AU Yafikisha miaka 50 Tangu kuanzishwa.

Umoja wa Afrika unatimiza miaka 50 tangu kuundwa kwake hapo tarehe 25 Mei 1963 kwa jina la Umoja wa Nchi Huru
za Afrika kuongoza mapambano dhidi ya ukoloni na kumaliza utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini.

Tokea mabadiliko ya kidemokrasia katika Rasi ya Matumaini Mema na kumalizika vita baridi, Umoja huo unatafuta njia
za kuwa na msimamo wake wenyewe. Unalenga kuleta ushirikiano wa kikanda, kuondoa vizuizi vya lugha na biashara
na hatimaye siku moja kuleta muungano wa bara zima la Afrika.

"Mtukufu Mfalme, mwenyekiti, waheshimiwa wenzangu, ndugu na marafiki: Kwa hakika ile hali ya viongozi 32
kukusanyika hapa Addis Ababa ni ushahidi wa wazi wa haja kubwa waliyonayo raia wetu baada ya uhuru. Bara zima
limetupa mamlaka ya kuwa na mkutano huu chini ya msingi wa Umoja wetu." Maneno hayo yalitamkwa tarehe 25 Mei
1963, mjini Addis Ababba, Ethiopia kwenye hotuba ya kusisimua Rais wa Ghana, Kwame Nkrumah, juu ya kibali cha
kuundwa kwa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU). Lengo la pamoja: Umoja wa bara hilo , lenye nguvu kiuchumi na
uhuru wa kisiasa.

Mwanzo wake
Miaka sita kabla ya hapo, muasisi Nkurumah kutoka kile
kilichokuwa kikijulikana kama koloni la Uingereza
"Pwani ya Dhahabu", leo hii Ghana, aliiongoza nchi hiyo
kuwa huru na akawa ndiye baba wa vuguvugu la
uzalendo wa Mwafrika katika kuliongoza jukwaa la
mataifa machanga kupambana dhidi ya ukoloni na
ubaguzi wa rangi.
Muongozo muhimu, ambao ni ule wa kutoingilia
mambo ya ndani ya mataifa mengine huru, ukageuka
hatimae kuwa janga kwa Umoja huo, kwani mtindo wa
mapinduzi ya kijseshi wa miaka ya 1960 na vita vya
wenyewe kwa wenyewe vilipotokea, viongozi wa
mataiafa ya Afrika walibakaia kimya wakiangalia.

Madai kwamba OAU ilishindwa wakati wote ni jambo linalopingwa na balozi wa zamani kutoka Ethiopia, Mengiste
Desta. "Ninayapinga vikali madai kawamba OAU ulikuwa Umoja uliokosa meno ya kuuma. Kinyume ulikua na meno
makali mno -ikiwa mtu atatambua malengo ya kuundwa kwake, yaani kulikomboa bara zima kutokana na ukoloni na
sera ya ubaguzi wa rangi."
Hata hivyo muda si mrefu ulishinddwa kutimiza fikara ya awali, anasema Dr Mehari Maru, mtaalamu wa masuala ya
Umoja wa Afrika kutoka Taasisi ya Masuala ya Usalama (ISS), mjini Addis Ababa. "Kumalizika kwa ukoloni na sera ya
ubaguzi wa rangi, kulifungua njia ya kuwepo mjadala. Nini maswala mapya ya Umoja huo na kutokana na hayo
pakahitajika taasisi mpya kuleta mabadiliko yanayohitajika na hivyo ukaazaliwa Umoja wa Afrika."

Umoja wa Afrika
Baada ya kuupa jina jipya la Umoja wa Afrika (AU) ambao
uliundwa 2002 mjini Durban, Afrika ya Kusini, baada ya
kumalizika vita baridi, madhumuni yake yakawa ni kuleta
muungano wa kiuchumi na demokrasaia.

Kiroja cha mambo katikati ya miaka ya 1990, kiongozi wa
Libya Muammar Gaddafi aliyejitangaza "Mfalme wa
Wafalme" wa Afrika, alilazimisha fikra ya mtazamo wa
Nkrumah wa "Muungano wa Afrika,", ingawa ilikuwa siasa
kwa masilahi ya kisiasa ya Gaddafi kuliko kuwa hatua ya
kifalsafa.

