Taarifa za karibuni kabisa zinaeleza kuwa mtu mmoja amekufa kwenye mripuko uliotokea katika ufunguzi wa kanisa la Katoliki la Olasiti, kwenye kitongoje cha Arusha, Tanzania.
Watu kama 50 wamejeruhiwa. Makamo wa rais wa Tanzania, Dr. Mohamed Gharib Bilal amewasili Arusha kwenda kupeleka pole ya serikali kwa viongozi wa kanisa na majeruhi.
Dr. Bilal alisema serikali ya Tanzania itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa inawapata watu waliohusika na mripuko huo. Mtu mmoja amekamatwa lakini haikuelezwa ni nani au kama amehusika na kundi lolote.