Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano na Kimataifa Bernard Membe,
amesema kuwa kamwe Tanzania haitaogopa
vitisho vinavyotolewa na Kikundi cha Waasi cha
M23 cha DRC, huku akitoa masharti matatu kwa
kikundi hicho kama hakitaki majeshi ya
Tanzania yaende nchini humo.
Membe alisema hayo, akijibu hoja iliyotolewa na
Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni kuwa kikundi hicho kimeandika barua ya wazi ikieleza kuwa,
kisilaumiwe kama raia wa Tanzania watapatwa na mauaji ya halaiki ikiwa vikosi vya majeshi yake
vitaenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
“Katika barua hiyo kiongozi huyo ametishia kwamba kikundi cha M23 kisilaumiwe kwa mauaji ya halaiki
yatakayotokea kwa raia wa Tanzania endapo Serikali itaendelea na mpango wa kupeleka askari wake
kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Congo DRC,” ilisema hotuba ya
kambi ya upinzani.
“Katika barua hiyo kiongozi huyo ametishia kwamba kikundi cha M23 kisilaumiwe kwa mauaji ya halaiki
yatakayotokea kwa raia wa Tanzania endapo Serikali itaendelea na mpango wa kupeleka askari wake
kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Congo DRC,” ilisema hotuba ya
kambi ya upinzani.
Akijibu hoja hiyo, Membe alikiri kuiona barua hiyo, aliyosema ilielekezwa kwake pamoja na Bunge na
kusema kuwa lengo lake ni kutoa vitisho kutokana na kuogopeka kwa vikosi vya Tanzania.
“Kuhusu M23 nimepata barua wizarani na bungeni imeletwa, hiyo barua wanasema imeandikwa kwangu
na Mungu na kuwa imesainiwa na Mungu, hawa wanatutisha kama tulivyotishwa na Kanali Mohamed
Bakari alipokuwa ameiteka Anjwani, pamoja na vitisho vyote alivyotoa yeye ndiye aliyeishia kutoroka
akiwa amevaa baibui,” alisema na kuongeza:
“M23 wanaua, wamebaka, wamedhalilisha wazee na mama, wameleta wimbi la wakimbizi zaidi ya
220,000, halafu wanamnukuu Mwalimu Nyerere wakisema binadamu wote ni sawa, huko ni kukufuru
Kama wangekuwa wanathamini kauli ya Mwalimu wasingeliua, wasingebaka, wasingedhalilisha wazee.”
Alibainisha kuwa, waasi wa kikundi hicho wamefanya uhalifu wa kutisha hadi kiongozi wao Bosco
Ntaganda akaamua kujisalimisha kwenye vyombo vya usalama na kwa sasa amepelekwa katika
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC.
“Kwa hiyo M23 hawawezi kutufundisha ubinadamu, hawawezi kutufundisha amani na wala hawawezi
kutumia jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kutuambia kitu kuwa binadamu wote ni sawa,”
alisema.
Alisema kuwa, vikosi vitakavyokwenda DRC vitakuwa na kazi ya kutekeleza mambo matatu akitaja la
kwanza kuwa ni kuhakikisha M23 hawajipanui kutoka idadi ya 600 waliopo sasa, kudhoofisha kundi hilo
kwa kuondoa silaha mikononi mwao pamoja na kutengeneza uhusiano.
“Ni vizuri, wale askari tutakaowaona wapo bora waingie kwenye Jeshi la Taifa la DRC ili kuleta amani
pale na tutalinda amani pale. Wakituchokoza tutajibu mapigo, lakini lengo la kwenda pale siyo kupigana
vita.
Sisi tunaenda na mandate (mamlaka) ya Umoja wa Mataifa ‘chapter’ 7 ya Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa,” alisema.
Aliongeza: “Jeshi letu ni imara sana, lenyewe halishindwi lipo Lebanon linafanya kazi nzuri na ya
kusifiwa. Lipo Darfur la linafanya kazi nzuri ya kustahili kusifiwa; na Watanzania wajue kuwa ‘United
Nation Mission ya Darfur’ sasa inaongozwa na jenerali Mtanzania kuanzia mwezi huu, kutokana na rekodi nzuri ya jeshi letu la Tanzania
Ndiyo maana hao wanaobaka na kuua wakisikia
tu Tanzania wanakwenda wanamsingizia Mungu,
eti Mungu anawaunga mkono na Mwalimu
Nyerere anawaunga mkono!”
“Wanataka Bunge hili liseme Serikali isipeleke
askari. Nalipongeza Bunge kwa uelewa mpana
na kuungana kuwa kitu kimoja tunapokabiliana
na vitisho vya aina hii.
Tanzania tuna nguvu, tuna historia, wakitaka M23 tusiende kule Alitaja mambo hayo kuwa ni; “Moja,
wafanye kama walivyofanya jana,(juzi) waanze kujitoa kwenye jeshi lile na kujisalimisha.
Pili, yapo mazungumzo yanayofanywa na Rais Museveni Kampala ya kuitaka M23 pamoja na majeshi na
Serikali ya DRC kukaa na kumaliza tofauti zao basi wamalize tofauti zao na kisha watupigie simu
kwamba wameshayamaliza matatizo yote.”
Sharti la tatu ambalo Membe alitoa kwa kikundi hicho ni kutaka kikundi hicho kuacha mara moja vitendo
vyao vya kubaka, kuua na kuwafanya wananchi kuwa wakimbizi Kuhusu suala la Malawi, alisema:
“Mazungumzo yataanza rasmi kwa maana ya kuitwa kuhojiwa sisi akiwemo Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.
Mwishoni mwa mwezi huu ataenda Maputo, watakuwa wanahojiwa, ni imani yetu Watanzania
kwamba jopo la marais wastaafu linaloongozwa na Joachim Chisano litafikia uamuzi.”
“Lakini ikishindikana itabidi tusonge mbele kwenda ICJ, Tanzania hatutasita kufanya hivyo na tuna kila
aina ya ushahidi wa kuhakikisha kwamba tunashinda kesi hiyo,” alisema Membe.
Source:Mwananchi.co.tz