Shaffih Kujibu Tuhuma za TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih
Dauda ambaye ni mmiliki wa tovuti
ya www.shaffihdauda.com kutoa
maelezo kuhusiana na barua ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye
mtandao wake huo.

FIFA ambayo ilisimamisha mchakato
wa uchaguzi wa TFF baada ya
baadhi ya wagombea kuulalamikia,
baadaye ilitoa maelekezo kuhusu
mchakato huo kwa barua ambayo
iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar
Lenga.

Rais wa TFF katika mkutano wake na
waandishi wa habari ambao Dauda
alihudhuria alibainisha kuwa barua
hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu,
na kuruhusu waandishi kuisoma
kwa Ofisa Habari wa TFF bila
kuondoka nayo.

Wakati Rais Tenga anazungumza na
waandishi wa habari (Mei 2 mwaka
huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA
ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF
pekee, na viongozi wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo.

Hivyo TFF imemtaka Dauda
kutoa maelezo ya mahali alipoipata
barua hiyo ndani ya siku saba.

Chanzo:shaffihdauda.com