Takriban watu sita wameuawa katika
shambulizi lililofanywa na wapiganaji
wa kiisilamu mpakani mwa Kenya na
Somalia, kaskazini mwa nchi.
Duru za polisi zinasema kuwa polisi
wawili walifariki kutokana na
shambulizi hilo lililofanywa katika
vituo vya Abdisugow na Damajale.
Msemaji wa kundi la wapiganaji wa
kiisilamu wa al-Shabab, limekiri
kufanya shambulizi hilo na kuwa watu
wanane waliuawa.
Jeshi la Muungano wa Afrika ambalo
limefurusha wapiganaji wa Al
Shabaab kutoka
Mogadishu,limewadhoofisha
wapiganaji hao ingawa hufanya
mashambulizi ya mara kwa mara
mpakani.
Al-Shabab, linatumia sheria za
kiisilamu katika maeneo wanayodhibiti
nchini Somalia.
Wamefurushwa
kutoka maeneo ya mijini ingawa
wanaendesha harakati zao katika
maeneo ya mashinani.
Mkuu wa polisi, Inspekta David
Kimaiyo, aliambia shirika la habari la
AP, kuwa watu sita wangali
hawajulikani waliko, kufuatia
shambulizi la jumamosi usiku.
Sheikh Abdiasis Abu Musab,ambaye
ni msemaji wa shughuli za kijeshi za
al-Shabab, aliambia shirika la habari
la Reuters kuwa siku ya Jumamosi
waliweza kuingia kilomita 35 ndani ya
Kenya na kuvamia kambi za polisi.
Mtandao mmoja wa kundi hilo
ulikuwa na ahabri kuwa watu wawili
walitekwa nyara na kuingizwa Somalia.
Mkuu wa wilaya karibu na kambi ya
Dadaab, Albert Kimathi, alithibitisha
mashambulizi hao mawili dhidi ya
vituo vya polisi.
Wanamgambo hao wamekuwa
wakifanya mashambulizi ya mpakani
nchini Kenya tangu mwaka 2011
ambapo majeshi ya Kenya kwa
ushirikiano na wanajeshi wa AU ,
walipoingia Somalia kupambana na
wanamgambo wa Al Shabaab.