutokea upepo mkali utakao ambatana na mawimbi makubwa katika maeneo ya pwani mwa bahari ya Hindi leo.

Taarifa iliyotolewa na TMA kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa tukio hilo litatokea leo, wakati wananchi wengi wakisherehekea sikukuu ya Krismasi.

Upepo huo ulielezwa na TMA kwamba ni mkali utakaovuma kilometa 40 kwa saa ambapo mawimbi ya bahari yanakadiriwa yatazidi kimo cha meta mbili.

Tukio hilo kwa mujibu wa TMA lina uhakika wa kutokea kwa asilimia 60 huku maeneo yatakayoathirika zaidi kuwa ni Tanga, Dar es Salaam,Pwani, Lindi na Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba.

"Hali hii inatokana na kuimarika kwa mfumo wa mgandamizo mdogo wa hewa katika bahari ya Hindi, karibu na visiwa vya Comoro. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta upepo kutoka pwani ya Somalia," ilisema taarifa hiyo.

TMA katika taarifa yake iliwahadharisha wakazi wa maeneo hatarishi kuchukua hadhari ili wasikumbwe na majanga yatakayosababishwa na upepo huo.

Hata hivyo, TMA ilieleza kuwa inaendelea kufuatilia hali hiyo na itatoa taarifa ya mrejeo.

MERRY CHRISTMAS

Tunawatakia heri ya sikuku za mwisho wa mwaka, Heri ya sikuku ya Noel wasomaji wa mtandao huu. Sherekeheni kwa furaha na upendo.

Kumbuka usalama wako na wa mwenzako katika maeneo yote mtakapo kuwepo, katika fukwe za bahari, ziwa makanisani au kumbi za starehe.
Tahadhari Usiendeshe chombo cha usafiri cha moto kama umetumia kilevi chochote.

MERRY CHRISTMAS EVERYONE

WANANCHI WENYE HASIRA WAMPIGA MPAKA KUMUUWA MTU MOJA ANAESADIKIWA KUWA MCHAWI

WANANCHI wenye hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.

Kijana huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za kishirikina.

Kabla ya kufariki alisema"mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu"
"Lakini mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu"
Hata hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka kwao.

Kwa mujibu wa mashuhuda wengine wa tukio hilo walisema baada ya kuanguka eneohilo walimkimbiza hadi ndani kwa mtu na kumtoa pamoja na zana zake za kichawi ambapo walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na ungo wenyewe ndipo wakaendelea kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta.

"Huyu jamaa bwana, ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu kama hawa tumemtoa huko alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi hapa baada ya kuhakikisha zana zake zote tumezichoma moto" alisema mkazi mmoja wa maeneo hayo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi (Kituo cha Polisi Kimara) kilichopo Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja kumuokoa kija huyo ingawa walipewa taarifa mapema.

"Sisi tumepiga simu kituoni hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia tukio limeanza saa 12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu uzembe"alisema mkazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Ali.

Ingawa katika tukioa hilo kulitokea mkazi mmoja aliyekuwa na silaha aina ya bastola na kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatawanyisha wananchi hao wenye hasira kali, haikusaidia kitu kwani waliendelea kumpiga hadi wakahakikisha amekufa.

Mtanzania lilibisha hodi katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana.

Aidha wakuu hao OC CID (ASP) M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawa kuwapo kituoni wakati Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili kudhibitisha tukio hilo kutokana na namba yake ya simu kuita bila kupokelewa.

MAUWAJI MAKUBWA YARIPOTIWA SUDAN KUSINI

Taarifa mpya zimeibuka zikieleza kuwepo kwa mauaji ya kikabila yaliyofanyika katika kipindi cha zaidi ya wiki moja ya ghasia nchini Sudan Kusini.

Mwandishi wa habari mmoja kutoka mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, amewakariri watu walioshuhudia mauaji hayo wakisema zaidi ya watu 200, wengi wao wakitoka kabila la Nuer , wameuawa kwa kupigwa risasi na majeshi ya usalama.

Mtu mwingine kutoka Juba amesema watu wenye silaha kutoka kabila la Dinka walikuwa wakiwashambulia kwa risasi watu kutoka maeneo ya Nuer.

Ghasia hizo zimekuja huku kukiwa na hali ya kugombea madaraka kati ya Rais Salva Kiir, kutoka kabila la Dinka, na aliyekuwa naibu wake Riek Machar kutoka kabila la Nuer.

Serikali ya Sudan Kusini imekanusha kuhusika na ghasia za kikabila.

Taarifa hizo zimekuja wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza askari 5,500wa Umoja wa Mataifa katika kikosi cha askari 7,000 wa Umoja wa Mataifa waliopo Sudan Kusini.

Waasi wanaomuunga mkono makamu wa rais aliyefukuzwa Riek Machar walitwaa miji mikubwa wiki iliyopita.

Maelfu ya watu wamekimbia mapigano.

WANAMGAMBO WA KIISLAMU WAUAWA HUKO NIGERIA

Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa wanamgambo hamsini wa Kiislamu waliuawa siku ya Jumatatu, wakati walipokuwa wakijaribu, kuvuka mpaka na kuingia taifa jirani la Cameroon.

Tukio hilo lilitokea baada ya wapiganaji wa Boko Haram, kushambulia kituo kimoja cha kijeshi Kaskazini Mashariki mwa mji wa Bama siku ya Ijumaa.

Waasi hao wenye msimamo mkali, walitoroka mji huo huku wakiwa wamewateka nyara wanawake na watoto.

Wanajeshi kumi na watano wa serikali na raia watano pia waliuawa.

Jeshi la Nigeria limekuwa likifanya operesheni ya kuwasaka wapiganaji hao wa Kiislamu, Kaskazini Mashariki na nchi hiyo tangu mwezi Mei mwaka huu, wakati serikali ilipotangaza hali ya hatari katika eneo hilo.

Kwa wakati huo, wapiganaji wa Boko Haram, walikuwa wametimuliwa kutoka miji mikuu, lakini mashambulio yaliendelea zaidi katika maeneo ya vijijini.

SNOWDEN ASEMA LENGO LAKE LIMEKAMILIKA

Mfanyakazi wa zamani wa muda katika Shirika la Usalama la Marekani, NSA, Edward Snowden, ambaye alifichua kuwepo kwa mipango ya Marekani kufuatilia taarifa za mawasiliano ya watu, amesema amefaniskisha lengo lake.

"Kwa kuridhika binafsi, mpango wangu tayari umefanikiwa," ameliambia gazeti la Washington Post.

"Tayari nimeshinda," amesema Bwana Snowden, ambaye ufichuaji wake mkubwa umesababisha Marekani kuangalia upya sera yake ya ufuatiliaji wa taarifa za siri za watu na mashirika.

Snowden mwenye umri wa miaka30, alifanya mahojiano na gazeti hilo nchini Urusi, ambako alipewa hifadhi ya ukimbizi wa muda tarehe Mosi Agosti.

Bwana Snowden aliondoka Marekani mwishoni mwa mwezi Mei, akichukua kiasi kikubwa cha nyaraka za siri kuhusu mpango wa udukuzi wa Marekani.

Anakabiliwa na mashitaka ya ujasusi nchini Marekani.

NSA iligundulika kuhusika katika udukuzi wa data za simu. Taarifa za kina za watu na taasisi zilizolengwa na udukuzi wa mashirika ya ujasusi ya Uingereza na Marekani zilichapishwa wiki iliyopita na magazeti ya The Guardian, The New York Times na Der Spiegel.

Magazeti hayo yamesema orodhaya watu na taasisi zipatazo 1,000 zilizolengwa ni pamoja na Kamishna wa Umoja wa Ulaya, mashirika ya kibinadamu na maafisa wa Israel akiwemo waziri mkuu.

Makampuni makubwa ya teknolojia ya mawasiliano nchini Marekani ya Google, Microsoft na Yahoo yanachukua hatua ya kuzuia ukusanyaji wa data unaofanywa na serikali yao.

Mwezi Oktoba, habari ziliposambaa kuwa NSA lilikuwa limedukua mazungumzo ya simu ya kiongozi wa Ujerumani Chansela Angela Merkel, kulisababisha mvutano wa kidiplomasia kati ya Ujerumani na Marekani.

