Polisi Mtwara Wapata tuhuma za Ubakaji

Hali ya usalama katika Manispaa
ya Mtwara Mikindani mkoani hapa
imezidi kuwa mbaya baada ya
askari polisi kudaiwa kufanya
unyama kwa k uwabaka
wanawake na kumpiga risasi
mjamzito
Mbali na unyama huo polisi pia
wanadaiwa kuchoma moto
nyumba tatu za wananchi katika
mtaa wa Magomeni na vibanda
vya maduka kadhaa na kupora
vitu vilivyomo ndani.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa
anasema hali ni shwari na kwamba
wananchi watoke nje kuendelea na
shughuli zao kama kawaida.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Rufaa ya Ligula,
Mohamedi Kodi amethibitisha
kupokea mwili wa mjamzito
ukiwa na tundu tumboni,
zinazoaminika kuwa za risasi na
hivyo kufanya idadi ya maiti
zilizopokelewa hospitalini hapo
kufikia mbili na majeruhi 18:

“Ni kweli kwa leo( jana)
tumepokea maiti moja ya
mwanamke ambaye ni mjamzito
wa miezi saba, amepigwa risasi
tumboni. Pia tumepokea
mwanafunzi wa shule ya
sekondari ya Chuno,amevunjwa
miguu yote kwa risasi.”
Habari zinadai kuwa mjamzito
huyo ameuawa akiwa nyumbani
kwake baada ya polisi kuvamia
makazi yake.

Huduma za kijamii zimesimama,
hakuna maduka yaliyo wazi,
hakuna usafiri wa daladala wala
pikipiki, mji upo kimya, sauti za
milio ya mabomu na bunduki
zimetawala, wanajeshi waliovalia
sare wameuzingira mji wakiwa
katika magari na pikipiki.
Wakizungumza na Waandishi wa
Habari kwa nyakati tofauti wakazi
hao wamelalamikia kitendo cha
askari wa jeshi la polisi kuingia
katika makazi yao, kuwapiga,
kuwabaka na kuwapora mali zao:

Popout
“Magomeni A hatuna amani
askari wanaingia majumbani
mwetu wanatupiga na
kutunyang’anya simu, yani
huku Magomeni hatuna amani
kabisa, tumepoteza watoto na
hatujui hata waume zetu wako
wapi” alisema Paulina Idd na
kuongeza:

“Majumba yetu yamechomwa
moto , wanaofanya fujo ni polisi
wenyewe halafu wanakuja
wanatubaka na kuiba mali zetu
halafu tunateseka sisi yaani
tumechoka kabisa na serikali
yenyewe,” alisema Paulina.

Kamanda Sinzumwa alipoulizwa
kuhusiana na tuhuma hizo alisema
hawezi kuzungumzia suala hilo
kwa madai kuwa atapingana na
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk
Emmanuel Mchimbi aliyewasili
Mtwara leo: “Kuhusiana na
suala hilo siwezi kulizungumzia
kwa sasa kwani nitapingana na
Waziri wangu kwani leo ametoa
tamko bungeni na leo
atawasili,” alieleza Sinzumwa
Wananchi wazungumzia bajeti
Wakizungumzia uwasilishwaji wa
hotuba ya Wizara ya Nishati na
Madini wakazi wa hapa
wamesema kuwa hawakubaliani
na ujenzi wa bomba la kusafirisha
gesi kwani mpango huo utawaletea
dhuluma:

“Mpango wa kusafirishwa kwa
gesi asilia hatuna mpango nao
kwa wakazi wote wa Mtwara
kwa kifupi akina mama wa
mtwara hatutaki itoke,” alisema
Fatuma Abdallah.


Chanzo:Mpekuzi