Sister(Mtawa) Feki Akamatwa Iringa

Mwanamke - anayejiita Sister Phylis
Wanjiru Kamau, raia wa Kitui nchini
Kenya akiwa ofisi za kamanda wa
jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, baada
ya kukamatwa
Taarifa za kipolisi, za kukamatwa kwa
Sister Feki Phylis Wanjiru Kamau.

JESHI la polisi mkoa wa Iringa
limemkamata mwanamke Phylis
Wanjiru mwenye umri wa miaka 44
aliyevalia mavazi ya kitawa wa
masister wa kanisa Kathoriki,
ambapo baada ya kupekuliwa
amekutwa na baadhi ya vielelezo
vilivyobaini kuwa ni tapeli.

Wanjiru ambaye ni raia wa nchi ya
Kenya amekamatwa na jeshi la polisi
baada ya masister wenzie kubaini
kama si mmoja wao, kutokana na
kushindwa kufanya baadhi ya
masuala ambayo ni msingi wa
utawa wao.

Akizungumzia mkasa huo, kamanda
wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa
Michael Kamuhanda amesema
mwanamke huyo kabila laKe ni
Muwembu wa nchini Kenya
amekamatwa katika nyumba  za
masista zilizopo Ipogolo mjini Iringa.

Aidha Kamuhanda amesema
mwanamke huyo ambaye awali
aligoma kutoa maelezo ya kina juu
ya ujio wake nchini Tanzania, katika
upekuzi walimkuta na baadhi ya chip
(Line) za makampuni mbalimbali ya
simu ya ndani na nje ya nchi.
Kamuhanda amesema Sister huyo
bandia alikutwa pia akiwa na hati za
kusafiria (Passport) mbili, moja ikiwa
niya Africa Mashariki yenye namba
Ke. 020659 huku hati ya nyingine
ikiwa na jumuiya ya Kenya namba A.
1790366.

Amesema Sister huyo feki katika hati
hizo ilionyesha kuwa alitembelea
nchi ya Rwanda, Uganda pamoja na
nchini Tanzania ambapo siku za hivi
karibuni alikuwa Mkoani Mara
Tarime.

Sister huyo FEKI amekuwa akitumia
mbinu ya kujiangusha kama mtu
mwenye ugonjwa wa kifafa pindi
anapofanyiwa mahojiano, jambo
linalowawia vigumu jeshi hilo kupata
maelezo ya kina dhidi ya dhamira
yake ya kuingia humu nchini.

Kamuhanda ameitaka jamii kuwa
makini na wageni mbalimbali, huku
akiwaasa kuacha tabia ya kuwaamini
watu kwa muonekano wao,
kutokana na mwanamke huyo
kutumia njia hiyo ambayo
inamfanya kila mtu kumuamini.