Rais wa Brazil Dilma Rousseff naye pia alikasirishwa na taarifa kwamba shirika la ujasusi la Marekani, NSA, liliingilia mtandao wa kompyuta wa kampuni ya mafuta ya serikali ya Brazil, Petrobras ili kukusanya taarifa na mawasiliano ya barua pepe na simu.

JENGO LA USALAMA NCHINI MISRI LASHAMBULIWA

Mlipuko mkubwa katika jengo moja la usalama kaskazini mwa Misri umesababisha watu wapatao 14 kuuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa.

Maafisa nchini humo pamoja na vyombo vya habari vya serikali wamesema, mlipuko huo, ambaoumeripotiwa kusababishwa na bomu lililotegwa katika gari, umesababisha kuporomoka sehemu ya jengo hilo katika mji wa Mansoura.

Waziri Mkuu wa Mpito Hazem Beblawi ameelezea tukio hilo kama "kitendo cha ugaidi".

Mashambulio dhidi ya majeshi yausalama na polisi nchini Misri yameongezeka tangu jeshi nchini humo limtoe madarakani rais wa Kiislam Mohammed Morsi mweziJulai, 2013.

Mpaka sasa hakuna kikundi kilichodai kuhusika na shambulio hilo.

Bwana Beblawi amekiambia kituocha televisheni cha ONTV:

"Serikali itafanya kila iwezalo kuwasaka wahalifu wote waaliotekeleza, kupanga na kusaidia kufanyika kwa shambuliohilo."

Athari za mlipuko huo zilipatika katika maeneo ya umbali wa kilomita 20 kutoka eneo la tukio.

Televisheni ya Misri imewaomba watazamaji wake kwenda hospitali kutoa damu.

Kikundi cha Muslim Brotherhood - kinachomuunga mkono Bwana Morsi na kilichopigwa marufuku na serikali ya mpito ya Misri, kimelaani shambulio hilo.

"Muslim Brotherhood kinachukulia kitendo hiki kama shambulio la moja kwa moja katika umoja wa watu wa Misri," kimesema katika taarifa yake.


Mkuu wa usalama amejeruhiwa'

Mlipuko huo ulipiga jengo hilo Jumatatu usiku wa manane.Zaidi ya watu 100 walijeruhiwa.

Taarifa za vyombo vya habari zinasema mkuu wa usalama wa jimbo ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa.

Mlipuko huo ulivunja vioo vya madirisha ya majengo jirani na athari zake kufika umbali wa kilomita 20 kutoka eneo la tukio.

Mansoura - mji wenye idadi ya watu 480,000 - ni makao makuu ya mkoa wa Dakahliya katika jimbo la Nile Delta.

Tangu kuondolewa madarakani kwa Bwana Morsi - rais wa kwanza wa Misri aliyechaguliwa kwa njia za kidemokrasia - wafuasi wake wamekuwa wakiandaa maandamano makubwa wakitaka kuachiliwa huru kwa kiongozi wao.

Zaidi ya wanachama 2,000 wa Muslim Brotherhood wamekamatwa, na 450 kati yao, siku ya Jumatatu walianza mgomo wa kususia chakula wakipinga kudhalilishwa."

Bwana Morsi kwa sasa anakabiliwa na kesi tatu tofauti zauhalifu zikihusishwa na nafasi yake akiwa madarakani.

Kesi ya kwanza ilifunguliwa tarehe Novemba, lakini imeahirishwa hadi Januari 8, 2014.

WAZIRI MKUU AWASILI MKOANI KATAVI KWA MAPUMZIKO YA CHRISTIMAS

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda jana mchana aliwasiri mkoani Katavi kwa ajiri ya mapumziko ya Krismasi na mwaka mpya na kupokewa na mamia ya wakazi wa mji wa Mpanda waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dokta Rajabu Rutengwe kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda Waziri Mkuu Pinda aliwasiri kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda majira ya saa nane na nusu mchana na kisha alikagua vikundi mbalimbali vya ngoma ya asili akiwa amefuatana na Balozi wa China Nchini Tanzania Baada ya kugagua vikundi hivyo vya ngoma Waziri Mkuu Pinda alielekea kijijini kwake kata ya Kibaoni kwa ajiri ya mapumziko ya Krismasi na mwaka mpya.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi siku ya jumanne ya tarehe 24 Desemba 2013.

Waziri Mkuu Pinda atatembelea na kukagua barabara inayojengwa kwa kiwango cha rami kutoka Mpalamawe Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa hadi Kibaoni Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.

Waziri Mkuu Pinda katika ukaguzi huo wa barabara ya Mpalamawe Kibaoni atakuwa ameongozana na Balozi wa China Nchini Tanzania ambapo barabara hiyo inajengwa na kampuni ya kutoka chIna

ACHEZEA KICHAPO MKAPA KUFA BAADA YA KUKUTWA UCHI KWENYE MACHIMBO YA DHAHABU

Mtu mmoja Yunge Maboja (70) Mkazi wa Kijiji cha Kapanda Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amefariki dunia baada ya kushambuliwa na wananchi kwa kupigwa na silaha za jadi ngumi na mateke baada ya kukutwa uchini usiku wa manane kwenye shimo la kuchimba dhahabu na kutuhumiwa kuwa alikuwa akiroga ili mwenye shimo hilo asipate madini ya dhahabu Kwa mijibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina Dhahili Kidavashari alisema tukio hilo la kushambuliwa kwa mtu huyo lilitokea hapo juzi majira ya saa saba usiku katika kijiji hicho cha Kapanda Alisema wiki tatu kabla ya tukio hilo marehemu alimuazimisha Idd Kipara shoka ambalo alikuwa akilitumia katika shughuli zake ulinzi katika shimo la kuchimba madini aina ya dhahabu la Juma Ngegeshi.

Alieleza marehemu alianza kumtafuta mtu aliye muazimisha shoka na ndipo siku hiyo ya tukio majira ya saa saba usiku alipofika kwenye shimo la kuchimba dhahabu la mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja La Abui ambapo alichungulia ndani ya shimo ambalo ndani yake walikuwemo watu wili wakifanya shughuli hizo za uchimbaji wa madini Kamanda Kidavashari alisema watu hao waliokuwa ndani ya shimo walishitushwa na kitendo cha marehemu kuwachungulia mida hiyo ya usiku wa manane wakiwa ndani ya shimo hivyo iliwalazimu watoke nje ya shimo hilo la kuchimba madini ya dhahabu ndipo walipotoka na kumkuta marehemu akiwa uchi.

Alisema ndipo watu hao wawili Abui na Hassan walipoanza kumshambulia marehemu kwa kashfa za kuwa marehemu kuwa ni mchawi na ndio maana amefika kwenye shimo lao akiwauchi na ndio maana wamekuwa hawapati madini ya dhahabu kwenye shimo hilo kwa muda mrefu.

Kidavashari alieleza ndipo walipoamua kumkamata huku akiwa uchi na kuanza kumshambulia kwa fimbo na mateke na kumlazimisha awapeleke kwa mwenyeji wake Juma Ngegeshi ili awapatie uchawi ambao ulikua umebaki atowe uchawi uliobaki nyumbani kwake.

Walipofika nyumbani kwa Juma Ngegeshi walimkuta mkewe aitwaye Asha Shaban ambae baada ya kuwafungulia mlango walimtaka awaonyeshe uchawi ilikuwa umebaki ndani ya nyumba hiyo na Asha aliwajibu ndani ya nyumba yake hakuna kitu kama hicho na hafamu kitu kama hicho na kisha alianza nae kushambuliwa kwa fimbo usoni na mgongoni.

Alieleza hari hiyo ilimfanya Asha apige mayowe ya kuomba msaada na ndipo majirani walipofika hapo na kukuta marehemu yuko uchi nao waliungana kuaanza kumshambulia yeye pamoja na Asha hari ambayo ilimfanya Asha ajifungie ndani ya nyumba yake.

Kidavashari alieleza majeruhi wote wawili walifikishwa kituo cha polisi cha Mpanda na kisha walipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda na marehemu alilazwa kutokana na hari yake kuwa mbaya na arifariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu.

