Timu ya Katavi Warriors inatarajia kupambana na timu iliyofanikiwa kupanda daraja mpaka ligi kuu timu ya Rhino Rangers kutoka mjini tabora, Katika uwanja wa Azimio katikati mwa mji wa mpanda.
Mpambano huo wa kirafiki unatarajiwa kutimua vumbi siku ya jumatano tarehe 29 May 2013.
Timu ya Katavi Warriors a.k.a Aston Villa ikifahamika hivyo katika viunga vya mji wa Mpanda ambayo inashiri ligi ya TFF ngazi ya kanda katika hatua ya mtoano itakuwa na kibarua pevu hapo siku ya Jumapili tarehe 26 May pale mjini Kigoma katika uwanja wa Tanganyika itakapo pambana na Saigon kutoka mkoani humo.
Mpaka kufikia hatua hiyo Saigon iliivurumisha bila huruma timu ya Mirambo kutoka mkoani Tabora kwa jumla ya mabao matano(5) kwa moja(1). Ambapo katika mtanange uliowakutanisha mjini tabora Katika uwanja wa Ali Hassan mwinyi Saigon waliibuka kidedea kwa goli 2-1, na kurudiwa tena katika dimba la Tanganyika mjini kigoma ambapo Saigon waiipa tena kipigo Mirambo cha goli tatu(3) kwa nunge.
Nayo Aston Villa wakiondosha timu ya Rukwa United kutoka mkoan Rukwa kwa jumla ya goli 2-1, Mchezo wa kwanza ulipigwa katika dimba la Azimio mjini Mpanda na matokeo kutoka sifuri kwa sifuri. Aston Villa walitumia vizuri nafasi ya ugenini walipoichapa Rukwa United 2-1 katika uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga na kujiakikishia nafasi ya kusonga mbele.
Mpambano kati ya Warriors na Rangers Utakuwa niwakujianda kwa raundi ya pili ya mtoano kati ya Katavi Warriors dhidi ya Saigon. Katavi Warriors wameondoka usiku huu kuelekea kigoma kujianda na Mtanange huo.
Kila la Heri Aston Villa