Hata hivyo, mpango wake wa kuwa na jeshi moja, sarafu
moja, biashara na kusafiri bila vizuizi kama ilivyo katika
Umoja wa Ulaya ulisababisha mgawanyiko zaidi kuliko umoja. Kutokana na mvutano huo kukazuka kambi mbili na
Afrika ya Kusini yenye nguvu kisiasa ikasimama kumpinga Gaddafi.

"Bila shaka matokeo kwetu si ya kuridhisha. lakini tunasonga mbele pamoja na nina hakika siku hadi siku tutafikia
karibu lengo la "Muungano wa Afrika." Alisema mjumbe wa Gaddafi kwenye Umoja huo, baada ya kuvunjwa moyo na
kile alichokiona ni udhaifu, aliwaambia wajumbe baada ya kuchaguliwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika 2009. Gaddafi
mara kwa mara alikuwa akitowa matamshi makali kwa waliompinga kwa kuzingatia kile alichokiona ni mapenzi ya
Waafrika wengi kwake.

Hatimaye
Ingawa wazo hilo lilizusha mabishano na kutoa sura ya
mgawanyiko miongoni mwa mataifa, Umoja wa Afrika
sasa una waziri wa ndani wa Afrika ya Kusini
Nkosazana Dlamini-Zuma kama Rais wa Halmashauri
Kuu ya Umoja huo, mwana mageuzi aliyetangaza haraka
kwamba anataka kuona unawajibika zaidi.

Halmashauri
hiyo kuu inataka kuendeleza sera ya kuadhibu kwa
kusimamisha uanachama na vikwazo kwa wanaokiuka
katiba na muongozo wake.
Mtihani kwa uwajibikaji na nguvu za kiutendaji za
Umoja wa Afrika, kandoni mwa pigo la ujumbe wake wa
AMISOM nchini Somalia, ni mgogoro katika mataifa ya
Afrika ya Magharibi ya Mali na Jamhuri ya Afrika ya
Kati.

Kwa Maoni ya Mehari Maru kutoka Taasisi ya
Masuala ya Usalama ni kwamba "Leo Afrika ni ya kidemokrasia zaidi kuliko miaka kumi iliyopita ambapo tulikuwa na
serikali chache zilizochaguliwa kidemokrasia. Lakini hili halipaswi kutafsiriwa kwamba ni uongozi wa kidemokrasi.

Demokrasia ni kutambua fikra tafauti, kwani ndiyo msingi wa matatizo ya kisiasa Afrika."

Sherehe za Jumamosi
Katika Sherehe za Jumamosi, miongoni mwa mambo
mengine ni mchuano wa kandanda kati ya wanachama
waasisi Ethiopia na Sudan. Pia Umoja huo unasherehekea
pamoja na Ujerumani, kwa sababu tangu miaka kadhaa,
Ujerumani imekuwa ikiliiunga mkono Baraza la Amani na
Usalama la Umoja wa Afrika kwa kusaidia mafunzo.

Afisa anayehusika na masuala ya Afrika katika Wizara ya
mambo ya nchi za nje mjini Berlin, Egon Kochanke,
anazungumzia mustakbali mwema akisema kwamba
malengo waliyokuwa nayo Rais wa Tanzania, Julius
Nyerere, na Kwame Nkrumah wa Ghana miaka 50 iliopita,
yalikuwa ni kuleta maendeleo ya kisiasa na kiuchumi barani
Afrika na kuwa na mtazamo wa pamoja kuweza kuyafikia.

Kidogo mafanikio si kama yalivyotarajiwa, lakini leo hii Umoja wa Afrika una nguvu na msimamo wenye nguvu sana
katika sera ya kigeni na usalama na pia upigaji kura."
Miaka 50 ya Umoja wa nchi huru za Afrika sasa Umoja wa Afrika, bara hilo limezindukana zaidi.

Wakati Rais wa
Ujerumani Joachim Gauck alipozuru Addis Ababa hivi karibuni na kupendekeza kuongezwa mchango wa wanajeshi wa
Ujerumani, hilo halikupata shauku kutoka kwa Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika Dlamini-Zuma.

Kauli
mbiu ya " Suluhisho la matatizo ya Afrika ni la Waafrika wenyewe," inapewa kipaumbele miaka 50 mengine ijayo ndiyo
itakayotowa jibu.

Habari kutoka DW