Jitihada za kuwasaka wahusika wa tukio zilifanyika ambapo watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano ambao ni Yunge Hassan 43 mkazi wa Mtaa ya Kashaulili na Ayub Samwel 30 Mkazi wa Kijiji cha Kapanda na wengine wamekimbia.

Chanzo: Katavi yetu

MCHINA ATUMBUKIA SHIMONO NA KUFA

Raia mmoja wa Nchi ya China Chen Gungson mmiliki wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya Got Accdent On Ming Camp amefariki dunia baada ya kutumbukia ndani ya shimo ambalo lilikuwa la mgodi wa dhahabu katika machimbo ya dhahabu ya Ibidi Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi Tukio hilo la kutumbukia kwenye shimo la mgodi huo na kusababisha kifo cha Raia huyo wa China lilitokea hapo jana majira ya saa tatu na nusu asubuhi katika eneo hilo la Ibindi.

Raia huyo wa China alipatwa na mauti hayo wakati akiwa anakagua maeneo ambayo anafanyia shughuli zake za uchimbaji wa madini aina ya dhahabu na ndipo alipoteleza na kutumbukia ndani ya shimo hilo la mgodi wa dhahabu Baada ya kutumbukia jitihada za kumwokoa zilianza kufanywa na watumishi wenzake wakiwemo na raia wengine saba wa Raia wa China na wananchi wanaofanyashughuli kwenye maeneo hayo ambapo waliigiza kamba ndani ya shimo ili marehemu aweze kuishika na wao waweze kumvuta kwa nje Hata hivyo baada ya kuona kamba waliojaribu kumwokolea haija shikwa Raia wanne wa China waliingia ndani ya shimo hilo kwa kutumia kamba na waliweza kutoka na marehemu huyo na wao hawakujua kama ameishafariki dunia na kumbiza hospitali ya Wilaya kwa kutumia gari yao Aina ya TOYOTA Walipofika Hospitalini walimshusha haraka haraka marehemu kwa kutumia machela na kwenda kumlaza katika kitanda kilichopo wodi namba moja na kuwataka wauguzi wampe huduma ndugu yao huyo ya matibabu Mganga wa zamu Dokta Benald Mbushi alifika kwenye wodi hiyona alipompima Raia huyo wa China aliwaeleza kuwa Mchina huyo ameisha fariki hata kabla ya kufikishwa hospitalini hapo.

Kwa upande wake Dokta Benald Mbushi ameeleza kuwa mwili wamarehemu huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuifadhi maiticha hospitali ya wilaya ya Mpanda ukisubili kufanyiwa uchunguzi kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu zake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi amethibitisha kutokea kwa kifo cha Raia huyo wa kutoka nchi ya China na ametowa wito kwa watu kutotembea karibu na mashimo ya migodi hasa katika kipindi hiki cha masika.

CHEKA ACHEZEA KICHAPO KWA KO

BONDIA Francis Cheka juzi alichezea kichapo cha KO kutoka kwa Fedor Chudinov wa Urusi na kuvuliwa rasmi mkanda wa WBF alioupata baada ya kumpiga bondia Phil Williams wa Marekani kwenye pambano la lisilokuwa na ubingwa la raundi 8.

Mpambano huo ulifanyika Urusi katika Ukumbi wa Dynamo Palace, Krylatskoye ni wa kwanza kuchapwa baada ya kutawazwa kuwa bingwa wa WBF, mkanda ambao anaushikilia lakini kutokanana sheria za WBF ukipigwa kwa KO kwenye mpambano wa kirafiki unapoteza mkanda huo.

Kwa kipigo hicho Cheka ameporomoka kwenye viwango vya ubora vya WBF toka nafasi ya 20 hadi 48 na inamlazimu kufanya kazi ya ziada kuhakikisha kuwa anaomba kugombea mkanda wa WBF kabla ya Januari mwakani.Akizungumza kwa masikitiko promota J. Msangi alisema kuwa Cheka hakupaswa kupigana pambano kama hilo kwani alikuwa hajajiandaa vya kutosha na bado yeye alikuwa anamwandalia pambano ambalo angepigana Februari, mwakani.

"Cheka alipokuwa amefikia hakupaswa kupigana mapambano ya kulipwa dola 10,000, kwa sasa yeye anatakiwa kupigana pambano ambalo anatakiwa kulipwa kuanzia dola 30,000 hadi 60,000 lakini nimesikitika zaidi baada ya kusikia kapigwa kwa KO raundi ya tatu na kupoteza mkanda wake," alisema Msangi.

Pia Msangi alisema kuwa watawasiliana na WBF kuomba Cheka agombanie huo mkanda hapa nchini mapema Januari 24, mwakani ili iwe rahisi kwake kushinda.

Katika pambano hilo bondia mwingine wa Tanzania Allan Kamote naye alipigwa kwa KO raundi ya saba kwenye pambano ambalo lilikuwa la raundi tisa.

Taarifa zilizopo kwa mwaka huu mabondia 16 waliokwenda kucheza nje ya nchi hakuna hata mmoja aliyeshinda jambo ambalo linaacha maswali mengi kwa wadau wa ngumi.

KENYA WAZIMA MITAMBO YA ANALOGIA

Vituo vitatu vikubwa vya televisheni nchini Kenya vimezima mitambo yao baada ya Mahakama Kuu nchini humo kutoa uamuzi kwamba vinapaswa kuingia katika mfumo wa utangazaji wa dijitali na kuachana na mfumo wa analojia.

Vituo hivyo vya Standard Group, Nation Media Group na Royal Media Services, awali vilikwenda mahakamani kuomba kuahirishwa muda wa kuhamia kwenye mfumo huo, hadi masuala kadhaa yatakapofafanuliwa

TANESCO KUPANDISHA BEI YA UMEME 2014

Watanzania wanataraji kuuanza mwaka 2014 kwa machungu ya kupanda kwa bei ya umeme, ambapo (leo) mamlaka ya udhibitiwa nishati na maji, EWURA imetangaza rasmi ongezeko la gharama za nishati hiyo kwa asilimia 39.19, kuanzia January mosi, mwakani.

Bei za umeme zinazotumika hivi sasa ziliidhinishwa January mwaka2012, ambapo zilipanda kwa asilimia 40.29, ikilinganishwa na maombi ya shirika la umeme, TANESCO lililopendekeza kupanda kwa bei kwa asilimia 155.

Watumiaji wakubwa wa umeme wa majumbani, biashara na viwanda vidogo vidogo, ambao wako kwenye kundi la wateja la T1, wanatarajia kuathirika zaidi ambapo ongezeko kwenye kundi hilo ni shilingi 85 kwa kila unit.

Kundi la T3-MV lenye wateja wakubwa waliounganishwa katika msongo wa kati, bei ya nishati imeongezeka kwa shilingi 45 na kundi T3-HV la wateja waliounganishwa kwenye msongo wa juu wakiongezewa kwa shilingi 53 kwa unit.

Kwa mujibu wa TANESCO, maombi haya yanalenga kuliwezesha shirika kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, kujiwezesha kukopesheka kwa masharti nafuu,kuweza kukabili ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye gridi ya taifa na uwezo wa kufanya marekebosho ya miundombinu yamara kwa mara.

Hasara kwenye shirika hilo la TANESCO linalojiendesha kwa hasara hivi sasa imefikia shilingi Bilioni 223.4, toka Bilioni 47.3 la mwaka 2010, na deni la zaidi ya shilingi Bilioni 400, huku pia shirika likigubikwa na kashfa ya ubadhirifu wa fedha.

Agizo hili la kupanda kwa bei za umeme, linafuta agizo la January 24, 2013 la TANESCO linalohusu marekeboshi ya bei za umeme.

SERIKALI YA SUDAN KUSINI YAJARIBU KUTWAA MAJIMBO YALIYOCHUKULIWA NA WAASI

Serikali ya Sudan Kusini imejaribu leo kuyatwaa tena majimbo mawili yaliyochukuliwa na wanajeshi waasi wanao mtii makamu wa rais wa zamani, Riek Machar, huku mapigano katika taifa hilo changa, yakiwa yameingia wiki yake ya pili.

Wakati huo huo, Rais wa Marekani, Barack Obama ameahidi kuchukua hatua zaidi iwapo itahitajika.

