Akizungumza na Radio One, Kamanda wa polisi Mkoani Dodoma, David Misime, amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 9 usiku kuamkia leo katika kijiji cha Namtumba Mkoani Dodoma na abiria waliokuwemo kwenye Bus hilo hakuna aliyejeruhiwa.
"Hakuna aliyejeruhiwa kutoka kwenye Bus hili, lakini Dereva aliyekuwa anaendesha abiria hao anafahamika kwa jina la Juma Mohamed, amekimbia mpaka sasa haijafahamika yuko wapi, ameongeza kuwa gari ndogo aina ya Toyota Corola imeharibika vibaya na baadhi ya miili ya askari hao imeharibika.
"Tumeipeleka miilihiyo hospital kwa ajili ya kuihifahi huku tukisubiri mipango ya mazishi," amesema David.
Chanzo: Radio 1