JWTZ Lakanusha Uvumi kutoka D.R Congo.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania, JWTZ, limekanusha taarifa
zilizotapakaa kwenye mitandao
kuwa askari wa jeshi hilo
waliokwenda huko kwa ajili ya
kulinda amani,wameanza
kujihusisha na makahaba.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi
ya Habari na Uhusiano, Mtandao wa
www.congodrcnews.com umedai
wanajeshi wa Tanzania wameanza
kujihusisha na ubakaji wanawake
katika Mji wa Sake ulioko Goma.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa askari
mmoja wa JWTZ alihitaji kujamiiana
na mwanamke mmoja(Kahaba) kwa
ujira wa Dola 50. Baada ya kumaliza
shida zake ambazo ilielezwa
alizifanya bila kinga yoyote,askari
huyo alikataa kumlipa ujira
wake,hali iliyoleta tafrani na
mwanamke huyo kupiga kelele.

“JWTZ linapenda kuwaeleza
wananchi kuwa taarifa hizo ni za
uongo mtupu wenye nia ya kulipaka
matope JWTZ na Tanzania kwa
ujumla. “Picha iliyotolewa kwenye
tovuti hiyo ya
www.congodrcnews.com ni ya
wanajeshi wa Tanzania walipokuwa
katika Operesheni ya huko Comoro
mwaka 2008.

Mtu anayeonekana kuwa chini ya
Ulinzi alikuwa ni mshiriki wa Kanali
Mohamed Bacar ambaye
aliondolewa madarakani.
“Vilevile picha hiyo ilitolewa vile vile
katika tovuti za www.apc.net.au/
news/stories ya Machi 26, 2008 na
ww.Seattletimes.com. na pia picha
hiyo ipo pia kwenye tovuti ya Jamii
Forum baada ya kufanya ‘link’
kutoka kwenye Mtando wa
www.google.com.”

Taarifa hiyo ilisema kuwa JWTZ
inapenda kueleza wananchi na
dunia kwa ujumla kwamba
wanaoneza taarifa hizo wana lengo
la kukatisha tamaa juhudi
zinazofanywa na nchi za Maziwa
Makuu na SADC kuleta amani nchini
DRC kwani JWTZ wako DRC kwa
mujibu wa taratibu za kiutendaji za
Umoja wa Mataifa.