Kwa upande wake Umoja wa Mataifa umeahidi kupeleka vikosi zaidi vya kulinda amani Sudan Kusini

BAADA YA MECHI YA NANI MTANI JEMBE, KIBARUA CHA KOCHA WA YANGA ASITISHIWA MKATABA WAKE

Uongozi wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.

Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.

Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.

Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.

Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.

Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix"Minziro".

Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapo kamilika tutawajulisha.

Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.

Mwisho tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL.

Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati ya Mashindano

Young Africans Sports Club.

DAR ES SALAAM

23 Disemba, 2013

TWEET YA KIBAGUZI YAMPONZA MZUNGU, AFUKUZWA KAZI

Mwanamke mmoja wa kizungu Justine Sacco amejikuta akipoteza kibarua chake kutokana na tweet yake ya utani lakini ya kibaguzi aliyoiandika Ijumaa ya wiki iliyopita.

Tweet hiyo iliyosomeka 'Going to Africa. Hope I don't get AIDS. Just kidding. I'm white!' akimaanisha (Naenda Afrika. Naamini sitapata UKIMWI. Mimi mzungu).

Kwa mujibu wa BBC, Kampuni ya Inter Actice Corp (IAC) ya Marekani aliyokuwa aikifanya kazi Justine kama Afisa wa juu wa PR, wamemuachisha kazi mara mbili kumuachisha kazi mara moja mwanamke huyo kwa maslahi ya kampuni.

"The offensive comment does not reflect the views and values of IAC. We take this issue very seriously, and we have parted ways with the employee in question. There was no excuse for the hateful statements that had been made, and judging from the decision to".

Baada ya tweet hiyo kusambaa kwenye mitandao Ijumaa bado haikufahamika kama ni kweli Justine mwenyewe alitweet au akaunti likuwa hacked, lakini sasa imethibitika kuwa ni kweli mwanamke huyo alitweet kwa utani na ameomba radhi baada ya maji kumwagika (japo hayawezi kuzoleka tena).

Amewaomba msamaha watu wa Afrika Kusini ambao amedai amewakosea heshima kwa tweet ya kijinga, na kuongeza kuwa hata yeye alizaliwa Afrika Kusini hivyo amepatwa na aibu kubwa kwa kile alichokifanya.

"Words can not express how sorry I am, and how necessary it is for me to apologize to the people of South Africa, who I have offended due to a needless and careless tweet. There is an AIDS crisis taking place in this country, that we read about in America, but do not live with or face on a continuous basis. Unfortunately, it is terribly easy to be cavalier about an epidemic that one has never witnessed firsthand. For being insensitive to this crisis – which does not discriminate by race, gender or sexual orientation,but which terrifies us all uniformly– and to the millions of people living with the virus, I am ashamed. This is my father's country, and I was born here. I cherish my ties to South Africa andmy frequent visits, but I am in anguish knowing that my remarks have caused pain to so many people here; my family, friends and fellow South Africans. I am very sorry for the pain I caused."

Justine ameendelea kushambuliwa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwemo twitter ambapo kuna hashtag imeanzishwa

#HasJustineLandedYet

NAFUU KWA WALIMU AJIRA ZAIDI KUTANGAZWA

SERIKALI imetangaza kutoa ajira mpya 26,000 za walimu kuanzia Januari mwakani, ikiwa ni mpango endelevu wa kupunguza uhaba wa walimu katika shule za msingi na sekondari nchini.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa, alisema hayo juzi mjini hapa wakati akifunga kikao cha kazicha siku tatu cha maofisa elimu wamikoa na halmashauri za wilaya nchini, wanaosimamia elimu ya msingi.

"Serikali inatambua uhaba wa walimu na kila mwaka inatoa ajira mpya za walimu. Januari 2014 Serikali itatoa ajira 26,000 za walimu wapya na maelekezo mengine yatafuata," alisema Majaliwa.

Aliwataka maofisa elimu hao kuzingatia uwiano wa walimu wakati wa kuwapangia vituo vya kazi, badala ya kuendelea kuwalundika maeneo ya shule za mijini pekee.

Pia aliagiza walimu hao watayarishiwe mazingira mazuri hasa katika maeneo ya pembezoni kwa kuwapatia motisha, ili kuwajengea moyo wa kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi katika vituo vyao vya kazi kwa lengo la kuwafanya wasikimbie vituo.

Licha ya kutangaza ajira hizo mpya, Majaliwa pia alisema Serikali imetenga Sh bilioni 18 za kutengeneza madawati yatakayo sambazwa shuleni na zabuni yake inatarajiwa kutangazwa mapema iwezekanavyo.

Alisema mpango huo unatarajia kuanza mapema mwakani baada yakumpata mzabuni, "najua kutokanana kiwango kidogo cha fedha, hatutaweza kutosheleza, lakini huuni mwanzo."

Aliwataka maofisa hao kujenga tabia ya ufuatiliaji shuleni, ili kusimamia utunzaji wa vifaa na wakikuta uzembe ni wajibu wao kuchukua hatua ya kumaliza matatizo yaliyo chini na uwezo wao.

MORSI AZIDI KULIMBIKIWA MASHITAKA

Maafisa wa mashtaka wa Misri wanasema rais aliyeondolewa madarakani, Mohamed Morsi, atafikishwa mahakamani kwa makosa ya kutoroka jela wakati wa maandamano ya mwaka wa 2011 dhidi ya Rais Hosni Mubarak.

Watu wengine 132 watakabili mashtaka kama hayo, pamoja na kuwauwa walinzi wa gereza.

Washtakiwa wengine ni viongozi wa chama cha Bwana Morsi, cha Muslim Brotherhood, shekhe mmoja Yousef al-Qaradawi na wafuasi wa chama cha Wapalestina cha Hamas na cha Libnan, Hezbollah.

Bwana Morsi, rais wa kwanza wa Misri kuchaguliwa kwa misngi ya kidemokrasia, alitolewa madarakani na jeshi mwezi Julai.

Tayari Bwana Morsi anafanyiwa kesi kwa kuchochea mauaji ya wanaharakati wa upinzani wakati wa utawala wake wa mwaka mmoja

WANAJESHI WA MAREKANI WAPIGWA RISASI SUDAN KUSINI

Jeshi la Marekani linasema kuwa wanajeshi wake wane wamejeruhiwa Sudan Kusini pale ndege yao ilipopigwa risasi karibu na mji wa Bor, wakijaribu kuwahamisha raia wao. Ndege kadha zililazimika kurudi Uganda.

Jeshi la serikali ya Sudan Kusini linajaribu kuukomboa mji wa Bor, kaskazini ya mji mkuu, Juba, kutoka wanajeshi walioasi na kujiunga na makamo wa rais wa zamani, Riek Machar ambaye aliuteka mji huo Jumatano.

Siku hiyo pia Marekani ilipeleka wanajeshi 45 kuwalinda raia na mali ya Marekani Sudan Kusini.

Kwa mujibu wa gazeti la taifa la Uganda, New Vision,ndege mbili za jeshi la Uganda pia yalinasa katika tukio hilo.

Pamekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari kutoka Sudan Kusini kwamba ndege za Uganda piya zimekuwa zikiisaidia serikali kuukomboa mji wa Bor kutoka kwa wanajeshi walioasi - taarifa ambazo zinakanushwa na nchi zote mbili.

MTANI JEMBE KAJULIKANA SASA

Umekwisha, na timu ya Simba imeibuka mshindi kwa bao 3 - 1 Yanga.

Ila wakati mechi ikiendelea baadhi ya mashabiki upande wa jukwaa la Yanga wametolewa kwa machela kufuatia kupoteza fahamu.

Wafungaji wa Simba ni Awadh Juma na Amisi Tambwe.

Mfungaji wa Yanga ni Emmanuel Okwi

WAZIRI KAGHASHEKI AJIUZURU, WAKATI NCHIMBI, NAHODHA NA MATHAYO WATIMULIWA UWAZIRI

Wakati waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dr. Emmanuel Nchimbi alikuwa wa pili na wa Ulinzi akiwa wa kwanza kwa kuitwa na spika kuwa wa kwanza kuzungumza lakini ikaonekana wameingia mitini na kuitwa kwa waziri wa utalii na maliasili ndugu Balozi Hamisi Kaghasheki
Waziri wa Maliasiri na utalii atangaza kujiuzuru rasmi akiwa ndani ya Bunge.

