Jeshi la polisi mkoa wa Katavi
limemkamata Hilali Abdalah
(30) mkazi wa mtaa wa majengo
mjini hapa kwa kumkamata
akiwa na vifaa vya kutengenezea
noti bandia akiwa katika nyumba
ya kulala wageni
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa
Katavi Dhahiri Kidavashari alisema
Hilali alikamatwa hapo jana majira
ya ssa 8 mchana katika nyumba ya
kulala wageni inaitwa
Ambassodor aliyoko katika mtaa
wa mji wa zamani Kata ya
kashaulili mjini hapa
Alisema mtuhumiwa alikamatwa
kufuatia taarifa za kiitelejensia
kulifikia jeshi la polisi mkoa wa
Katavi kutoka kwa raia wema
kuwa Hilali anajihusisha na
shughuli hiyo ya utengenezaji wa
noti bandia.
Kidavashari alivitaja vifaa
aliwavyo kamatwa navyo
mtuhumiwa kuwa ni karatasi
ngumu 217 ambazo hutumika
kutengenezea noto bandia za
shilingi 10,000 bomba mbili za
sindano zenye dawa maalumu
kwa ajiri ya kubadilishia rangi ya
karatasi hizo ili zifanane na pesa
hizo.
Alivitaja vifaa vingine kuwa ni
powder chupa moja kwa ajili ya
ya kumfanya mteja ataakizishika
mapema zisiache alama ya
vidole kwenye pesa beseni moja
jeusi kwa ajiri ya kusafishia
karatasi hizo mara baada ya
kuzipitishia kwenye hatua kadha
vifaa ningine alivyo kamatwa
navyo Hilali ni karatasi 21 plain
kwa ajiri ya kufunikia karatasi
ngumu zisipate hewa wakati wa
utengenezwaji wa noti bandia
soltap 2 kwa ajiri ya kubania
karatasi zisipate hewa mapema
pasi moja ya umeme kwa ajili ya
kukaushia pesa hizo mara baada
ya kuziosha na ugolo vijiko
vitatu ambao alikuwa akiutumia
kama kilevi wakati akifanya
shughuli hiyo haramu.
Kamanda waa polisi mkoa wa
Katavi alieleza awali mtuhumiwa
alikuwa akijishughulisha na
shughuli za kuuza mitumba
kaika soko la Buzogwe mjini hapa
na baadae alihamia mkoani
Tanga na ndiko aliko patia ujuzi
wa kutengeneza noti bandia
Kidashari alieleza hatimaye baada
ya kupata utaalamu huo alirejea
Mpanda na kuanza kazi hiyo
mbaya ya kuvunja sheria za
Nchi.
Alisema katika maelezo yake ya
awalialikiri kufanya shughuli hiyo
kwa kile alicho kieleza ni
kutokana na yeye hapo siku za
nyuma aliwahi kutapeliwa pesa
kwa kupewa noto bandia ndio
maana ameamua na yeye kulipa
kisasi kwa watu wengine
Pia mtuhumiwa alitaja sababu
nyingine kuwa ni katika kujitafutia
maisha kwa njia ya ytafuataji ndio
maana akaamua kujitafutia pesa
kwa njia hii
mtuhumiwa anategemewa
kufikishwa mahakamani mara
upelelezi wa kesi hii utakapo
kamilika ili aweze kujibu
mashitaka yanayo mkabili.
Chanzo:kataviyetu.blogspot.com