Hatimae timu kutoka mkoa wa Katavi, Katavi Warriors wameifurumusha timu kutoka mkoa wa Rukwa, Rukwa United kwa ushindi wa Goli mbili kwa moja (Rukwa United 1-2 Katavi Warriors).
Timu hizi ziko katika ligi ya TFF ngazi ya kanda ambapo mechi huchezwa katika mfumo wa nyumbani na ugenini.
Ushindi wa leo umekuja baada ya mechi ya kwanza iliyopigwa katika uwanja wa Azimio mjini mpanda na matokeo kutoka bila.
Rukwa United wamekubali kichapo hicho katika uwanja wao wa Mandela mjini sumbawanga. Katika Mechi hiyo Katava Warriors walitangulia kufunga katika kipindi cha kwanza kwa goli lilofungwa na Macky kabla ya kusawazisha katika kipindi cha pili na kufanya matokeo kuwa moja moja mpaka dakika za lala salama ambapo katavi warriors hali maarufu kama Aston villa walipoandika goli la pili kupitia mkwaju wa penalti.