Asema yeye ni mtu mzima na kasikia mengi, kateuliwa na rais kwa matakwa ya rais na hakuomba hivyo ana resign.

Mathayo yeye anadai ameshutumiwa mambo mengi kama sana na mgumo vyote vipo ila hakuhojiwa katika swala lolote, adai tatizo ni mfumo na swala la ardhi liko chini ya wizara ya ardhi na si wizara ya ardhi.

Na swala la mifugo na majosho ni swala la halmashauri na si wizara ya mifugo yeye anaonewa tu.

Asema hajawahi kupewa fedha za bajeti kama anavyoomba ajilinganisha na Yesu kuwa anasurubiwa lakini hana hatia.

Waziri mkuu anaongea kwa kujumuhisha kwa mawaziri waliosalia na anaanza kwa kauli zake na kuomba radhi kwa waliotendwa na operation tokomeza.

Anachojaribu kusema kama serikali wanatafakari na watafanyia kazi kama serikali kwani operationi ilikuwa chini ya wizara tatu.

Na anaendelea kutazama na kuangalia na anapendekeza iundwe tume ya kuthibitisha hayo kama alivyoshauri Mwanasheria mkuu wa serikali.

Waziri mkuu atangaza kuwa rais ametengua uwaziri wa wizara tatu rasmi zikiwemo ya Ulinzi chini ya Nchimbi, ya ulinzi chini ya Nahodha, ya mifugo chini ya Mathayo na Kagasheki aliyojiuzuru ya maliasili na utalii.

TAKRIBANI WATU 1000 WAMEUAWA AFRIKA YA KATI

Takriban watu elfu moja wameuawa na waasi wa zamani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mapambano yaliyodumu kwa siku mbili yaliyojitokeza mwezi huu, makadirio haya yanazidi yale ya Umoja wa Mataifa. Shirika la Amnesty International limesema.

Shirika hilo limesema kuwa uhalifu wa kivita bado unaendelea kufanyika nchini humo.

Wapiganaji hao ambao wengi waoni Waislamu walimuondoa madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo, Francois Bozize mwezi March, hali iliyosababisha mgogoro ndani ya jamii nchini humo.

Kiongozi wa waasi Michel Djotodia hivi sasa ni kiongozi wa kwanza kutoka jamii ya Waislamu anayeongoza taifa lenye Wakristo wengi na ndiye kiongozi wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya kati.

Katika ripoti hiyo, Amnesty International imesema waasi wa zamani wa Seleka waliwaua takriban watu 1000 mjini Bangui, kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kulipa kisasi dhidi ya wapiganaji wa Kikristo wanaodaiwa kuwashambulia waasi wa Kiislam.

Idadi ya waliopoteza maisha imeelezwa kuongezeka kuliko ile iliyotolewa na Umoja wa Mataifa ambao ulisema watu 450 waliuawa mjini Bangui na wengine 150 sehemu nyingine nchini humo.

Mashambulio hayo yamekuja baada ya wanamgambo wajulikanao kwa jina la anti-balaka ambao walikuwa wakiingia kila nyumba na kuwaua watu 60 wa jamii ya Kiislamu. Amnesty International imeeleza.

Mashambulio yaliyofanywa na wanamgambo wa zamani wa Seleka yamehusisha mauaji pia uvamizi na uporaji katika nyumbaza raia,ambapo wanawake na watoto kadhaa wameuawa.

Shirika hilo limesema kuwa raia huuawa kila siku mjini Bangui, ingawa kumekuwepo na vikosi vya Ufaransa na Umoja wa Afrika,Ufaransa ikiwa na askari 1,600 nchini humo.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema wapiganaji wa Kikristo walishambulia jamii ya kiislamu kaskazini mwa mji wa Bossangoa na kuwachinja watoto huku wakiwashinikiza wazazi wao kushuhudia mauaji hayo.

Mwanzoni mwa mwezi huu, Rais Djotodia aliiambia redio ya Kifaransa kuwa yuko tayari kuzungumza na viongozi wa wanamgambo wa Kikristo ili kutatua mzozo huo.

Kauli hiyo imekuja baada ya Umoja wa Afrika kuidhinisha kuongeza vikosi vyake na kufikia askari 6,000.

Vikosi vya Umoja wa Afrika na vya Ufaransa vinafanya jitihada za kuwanyang'anya silaha wanamgambo hao.

UGANDA YAPITISHA MUSWADA KUPINGA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Uganda imepitisha mswada unaopinga mapenzi ya jinsia moja.

Iwapo Rais Yoweri Museveni ataidhinisha sheria hiyo inamaanisha atakayepatikana na hatia atahukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Mswaada huo uliopitishwa na bunge siku ya Ijumaa halikadhalika inasema mtu yeyote aliye na taarifa za watu wanoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kushindwa kuripoti habari hizo kwa maafisa wa polisi atafungwa gerezeni maisha.

Wakati hu huo bunge hilo hilo la Uganda siku ya Alhamisi liliidhinisha mswaada unaopiga marufuku maonyesho ya picha chafu.

Mswada huo unaharamisha kitu chochote kitakacho onyesha sehemu nyeti kama vile matiti, mapaja, makalio au tabia yoyote inayozua uchu wa mapenzi.

Kulingana na mswada huo, sheria iliyopo sasa kuhusu picha chafu haihusu zaidi picha hizo bali linahusu uchapishaji, mawasiliano, taarifa , burudani, maonyesho katika kumbi za kuigizia, miziki inyochezwa katikavyombo vya habari, densi, sanaa, mitindo na picha za runinga.

Mapema mwaka huu Waziri wa maadili wa Uganda, Simon Lokodo, alipendekeza kuwa mwanamke yeyote anayevalia nguo ambayo inafika juu ya magoti anatakiwa kukamtwa na kuadhibiwa kisheria.

Mswada huo unahitaji kuidhinishwa na Rais kabla ya kufanywa sheria.

Uganda ni nchi inayoshikilia mawazo ya kihafidhina yaani isiyopendelea mageuzi katika mawazo na inaandaa sheria ya kuwaadhibu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ikijumuisha hukumu ya kifo katika baadhi ya kesi.

ICC YAAHILISHA KESI YA RAIS KENYATTA

Kesi inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta huenda ikachelewa kuanza baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai (ICC) Kukiri kuwa hana ushahidi wa kutosha wa kuendeleza kesi hiyo.

Rais wa Kenya amekanusha mashtaka ya dhulma dhidi ya ubinadamu zinazohusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuuwa mwaka 2007. Zaidi ya watu elfu moja waliuawawa katika mapiganao hayo na maelfu yaw engine kupoteza makazi yao.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Bi. Fatou Bensouda amesema kuwa uamuzi huo unatokana na mashahidi wawili wakuu katika kesi hiyo kukataa kutoa ushahidi dhidi ya Rais Kenyatta. Mmoja wao amesema kuwa hayuko radhi kusema anayojua kuhusu kesi hiyo ilhali wa pili amesema kuwa alidanganya katika ushahidi wake wa awali katika kesi hiyo.

Kujiondoa kwa mashahidi hao imemfanya kiongozi wa mashtakakusema kuwa kesi dhidi ya BwanaKenyatta haifikii kiwango cha ushahidi kinachohitajika jambo lililomchochea kuomba kesi hyo isimamishwe kwa muda ili awezekusawazisha na kukusanya ushahidi zaidi.

Kesi ya Bwana Kenyatta ilipaswa kuanza huko The Hague tarehe 5 Februari mwaka ujao.

Bwana Kenyatta alishtakiwa pamoja na naibu wake William Ruto na mtangazaji Joshua Arap Sang kwa makosa ya mauji, kusababisha watu kuhamishwa kwa nguvu katika makazi yao, kusababisha mateso kwa umma na ubakaji kufuatia ghasia zilizotokana na matokeo ya urais katika uchaguzi huo.

