Chadema yaitupia Cuf tuhuma za Ushoga

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa
ripoti iliyotolewa na Umoja wa
Mataifa ‘United Nations
University’(UNU-WIDER) ya mwezi
Aprili 2012 iliyoandaliwa na Aili Mari
Tripp ilionyesha kuwa misaada ya
wahisani kutoka nje katika
mabadiliko ya kisiasa Tanzania
‘Donor Assistance and Political
Reform in Tanzania’, inaonyesha
kuwa Tanzania imepokea misaada
kutoka nje yenye thamani ya dola za
kimarekani bilioni 26.85 toka mwaka
1990-2010.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa
ripoti hiyo ni kuwa Tanzania ni nchi
inayoongoza kusini mwa jangwa la
Sahara kwa kupokea misaada mingi
kutoka nje ya nchi na hasa kutoka
mataifa ya Ulaya na taasisi za nchi za
Uingereza, Marekani, Ujerumani,
Uholanzi, Norway, Canada, Sweden,
na taasisi kama Benki ya Dunia,
IMF ,UNDP ,UNICEF na mengineyo.
Pamoja na misaada yote hiyo, bado
tumeendelea kuwa nchi maskini
sana duniani pamoja na kuwa na
rasilimali lukuki ambazo tumepewa
na Mungu ila tunashindwa kuzitumia
kwa manufaa ya watanzania na
badala yake tumeendelea
kudanganywa na vimisaada vidogo
vidogo na kubadilishana na
rasilimali zetu kama madini,
misitu ,wanyama nk kwa ajili ya
misaada hiyo
.
Mheshimiwa Spika, pamoja na
misaada hiyo kwa serikali hii ya CCM
bado vyama vya siasa vimekuwa na
mahusiano na baadhi ya vyama
vingine vya siasa katika mataifa ya
magharibi na vimekuwa vikipokea
misaada ya aina mbalimbali kama
fedha , nyenzo na mengineyo kadiri
ya makubaliano na mirengo ya
kiitikadi ya vyama husika.
Pamoja na
ukweli huo bado vipo vyama vya
siasa vinavyopotosha umma
kuhusiana na misaada vinayopokea
kutoka nje ya nchi na vyama hivi
vimekuwa mstari wa mbele kueneza
propaganda za uongo kuwa
vyenyewe havipokei misaada kutoka
nchi za magharibi
.
Mheshimiwa Spika, CCM wao
‘wanajiita’ kuwa wapo mrengo wa
kijamaa/kikomunisti na wamekuwa
wakipokea misaada mingi sana ya
fedha na nyenzo kutoka Umoja wa
Vyama vya Kikomunisti Ulimwenguni
‘Socialist International’ kutoka katika
nchi kama za Ujerumani kupitia
SDP ,Uingereza kupitia chama cha
Labour,China kupitia chama cha
Kikomunist ,Marekani kupitia chama
cha Democrats
.
Pamoja na misaada
ya kifedha na kiufundi ambayo CCM
imekuwa ikipata kutoka nje
wamekuwa hawatangazi hadharani
hata mara moja kuhusiana na kiasi
ambacho wamekuwa wakipokea na
hivyo kila kitu kwao imekuwa ni siri
kuu ya viongozi wao.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa
chama cha CUF, kutokana na itikadi
zake za mrengo wa Kiliberali
ambazo miongoni mwa misingi yake
mikuu ni pamoja na “kupigania haki
za ndoa ya jinsia moja, usagaji na
ushoga”

Hii ni kwa mujibu wa
tangazo lao kwenye mtandao wao
wa umoja wa maliberali
ulimwenguni, likiungwa mkono na
Waziri wa Haki na Usawa wa
Uingereza, Lynn Featherstone kutoka
chama cha Liberal Democrats wakati
chama hicho (www.liberal-
international.org) kilipokuwa
kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa
za jinsia moja kama haki ya mtu
mmoja mmoja, wanashirikiana na
vyama kama vile LPC ya Canada, Det
Radikale Venstre cha Norway, FDP
cha Ujerumani, Israel Liberal Group
cha Israel,PDS cha Senegal na
Liberal Democrats cha Uingereza.
Kutokana na umoja huo, CUF
wamekuwa wakipata msaada wa
kifedha na nyenzo nyingine
mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo
vya mrengo wa Kiliberali na msaada
wa mwisho ni hivi majuzi mwezi
Machi 2013 waliposaini makubaliano
na chama cha Kiliberali kutoka
Norway.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa
CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa
Vyama vya Kidemokrasia
Ulimwenguni (International
Democratic Union - IDU). Huu ni
umoja wa vyama ambavyo vipo
kwenye mrengo wa kati na ambavyo
msingi wake mkuu ni pamoja na
kuwa na familia, kama taasisi
muhimu katika jamii, ikimaanisha
kwamba: “tunapinga vitendo vyote
vya ushoga na usagaji”.
Tunatetea
demokrasia, haki za binadamu na
kupambana na ufisadi katika serikali.
Vyama wanachama wa umoja huu
ni pamoja na Conservative Party cha
UK, CPP cha Norway, Republican cha
Marekani na vingine vinavyofuata
mrengo huo
.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya
upinzani Bungeni, inavitaka vyama
vyote ambavyo vimekuwa na
mahusiano na vyama vya nje viweke
wazi mikataba yao na malengo ya
mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na
misaada ambayo vimekuwa
vikipokea kutoka kwenye nchi hizo.