Kesi ya Kenyatta na naibu wake imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na jamii ya kimataifa haswa baada ya Umoja wa Afrika kutishia kuyaondoa mataifa ya Afrika katika uanachama wa mahakama hiyo iliyobuniwa chiniya mkataba wa Roma. Umoja wa Afrika umekuwa ukidai mahakama hiyo imekuwa ikiwalenga viongozi wa bara Afrika.

BUNGE LAAHIRISHWA, WAZIRI DAVID MATHAYO ATAKWA KUJIUZULU.

Kamati ya Lembeni ambaye amesoma Taarifa Uchunguzi ya Kamati kwa Bunge Hivi Punde imependekeza Waziri wa Maendeleo na Uvuvi, Dk David Mathayo David , Mkurugezi wa Wanyamapori na maofisa wengine wajiuzulu mara moja kutokana na kuwapo kwa matukio ya kuchomwa moto kwa nyumba za wananchi na kuuawawa kwa baadhi ya watu wakati wa operesheni tokomeza majangili.

Bunge Limeahirishwa kwa muda ili kujadili muda uliopendekezwa na Wabunge wa kujadili ripoti ya uchunguzi ya Lembeni kuhusu mauaji na nyumba kuchomwa moto wakati operesheni tokomeza majangili nchini.

Katika taarifa hiyo imependekeza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo David ajiuzulu, mkurugenzi wa Wanyamapori Tanzania, maofisawa jeshi na mgambo kwa kuhusika katika mauaji hayo.

Wabunge wamehoji wakiwamo Zitto Kabwe (Chadema) kwanini kamati ya Lembeni inamtaka Dk David Mathayo David ajiulu wakati kuna viongozi wengi wanahusika katika kashfa hiyo.

Katika ripoti ya Lembeni imemruka Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kagasheki na naibu waziri wake, pamoja na mawaziri wengine hawatajwa.

Kwa uamuzi wa Naibu Spika kuahirisha Bunge inamaanisha amekubaliana na hoja ya Tundu Lissu (Chadema) ya kuahirishwa Bunge hilo. Pia Mbunge, Ligora(CCM) naye alichangia hoja hiyo na wabunge wengine.

WATOTO WA DIWANI WACHINJWA HUKO MBEYA

Watu wasiojulikana wamewaua watoto wawili, mmoja akiwa ni binti wa kazi wa Diwani wa CCM kata ya Mkingamo wilaya Momba mkoani Mbeya.

Chanzo cha mauaji inasemekana ni dhuluma ya viwanja kwa wananchi wa kawaida.

Habari zaidi zinasema kawadhurumu wananchi viwanja vingi sana,wakati mwingine huuza kiwanja kimoja kwa zaidi ya watu watatu.

Inasemekana hata ukimpeleka mahakamani anakushinda kesi,kifupi ni kuwa mahakama aliiweka mfukoni.

Chanzo: Jf

RASIMU YA PILI YA KATIBA MPYA KUKABIDHIWA KWA RAIS 30 DECEMBER

RAIS Jakaya Kikwete, Desemba 30 atakabidhiwa Rasimu ya Katiba mpya, baada ya kufanyiwa marekebisho na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya.

Makabidhiano hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam, mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein, kuashiria kuanza kwa hatua inayofuata ya uundaji wa Bunge Maalumu la Katiba.

Taarifa ya Katibu wa Tume, Assaa Rashid, iliyotumwa jana kwa vyombo vya habari, ilifafanua kwamba mbali na Dk Shein, makabidhiano hayo yanatarajiwa kushuhudiwa na viongozi wengine wa Serikali, vyama vya siasa, taasisiza dini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.

Awali Rasimu hiyo ilitarajiwa kukamilika kabla ya Desemba 15 baada ya kuongezwa muda na Rais kwa mara ya kwanza, lakini Tume iliomba kuongezwa muda wa kukabidhi Rasimu hiyo kwa mara ya pili na kuongezwa siku 14 kuanzia Desemba 16.Kwa hatua hiyo, Rais Kikwete alikuwa ameiongeza muda Tume hiyo kwa siku 59, kati ya siku 60 ambazo anaruhusiwa kuongeza kisheria.

Bunge la Katiba Kwa mujibu wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013, baada ya Rasimu hiyo kukabidhiwa, Tume itavunjwa ili kutoa nafasi kwa uundwaji wa Bunge Maalumu la Katiba.

Bunge hilo litaundwa na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao ni 357, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar 76 na wajumbe wengine 201 watakaoteuliwa na Rais kutoka mashirika yasiyo ya Serikali na taasisi za kidini.

Mashirika yasiyo ya Serikali na taasisi za kidini, yatatakiwa kupendekeza majina ya watu wanne hadi tisa, ambayo yatapelekwa kwa Rais, naye atateua majina matatu.Rais kabla ya uteuzi huo, atakaa na vyombo vyake na kuteua majina yawajumbe ndani ya mapendekezo ya mashirika na taasisi hizo.

Uamuzi wa vipengele vya Katiba mpya ndani ya Bunge hilo, unatarajiwa kufanyika kwa kupigiwa kura ambapo kila kipengele kitapita kwa kupata kura ya zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, na hivyo kutoa Rasimu yatatu ya Katiba ambayo itapelekwa kwa wananchi.

Kura ya maoni Baada ya Bunge Maalumu la Katiba, kukamilisha kutengeneza Rasimu ya tatu ya Katiba, makundi ya watu, vyama naasasi za kiraia wanaokusudia kupinga na kuunga mkono Rasimu hiyo yataundwa katika kamati na kusajiliwa katika majimbo.

Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ndizo zitakazo wajibika katika kusajili kamati hizo katika majimbohusika.

Kamati hizo zitateua mawakala wa kusimamia kura zitakazokataa au kukubali Katiba mpya, ambazo zitapigwa na wananchi.

Upigaji kura Katika upigaji kura ya maoni kwa ajili ya upatikanaji wa Katiba mpya, kutakuwa na maswali, likiwamo la wapigakura kutakiwa kujibu ndiyo, kwamba wanaikubali Katiba mpya au hapana, kwamba wanaikataa.

Swali hilo la kura ya maoni litaandaliwa na NEC na ZEC na litahitaji jibu la ndiyo au hapana, tofauti na utaratibu wa uchaguzi uliozoeleka wa kupigia kura mtu auchama.

Aidha, NEC na ZEC ndizo zilizopewawajibu kisheria wa kusimamia uendeshaji wa kura ya maoni na kusimamia elimu ya wapiga kura ya maoni.

Tume hizo pia ndizo zitateua wasimamizi wa kura ya maoni wa kila jimbo kusimamia uendeshaji wa kura ambapo kila msimamizi kwa kushirikiana na tume zote mbili, atateua maofisa na naibu maofisa wa kura ya maoni kwa ajiliya kusimamia vituo vya kupigia kura.

Wapiga kura watakuwa waliosajiliwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura la NEC na ZEC.

Hivyo kila mwananchi mwenye sifana aliyeandikishwa kwenye madaftari hayo ya kupiga kura, atashiriki kura ya maoni.

RAIS ASAINI HATI YA DHARURA KUFANYA MAREKEBISHO WA MUSWADA WA KODI ZA SIMU

RAIS ATIA SAINI HATI YADHARURA KUFUTA KODI YA LAINI ZA SIMU

Miongoni mwa mambo yaliyolalamikiwa sana na wananchimwaka huu ni kitendo cha Bunge kupitisha uanzishwaji wa tozo ya kodi ya TShs. 1,000/- kwa kila laini ya simu. Hii ilikuwa wakati wa Bunge la Bajeti la mwaka 2013/2014.

Kufuatia hali iliyojitokeza, Rais Jakaya Kikwete alilazimika kutoa agizo kwa wahusika kulishughulikiasuala hilo.

Taarifa kutoka Ofisi ya Rais zimethibitisha kuwa wahusika walilifanyia kazi suala hilo na kuliwakilisha kwa Rais.

Mheshimiwa Rais ametia sahihi Hati ya Dharura (Certificate of Emergency) kufanyika marekebisho kwa Muswada wa Fedha wa mwaka 2013 kuondoa tozo ya kodi kwa laini za simu (SimCard Tax).

MKALIMANI KATIKA IBADA YA MAZISHI YA MADIBA ALAZWA HOSPITALINI

MKALIMANI mtata katika ibada maalumu ya kumkumbuka kiongozi wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela katika uwanja wa FNB jijini Johannesburg Desemba 10 amelazwa hospitalini kwa matatizo ya akili.

Kwa mujibu wa taarifa, mke wa Thamsanga Jantjie, Siziwe, alimpeleka mumewe katika Hospitali ya Krugersdorp Jumanne,kufanyiwa vipimo, lakini ikapendekezwa alazwe mara moja.

Mkalimani huyo wa lugha ya alamakatika kumbukumbu hiyo, amelazwa katika Hospitali ya wagonjwa wa akili ya Sterkfontein, gazeti la The Star la Afrika Kusini liliripoti jana.

"Siku chache zilizopita, zilikuwa ngumu. Tumekuwa tukiishi kwa hadhari kubwa kwa sababu wakati wowote angeweza kuharibikiwa," aliongeza Siziwe. Jantjie alipaswa Desemba 10 awe amepelekwa Sterkfontein kwa ajili ya uchunguzi wa afya.

Hata hivyo, baada ya kupata 'dili' yakufanya ukalimani katika ibada ya kumbukumbu ya Mandela kwenye uwanja wa FNB siku hiyo, Jantjie aliwasiliana na hospitali ili kubadilisha miadi yake.

Juzi, Waziri wa Ofisi ya Rais, Collins Chabane alisema Serikali itachunguza madai kuwa Jantjie hakutumia ukalimani mwafaka siku hiyo.

Baada ya shughuli hiyo, Jantjie aliviambia vyombo vya habari kuwa ana matatizo ya uchizi na sikuhiyo alijikuta akiona maluweluwe wakiwamo malaika wakishuka, na kwamba alipatwa kiwewe alipogundua kuwa alikuwa amezungukwa na polisi wenye silaha.

Familia ya Mandela Wakati huo huo, mjane wa Mandela, Winnie amekanusha kuwapo kwa mzozo ndani ya familia ya kiongozi huyo wa zamani.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo mbalimbali, inadaiwa kwamba mjukuu mkubwa wa Mandela, Mandla ambaye ni mrithi wa uchifu wa ukoo wa Madiba ametengwa na familia hiyo.

Lakini Winnie alikanusha uvumi huo potofu aliouita ni "staili ya ubaguzi wa rangi." "Habari, taarifa na tahariri za vyombo vya habari…zinasema familia ya Mandela iko vitani tangu habari za kwanza kwamba Madiba hayuko nasi tena," alisema msemaji wake, Thato Mmereki katika taarifa yake.

"Taarifa hizi hazijafanya lolote zaidiya kuja na ukweli nusu nusu kwa lengo la kuichafua familia ya Mandela katika kipindi hiki kigumucha maombolezo."

Kwa mujibu wa vyombo vya habari ndani ya Afrika Kusini, vitasa vya nyumba ya Mandela iliyoko Estern Cape vilibadilishwa baada ya bintiye mkubwa, Makaziwe, kuwasili hapo Alhamisi – wiki moja baada ya kifo cha baba yake na sikutatu kabla ya maziko.

Maji na umeme vilikatwa siku ya mkesha wa maziko ya Mandela kijijini Qunu Jumapili ukiwa ndio mwisho wa siku 10 za maombolezo ambayo yalifuatiliwa na mamilioni ya watu duniani.

Makaziwe inasemekana alisimamia maandalizi ya mazishi, huku Mandla akionekana kiongozi wa familia-akisimamia jeneza lenye mwili wa babu yake katika siku zote tatu za kuagwa katika majengo ya Serikali ya Union jijini Pretoria, wiki jana.

Mandla, akishutumu baadhi ya shangazi zake kwa kujaribu kudhibiti fedha za Mandela, alipata kuhamisha mabaki ya marehemu baba yake, Makgatho, ambaye alifariki dunia kwa Ukimwi mwaka 2005 na watoto wengine wawili wa Mandela kutoka Qunu kuyapeleka Mvezo ambako Mandela alizaliwa.

Familia yake ilidai, kwamba huo ulikuwa mpango wa kulazimisha maziko ya Mandela yafanyikie Mvezo – kwa kuwa Mandela katika wosia wake alitaka azikwe karibu na makaburi ya wanawe hao-kwa lengo la kuvutia utalii.

Mandla hatimaye alilazimishwa na Mahakama kurudisha mabaki hayo Qunu. Winnie alisema juzi, kwamba, "hakuna mgogoro wala majadiliano ya urithi ndani ya familia ya Mandela. Na kwa mujibuwa sheria za kimila na utamaduni binti mkubwa, ambaye ni Makaziwe, ataongoza familia na kuchukua uamuzi akishirikiana na wadogo zake wa kike.

"Mandla anaheshimiwa kama mmoja wa wajukuu wa Mandela, kizazi kijachocha familia ya Mandela."

TANZANIA YAPAA VIWANGO VYA FIFA

TANZANIA imezidi kupaa kwenye viwango vya ubora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) baada ya kupanda kwa nafasi nne na sasa ni ya 120 kutoka nafasi ya 124 mweziuliopita.

Viwango hivyo vimetoka ikiwa ni takribani wiki moja kupita tangu Tanzania itoke kwenye michuano ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambapo Bara ilishika nafasi ya nne na Zanzibar kuishia hatua ya makundi.

Kwa mujibu wa viwango hivyo vya FIFA, Uganda bado inaongoza katika ubora wa viwango kwa nchi wanachama wa Cecafa ikiwa nafasi ile ile ya 86 kama mwezi uliopita huku Ethiopia ikifuatia katika nafasiile ile ya 93.

Kenya inafuata ikiwa nafasi ya 109 na Sudan ni ya 119 huku Burundi ikishika nafasi ya 124, Rwanda ya 133, Eritrea ya 200, Sudan Kusini ya 201, Somalia ya 203 na Djiboutiya 204.

Ivory Coast inaendelea kuongoza kwa upande wa Afrika ikiwa nafasi ya 17 ikifuatiwa na Ghana katika nafasi ya 24 huku Algeria ikiwa ya 26. Nigeria ni ya 37, Misri ya 41, Mali ya 45, Cameroon iko katika nafasi ya 50, Burkina Faso ya 53, Libya ya 59 na Guinea ya 61.

Aidha katika viwango hivyo vya kufungia mwaka, nafasi kumi bora haijabadilika, Hispania ikiendelea kukaa kileleni ikifutiwa na Ujerumani na Argentina. Kwenye nafasi ya nne ikikaa Colombia, Ureno ni ya tano, kisha Uruguay.

Timu mbili za Asia zimepanda kwa kiwango kikubwa, Ufilipino (127 ikipanda kwa nafasi sita) na Guam (161, ikipanda nafasi nane 8).

Bingwa wa Ulaya na Dunia, Hispania inaongoza viwango hivyo kwa matoleo sita mfululizo, ikijiwekea mazingira mazuri ya kutwaa tuzo ya timu bora ya mwaka.

Timu iliyopanda kwa kiasi kikubwa katika viwango vya kumalizia mwaka, shukrani kwa ushindi wa mechi nane sare mbili, na kipigo kimoja ni Ukraine, ambayo imekusanya pointi 312 tangu Desemba 2012, ikipanda kwa nafasi 29 na sasa iko nafasi ya 18.

Pia ni mwaka wa mafanikio kwa Armenia (nafasi ya 35 ikikusanya pointi 259 tangu Desemba 2012) na Marekani USA (nafasi ya 14 ikikusanya pointi 237 tangu Desemba 2012).

WABUNGE WAUMBUANA BUNGENI

Wabunge jana waliumbuana kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma huku Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe akituhumiwa kuagiza kubadilishwa kwa tiketi ya ndege ya Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Joyce Mukya ili afupishe ziara yake ya kikazi huko Marekani na kwenda Uarabuni kwa shughuli binafsi.

Mbali ya Mbowe, Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM) anadaiwa kuchukua poshoya Kamati ya Hesabu za Bunge (PAC), kwa safari ya kwenda Dubai na wenzake lakini badala yake akaenda Mbeya kwenye ziara za chama chake.

Malumbano hayo yaliibuka jana baada ya Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM), kuomba mwongozo wa Spika akitaka kufahamu kauli ya ofisi yake kwa Mbowe kutumia nafasi yake kumrudisha mbunge ambaye ameshatumia fedha za Serikali.Alidai kwamba Mbowe aliagiza Mukya aanze safari Desemba Mosi, mwaka huu kutoka New York, Marekani ili aende Dubai, Falme za Kiarabu (UAE) kabla ya kwenda Dar es Salaam, Desemba 3, mwaka huu.

Alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo jana, Mbowe alisema hawezi kuzungumza chochote kwa kuwa hakuwapo bungeni akisema alikuwa Dar es Salaam kwenye kikao.... "Siwezi kusema lolote mpaka nipate hansard (kumbukumbu rasmi ya Bunge) na kutoka kwa wabunge wangu walioko Dodoma kujua nini kimesemwa."

Akiomba mwongozo Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM alisema: "Jambo hili limechukua taswira kama ni Bunge lote linafanya mambo haya na limevunja heshima ya Bunge. Jambo hili linatuvunjia heshima hata watu ambao tuna maadili ya uongozi na tunaliheshimu taifa letu..."Pamoja na kuwa jambo hilo lilikuwa la binafsi, lakini kuna ujumbe tumeupata kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani amemzuia mbunge wake kusafiri na magazeti yakaandika kwamba wana mahusiano. Mimi sipendi kwenda kwenye uhusiano, natakakwenye taswira ya Bunge na Taifa."

Alisema Bunge linapopanga safari za wabunge linazingatia wachama tawala na wapinzani ili kuweka uwakilishi.

Nchemba alisema Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, aliandika ujumbe mfupi wa simu kwa mtumishi mmoja wa Bunge akitaka kubadilishwa kwa tiketi ya ndege ya mbunge.

Aliusoma ujumbe huo: "Rejea mazungumzo yetu bwana Kabunju kuhusu mheshimiwa Joyce Mukya ambaye yupo safarini. Nitashukuru kama utambadilishia booking (safari) yake ili aweze kurudi, aondoke New York tarehe moja Desemba na kurejea Dubai baadaye ataunganisha kurejea Dar es Salaam by Mbowe kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni nakala kwa Joyce Mukya." Kabunju S. Kabunju ni Ofisa wa Bunge anayeshughulikia masualaya usafiri.

Nchemba alisema: "Ameshakatiwa tiketi, ameziba nafasi ya kwenda kuliwakilisha taifa kule, anamwita arudi Dubai na ni mbunge viti maalumu. Je, hili lina taswira gani kwa taifa na kiti chako kinatoa kauli gani kwa watu ambao wanakwenda kutumia fedha za Serikali kwa mambo binafsi, Dubai?" alisema.

Pia alitaka kufahamu Bunge linachukua hatua gani stahiki kwa mbunge anapoingilia kazi za kiti na pia watumishi wanapoingiliwa na kubadilisha yale waliyotumwa kwa ajili ya Serikali.

Tuhuma za ZambiMbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde alisemaNchemba anaegemea zaidi wabunge wa upinzani wakati wapo wa CCM waliochukua posho.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, yaliyosemwa na magazeti na mwombaji wa mwisho (Nchemba), alipokuwa anatoa mwongozo amejaribu kuainisha wabunge wa upande mmoja wa upinzani," alisema.

Alimtaja Zambi kuwa alichukua fedha ili kwenda Dubai na wenzake lakini badala yake alikwenda Mbeya wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokuwa katika ziara mkoani humo. Zambi pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya.

"Tunaomba mwongozo wako namna gani hili suala litachukuliwa hatua na wala siyo kufanya propaganda za kisiasa ndani ya Bunge lako," alisema Silinde.

Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Mariam Msabaha alisema kuna mambo mengi yanayofanyika ndani ya Bunge hilo lakini hayasemwi."

Kuna watu wameandikwa ndani ya magazeti wanaiba vidani licha ya kutosemwa lakini imeonekanika huku. Mambo ya mapenzi ni ya mtu na mtu wake, humu kila mtu ana mpenzi wake,"alisema.

Mwenyekiti wa PAC na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe alisema: "Kamati ya PAC ambayo inahusika na masuala ya fedha za umma tayari imeshamwomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), afanye uchunguzi kuhusiana na safari zote ili jambohili liweze kufika mwisho."

Alisema taarifa hiyo itapelekwa kwa Spika na kama atapendezwa italetwa bungeni ili jambo hilo liweze kumalizika.

Akijibu mwongozo huo, Mwenyekiti wa Bunge aliyekuwa akiongoza shughuli za jana asubuhi, Mussa Azzan Zungu alisema: "Nimepokea miongozo yote na kiti kinasema hakina lazima ya kujibu sasa hivi, kitatoa mwongozo baada ya kufikiria na kuyatafakari hapo kitakapopata nafasi."

Hata hivyo, kabla ya kuahirisha Bunge jana mchana, Zungu alisema suala hilo ni la kiutawala na masuala yote yanayohusu masuala ya fedha yanatawaliwa na sheria na kanuni za fedha.

Sakata hilo liliibuliwa bungeni wiki iliyopita na Mbunge wa NkasiKaskazini (CCM), Ally Keissy alipokuwa akichangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac).

ABIRIA 200 WANUSURIKA KIFO

Abiria zaidi ya 200 waliokuwa wakisafiri na ndege ya shirika la ndege la Ethiopian airline iliyokuwa inatoka Adiss Ababa nchini Ethiopia kwenda uwanja wa ndege wa Kilimanjaro wamenusurika kufa baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha na kuserereka hadi pembezoni mwa uwanja huo.

Ndege hiyo aina ya Boing 767 yenye uwezo wa kubeba abiria 300 ilikuwa na abiria 213 na wahudumu 23 na ilitua katika uwanja huo majira ya sita mchana baada ya kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa kilimanjaro kwa sababu ambazo hazikuweza kufahamika mara moja.

Baadhi ya viongozi na akiwemo mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo na baadhi ya watendaji wa sekta ya usafiri wa anga wamesema sababu zandege hiyo kutua katika uwanja wa Arusha badala ya uwanja wa KIA bado hazijajulikana lakini wamethibitisha kuwa abiria wotewako salama.

Pamoja na viongozi na watendajiwa sekta mbalimbali kuwasili katika uwanja huo abiria waliokuwa katika ndege hiyo waliendelea kukaa ndani ya ndege kwa zaidi ya masaa matano kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kukosekana kwa ngazi inayoweza kutumika kuwashusha abiria hao na mwishowe walilazimika kushushwa kwa utaratibu usio rasmi.

Wakizungumza baada ya kushushwa kwenye ndege na kupakiwa kwenye magari hayo baadhi ya abiria wamesema walianza kusikia mtikisiko mkubwa kabla ya ndege hiyo.

JAMAA AISHI KWENYE HANDAKI KWA MIAKA MINNE

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Chacha Makenge anaishi na kuendesha maisha yake katika handaki alilolichimba katikati ya pori lililopo katika eneo la chuo kikuu jijini Dar es Salaam kwa miaka minne sasa,huku akiitaka serikali kuwa na utaratibu wa kuratibu shuguli za vijana ili kulinda amani na usalama wa taifa.

Mara baada ya kukaribishwa katika nyumba anayoishi bwana Chacha Makenge mwenye umri wa miaka 36 na kutakiwa kusaini katika kitabu cha wageni, mwenyeji wetu anaanza kwa kuwataka watanzania kutokuwa na moyo wa visasi kwa wale ambao wametutendea vibaya na kuharibu maisha yetu huku akimtaja rafiki yake kuwa chanzo cha yeye kuishi maisha hayo baada ya kumchomea nyumba yake miaka minne iliyopita.

Pia anailalamikia serikali kwa kutokuwa na utaratibu mzuri wa kuwahudumia wananchi wenye shida pale wanapo kwenda katika ofisi za umma kwa ajili ya kuelezea matatizo yao.

Pia bwana Chacha anailaumu serikali kwa kushindwa kukusanya kodi jambo ambalo limesababisha uwepo wa maisha duni na upatikanaji duni wa huduma za kijamii kwa madi kuwa hakuna fedha za kutoa huduma hizo ipasavyo kwa wananchi.

Chanzo:ITV